Connect with us

Jamii

Kesi 456 inayowakabili Wakurugenzi wa JamiiForums, mawakili wavutana kuhusu mahakama kupokea kielelezo cha shahidi

Published

on

Wakili wa upande wa utetezi  avutana na Wakili wa Jamhuri ambayealiiomba mahakama ipokee kielelezo cha taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa JamiiForums ikisadikiwa kuichafua kampuni ya mafuta ya Oilcom.

 Kesi 456 ni ile inayoikabili JamiiForums  na  kampuni ya Oilcom inadaiwa kukwepa kodi na uchakachuaji wa mafuta katika bandari ya Dar es Saalam imeendelea tena leo kwa kusikilizwa kwa mashahidi wawili wa upande wa Jamhuri.

Kesi hiyo ilibadilishiwa hati ya mashtaka (ingawa shahidi wa kwanza alishasikilizwa na ushahidi kuletwa mbele za mahakama). Kilichobadilika katika hati hiyo ni kifungu cha sheria (Kifungu cha 22(1) badala ya 22(2) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao), ilianza leo kwa shahidi wa kwanza kutoa ushahidi wake kabla shahidi wa pili Usama Mohammed kujieleza mbele ya mahakama na kuibua mvutano wa mawakili.

Mvutano huo wa maneno ulijitokeza baada ya Wakili wa Jamhuri Kisheji kuomba Mahakama ipokee   kielelezo cha maudhui ya taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa JamiiForums mnamo 13 Februari 2016 ambazo  zililenga kuichafua kampuni ya Oilcom. Kielelezo hicho kilitolewa na shahidi wa pili wa kesi hiyo aliyejitambulisha kwa jina Usama Mohammed, Meneja Forodha wa kampuni ya Oilcom.

Usama amesema baada ya kuthibitisha kuwa taarifa hiyo iko kwenye mtandao alichapisha kwenye karatasi na kuwasilisha kielelezo hicho Polisi kwa ajili ya uchunguzi dhidi ya madai yaliyotolewa na mtumiaji wa mtandao huo aliyejulikana kwa jina la Furheer kuandika ujumbe wenye kichwa, “USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar…”.

 Licha ya Wakili Kisheji kutaka ombi lake likubaliwe, Wakili wa upande wa utetezi Peter Kibatala alipinga maombi hayo kwa madai kuwa hayakidhi  matakwa ya Sheria ya Kielekroniki ambayo imefafanua hatua za kufuata ili kutoa ushahidi kama huo.

Wakili Kibatala amesema  kulingana na uamuzi wa Jaji Mwakilamba juu ya mchakato wa kielekrotoniki wa kuwasilisha ushahidi  kama huo, umemuomba Hakimu Simba asipokee kielelezo hicho ambacho maudhui yake yamewekwa kwenye karatasi  ambapo taarifa hiyo ilikuwa ya mtandaoni.  

Wakili Kibatala amesema  ushahidi wanaotaka kuutoa unaangukia katika ‘electronic evidence’ na  kuna masharti ya kisheria mahakama kupokea electronic evidence. Vigezo hivyo vitano ambavyo vyote lazima viendane kwa pamoja viliwekwa na shauri la Kesi ya Biashara (Commercial case) namba  10 ya mwaka 2008 kati ya Lazurius Mirisho Mafie  dhidi ya Gasper Kilenga  Alias na  Moiso Gasper uamuzi wa Jaji Makaramba.

Anaongeza kusema kuwa vigezo hivyo ni mfanano (Upande unaoleta ushahidi lazima ulete misingi ili uonekane wa kweli) na sheria ambayo inataka maandishi kama yalivyo kwenye kifaa husika.

Anabainisha kuwa “ Shahidi hajajengewa misingi  ya kukidhi hivyo vigezo na vinatakiwa kuzibwa na Shahidi. Pia haipo katika uhalisia (original form), hiyo  ni kopi na kwa misingi hiyo miwili tunapinga ushahidi kupokelewa”.

