Connect with us

Featured

Godbless Lema ‘aichana’ Idara ya Usalama wa Taifa

Published

on

MBUNGE wa Jimbo la Arusha Godbless Lema CHADEMA) ameionya na kuitaka Idara ya Usalama wa Taifa nchini kujifunza kutoka kwa Kiongozi wa Libya Muammar Gadaffi.

Mbali na kuinyoshea vidole Idara hiyo Lema pia amewataka Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha na Kamanda wa Polisi mkoani hapa kutambua kuwa kazi yao si kukitetea Chama cha Mapinduzi (CCM) bali ni kutetea maslahi ya taifa.

“Kama Idara ya Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi wanafikiri wao wana nguvu sana wanapaswa kujua kwamba wanajidanganya. Kama wanataka kujua nguvu zao zina uwezo kiasi gani, wasafiri kwenda kuiuliza Idara ya Kijasusi ya Libya kama ilimsaidia Gadaffi asipinduliwe kwenye nchi aliyoingoza kwa miaka zaidi ya 40,” alidai Lema.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana mjini Arusha Lema alidai taarifa za Kiintelijensia walizonazo zimedhibitishia pasipo shaka kuwa Idara ya Usalama wa Taifa mkoani Arusha inatumika kwenye mgogoro wa Meya.

godbless lema

Godbless Lema akiongea na waandishi

Alidai kuwa mtu anayetuhumiwa kuongoza mpango huo mchafu unaolenga kuwaangamiza viongozi wa kisiasa wa CHADEMA ni Msaidizi wa Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa wa Arusha.

“Vitisho ni vingi hatutaogopa nipo tayari kwa jambo lolote lile sitaacha harakati nipo tayari kufa hata sasa. Taarifa na ushahidi tunao kwamba kila kinachoendelea sasa kwenye siasa kinaratibiwa na Idara hii. Katika kutafuta ufumbuzi wa nchi kuna watu ambao watatolewa sadaka na sisi tupo tayari kutolewa sadaka,” alidai Lema na kuongeza:

“Kuanzia Jumatatu tutaendesha ‘movement’ ambayo hawajawahi kuiona na wakiendelea hivi pengine ukombozi wa nchi unaweza kuanzia Arusha,” alidai.

Katika hatua hiyo Lema aliyataja majina ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA ambao wapo kwenye mkakati wa kuhujumiwa wakati wowote na vyombo vya usalama kuwa Ephata Nanyaro ambaye tayari amehojiwa, Joseph Kredo Katibu.

Wengine ni Emanuel Kombe ambaye naye amehojiwa, Hilary Mkonya Mhazina wa Chama, Odelo Odelo Mwenyekiti wa BAVICHA, Kamnde tayari amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kukutwa na silaha aina ya SMG na Bastola,Glory Shio Mwenyekiti wa BAWACHA, Happy Charles, Sarungi, na wengine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Arusha Ephata Nanyaro kwa upande wake aklibainisha kuwa tayari ameandika maelezo polisi akikanusha kuhusika na kikao cha kupanga njama za kumuua Meya wa Jiji la Arusha Gaudence Lyimo.

“Nimehojiwa kwa zaidi ya Saa 7 tena ni Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha (RCO) akiwa na maofisa kutoka Dar es Salaam makao makuu ya Polisi.

“Katika maelezo yangu bado nilikana sina ugomvi na Gaudence, sijahusika na madai ya kupanga kumuua niliwaambia sintamtambua kamwe kwa nafasi  aliyonayo,” alisema Nanyaro na kuongeza:

“Tunaushahidi katika kuhojiwa kwangu kwamba Usalama wa Taifa, Jeshi la Polisi wanahusika kwani wameonyesha uwazi wa kuwatisha viongozi wa CHADEMA.

“Martine Luther King mwanaharakati wa Kimarekani aliwahi kusema; “Kama hakuna jambo lolote binadamu yupo tayari kufa kwalo huyo binadamu hastahili kuishi”. CHADEMA tuna amini uchaguzi wa Meya Arusha ulikuwa ni batili hilo tutaendelea kuliamini mpaka mwisho,” alidai Nanyaro.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Maendeleo Arusha (ArDF) Elifuraha Mtoe kwa upande wake alithibitisha kupokea taarifa za kutafutwa na vyombo vya usalama.

