Connect with us

Featured

Dk. Slaa: Video ya Lwakatare ni feki!

Published

on

KATIBU  Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa amezungumzia video aliyorekodiwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama hicho, Wilfred Lwakatare na kusema ni ya kutungwa na vyombo vya dola.

Dk. Slaa pia amelituhumu Jeshi la Polisi kufanya mchezo mchafu kwa maslahi ya kisiasa.

Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari Makao makuu ya chama hicho kufafanua suala la kushikiliwa kwa Lwakatare.

Dk. Slaa, alilalamikia jeshi la polisi kuwa limekuwa likitumika kisiasa huku akitoa mfano wa chama hicho kuwa kimekuwa kikitaarifu jeshi la polisi kuhusu mambo hayo lakini halijawahi kuchukua hatua.

Alisema  jeshi la polisi halijawahi kuchukua hatua stahiki kwa suala la mauaji ya Daudi Mwangosi kumwajibisha Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Iringa aliyesimamia na kufanikisha kifo cha mwandishi huyo wa habari, jeshi la polisi pia halikuchukua hatua za kumhoji Dk. Stephe Ulimboka baada ya kuteswa na mtu anayedaiwa kuwa ni Afisa wa usalama wa Taifa wa Ikulu, hali kadhalika hawezi kushangaa ikiwa jeshi la polisi halitaacha kumhoji Absalom Kibanda.

Amesema, jeshi la polisi limekuwa likitoa taarifa za kukichafua chama, akikumbushia suala la Mwangosi, alisema kuwa mara tu baada ya tukio la Mwangosi kuuawa, jeshi la Polisi kupitia kwa Kamishna wake lilitoa taarifa kuwa alilipuliwa na kitu kilichorushwa kwake akikimbilia kujisalimisha kwa polisi akitoka kwa wafuasi wa Chadema, jambo ambalo lilikuwa sio kweli.

Hivyo alisema, Mkurugenzi  wa ulinzi na usalama wa Chama hicho kuhusishwa kwa sakata la sasa la mkanda wa video uliopo katika mtandao na Kibanda ni mwendelezo tu wa kukihujumu chama, unaoratibiwa na Usalama wa Taifa, huku ukitekelezwa na jeshi la polisi.

“CHADEMA kinafahamu kwa undani, kwamba uzushi huu wa Tape ya “Bukoba Boy”.Tunajua huu umeanzishwa na kuhusisha Usalama wa Taifa, akiwemo Ighondo na wenziwe pale Ada Estate. Huyu  Ighondo ambaye anafahamika pia kwa jina la “Rama” tunamfahamu vizuri sana," alisema.

Video iliyozua utata ni hii

Dk Slaa aliingiza suala la kufungiwa suala la kufungiwa kwa gazeti la MwanaHalisi akiituhumu serikali kutokua makini.

Akakumbushia kuwa waliwahi kutuma barua mbalimbali polisi zinazothibitisha kuwa wanafanyiwa michezo michafu huku zikiwa zimeandikwa majina ya viongozi wa CHADEMA, au taarifa za Vikao vya Chadema zilizopotoshwa lakini polisi hawakuchukua hatua.

Aliongeza kuwa wakati wa uchaguzi wa Igunga walisema kuwa kuna mtu anamiliki bastola isisvyo halali, wakataja hadi namba za bastola iliyoingizwa lakini polisi hawajawahi kushughulika nayo.

Hata hivyo alishangazwa na jeshi la polisi kufanya haraka kumshikilia Lwakatare, kwani vyombo vya habari hivi majuzi vimemtaja kwa majina ya watu kuhusishwa na utekwaji na uteswaji wa Kibanda, lakini jeshi halikusema lolote hadi sasa.

Akaongeza kuwapo watu aliowataja kwa majina kwamba waliingia kwa ID zao kwenye mitandao kukejeli suala la kuteswa Absalom Kibanda lakini jeshi halikuchukua hatua.