Kauli hiyo ya Kibatala iliibua mabishano baina ya mawakili hao wawili ambapo Wakili Kishenyi alimwambia Hakimu kuwa mapingamizi yaliyotolewa na Kibatala hayana uzito kisheria huku akifungua vifungo vya sheria kujibu hoja za wakili wa utetezi.

Wakili Kishenyi  anasema  “mapingamizi ya wakili msomi Kibatala hayana uzito kwenye ombi la kupokea kielelezo. Upokeaji wa electronic printout inaongozwa na Sheria namba 18 ya Electronic Act” (Anavitaja vifungu na kujibu mapingamizi yaliyotolewa na wakili Kibatala).

Kwa mara nyinge, Wakili Kibatala anasema vifungu vya Sheria ya Kielekroniki viko sawa utofauti unaojitokeza ni lugha iliyotumika kwani  kifungu cha 18 kimefanana na hukumu ya Jaji  Makaramba na ufafanuzi umetolewa kwenye kifungu cha 19 cha sheria hiyo.

Baada ya mfutano huo wa mawakili wa pande mbili, Hakimu hajatoa uamuzi wa kupokea kielelezo hicho na amesema atatoa uamuzi huo Desemba 20 mwaka huu.

 

 Shahidi wa kwanza azungumza

 Hata hivyo, kesi hiyo ilianza kwa shahidi wa kwanza, ASP Fatuma Kigondo, Afisa Kikosi cha Reli (RCO) kuapa na Hakimu kumruhusu Wakili wa Jamhuri kumuuliza maswali.

Shahidi huyo amesema mnamo 23 Februari, 2016 alikuwa anafuatilia kesi ambayo jalada la uchunguzi lilikuwa linahusu taarifa za mtandao za kuchafuliwa kwa kampuni ya Oilcom baada ya mtumiaji wa JamiiForums aliyejulikana kwa jina la Furheer kuandika ujumbe wenye kichwa, “USHUHUDA: Hivi ndivyo mafuta yanavyoibiwa Bandarini Dar…”.

Anasema aliandika barua kwa Wakurugenzi wa JamiiForums ili apatiwe taarifa muhimu za mtumiaji huyo ili zitumike kwenye uchunguzi wa tuhuma lakini hakujibiwa barua hiyo. Shahidi anaisoma barua hiyo mbele ya Hakimu Simba na Wakili wa Jamhuri anaomba Barua ipokelewe Kama kielelezo baada ya upande wa mashtaka kutokuwa na pingamizi.  

Kwa upande wake, wakili wa Utetezi Peter Kibatala alimtaka shahidi aimbie mahakama kama barua hiyo iliyoandikwa kwenda JamiiForums ilikuwa ni ombia au amri? Shahidi amesema barua hiyo ilikuwa amri. Lakini Kibatala alipomuhoji kwa kiasi gani barua hiyo ilikidhi matakwa ya kisheria, shahidia alibadilisha kauli yake na kusema barua hiyo ilikuwa ni ombi. Haya yalikuwa sehemu ya mahojiano yake na wakili Kibatala:

Kibatala: Kosa mnalotaka kuchunguza, Ni kosa lipi?

ASP Fatuma: Kosa linabainishwa baada ya kufungua jalada la uchunguzi.

Kibatala: Kosa Ni nini?- Kwa hio mpaka mnafungua jalada mlikuwa hamjuhi kosa?

ASP Fatuma: Tulikuwa tunachunguza Preliminary investigation.

Kibatala: Kosa gani?

ASP Fatuma: Kosa ndio Hilo jalada la uchunguzi. Kosa linakuja baada ya kuchunguza.

Kibatala: Taarifa zilizoandikwa na JF expert member Ni za kweli au sio kweli?

ASP Fatuma: Mimi nilifungua jalada la hii Kesi na Wala sio mpelelezi.