“Nimepata habari na ujumbe kwamba ninatafutwa hivi chombo cha usalama kinapokuhitaji kama kina lazimika kumtumia Mwenyekiti wa wilaya CHADEMA. Kama kuna tuhuma zinazonihusu ambazo Usalama wa Taifa wanazo au jeshi la polisi nawaruhusu wanitafute waniulize hii nchi inaendeshwa kwa mujibu wa sheria,” alisema Elifuraha.

Mwenyekiti huyo wa ArDF aliendelea kubainisha kuwa kinachoonekana kwa sasa mkoani Arusha na nchini kwa ujumla ni Idara ya Usalam wa Taifa badala ya kuangalia usalama wan chi inaasimamia matakwa ya chama cha siasa.

“Kuna Kada wa CCM aliwahi kuniambia kuna mambo mabaya yanandaliwa dhidi yangu hivyo aliomba anikutanishe na Msaidizi wa Mkuu wa Usalama wa Taifa Mkoa (Mombo) tukae tuzungumze tuyamalize. Kinachoonekana hivi sasa kuna wanasiasa wana nguvu kuliko Dola na Dola hiyo hiyo inajaribu kupambana nao ili kumaliza nguvu za wanasiasa. Sasa inapopambana kutafuta nguvu ya kupambana na wanasiasa hao inaanza kutafuta watu waliopo karibu na wanasiasa,” alidai Elifuraha.

Continue Reading
19 Comments

19 Comments

 1. Bajabiri

  01/09/2011 at 6:16 pm

  Hawa wehu kweli, kama wanafanya ujinga huu basi kuna masuala meeengi sana.

  Jaman hebu tuacheni uzandiki, USALAMA WA TAIFA KWANI NDIO KAZI MLIYOJIFUNZIA NDIO HII? AAAARGH,

 2. Waheed Suday

  01/09/2011 at 9:34 pm

  Mi nawashangaa sana kwa kuendelea kuwaita usalama wa taifa ili hali hao ni usalama wa ccm aka magamba

  • julieth

   22/03/2012 at 4:35 am

   achene ku suport ujinga hivi ni lini tuta pigana na maradhi, umaskini, na ujinga kama kila siku ni sisi wenyewe kwa wenyewe kama tumempa ubunge bac afanye kaziyake na tuone maendeleo ya kiuchumi siasa na jamii na si maandeleo ya machafuko vifo vya maskini na migomo isiyo na msingi….hivi inamaana sisi chadema kila mtu kwetu ni mbaya sasa tutaleta maendeleo kwa nani kama kila anaye fanyakaz serekalini ni mbaya siasa ni sera so vita matusi migomo na ushawishi kwa wasojua wanachoifanya

 3. john michael

  02/09/2011 at 11:27 pm

  hakuna mwenye nguvu zaidi ya mungu..ccm waendelee na mchezo wao wa kutumia vyombo vya dola wataona mwisho wake.na hao usalama wa taifa wataweka wapi sura zao siku upinzani wakichukua madaraka?

 4. Maxon

  05/09/2011 at 8:51 pm

  We lema acha unafiki mbona unaamua kuyasema hayo baada ya kutuhumiwa kuhusika na mtandao wa wizi wa magari? Tushawashtukia nyote wanafiki tu.Waacheni usalama wa taifa wafanye kazi zao

  • julieth

   22/03/2012 at 4:39 am

   tena pia mimi ni chadema lakini viongozi wa chadema wasi sahau kuwa pia mabaya wanao yafanya yanaonekana live na tulio wachagua kwaiyo usalama wafanye kazi yao tena kwabidii ili tutambue maovuyenu ambayo mnayasiriba na siasa chafu na migomo isiyo na msingi

 5. Maxon

  05/09/2011 at 8:58 pm

  Ninyi chadema wachoyo wa madaraka wakati mkishapewa mwaanza kugombana wenyewe.Mfano mzuri ni ugonvi kati ya madiwani wenu wa mwanza dhidi ya meya wa jiji la mwanza ambaye hata hivyo ni mwana chadema.Acheni kucheza na akili za watanzania,hiyo saikologia mbaya itawaponza hapo baadae

 6. A M

  08/09/2011 at 4:39 pm

  Unaonekana ni mmoja wa magamba ambayo tunahitaji kuyavua kwa nguvu , Mwisho wenu umefika we Uishie kutegemea dola ukinyanyasa wananchi subirini muone kama una akili kimbia.