Alishangazwa jinsi polisi walivyofanya haraka kumkamata Lwakatare, akasema ni mbinu tu za kukichafua CHADEMA.

Hadi tunaenda Mitamboni, Jeshi la polisi lilikuwa halijatoa taarifa kuwa Mkurugenzi huyo wa Ulinzi na usalama wa Chadema angepata dhamana au la, lakini Wakili wake alilithibitishia gazeti hili kuwa wameenda tena kumpekua kwa mara nyingine nyumbani kwake.

Kutokana na hali hiyo, Dk Slaa alisisitiza kuwa “madai yaliyotolewa mara nyingi na CHADEMA, kwa Rais kuandikiwa barua na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, iundwe Judicial Commission of Inquiry (Tume Huru ya Kimahakama kuchunguza vifo vyote vyenye utata na sura ya kisiasa).

Akahoji ,Serikali inaogopa nini kuunda Tume hii huru ili ukweli Ujulikane? Iweje CHADEMA inayotuhumiwa Kupanga njama wanaishinikiza Serikali kuunda Chombo huru na Serikali ndiyo inayopata kigugumizi?”

Aliongeza kuwa “kwa wale walioumizwa na kujeruhiwa kama kina Ulimboka Kibanda na wengine, tunarudia Tamko letu la kuwa hatuna Imani na uchunguzi unaofanywa na Jeshi la Polisi kwa kuwa viongozi wa Jeshi hilo ni sehemu ya watu tunaowatuhumu kwa kuhusika kwa njia mbalimbali, na Ushihidi wa wazi na Taarifa mbili za Serikali kupingana yaani Taarifa ya Kamati yqa Nchimbi na Tume ya Haki za Binadamu.

"Tutaiaminije Polisi na Serikali kwa Taarifa ya Kamati ya Nchimbi? Hatuwezi kuendelea kuvumilia ukandamizaji huu wa uhuru wa habari, ambao sasa unaelekea kuota mizizi nchini kwetu. Na kweli ninawaomba na kuwataka waandishi wote msimame imara, bila kujadili itikadi, au tofauti zetu zozote zile na kusimamia uhuru wa Habari. Tunataka vivyo hivyo, kwa wanaharakati mbalimbali. Waache hofu, eti wanaogopa kuhusishwa na vyama vya Siasa! Haki ni haki na haina rangi ya bendera ya chama chochote," alisema.

Azungumzia Bunge:
Dk Slaa amesema kuwa usalama wa Taifa, unafanya kazi kwa maslahi ya Chama cha Mapinduzi hadi ndani ya bunge, ndio maana sasa wabunge wa Chama hicho wameondolewa katika kamati muhimu ambazo walikuwa wanazisimamia, bila wao kuulizwa, tofauti na walivyojaza katika fomu na nje ya ushauri wa Kiongozi wa upinzani bungeni.

Dk slaa alisema hiyo yote ni hujuma, Mnyika amepelekwa Ardhi maliasili na Mazingira, huku Msigwa akiondolewa maliasili na utalii kwa kuwa alikuwa anawataja viongozi wa CCM , jeshi la Polisi, jeshi la Wana nchina Ikulu yenyewe kuhusishwa na ujangili wa wanyama.

Amesikitishwa na wabunge wa Chama chake kuhamishwa kamati muhimu walizokuwa wanazisimamia, huku wengine wakiachwa kuingizwa katika kamati jambo ambalo linawanyima ufuatiliaji wa utendaji wa serikali, ilihali wabunge wengi wa CCM wengine wamewekwa kamati mbili kwa mbunge yule yule.