Kibatala: Bado mpaka leo taarifa zinachunguzwa?

ASP Fatuma: Nilihama May mwaka jana.

Kibatala: Mpaka unahama?

ASP Fatuma: Niliacha under investigation

Kibatala: Unaifahamu nchi inaitwa Brunei mji wake mkuu ni Dar es Salaam.

ASP Fatuma: Sifahamu

Kibatala: Barua yako imesema Dar es Salaam iko nchi gani?

ASP Fatuma: Jeshi la Polisi la Tanzania

Kibatala: Sio kwenye barua, Kwenye post aliandika Dar es Salaam inayoibiwa mafuta Ni ya nchi gani?

ASP Fatuma: Alisema Tanzania.

Kibatala: Wapi? Msomee hakimu hiyo Dar es Salaam ni ya nchi gani.

ASP Fatuma: Oilcom iko Tanzania

Kibatala: Ni wapi kwenye post wameandika Ni Dar es Salaam ya Tanzania?

ASP Fatuma: Haipo.

Kibatala: Hii kampuni ya Oilicom unafahamu imesajiliwaje?

ASP Fatuma: Sifahamu

Kibatala: Ulifatilia bandarini ukweli wa tuhuma?

ASP Fatuma: Sikwenda(kwa sababu Mimi sio mpelelezi)

Kibatala: Content zake za hio post unazifahamu?

ASP Fatuma: Kwa wakati huo niliziona, Sifahamu.

Kibatala: Leo huwezi kuzitolea ushahidi mahakamani?

Kibatala: Mlipopeleka hio barua mliprint content?

ASP Fatuma: Sikumbuki, hatukuweka

Kibatala: Mpaka unaondoka, ulikuwa unajua JamiiForums wana taarifa ulizoomba?

ASP Fatuma: Ndio

Kibatala: Nini kilikufahamisha?

ASP Fatuma: Kwa uelewa wangu Mdogo, nilijua wanafahamu, mtu anaweza kuacha namba za simu.

Kibatala: Unafahamu steps mpaka mtu anajisajili JamiiForums?

ASP Fatuma: Sifahamu.

Kibatala: Mlichukua Hatua gani nyingine kumfikia Furheer

ASP Fatuma: Mimi nilihama na sikuwa mpelelezi?

Kibatala: Mpaka unahama ulichukua Hatua yoyote kumfahamu Furheer JF

ASP Fatuma: Mimi sikuchukua Hatua yoyote(kwa sababu sikuwa mpelelezi)

Kibatala: Hii barua ilielekezwa kwa nani?

ASP Fatuma: Mkurugenzi mkuu.

Kibatala: Nani?(Maana naona washtakiwa wawili)

ASP Fatuma: Sifahamu

Kibatala: Mpaka unatoa ushahidi, ulifanya chochote kujua Max Melo na mwenzake wana uhusiano gani na hicho cheo.

ASP Fatuma: Sikufanya

Kibatala: Kwa ufahamu wako, Je Kuna Kesi yoyote iliyowahi kufunguliwa na Oilcom dhidi ya JamiiForums?(Defamation)

ASP Fatuma: Sijui

Kiabatala: Hapa mahakamani umetoa kithibitisho chochote kwamba haya yaliandikwa JamiiForums?

ASP Fatuma: Binafsi sijatoa

 

Mwenendo wa kesi

Kesi hiyo ambayo ilianza kusikilizwa Disemba 13, 2016 inawahusu Wakurugenzi wa JamiiForums, Maxence Melo na Micke Williams kukataa kutoa ushirikiano kwa Polisi ili wasaidie kupatikana kwa taaarifa za mtumiaji wa mtandao wa JamiiForums, Furheer katika upepelezi wa jalada la uchunguzi lililofunguliwa na kampuni ya Oilcom ikidai kuchafuliwa kwa kukwepa kodi na kuchakachua mafuta bandari ya Dar es Salaam.