 7. Castro Pius

  09/09/2011 at 3:21 pm

  Greetings,

  hehehehhehe hii habari kidogo inasikitisha na hii ni dhahiri kuwa serikali na CCM inatumia dola kisiasa zaidi kuliko kiutendaji. Inakuwaje jeshi/ usalama wa Taifa kuhusika na ugomvi wa siasa?

  Mm nafikiri tatizo ni ufahamu mdogo na mfumo duni wa majeshi yetu kama vile polisi JW, n.k kwani wao wnenyewe hawajui kuwa tunachokipigania ni kwa ajili ya matokeo mazuri kwa watu wote? au wanadhani CCM ikianguka basi nao wameanguka? wao ni watumishi wa serikali kupitia majeshi yao hivyo serikali ya chama chochote itawatambua tu.

  Wanaharakati tuna kazi kubwa kuifungua jamii yetu toka kwenye wimbi kuu la umasikini na ujinga uliokithiri. Hii itawezekana tu pale ambapo tutatwaa serikali na uongozi wa nchi yetu kwa watu wanaofahamu ni nini haswa maana ya utumishi wa umma.

  Best Regards,

 8. selis

  13/09/2011 at 9:20 am

  ndugu zangu naomba tujielekeze ktk kuangalia mistakabali wa taifa letu na matatizo makubwa yanayoikumba taifa letu.Hivi mtu mwenye utimamu akili aliopewa na mwenyezi Mungu anaweza kweli kupoteza mda wake ktk kuwinda maisha ya wenzake?mie naomba tusitumike ktk hii mikakati ya hovyo kupita zote,tuyungumzie maswala na si kuzungumzia watu.maana inatakakuonekana hivi sasa kuwa anapoonekana mtu anaibua maswala ya kuisaidia jamii kwa kueleza maovu yanayofanywa na baadhi ya viongozi basi anaanza kusongwasongwa.

 9. mmm

  13/09/2011 at 2:10 pm

  tangu nikue hapa bongo sijawahi kuona mwanasiasa yeyote bongo ameibuka tu ivivi mm nanona wote hao ni watumishi wa uma ila ndo ivyo

 10. elisha

  13/09/2011 at 7:42 pm

  The freedom is coming tomorrow

 11. BERNARD KOMBA

  19/09/2011 at 7:52 pm

  Mnaidhalilisha idara kutokana na utaratibu mkongwe mliojijengea wa kurithishana kazi hiyo, matokeo yake kufanya kazi kwa mazoea marehemu baba yake nilifanya naye kazi sehemu fulani, matokeo yake mnakosa mawazo mapya ua mnapitwa na wakati kwa kuifanya idara ka MAFIA MOB.

 12. Baba Collins

  21/09/2011 at 4:40 pm

  Ukombozi wa Mtanzania dhidi ya wizi,dhuluma na unyanyasaji unaofanywa na Magamba uko njiani. CCM inatumia nguvu zaidi kuliko ukweli ktk kujibu tuhuma walizonazo;wamechoka ndiyo maan hata baba yao hapendi tena kukaa hapa nchini. Your day is coming!!! PEOPLES POWER!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 13. chinga

  12/01/2012 at 12:29 am

  duh! hi sasa kali ccm kaa chonjo!

 14. julieth

  22/03/2012 at 4:29 am

  dah kama chadema mmeanza vita adi na usalama wataifa kazi kwenu kwani ivi siasa bila kutukana chamakingine kuleta fujo migomo na uchochezi unao pandikizwa kwa watanzania wa hali ya chini tena wasojua hata sheria na katiba nini hivi haiwezekani na nilini tutapata muda wa kufanya maendeleo kama malumbano hayaishi inasikitisha kuona kwamba mbunge wananchi wa arusha walomchagua kuwakilisha maslahi yao ndani ya bunge la jamuhuri eti anatoka nje ya bunge akigoma sasa matatizo yetu yatatatulikaje nje yabunge? sini wewe ulie waambia maaskari kuwa hajui chochote zaidi ya kirungu….alaf haohao ndo wakulinde na dharau zako naskitika kuwa watanzania wa chini ambao wana elimu duni ndo itawapashida kutambua siasa ya kweli na kubaki kuyumbishwa kwenye machafuko yanao sababisha vifo vya watanzania uku viongozi hao wakitoa salam zarambirambi na kuendelea na maisha yao uku wakisisitiza eti marehem kafa kishujaa kumbe ni siasa potofu isiyo na chembe ya usomi ndaniyake

 15. GANDISM

  13/04/2012 at 2:18 pm

  ccm waache watu watfute maendeleo na si vitisho visivyokuwa na maana kwa waleta maendeleo. Nani asiyejua umuhimu wa CHADEMA? Tunajua siri iliyopo ni kuwalinda vigogo na watoto wao waendelee kutunyonya bila kupingwa.

