Connect with us

Investigative

Wajawazito wanahudhuria kliniki lakini wanajifungulia nyumbani na kwa wakunga wa jadi

Published

on

Wajawazito wengi nchini wanahudhuria Kliniki lakini wengi hawataki kujifungulia katika vituo vya afya imebainika.

Katika hospitali ya manyamanyama wilayani Bunda mkoani Mwanza asilimia 96 ya wajawazito wanahudhulia kliniki lakini wakati wa kujifungua ni asilimia 56 tu ndiyo wanaenda kujifungulia katikavituo vya afya.

Wajawazito wengi wanasema kuwa wanapoenda kujifungulia katika vituo vya afya wanakumbana na gharama kubwa zikiwemo zile za kununua karatasi ya kulala wakati wa kujifugua, matusi na gharama za mwendo kutoka mahala wanakoishi mpaka kufikia huduma kuna umbali mrefu.

Kwa mfano katika hospitili ya Butiama., wanawake wanahitaji kujifungulia katika eneo la vituo vya afya lakini wanaishi umbali wa kilomita 100 na vituo hivyo na wanalazimika kujifungulia nyumbani au kwa wakunga wa jadi.

Usafiri
Jiografia ya maeneo mengi katika mikoa ya Mbeya na Mara kufikia huduma za kisasa hasa kwa wajawazito siyo nzuri.

Kwa mfano katika wilaya mpya ya Butiama kuna wajawazito wanaishi kilomita 100 na hospitali ya wilaya ambayo ndiyo tegemeo lao katika kujifungua hasa wale wenye matatizo ambapo ambao hawana matatizo hulazimika kujifungulia nyumbani au kwa wakunga wa jadi.

Kuhusu ahadi ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa mwaka 2010 wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu kuwa serikali ingenunua pikipiki za matairi matatu(Bajaji) ahadi hiyo imetekelezeka na baadhi ya vituo vya afya zipo bajaji hizo lakini hazifanyi kazi kutokana na dosari mbalimbali ikiwemo kutokata kona upande wa kushoto na muundo wake kuonekana kuwa wa udhalilishaji kwa wanawake.

Bajaji hizo 400 zilizosambazwa maeneo mengi nchini zinadaiwa kununuliwa kwa Shilingi Milioni 40 na kusambazwa katika vituo vya afya 134 lakini hakuna mahala zinapofanya kazi ya kusaidia wajawazito na maeneo mengine wamefungua kitanda na kuamua kutumia pikipiki kwa ajili ya kazi za kubebea dawa na vifaa vya hospitali.

Hali hiyo inajidhihilisha kuwa nchi aina wataalam wa utafiti bali mambo mengi utafiti unafanywa nje ya nchi hatimaye utafiti wao unatekelezwa Tanzania bila kuangalia mazingira na miundombinu ya nchi yetu hatimaye kuonekana kuwa fedha nyingi zinatumika bila faida.

Kutokana na ukweli, takwimu na ushahidi huo, kazi inabaki kwa serikali kuchukua hatua ili kutekeleza malengo ya milenia ambayo yanasema kuwa kufikia mwaka 2015 inatakiwa kuwe kumepungua kwa vifo vya mama na mtoto.

Vinginevyo hatutafikia malengo hayo ya milenia hasa vijijini.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Investigative

‘UBESHI’: Safari ya Vijana Kuifikia Almasi Mwadui-Shinyanga

Published

on

MAJUZI nilikuwa katika utafiti wa namna gani Madini ya Almas yanayopatikana katika Mji Mdogo wa Maganzo Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga umewanufaisha wananchi wanaozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui.

(more…)

Continue Reading

Investigative

Hofu ya Usalama kwa wafanyakazi GGM Yatanda

Published

on

SIKU chache baada ya moto kuzuka ndani ya mgodi wa Geita (GGM) na kuteketeza mali zenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 25,hofu kubwa ya kupoteza maisha imeibuka kwa uongozi na wafanyakazi wa mgodi huo.

(more…)

Continue Reading

Investigative

If we can’t give people’s priorities the attention they deserve, why ask them to prioritize?

Published

on

In a move intended to empower the citizens and give them mandate to decide on their own development priorities, the government adopted the decentralization policy.

(more…)

Continue Reading

Muhimu Kusoma