Continue Reading
26 Comments

26 Comments

 1. Tino

  14/03/2013 at 8:43 pm

  Mwenye uelewa ataelewa

 2. baba projestus

  14/03/2013 at 9:07 pm

  itajulikana tu hii ndio tanzania

 3. Lucas Evaristo

  14/03/2013 at 9:11 pm

  Hivi kwa mtindo huu,wanatutakia nini sisi watanzania?mpaka kufikia stage ya kuunda video za namna hii? Nchi ina mambo mengi yaloaidiwa na hayajatimizwa na mengine hata ndoto kua yatakuja timizwa zishafutika.wanakazana kuunda vitu visivyokua na maslahi wala maadili yeyote kwa wa Tz ili mradi kutupotosha na kutulisha imani mbovu ya kuendelea kuwaamini.aisee Mungu aisaidie nchi hii ili uongozi tawala uone aibu kwa mambo yao ya aibu namna hii.

  • maadili ethics

   18/03/2013 at 6:50 pm

   Haya ndiyo matokeo ya SIASA ZA UPINZANI, mkishakuwa wapinzani basi hakuna kujenga ila ni kubomoa kwa kwenda mbele. Wengi hatukutaka utitiri wa vyama kwa kujua fika kuwa vitaleta UPINZANI, mlio wachache ambao mlikuwa mmeshapumbazika na itikadi za wasiotutakia mema mkang'ang'ania, demokrasia ikatupwa, mkafurahia wachache kupewa ushindi bila kujua kuwa tunaingia korongoni. Brother Everisto utambue fika kuwa hili limefanyika na kwa vyovyote vile ndiyo ubaya wa UTITIRI WA VYAMA na ndiyo UOZO WA UPINZANI….. turudi nyuma, turudishe UMOJA WETU, ITIKADI YETU KISIASA IWE MOJA haya yote yatakwisha kwani wakati tuko hivyo haya hayakuwepo kwa kiwango hiki na tunaona kila siku yanazidi….CDM anaua ili shipa limuangukie CCM lakini anayeuliwa au kuumizwa ni MTANZANIA mwenzetu……TUACHE KUPINGANA, TUWE WAMOJA TUJENGE NCHI. VYAMA VINGI NI CHACHU YA UDINI, UKABILA, UKANDA NA KILA KINACHOWAGAWA WANANCHI.

 4. Hildephonce Henryco

  14/03/2013 at 10:10 pm

  Mungu itangulie Chadema na wana wa nchi hii usalama wa ccm sio usalama wa taifa unatumaliza.

 5. Aloyce

  14/03/2013 at 11:54 pm

  Hii style imevuka mipaka,na sio kitu cha kuonyesha watu wenye akili,yeyote anayejaribu kuweka mawazo potofu kwenye akili za watu,siku si nyingi ukweli utakua bayana.

 6. Deodatus

  15/03/2013 at 12:29 am

  Kila jambo lina mwanzo na mwisho wake,mwisho wa yote haya ukweli utatuweka huru penye ukweli uongo hujitenga.

   

 7. Steven Swai

  15/03/2013 at 6:51 am

  Watajaribu sana kukiua chama cha Wananchi ila nguvu ya Mungu itaonekana Juu ya Damu wanazomwaga za wasiokuwa na hatiya!

 8. Benjamin Nicodemas

  15/03/2013 at 7:46 am

  JamiiForum unatupa habari nzuri na zenye uhakika bila kificho kabisa!

 9. Benjamin Nicodemas

  15/03/2013 at 7:49 am

  hii yote ni mbinu ya CCM katika nyanza za kisiasa chafu tu, Chadema yatupasa tusirudi nyuma na tukomae kama kawaida CCM atadondoka tu!

  • SENTEUH SENTEUH

   20/03/2013 at 6:48 pm

   FORGET ABOUT IT!!!!! CCM NOMA ,,,,,,KUMBUKA HOTUBA YA BABA WA TAIFA,,,,MWALIMU NYERERE ,,,,,,BILA YA CCM MADHUBUTI TANZANIA PATAKUWA NA NOMA HASA WATU WENYE  NIA YA KUIHALIBU TANZANIA KAMA WEWE UNAYEONGOZWA KWA HISIA ,,,,,FIKIRI SANA ,,,,,,MBONA VIJANA MMTEKWA NA UCHADEMA SANA BILA KUFILI MUSTAKABALI WA TAIFA HILI??????