Kwa kutambua uhuru wa kujielezwa JamiiForums hawakutoa taarifa hizo na waliitaka polisi kufuata taratibu za kimahakama. Desemba, 2016 Maxence Melo alikamatwa na kufunguliwa mashataka  akiwa kama Mkurugenzi wa Kampuni ya Jamii media inayoendesha mtandao wa JamiiForums alishindwa kutoa taarifa za kiuchunguzi zilizochapishwa kwenye mtandao huo kwa Jeshi la polisi.

Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na hukumu ya mwisho inatarajiwa kutolewa kabla ya mwaka huu kuisha. Kesi hiyo itaendelea tena Desemba 20, mwaka huu.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Afya

Watumishi wa afya 200 kupatiwa mafunzo ya utoaji dawa ya usingizi kuokoa maisha wajawazito

Published

on

Kufuatia upungufu wa wataalamu wa dawa za usingizi (anaesthesia), serikali itatoa mafunzo ya dawa za usingizi kwa watumishi wa afya 200 katika vituo vya afya vya upasuaji wa dharura kwa akina mama wajawazito.

Hatua hiyo inakuja ikiwa imepita miezi 6 baada ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kutangaza kuanza kutoa shahada ya dawa ya usingizi (Bsc. Anaesthesia Nursing).

Katika taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano serikalini cha Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, inaeleza kuwa mafunzo hayo yatatolewa sambamba na uboreshaji wa huduma ya upasuaji wa dharura kwa wajawazito ili kuokoa maisha ya wanawake na watoto ambao hufariki kwa kosa huduma muhimu za uzazi kwenye vituo vya afya.

“Mkakati wa kuhakikisha huduma za afya kwa akina mama wajawazito zinakuwa salama na uhakika kwa kuandaa rasilimali watu, miundombinu ya majengo na vifaa vitakavyowezesha huduma hizi ikiwemo upasuaji wa dharura kwa akina mama wajawazito wakati wa kujifungua,” imeeleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Afya, vifo 556 vitokanavyo na uzazi kwa kila viumbe hai 100,000 huripotiwa kila mwaka katika maeneo mbalimbali nchini. Maana yake ni kwamba watoto na wajawazito hufariki hasa wakati wa mama akijifungua.

Aidha, serikali itaboresha vituo vya afya 288 vya serikali vilivyopo nchini ili kuviwezesha kutoa huduma ya dharura ya upasuaji kwa wajawazito ambapo waaguzi katika vituo hivyo watapatiwa mafunzo ya dawa za usingizi ili kuokoa maisha ya akina mama na watoto wachanga.

Utekelezaji wa mafunzo hayo ni matokeo ya ushirikiano wa Wizara ya Afya na Mfuko wa Pamoja wa Afya ambapo zaidi ya sh1,079 bilioni zimepatikana kufakisha mafunzo hayo ya dawa ya usingizi kwa wauguzi na matabibu waliopo kwenye vtuo vya afya nchini.

“Fedha hizo zitasomesha watumishi wapatao 200, kati ya watumishi hao 100 watapata mafunzo yao katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na MOI, watumishi 50 watafanya mafunzo katika hospitali ya KCMC, na 50 watafanya mafunzo hayo kwenye hospitali ya Bugando,” imefafanua taarifa ya wizara.

Lengo la serikali ni kuhakikisha ifikapo 2019 na kabla ya 2020 vituo vyote vya afya vinavyomilikiwa na serikali vinakuwa na watumishi maalum wa kutoa huduma ya dawa ya usingizi kwaajili ya wapasuaji wasiopungua wawili kwa kila kituo.

Mafunzo hayo ya mwaka mmoja ni mpito wakati serikali ikiendelea kukamilisha taratibu za kurasimisha utoaji wa shahada ya kwanza ya kutoa dawa ya usingizi katika Chuo cha MUHAS katka mwaka huu wa 2018/2019.