 16. GANDISM

  13/04/2012 at 2:27 pm

  Kama CCM haikujua hasira za wanyonge isubiri uchaguzi mdogo wa ARUSHA, wanafikiri Tanzania ya leo ni ile ya akina Mangungo? watu wanataka kusoma, matibabu, barabara na si braabraa tupuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu. Hata hivyo MUNGU hakuwapa chapa kututawala kwa nguvu.

 17. Jobalo josiah

  16/03/2013 at 11:34 am

  Kati ya wabunge ambao hawajui wajibu wake ni Lema. Anaacha kutekeleza wajibu wa kuwaletea wananchi wa jimbo lake maendeleo yy anahamasisha vurugu na maandamano. Kwani watu kuhojiwa na polisi ni ajabu au ni sehemu ya wajibu wao. Pia wakati wa kampeni yako mbona hukutuambia kwamba bila meya hatutatawala hili jimbo. Unatuchosha best na siasa za vijiweni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Featured

UJASUSI: Jinsi kijana wa kiume kutoka New Zealand alivyojaribu  kumuua Malikia Elizabeth II

Published

on

Shirika la Ujasusi la New Zealand  (SIS) limethibitisha kwa mara ya kwanza kwamba kulikuwa na jaribio la kumuua Malikia Elizabeth II wakati alipotembelea jiji la Kusini la Dunedin mwaka 1981.

Jaribio hilo la kumuua Malikia linalodaiwa kutekelezwa na kijana wa kiume limechochea hamasa ya polisi kutaka kujua ni kwa kiasi gani wanausalama hao walifanikiwa kuzima njama hizo.

Taarifa iliyotolewa na SIS  zinaonesha kuwa kijana huyo, Christopher Lewis (17) alipiga risasi kuelekea kwa Malikia wakati akishuka kwenye gari lake ambapo alikuwa anaenda kushuhudia Maonyesho ya Sayansi yaliyofanyika Oktoba 14, 1981 katika jiji hilo. Tukio hilo lilitokea akiwa katika ziara ya siku 8 kutembelea nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.

“Lewis alidhamiria kumuua Malikia, hata hivyo hakuwa katika nafasi nzuri ya kurusha risasi, hata silaha iliyotumia haikuwa katika umbali wa kuweza kumfikia mhusika,” imesema taarifa iliyotumwa SIS kwa vyombo vya habari.

Lewis ambaye anatajwa kwenye taarifa ya ujasusi kama ‘kijana msumbufu’ hakuhukumiwa kwa jaribio la kutaka kuua au kosa la uhaini. Tukio hilo lilifanywa kuwa siri ili kuzuia sifa mbaya kwa nchi (New Zealand) ambayo ilitembelewa na mgeni wa heshima. Badala yake Lewis alihukumiwa kwa kumiliki silaha kinyume na sheria na kufyatua risasi.

                       Malikia Elizabeth II akiwa ameambatana na walinzi wake alipotembelea New Zealand

Inaelezwa kuwa watu waliohudhuria tukio la kuwasili kwa Malikia walisikia mlio wa risasi lakini Polisi waliokuwa wanasimamia usalama katika eneo hilo la Dunedin waliwaambia kuwa ilikuwa ni sauti ya kuanguka kwa kitu au magari kugongana.

“Uchunguzi wa sasa wa polisi juu milio iliyosikika umefanywa kwa umakini na wawakilishi wa vyombo vya habari wamepata mrejesho kuwa kelele zilisababishwa na baruti”, inaeleza ripoti kutoka SIS iliyotolewa mwaka 1981 baada ya kutokea tukio hilo.