 10. Nteze John

  15/03/2013 at 9:22 am

  Hii ni komedi, kama za akina Masanja. mwenye akili ya kawaida hawezzi kuiamini. sanasana polisi wanatangazia umma kuwa bado wako katika ulimwengu wa analogia…

   

 11. fatuma dady

  15/03/2013 at 9:30 am

  Siku zote haki huzuiliwa kwa njia zote, lakini kuna cku watu watajua mbichi na mbivu. Peoples power

 12. shaban mputa

  15/03/2013 at 11:06 am

  Mwenye macho haambiwi ona………ila mungu muweza wa yote

 13. Rogers

  15/03/2013 at 11:49 am

  Harakati zinaendelea mpaka kieleweke!!

 14. syte

  15/03/2013 at 1:15 pm

  kama ipo ipo2, watanzania sisi ye2 macho na fainali 2015 ndo 2tachambua mchele na chuya.

 15. andrew rambau

  15/03/2013 at 1:50 pm

  hivi kweli hawa ccm wanataka kutuona cc watanzania ni mapoyoyo kiac gani? Mtu na akili zake timamu anapost video ya namna hii kwa madhumuni ya kurubuni fikra za watu. Haiwezekani cdm tutapigania hii nchi mpaka dk za mwisho haturudi nyuma kwa upuuzi tena ufedhuli kama huu…peoples power..

  • SENTEUH SENTEUH

   20/03/2013 at 6:38 pm

   shida hujielewi ila unaishi kwa hisia sana……..kama wewe mtanzania na mzalendo acha mambo ya CCM na CDM jadili juu ya haya yanayoendelea nchini,,,,,,!!!!! kwani LWAKATARE  yeye YESU hawezi!!!!!!! je angekuwa CHENGE  c ungefulahi

    

 16. Idsam mapande

  15/03/2013 at 4:53 pm

  Kama ndivyo tusubiri tamko la polisi.

 17. Edward Sambai

  15/03/2013 at 4:55 pm

  Mfa maji………………
  Ccm uongozi mmeshindwa na hii sanaa ya uigizaji nayo pia mmefely labda mtafute fani ingine

 18. flor

  17/03/2013 at 3:53 pm

  end of ccem

  • SENTEUH SENTEUH

   20/03/2013 at 6:33 pm

   utakufa wewe CCM utaiacha ,,,,,,shida unaota mchana

 19. MASHAKA SHAABAN

  19/03/2013 at 4:21 pm

  Da kweli serikali yetu haina aibu

 20. Benard

  27/03/2013 at 9:01 am

  Labda mimi sioni vizuri. Hiyo sura si ya Lwakatare kweli? mbona sauti inamatch na midomo? Au Lwakatare aliirekodi makusudi??

  Ni vizuri sana kuisingizia dola. Lakini tulezwe basi na uongo kwenye Tape hiyo uko wapi?? Mwenye macho haambiwi tazama. kila kitu kikowazi hapo.

 21. kwadelo

  31/03/2013 at 8:35 pm

  Mungu uilinde Tanzania tuzidi kuwa na Amani, umoja na mshikamano.

 22. abihudi james

  23/04/2013 at 3:55 pm

  DA KWELI NYANI AKITA KUFA MITI YOTE INATELEZA.
  HAWA JAMAA WAMEKWISHA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Featured

UJASUSI: Jinsi kijana wa kiume kutoka New Zealand alivyojaribu  kumuua Malikia Elizabeth II

Published

on

Shirika la Ujasusi la New Zealand  (SIS) limethibitisha kwa mara ya kwanza kwamba kulikuwa na jaribio la kumuua Malikia Elizabeth II wakati alipotembelea jiji la Kusini la Dunedin mwaka 1981.

