Connect with us

Investigative

KWAYA YA MT. CECILIA MERERANI YAJIZATITI KATIKA UINJILISHAJI KWA KUTUMIA WATOTO,VIJANA NA WAZEE.

Published

on

Kwaya ya Mt. Cecilia Mirerani ni kati ya kwaya kongwe hapa nchini iliyoanzishwa zaidi ya miaka 15 iliyopita ikiwa na wanakwaya 40 wakati huo.
Kwaya hii inapatikana katika mji mdogo wa Mererani,mkoani Manyara,ndani ya parokia ya Bikira Maria Malkia wa Rozari.
Pamoja na kwaya hii kuwepo katika eneo la machimbo ya tanzanite, wakazi wake kuwa wachimbaji wadogo wa madini haya , lakini suala la imani liko thabiti, na kwaya hii imeendelea kufanya vizuri ikiwa na albamu saba mpaka sasa.
Mwenyekiti wa kwaya hii Sostenes Msechu alisema albamu ya kwanza ilibeba jina la Uwe kwangu mwamba wa nguvu,ya pili Siri yangu anaijua Mungu, ya tatu Upendo na Amani,na nne Maajabu ya Mungu.
Nyingine ni bwana Yesu amekaa, Hebu jiulize, Mkataa pema pabaya panamwita, na kuongeza zilizofanyiwa video ni albamu tatu ile ya maajabu ya Mungu,Mkataa pema pabaya panamwita na Mchanganyo bwana Yesu amekaa.
Albamu mbili nyimbo zake zilichanganywa wakati wa kufanya video katika albamu ya Maaajabu ya Mungu na Mchanganyo bwana Yesu amekataa,nazo ni zile za siri yangu anaijua Mungu na Uwe kwangu mwamba wa nguvu. NITAHAKIKISHA BAADAE.
Msechu alisema mlezi wa kwaya hii ni paroko wa kanisa hilo padre Aloyce Kitomari, na kwa sasa wanakwaya wamefikia 45 ingawa wanapungua wakati mwingine kutokana na kuhama hama kwani wengi hufika hapo kwa shughuli mbalimbali.
“Wengine walimu wa shule wakihama tunapata upungufu,wengine wachimbaji na wengine huwa wanakaa na wlezi wakihama katika kwaya tunapata pengo”.aliongeza.
Akizungumzia suala la watuzi wa nyimbo zao amesema wako tofauti tofauti,aliwataja kuwa ni Bernard Mkasa, JB Manota, Evodious Minja ambaye alikuwa mwanakwaya na sasa amehamia Dar es salaam.
Ameongeza mtunzi mwingine ni Padre Aloyce Msigwa yuko Njombe kwa sasa lakini hafahamu parokia anayotoka na ndio mtunzi wa wimbo wa Maajabu ya Mungu, uliobeba jina la albamu ya nne.
Mwenyekiti amesema kwaya yao inachanganya watoto, vijana na wazee kwa sababu mbalimbali,ikiwemo kwa watoto wanakuza vipaji,vijana ni uimara wa kwaya na wazee huchota hazina yao (busara).
“Tunafanya hivi kwasababu wazee nguvu itakwisha na tutakuwa na kwaya bado,ili kuiweka imara tunawatumia watoto” alisema Msechu.
Ameongeza albamu iliyofanya vizuri kwa mauzo katika upande wa audio na video ni ile ya Mchanganyo bwana Yesu amekataa ingawa maajabu ya Mungu imesambaa sana hadi Marekani (wanapokea simu) Ulaya na nchi nyingine za Afrika.
Msechu alisema nyakati zote wakiwa na uzinduzi kanisani hapo kuanzia katika ibada ya misa takatifu, huwakaribisha kwaya jirani kutoka kanisa la KKKT Mererani inayojulikana kwa jina la Sauti ya mtu aliyae nyikani kushirikiana nao kwa kuwa ni marafiki zao pia.
Mwandishi mkongwe kutoka The Standard , nchini Kenya, Luke Anami alisema anafurahishwa sana na kwaya hii kwa mpangilio wa sauti, kuchanganya umri watoto,vijana na wazee, huleta raha kusikiliza na kuangalia video pia na wote huonekana kujituma; Na albamu anayoipenda zaidi ni ya Maajabu ya Mungu

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Continue Reading
3 Comments

3 Comments

 1. ANNORD MWAPINGA

  19/07/2013 at 4:30 pm

  yah, hongera zao, wanafanya vizuri sana. waendelee na utume huo

 2. gaspar tesha

  23/11/2013 at 4:10 pm

  sooo nice work from our fellow hongereni sana. na Mungu awatie nguvu zaidi waweze kumtumikia kwa nguvu na ari zaidi

 3. mosses komba

  03/02/2014 at 4:09 pm

  kweli vijana wa mchanganyo mnatisha hongereni sana naamini mkiimbacho ndicho kilicho moyoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Investigative

‘UBESHI’: Safari ya Vijana Kuifikia Almasi Mwadui-Shinyanga

Published

on

MAJUZI nilikuwa katika utafiti wa namna gani Madini ya Almas yanayopatikana katika Mji Mdogo wa Maganzo Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga umewanufaisha wananchi wanaozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui.

(more…)

Continue Reading

Investigative

Hofu ya Usalama kwa wafanyakazi GGM Yatanda

Published

on

SIKU chache baada ya moto kuzuka ndani ya mgodi wa Geita (GGM) na kuteketeza mali zenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 25,hofu kubwa ya kupoteza maisha imeibuka kwa uongozi na wafanyakazi wa mgodi huo.

(more…)

Continue Reading

Investigative

If we can’t give people’s priorities the attention they deserve, why ask them to prioritize?

Published

on

In a move intended to empower the citizens and give them mandate to decide on their own development priorities, the government adopted the decentralization policy.

(more…)

Continue Reading

Muhimu Kusoma