Kulingana taarifa za ujasusi zinaeleza kuwa polisi wamekuwa wakifuatilia nyendo za Lewis tangu 1986 ambapo Malikia alitembelea tena New Zealand wakiogopa kuwa anaweza kutekeleza tena uhalifu huo. Kuwekwa wazi kwa siri hiyo kumewaibua polisi ambao wameanza kuchunguza upya kesi hiyo.

Zaidi ya muongo mmoja uliopita, Lewis alihukumiwa kwa mauaji ya mwanamke mmoja katika mji wa Auckland na kumteka mtoto wa kike ambapo baadaye alimtupa karibu na kanisa.

Kulingana na taarifa mbalimbali za wakati huo zinaeleza kuwa Lewis alijidhuru kwa umeme akiwa gerezani mnamo 1997 akisubiri hukumu ya kuua. Lakini alikana mashtaka ya kuua kwa ujumbe mfupi wa kifo (suicide note).

New Zealand ilipata uhuru mwaka 1947 kutoka kwa Uingereza lakini inamuheshimu Malikia kama kiongozi wa taifa. Ameitembelea nchi hiyo kama Malikia mara 10 na mara ya mwisho ilikuwa 2002.

Continue Reading

Featured

FREEDOM HOUSE: Tanzania ina uhuru kiasi, kufungiwa vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya kisiasa kuididimiza kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa

Published

on

Ripoti mpya iliyotolewa na taasisi huru ya Freedom House imesema misingi ya demokrasia ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kukusanyika imeendelea kudhoofika nchini Tanzania na hali hiyo isiporekebishwa itaingia kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa duniani.

Kulingana na  Freedom House  ambao walichambua data katika nchi 195 za ulimwenguni katika mwaka 2017 wamebaini kuwa nchi 88 zina uhuru,  58 zimejumuishwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku 48 zikiwekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa misingi ya demokrasia ikiwemo uchaguzi usio huru na haki, uhuru wa kujieleza umeendelea kushuka kwa mwaka wa 12 mfufululizo duniani kote. Miongoni mwa matokeo yaliyostaajabisha ni kudhoofika kwa  Marekani ambayo ni mama wa demokrasia kutokana na uchunguzi unaofanywa na Mwendesha Mashtaka Maalumu kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 ambao ulimpa ushindi Rais Donald Trump.

Tanzania imewekwa kwenye nchi 88 ambazo zina uhuru kiasi lakini inatahadharishwa kuwa inaweza kuingia kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa. Tahadhari hiyo inatokana na mwenendo wa viongozi wa serikali kufungia vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kushtakiwa kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa tuhuma za uchochezi na kukamatwa kwa wapinzani wa kisiasa ambao wanakosoa na kutoa mawazo yanayotofautiana na serikali.

Pia utekelezaji wa Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 na Sheria ya Makosa ya Mtandao  ya mwaka 2015 umekuwa ukilalamikiwa na wadau wa maendeleo kuwa ni mkakati wa kudhoofisha uhuru wa kutoa maoni, uwazi na uwajibikaji.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini hivi karibuni kilitoa tamko la tathmini ya uchaguzi mdogo wa marudio wa kuchagua madiwani uliofanyika katika kata 43 kwenye mikoa 19 ya Tanzania  Novemba 24 mwaka jana ambapo kilibaini mambo mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Tathmini hiyo iliibua mambo mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya nguvu ya vyombo vya dola, matukio ya watu kutekwa na watu wasiojulikana, watu kupigwa, kujeruhiwa  kwa lengo la kuharibu na kuvuruga uchaguzi  na vilevile kuwatia hofu wapiga kura.

 

Afrika Mashariki hali bado tete

Tanzania inaungana nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya na Uganda ambazo nazo zimewekwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku za Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini zimejumuishwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa.

Awali Uganda ilikuwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa lakini imepanda hadi kwenye uhuru kiasi kwasababu ya  kuimarika kwa tasnia ya habari na utashi wa wanahabari, blogu na  uhuru wa wananchi kutoa maoni yao licha ya mazingira ya kisiasa kuminywa na utawala wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni.

Rais Museveni mwenye umri wa miaka 73 amekuwepo madarakani  tangu 1986 amefanikiwa kubadilisha sheria  ya ukomo wa umri wa miaka 75 wa kugombea urais ambapo atapata fursa ya kugombea tena mwaka 2021. Chaguzi nchini Uganda zimekuwa zikitawaliwa na vurugu za polisi na wananchi, kuzimwa kwa intaneti na kuwekwa kizuizini kwa viongozi wa upinzani ikiwemo Kizza Besigye wa chama cha Forum for Democratic Change.