Jaribio hilo la kumuua Malikia linalodaiwa kutekelezwa na kijana wa kiume limechochea hamasa ya polisi kutaka kujua ni kwa kiasi gani wanausalama hao walifanikiwa kuzima njama hizo.

Taarifa iliyotolewa na SIS  zinaonesha kuwa kijana huyo, Christopher Lewis (17) alipiga risasi kuelekea kwa Malikia wakati akishuka kwenye gari lake ambapo alikuwa anaenda kushuhudia Maonyesho ya Sayansi yaliyofanyika Oktoba 14, 1981 katika jiji hilo. Tukio hilo lilitokea akiwa katika ziara ya siku 8 kutembelea nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.

“Lewis alidhamiria kumuua Malikia, hata hivyo hakuwa katika nafasi nzuri ya kurusha risasi, hata silaha iliyotumia haikuwa katika umbali wa kuweza kumfikia mhusika,” imesema taarifa iliyotumwa SIS kwa vyombo vya habari.

Lewis ambaye anatajwa kwenye taarifa ya ujasusi kama ‘kijana msumbufu’ hakuhukumiwa kwa jaribio la kutaka kuua au kosa la uhaini. Tukio hilo lilifanywa kuwa siri ili kuzuia sifa mbaya kwa nchi (New Zealand) ambayo ilitembelewa na mgeni wa heshima. Badala yake Lewis alihukumiwa kwa kumiliki silaha kinyume na sheria na kufyatua risasi.

                       Malikia Elizabeth II akiwa ameambatana na walinzi wake alipotembelea New Zealand

Inaelezwa kuwa watu waliohudhuria tukio la kuwasili kwa Malikia walisikia mlio wa risasi lakini Polisi waliokuwa wanasimamia usalama katika eneo hilo la Dunedin waliwaambia kuwa ilikuwa ni sauti ya kuanguka kwa kitu au magari kugongana.

“Uchunguzi wa sasa wa polisi juu milio iliyosikika umefanywa kwa umakini na wawakilishi wa vyombo vya habari wamepata mrejesho kuwa kelele zilisababishwa na baruti”, inaeleza ripoti kutoka SIS iliyotolewa mwaka 1981 baada ya kutokea tukio hilo.

Kulingana taarifa za ujasusi zinaeleza kuwa polisi wamekuwa wakifuatilia nyendo za Lewis tangu 1986 ambapo Malikia alitembelea tena New Zealand wakiogopa kuwa anaweza kutekeleza tena uhalifu huo. Kuwekwa wazi kwa siri hiyo kumewaibua polisi ambao wameanza kuchunguza upya kesi hiyo.

Zaidi ya muongo mmoja uliopita, Lewis alihukumiwa kwa mauaji ya mwanamke mmoja katika mji wa Auckland na kumteka mtoto wa kike ambapo baadaye alimtupa karibu na kanisa.

Kulingana na taarifa mbalimbali za wakati huo zinaeleza kuwa Lewis alijidhuru kwa umeme akiwa gerezani mnamo 1997 akisubiri hukumu ya kuua. Lakini alikana mashtaka ya kuua kwa ujumbe mfupi wa kifo (suicide note).

New Zealand ilipata uhuru mwaka 1947 kutoka kwa Uingereza lakini inamuheshimu Malikia kama kiongozi wa taifa. Ameitembelea nchi hiyo kama Malikia mara 10 na mara ya mwisho ilikuwa 2002.

Continue Reading

Featured

FREEDOM HOUSE: Tanzania ina uhuru kiasi, kufungiwa vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya kisiasa kuididimiza kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa

Published

on

Ripoti mpya iliyotolewa na taasisi huru ya Freedom House imesema misingi ya demokrasia ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kukusanyika imeendelea kudhoofika nchini Tanzania na hali hiyo isiporekebishwa itaingia kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa duniani.