Hali halisi ya huduma ya dawa za usingizi nchini
Takwimu za wizara ya Afya zinaonyesha kuwa kuna upungufu mkubwa wa madaktari wenye utaalamu wa kutoa dawa ya usingizi hasa wakati wa huduma ya upasuaji ambapo kwa sasa waliopo ni asilimia 1.2 tu ya mahitaji yote.

Ili kuweza kukidhi mahitaji yote ya huduma hiyo wanahitajika madaktari 2000, lakini waliopo sasa ni madaktari 30 pekee.

Kufuatia changamoto hiyo Januari 31, mwaka huu wadau mbalimbali wa afya na elimu walikutana na kujadili namna ya kuondoa changamoto hiyo na kupendekeza mtaala utakaotumika kufundishia kozi ya Aesthesia kabla ya kuupeleka kwa Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU).

” Ni kweli kumekuwepo kwa changamoto hiyo ya watalaamu wa dawa hizo lakini sasa mpango huu ukikamilika maana yake tutaongeza idadi ya madaktari kamili maana hawa waliopo wengi ni wale ambao wamesoma kozi kwa mwaka mmoja au miwili.

” Mafunzo yakianza kutolewa hapa chuoni Muhimbili wataweza kuchukua wanafunzi 200, Bugando 50 na KCMC 50 jambo ambalo litaongeza idadi kubwa ya watalaamu ili kuweza kufikia lengo letu la kuwa na wataalamu 2000 nchi nzima,” alinukuliwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulisubisya.

Continue Reading

Jamii

Waziri Mkuu Majaliwa: Hatutangazi nyongeza ya mshahara hadharani kuepusha athari kwa jamii

Published

on

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameweka wazi kuwa serikali haitatangaza nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma hadharani ili kuepusha athari kwa jamii ikiwemo kupanda kwa bei ya bidhaa.

Akizungumza leo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu (CHADEMA), Susan Lymo ambaye alitaka kufahamu kwanini Serikali imewanyima au imeshindwa kuwalipa watumishi wa umma nyongeza ya mishahara ambayo ni haki yao ya msingi kulingana na miaka waliyokaa kazini.

Akijibu swali la Mbunge huyo, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali ina utaratibu wa kutoa nyongeza ya mishahara kwa watumishi wake lakini haitangazi kwa wananchi wote kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwenye sherehe za wafanyakazi za Mei Mosi kila mwaka.

Amesema Serikali ikitangaza mishahara hadharani inaweza kusababisha usumbufu kwa watu wasio watumishi wa umma na inaweza kupandisha bei ya bidhaa na kuathiri mwenendo wa mahitaji ya wananchi sokoni.

Nyongeza za mishahara ambazo zinatangazwa hadharani, mara nyingi zina athari yake sio kwamba Serikali haikusudii kutoa nyongeza ya mshahara kwa mwaka, lakini unapotumia Mei Mosi kutangaza nyongeza ya mshahara unaleta athari kwenye jamii kwasababu vitu vinaweza vikapanda bei, vikawasumbua hata na wananchi ambao hawalipwi mshahara,” amesema Waziri Mkuu.

Amebainisha kuwa siyo lazima Serikali itangaze hadharani kila inapoongeza mishahara kwa watumishi wa umma lakini ifahamike kuwa Serikali ina utaratibu wake mzuri wa kuboresha stahiki za wafanyakazi wake kila mwaka.

Suala la nyongeza ya mishahara liko Serikalini na Mhe Rais ameishawahakikishia wafanyakazi atawaongeza mishahara na sio lazima litangazwe hadharani. Mshahara ni suala la mtu binafsi hata ukiongezwa leo kuwa tumeitangaza leo tumeongeza mshahara kwa kiwango hiki. Ukifanya hivi tayari umeleta kupanda kwa gharama’” amebainisha Waziri Mkuu.