Kwa upande wa Kenya ambayo imekuwa ikisifika kwa kuimarisha misingi ya demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo kwa mara ya kwanza mahakama ilifanikiwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Urais yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta uliofanyika Agosti 2018. Uchaguzi ulirudiwa na Rais Kenyatta alichaguliwa tena.

Marudio ya uchaguzi yalilamikiwa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa hayakuzingatia haki za binadamu ambapo watu ambao walipinga uchaguzi huo walikumbana na mkono wa dola. Matendo hayo ndiyo yaliiweka Kenya kwenye kundi la nchi zilizo na uhuru kiasi.

Burundi na Sudan Kusini zimewekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa kutokana na mapigano ya kikabila ambayo yamedhoofisha mfumo wa kisiasa wa kuongoza nchi. Vyombo vya habari na wananchi wanaotoa maoni tofauti na serikali wamekuwa wakiteswa, kufungwa na kuuwawa.

Chanzo: Freedom House           – Nchi zisizo na  uhuru  – Nchi zenye uhuru     – nchi zenye uhuru kiasi   

 

Hali ilivyo Afrika

Afrika kama zilivyo nchi za Afrika Mashariki hali ya demokrasia siyo ya kuridhisha ikizingatiwa kuwa asilimia 11 ya wakazi wapatao bilioni 1.02 wa bara hilo ndio wana uhuru wa kweli, huku 52% wana uhuru kiasi na 37% hawa uhuru kabisa.

Ripoti ya Freedom House inaeleza kuwa waliangazia nchi 49 za Afrika na kugundua kuwa nchi 8 (18%) ndio zina uhuru wa kweli, nchi 22 (43%) zina uhuru kiasi na 19 (39%) hazina uhuru kabisa. Nchi zinazotajwa kuwa na uhuru ni Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Ghana, Togo, Senegal na Kisiwa cha Sao Tome.

 Sababu ya nchi nyingi za Afrika kuwepo kwenye kundi la zisizo na uhuru ni matokeo ya viongozi kukaa madarakani muda mrefu, vurugu za kisiasa na kikabila ambazo zimekuwa zikihatarisha haki za binadamu.

 

Demokrasia ya Dunia

Demokrasia ya dunia inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kisiasa kuliko wakati mwingine ambapo mwaka 2017 ulishuhudia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo kuminywa kwa  uchaguzi huru na kweli, haki za watu wachache, uhuru wa kujieleza, utawala wa sheria.

Nchi 71 kati ya 195 zimeshuhudiwa zikiteteleka katika kulinda haki za kisiasa na jamii ambapo ni nchi 35 tu ndizo zimeweza kulinda haki hizo. Kudhoofika kwa demokrasia kunaendelea kushuka kwa miaka 12 mfululizo na hatua muhimu zisipochukuliwa amani ya dunia itawekwa rehani.

Marekani ambayo ni bingwa wa demokrasia duniani nayo imeripotiwa na taasisi ya Freedom House kudhoofika katika kulinda haki za kisiasa na kijamii na kuzua mgongano wa mawazo miongoni mwa nchi zinazoibukia katika kujenga demokrasia ya dunia.

Tangu kuisha kwa vita baridi, nchi nyingi ziliachana na utawala wa kiimla na kugeukia demokrasia ya vyama vingi lakini hali hiyo imeanza kujitokeza tena ambapo idadi ya viongozi wanaoongoza kwa udikteta inaongezeka.

 

Uhuru wa nchi moja unategemea uhuru wa nchi zote

Demokrasia itabaki kuwa tunu muhimu kwa jamii zilizostaarabika, ikifungua milango ya uwazi, mawazo na fursa mpya na zaidi ya yote kulinda uhuru wa mtu mmoja mmoja. Ikiwa watu duniani kote wanadai mazingira mazuri ya kisiasa ni dhahiri wanakumbatia misingi ya demokrasia: uchaguzi huru, uhuru wa kujieleza, uwazi na uwajibikaji wa serikali, utawala wa sheria ambao hauingiliwi na polisi, jeshi au taasisi nyingine za nchi.