Kulingana na  Freedom House  ambao walichambua data katika nchi 195 za ulimwenguni katika mwaka 2017 wamebaini kuwa nchi 88 zina uhuru,  58 zimejumuishwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku 48 zikiwekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa misingi ya demokrasia ikiwemo uchaguzi usio huru na haki, uhuru wa kujieleza umeendelea kushuka kwa mwaka wa 12 mfufululizo duniani kote. Miongoni mwa matokeo yaliyostaajabisha ni kudhoofika kwa  Marekani ambayo ni mama wa demokrasia kutokana na uchunguzi unaofanywa na Mwendesha Mashtaka Maalumu kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 ambao ulimpa ushindi Rais Donald Trump.

Tanzania imewekwa kwenye nchi 88 ambazo zina uhuru kiasi lakini inatahadharishwa kuwa inaweza kuingia kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa. Tahadhari hiyo inatokana na mwenendo wa viongozi wa serikali kufungia vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kushtakiwa kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa tuhuma za uchochezi na kukamatwa kwa wapinzani wa kisiasa ambao wanakosoa na kutoa mawazo yanayotofautiana na serikali.

Pia utekelezaji wa Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 na Sheria ya Makosa ya Mtandao  ya mwaka 2015 umekuwa ukilalamikiwa na wadau wa maendeleo kuwa ni mkakati wa kudhoofisha uhuru wa kutoa maoni, uwazi na uwajibikaji.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini hivi karibuni kilitoa tamko la tathmini ya uchaguzi mdogo wa marudio wa kuchagua madiwani uliofanyika katika kata 43 kwenye mikoa 19 ya Tanzania  Novemba 24 mwaka jana ambapo kilibaini mambo mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Tathmini hiyo iliibua mambo mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya nguvu ya vyombo vya dola, matukio ya watu kutekwa na watu wasiojulikana, watu kupigwa, kujeruhiwa  kwa lengo la kuharibu na kuvuruga uchaguzi  na vilevile kuwatia hofu wapiga kura.

 

Afrika Mashariki hali bado tete

Tanzania inaungana nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya na Uganda ambazo nazo zimewekwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku za Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini zimejumuishwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa.

Awali Uganda ilikuwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa lakini imepanda hadi kwenye uhuru kiasi kwasababu ya  kuimarika kwa tasnia ya habari na utashi wa wanahabari, blogu na  uhuru wa wananchi kutoa maoni yao licha ya mazingira ya kisiasa kuminywa na utawala wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni.

Rais Museveni mwenye umri wa miaka 73 amekuwepo madarakani  tangu 1986 amefanikiwa kubadilisha sheria  ya ukomo wa umri wa miaka 75 wa kugombea urais ambapo atapata fursa ya kugombea tena mwaka 2021. Chaguzi nchini Uganda zimekuwa zikitawaliwa na vurugu za polisi na wananchi, kuzimwa kwa intaneti na kuwekwa kizuizini kwa viongozi wa upinzani ikiwemo Kizza Besigye wa chama cha Forum for Democratic Change.

Kwa upande wa Kenya ambayo imekuwa ikisifika kwa kuimarisha misingi ya demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo kwa mara ya kwanza mahakama ilifanikiwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Urais yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta uliofanyika Agosti 2018. Uchaguzi ulirudiwa na Rais Kenyatta alichaguliwa tena.

Marudio ya uchaguzi yalilamikiwa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa hayakuzingatia haki za binadamu ambapo watu ambao walipinga uchaguzi huo walikumbana na mkono wa dola. Matendo hayo ndiyo yaliiweka Kenya kwenye kundi la nchi zilizo na uhuru kiasi.

Burundi na Sudan Kusini zimewekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa kutokana na mapigano ya kikabila ambayo yamedhoofisha mfumo wa kisiasa wa kuongoza nchi. Vyombo vya habari na wananchi wanaotoa maoni tofauti na serikali wamekuwa wakiteswa, kufungwa na kuuwawa.

