Connect with us

Education

Kishapu: Wanafunzi Magalata huponea njaa shuleni

Published

on

WANAFUNZI wa shule ya msingi Magalata, wilayani Kishapu, wameendelea kuhudhuria vizuri shuleni tangu utaratibu wa kutoa huduma ya chakula ulipoanza.

Utaratibu wa kutoa huduma hiyo ulianza miaka mitatu iliyopo ambapo unafadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) kwa ushirikiano na Mpango wa Chakula wa Kimataifa (WFP).

uji-shuleni

uji-shuleni2

Wakinywa-uji

Wanafunzi wa Shule ya msingi Magalata, wakifurahia kifungua kinywa cha uji wanaogawiwa shuleni hapo

Kwa mujibu wa Kaimu mwalimu mkuu wa shule hiyo, Cyprian Mabele, tangu utaratibu huo ulipoanza, mahudhurio ya wanafunzi yameongezeka na kuwatia moyo walimu.

Mabele alisema, chakula hicho kimekuwa kikisababisha wanafunzi hao kuhudhuria kwa wingi shuleni, ikizingatiwa kwamba katika miaka ya hivi karibuni, familia nyingi zimekumbwa na upungufu wa chakula.

“Watoto wanakuwa wengi sana maana wanajua wakija watakunywa uji asubuhi na kula makande mchana, tofauti na wakikaa makwao ambapo wakati mwingine hata hicho chakula wanaweza wasikipate,”anasema mwalimu huyo.

Kutokana na utaratibu huo kusaidia mahudhurio ya wanafunzi, wanaiomba serikali iendelee kuwakumbatia wafadhili hao ili waendelee kusaidia mpango huo.

Mwaka jana, shule hiyo ilifaulisha wanafunzi wanane kati ya 32 wa darasa la saba, ambapo mwaka uliotangulia wanafunzi sita ndio waliokwenda sekondari.

Kwa sasa shule hiyo ina wanafunzi 386 ambapo mwaka huu imeandikisha wanafunzi 49 katika matarajio ya kuandikisha watoto 60, huku ikiwa na walimu 10. Hata hivyo shule hiyo ina upungufu wa vyumba vinne vya madarasa.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Education

Kwanini ni vigumu kuomba msaada?

Published

on

Ni matarajio au matamanio ya kila mtu kusaidiwa kukamilisha jambo fulani. Iwe kazini au kwenye shughuli yoyote ya kijamii, utahitaji watu wenye ujuzi na maarifa tofauti tofauti kufanikisha malengo yako. Mfano, wachezaji wakiwa uwanjani wanacheza kwa kusaidiana kila mmoja katika nafasi yake ili kuifunga timu pinzani na kuibuka na ushindi.

Hakuna jambo lolote linaloweza kukamilika bila ya kuwa na usaidizi wa namna fulani. Lakini umewahi kujiuliza kwanini ni vigumu kwa watu kuomba msaada?

Jibu linatolewa na Mwanasaikolojia ya Jamii, Heidi Grant anaeleza kuwa, kilichopo nyuma ya kuomba msaada ni hofu ya kukataliwa ambayo imekita mizizi katika saikolojia ya uumbaji wa mwanadamu.

Katika kitabu chake kiitwacho, Reinforcements anaandika kuwa kuomba msaada ni jambo lisilopendeza linalomfanya mtu ajisikie mgonjwa.

Hilo linathibitishwa na Mtaalamu wa Saikolojia mwingine nchini Marekani, Stanley Milgram ambaye alifanya jaribio la utii na mamlaka ambapo aliwaelekeza wanafunzi wake ambao walikuwa wamesimama ndani ya treni kuomba nafasi ya kukaa kwenye viti. Anasema majibu aliyopata ni kwamba wengi wao waliogopa kuomba msaada huo. “Niliogopa ningesingeweza,” alisema mmoja wa wanafunzi.

Lakini  Milgram aliamua  kuomba siti na akakubaliwa , “ Kichwa changu kilizama katikati ya miguu yangu na nilihisi nimepigwa na butwaa,” anaandika. “Sikufanya wajibu wangu. Nilikuwa najisikia kama naenda kupotea.”

Muitiko huo ambao Grant ameuelezea unahusiana na tabia za kijamii ambazo zimeunganishwa kwenye ubongo wa mwanadamu tangu karne nyingi za uumbaji. Kama wanyama wengine, binadamu wameumbwa kupata msaada kutoka kwa familia na jamii zao ili waweze kuishi. Lakini inafika wakati tunaogopa kuomba msaada hata kama tuna shida.

 

Kwanini watu wanaogopa kuomba msaada?

Zipo sababu mbalimbali ambazo zinasababisha watu kuogopa kuomba msaada ni kupoteza  hadhi na heshima katika jamii. Wapo baadhi ya watu wana hadhi fulani ambayo anahisi akiomba msaada kwa watu  atadharaulika. Pia kukataliwa, siyo kila ombi linakubaliwa, mengine yanakatiliwa; hofu hiyo huwazuia watu kuomba msaada. Wakati mwingine ukiomba msaada inakuwa ni njia ya watu kufahamu matatizo yako na kuwaambia wengine; jambo linaloweza kutengeneza huzuni katika maisha.

Grant anaeleza kuwa kuomba msaada kunakuweka wazi zaidi na hatari za kijamii ambazo zinaweza  kudhihirisha unyonge  na kukaribisha maumivu.

Anaeleza zaidi kuwa inatengeneza huzuni, na kukaribisha uwezekano wa kukataliwa. “Hajalishi, ndiyo maana tunaogopa kuomba msaada kama tunavyogoopa maradhi,” ameandika. “Maradhi yanaweza kuwa  na hatari ndogo kwetu ukilinganisha na kuomba msaada.”

Hata hivyo, ni mara chache sana matokeo hasi tuliyoyaona hapo juu kutokea mara tunapoomba msaada. Katika utafiti mwingine, Mwanasaikolojia  Vanessa Bohns alichunguza sampuli ya watu 14,000 ambao walitakiwa kuomba msaada. Na alibaini kuwa idadi kubwa ya walioomba msaada walikuwa na uwezekano mkubwa wa kupata kuliko ambavyo walikuwa wanaamini awali.

Katika semina mbalimbali, Mhamasishaji, Antony Luvanda amekuwa akisisitiza kuwa kuomba msaada siyo ishara ya unyonge bali ni ishara kuwa umeimarika kimaisha.

Kwa maneno mengine, inaweza kuwa rahisi kupata msaada kuliko kuomba.

Continue Reading

Education

Utunzaji nyaraka za serikali katika kijiji cha Magalata

Published

on

NYARAKA mbalimbali za serikali na kumbukumbu za ofisi ya kijiji cha Magalata, kilichoko katika wilaya ya Kishapu, ziko hatarini kuharibika na kulowana na maji iwapo mvua zitanyesha.

(more…)

Continue Reading

Education

Historia ya Shule ya Msingi Nachingwea imebaki katika ‘kava’ la daftari…

Published

on

Historia ya shule ya msingi Kiegei katika kata ya Kiegei wilaya ya Nachingwea mkoa wa Lindi, imebaki katika kava moja tu la daftari, lakini shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa vitabu, vitendea kazi vya kufundishia na walimu.

(more…)

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com