Hata hivyo, Karne ya 21 imeshuhudia ugumu wa kuifanya demokrasia kuwa endelevu ambapo baadhi ya nchi zinatekeleza lakini zingine zinapuuza. Utawala wa kidekteta wa Urusi na China unatambua wazi ili uendelee kuwepo unahitaji kuimarisha demokrasia katika nchi nyingine ili ziendelee kufaidika na mahusiano ya kidiplomasia. Ukuaji wa  demokrasia ni kulinda haki za watu wote duniani kupitia utandawazi   

Continue Reading

Afya

Is Tanzania’s Adolescent Fertility Rate Three Times Higher Than Global Counterparts?

Published

on

The Comprehensive Community-Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT), an organization ​which works to provide affordable medical and rehabilitative services for mothers and newborns throughout Dar-es-Salaam, marked World Contraception Day on September 26 with a call for more efforts to meet the reproductive health needs of teens between 15 and 19 years old.

The report highlights a worrying statistic — Tanzania’s adolescents are having almost three times as many children on average as their global counterparts, with 135 births per 1000 girls reported in the country, compared to an average of 44 per 1000 girls aged 15–19 worldwide in 2015.

CCRBT attributes the high adolescent fertility rate to a lack of access to contraceptive services, with Technical Advisor for Nursing Bola Abbas saying, that only about 8 per cent of current family planning clients are between the ages of 15 to 19.

On a national scale, Abbas explains, demand for family planning among adolescent girls is still very low, with only one out of every three of those who are sexually active within the 15 to 19 age group using modern contraceptive methods.

So the question is, how does Tanzania’s adolescent fertility rate compare to that of the rest of the world?

Pesacheck investigated the claim that Tanzanian adolescents are having three times as many children as their peers in the rest of the world and found that the statement is TRUE for the following reasons:

Tanzania’s adolescent fertility numbers are rather high, with 4.4% of girls aged 15 having given birth according to the country’s Demographic and Health Survey.

The Sustainable Development Goals call for countries to ensure universal access to sexual and reproductive healthcare services, including family planning, information and education, and the integration of reproductive health into national strategies and programmes by 2030.

The indicators for this goal are the proportion of women of reproductive age (15–49 years) who have their need for family planning satisfied with modern methods, and the adolescent birth rate (10–14 years and 15–19 years) per 1,000 women in that age group.

For several sub-Saharan countries, Tanzania included, access to modern family planning methods is low for this particular age group, and as a result, the regional average is 105 births per 1,000, which is more than double the global average.

Tanzania’s National Bureau of Statistics produced a national fertility and nuptiality report based on data from the 2012 national census, which shows that Adolescent Fertility Rate (AFR) was 81 births per 1,000 women aged 15–19.

The report further shows that in 2012, 23.3% of adolescent girls in the country had given birth to at least one child. Additionally, 42.2% of girls who had never attended school had given birth, compared to just 9% of those who had reached university.

This shows that there is a need for contraceptive access for teenage girls in Tanzania, especially for girls in rural areas and those with limited access to education.

The Tanzania Demographic and Health Survey 2015–16 indicates that 27% of girls aged 15–19 have given birth. Crude birth rates for girls aged 15–19 show that there 135 births per 1,000 girls in Mainland Tanzania and 132 per 1,000 girls in Zanzibar, way above the global average of 44. The data also shows that contraceptive access for this age group is also quite low, with 10.4% of girls aged 15–49 using any form of contraception.

It would therefore appear that the lack of access to contraceptives is contributing to the increased likelihood of adolescent girls getting pregnant.

So the claim by CCBRT that Tanzania’s adolescent fertility rate is almost three times the global average is TRUE. This is driven largely by a lack of access to contraceptives for young people in the 15–19 age group, and the relatively high levels of poverty that have driven many out of school and into early marriage.

As a result, the country is unlikely to meet the Sustainable Development Goal of overall good health and wellbeing of mothers unless it puts measures in place to ensure universal access to sexual and reproductive health-care services for girls and women of all ages.

Do you want us to fact-check something a politician or other public figure has said about public finances? Complete this form, or reach out to us on any of the contacts below, and we’ll help ensure you’re not getting bamboozled.

This report was written by PesaCheck Fellow Belinda Japhet, a Communications Consultant, Online Editor based in Tanzania. The infographics are by PesaCheck Fellow Brian Wachanga, who is a Kenyan civic technologist interested in data visualisation. This report was edited by PesaCheck Managing Editor Eric Mugendi.

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com