Chanzo: Freedom House           – Nchi zisizo na  uhuru  – Nchi zenye uhuru     – nchi zenye uhuru kiasi   

 

Hali ilivyo Afrika

Afrika kama zilivyo nchi za Afrika Mashariki hali ya demokrasia siyo ya kuridhisha ikizingatiwa kuwa asilimia 11 ya wakazi wapatao bilioni 1.02 wa bara hilo ndio wana uhuru wa kweli, huku 52% wana uhuru kiasi na 37% hawa uhuru kabisa.

Ripoti ya Freedom House inaeleza kuwa waliangazia nchi 49 za Afrika na kugundua kuwa nchi 8 (18%) ndio zina uhuru wa kweli, nchi 22 (43%) zina uhuru kiasi na 19 (39%) hazina uhuru kabisa. Nchi zinazotajwa kuwa na uhuru ni Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Ghana, Togo, Senegal na Kisiwa cha Sao Tome.

 Sababu ya nchi nyingi za Afrika kuwepo kwenye kundi la zisizo na uhuru ni matokeo ya viongozi kukaa madarakani muda mrefu, vurugu za kisiasa na kikabila ambazo zimekuwa zikihatarisha haki za binadamu.

 

Demokrasia ya Dunia

Demokrasia ya dunia inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kisiasa kuliko wakati mwingine ambapo mwaka 2017 ulishuhudia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo kuminywa kwa  uchaguzi huru na kweli, haki za watu wachache, uhuru wa kujieleza, utawala wa sheria.

Nchi 71 kati ya 195 zimeshuhudiwa zikiteteleka katika kulinda haki za kisiasa na jamii ambapo ni nchi 35 tu ndizo zimeweza kulinda haki hizo. Kudhoofika kwa demokrasia kunaendelea kushuka kwa miaka 12 mfululizo na hatua muhimu zisipochukuliwa amani ya dunia itawekwa rehani.

Marekani ambayo ni bingwa wa demokrasia duniani nayo imeripotiwa na taasisi ya Freedom House kudhoofika katika kulinda haki za kisiasa na kijamii na kuzua mgongano wa mawazo miongoni mwa nchi zinazoibukia katika kujenga demokrasia ya dunia.

Tangu kuisha kwa vita baridi, nchi nyingi ziliachana na utawala wa kiimla na kugeukia demokrasia ya vyama vingi lakini hali hiyo imeanza kujitokeza tena ambapo idadi ya viongozi wanaoongoza kwa udikteta inaongezeka.

 

Uhuru wa nchi moja unategemea uhuru wa nchi zote

Demokrasia itabaki kuwa tunu muhimu kwa jamii zilizostaarabika, ikifungua milango ya uwazi, mawazo na fursa mpya na zaidi ya yote kulinda uhuru wa mtu mmoja mmoja. Ikiwa watu duniani kote wanadai mazingira mazuri ya kisiasa ni dhahiri wanakumbatia misingi ya demokrasia: uchaguzi huru, uhuru wa kujieleza, uwazi na uwajibikaji wa serikali, utawala wa sheria ambao hauingiliwi na polisi, jeshi au taasisi nyingine za nchi.

Hata hivyo, Karne ya 21 imeshuhudia ugumu wa kuifanya demokrasia kuwa endelevu ambapo baadhi ya nchi zinatekeleza lakini zingine zinapuuza. Utawala wa kidekteta wa Urusi na China unatambua wazi ili uendelee kuwepo unahitaji kuimarisha demokrasia katika nchi nyingine ili ziendelee kufaidika na mahusiano ya kidiplomasia. Ukuaji wa  demokrasia ni kulinda haki za watu wote duniani kupitia utandawazi   

Continue Reading

Afya

Is Tanzania’s Adolescent Fertility Rate Three Times Higher Than Global Counterparts?