Ameongeza kuwa mkakati wa Serikali ni kupunguza gharama za mahitaji kwenye masoko ili kuzuia mfuko wa bei za bidhaa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu Mjaliwa amesema Serikali inaendelea kufanya sensa ya watumishi wote nchi nzima na zoezi hilo likikamilika itaboresha nyongeza ya mwaka, nyongeza ya mishahara na upandishaji wa madaraja.

Awali katika swali lake, Mbunge Lyima amesema Serikali inakiuka Sheria ya Utumishi wa Umma ya kuwapatia watumishi stahiki zao na kuwapunguzia motisha ya kufanya kazi kwa ufanisi katika maeneo yao ya kazi na kuathiri mafao baada ya kustaafu.

Hoja ya Mbunge huyo ni muendelezo wa malalamiko ya watumishi dhidi ya Serikali kwamba hawajapata stahiki zao tangu ilipoanza zoezi la ukakiki wa watumishi wa umma mwaka 2015. Katika zoezi hilo watumishi zaidi ya 9,000 walibainika kutokukidhi vigezo vya utumishi na hivyo kuondolewa kazini.

Huenda kauli aliyoitoa Waziri Mkuu leo Bungeni inaweza ikatofautiana na ile ya Rais John Magufuli aliyoitoa wakati wa sherehe za Mei Mosi, 2018 mijini Iringa ambapo alinukuliwa akisema hawezi kutoa nyongeza ya mishahara akidai Serikali haina fedha.

Kwangu mimi ninafikiria hizi pesa tunazotoa kwa ajili ya elimu bure ni nzuri kuliko fedha hizo kuzipeleka kuongezea mishahara, naona bora kuwapa mikopo wanafunzi wa vyuo vikuu kuliko kuongezea wafanyakazi mishahara,

Nikisema nitaongeza hizo pesa mimi nitazitoa wapi? naogopa kusema uongo. Hata mimi napenda kupandishiwa mshahara lakini kwa hali halisi ya sasa hivi lazima niwaeleze ukweli,” alinukuliwa Rais Magufuli.

Hata hivyo alibainisha kuwa kabla ya kuondoka madarakani ataboresha maslahi ya wafanyakazi wa umma, “Nawaahidi, kipindi changu cha urais hakitaisha kabla sijapandisha mishahara kwa wafanyakazi, kupandisha kwangu haitakuwa kwa shilingi elfu kumi, itakuwa ni kupandisha kwelikwel.”

Continue Reading

Jamii

Maaskofu KKKT wapewa siku 10 kufuta waraka

Published

on

Serikali imetoa siku 10 kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), kuufuta kwa maandishi waraka wao waliotuoa Machi 24 mwaka huu na kisha kuujulisha Umma kwa njia mbalimbali walizotumia kuusambaza.

Kanisa la KKKT kupitia Baraza lake la Maaskofu lilitoa waraka uliopewa jina la ‘Taifa Letu Amani Yetu’ wakati wa Pasaka ambao mbali na masuala ya kiroho, ulibainisha mambo kadhaa yanayogusa mstakabali wa taifa.

Katika mitandao ya kijamii leo imesambazwa barua yenye kumbukumbu no. SO.748/25 inayoonyesha imeandikwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Wizara ya Mambo ya Ndani kwenda kwa Mwenyekiti /askofu Mkuu wa KKKT iliyoandikwa Mei 30, 2018 ikitoa maelekezo ya kufutwa waraka huo ndani ya siku 10 tangu ilipoandikwa barua hiyo.

Ikiwa na kichwa cha habari ‘Ujumbe wa Baraza la Maaskofu wa KKKT’ barua hiyo inaeleza baraza hilo halitambuliki kisheria katika ofisi ya msajili.