Published

on

The Comprehensive Community-Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT), an organization ​which works to provide affordable medical and rehabilitative services for mothers and newborns throughout Dar-es-Salaam, marked World Contraception Day on September 26 with a call for more efforts to meet the reproductive health needs of teens between 15 and 19 years old.

The report highlights a worrying statistic — Tanzania’s adolescents are having almost three times as many children on average as their global counterparts, with 135 births per 1000 girls reported in the country, compared to an average of 44 per 1000 girls aged 15–19 worldwide in 2015.

CCRBT attributes the high adolescent fertility rate to a lack of access to contraceptive services, with Technical Advisor for Nursing Bola Abbas saying, that only about 8 per cent of current family planning clients are between the ages of 15 to 19.

On a national scale, Abbas explains, demand for family planning among adolescent girls is still very low, with only one out of every three of those who are sexually active within the 15 to 19 age group using modern contraceptive methods.

So the question is, how does Tanzania’s adolescent fertility rate compare to that of the rest of the world?

Pesacheck investigated the claim that Tanzanian adolescents are having three times as many children as their peers in the rest of the world and found that the statement is TRUE for the following reasons:

Tanzania’s adolescent fertility numbers are rather high, with 4.4% of girls aged 15 having given birth according to the country’s Demographic and Health Survey.

The Sustainable Development Goals call for countries to ensure universal access to sexual and reproductive healthcare services, including family planning, information and education, and the integration of reproductive health into national strategies and programmes by 2030.

The indicators for this goal are the proportion of women of reproductive age (15–49 years) who have their need for family planning satisfied with modern methods, and the adolescent birth rate (10–14 years and 15–19 years) per 1,000 women in that age group.

For several sub-Saharan countries, Tanzania included, access to modern family planning methods is low for this particular age group, and as a result, the regional average is 105 births per 1,000, which is more than double the global average.

Tanzania’s National Bureau of Statistics produced a national fertility and nuptiality report based on data from the 2012 national census, which shows that Adolescent Fertility Rate (AFR) was 81 births per 1,000 women aged 15–19.

The report further shows that in 2012, 23.3% of adolescent girls in the country had given birth to at least one child. Additionally, 42.2% of girls who had never attended school had given birth, compared to just 9% of those who had reached university.

This shows that there is a need for contraceptive access for teenage girls in Tanzania, especially for girls in rural areas and those with limited access to education.

The Tanzania Demographic and Health Survey 2015–16 indicates that 27% of girls aged 15–19 have given birth. Crude birth rates for girls aged 15–19 show that there 135 births per 1,000 girls in Mainland Tanzania and 132 per 1,000 girls in Zanzibar, way above the global average of 44. The data also shows that contraceptive access for this age group is also quite low, with 10.4% of girls aged 15–49 using any form of contraception.

It would therefore appear that the lack of access to contraceptives is contributing to the increased likelihood of adolescent girls getting pregnant.

So the claim by CCBRT that Tanzania’s adolescent fertility rate is almost three times the global average is TRUE. This is driven largely by a lack of access to contraceptives for young people in the 15–19 age group, and the relatively high levels of poverty that have driven many out of school and into early marriage.

As a result, the country is unlikely to meet the Sustainable Development Goal of overall good health and wellbeing of mothers unless it puts measures in place to ensure universal access to sexual and reproductive health-care services for girls and women of all ages.

Do you want us to fact-check something a politician or other public figure has said about public finances? Complete this form, or reach out to us on any of the contacts below, and we’ll help ensure you’re not getting bamboozled.

This report was written by PesaCheck Fellow Belinda Japhet, a Communications Consultant, Online Editor based in Tanzania. The infographics are by PesaCheck Fellow Brian Wachanga, who is a Kenyan civic technologist interested in data visualisation. This report was edited by PesaCheck Managing Editor Eric Mugendi.

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com