“Unaelekezwa kuufuta waraka husika kwa maandishi na kuujulisha umma kuwa taasisi yako haikuwa na haina uwezo kisheria kufanya kile mlichokifanya. Maandishi hayo yaufikie umma wa Watanzania kwa kupitia vyombo vya habari na njia zingine zilezile zilizotumika kuufikisha waraka ule mliouita ‘Ujumbe wa Baraza la Maaskofu KKKT’.

Hata hivyo, barua hiyo imetoa onyo kali kwa taasisi hiyo dini nchi kutekeleza agizo mara moja la sivyo itachukuliwa hatua za kisheria.

“Maelekezo haya yatekelezwe ndani ya siku kumi tangu kupokea kwa barua hii vinginevyo hatua kali zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi ya taasisi hii,” inasema barua hiyo.

Ikumbukwe kuwa  waraka huo ulisainiwa na maaskofu 27 wa kanisa hilo nchini na kutaja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na utekaji, utesaji, kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi.ni hali ya kijamii na kiuchumi, maisha ya siasa, na masuala mtambuka likiwamo suala la Katiba Mpya.

Waraka uliongeza pia kwamba uhuru wa kujieleza, kutoa na kupokea habari umeendelea kutoweka nchini huku ukionya kubanwa na hatimaye kuelekea kupungua kwa uhuru wa Bunge, Mahakama, na Tume ya Uchaguzi, ukisema hatua hii ni pamoja na kudhoofishwa kwa serikali za Mitaa.

Lakini kabla ya KKKT kutoa waraka wao, Kanisa Katoliki nalo lilitoa waraka kama huo likionya baadhi ya mambo ikiwemo uminywaji wa misingi ya demokrasia ya vyama vingi na uhuru wa kujieleza.

Baada ya kusambaa kwa waraka huo, yalijitokeza mambo mengi ikiwemo kutofautiana na kwa mawazo ya wananchi kuhusu wajibu wa viongozi wa dini katika kutoa ushauri, kuonya au kukemea pale mambo yanapoenda mrama.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Maaskofu wa KKKT

Hata hivyo, barua hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti na watumiaji wa mitandao ya kijamii ikizingatiwa kuwa suala hilo lilijadiliwa na kupita, iweje linaibuka tena wakati huu ambapo kuna utulivu na yale mambo waliyoyapigia kelele na maaskofu  yamepungua ikiwemo kuteswa, kupotea kwa watu na vitisho dhidi ya viongozi wa kisiasa.

 

Wananchi bado wanawaamini viongozi wa dini

Wadau mbalimbali wa masuala ya kijamii wamesema kama kweli barua hiyo imetolewa na serikali, inaweza kuchochea taharuki zaidi kwa waumini wa kanisa hilo na wananchi kwasababu linagusa moja kwa moja imani zao.

Amebainisha kuwa bado waumini wengi wana imani na viongozi wao dini na kwamba yale wanayotamka yanakuwa na nia njema kwa jamii yao. Na katika muktadha huo serikali inapaswa kuwa makini ili kuepusha matatizo zaidi yanayoweza kutokea.

Akizungumza na FikraPevu, Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena amesema kama serikali ilibaini kuna tatizo kwenye usajili wa Baraza la Maaskofu la KKKT ingekaa na wahusika na kulimaliza kuliko kujitokeza hadharani na kuendeleza jambo ambalo limepita.

“Mimi namwamini Mungu kuliko serikali na viongozi wangu wa dini hasa Maaskofu. Hivyo serikali inapaswa kuwa makini na mambo yanayogusa imani za watu. Katika hili walipaswa kutafakari sana jinsi ya kushughulika nalo. Vinginevyo halina afya kwa ustawi wa taifa letu,” amesema Meena.

Amesema Maaskofu walitimiza wajibu wao wa kuonya kabla mambo hayajaharibika na serikali inapaswa kuyafanyika kazi yale yalyotajwa kwenye waraka au kukaa kimya ili kuepusha migongano isiyo na faida kwa taifa.

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com