Connect with us

Featured

Kuwatisha madaktari ni hatari kwa maisha yetu, tujadiliane nao sasa

Published

on

Kuwalazimisha madaktari kurudi kazini mara moja ama sivyo watajifukuzisha kazi hakubadilishi ukweli wa hali iliyopo. Hata kuwabembeleza warudi kazini mara moja kwa sababu “wagonjwa wanakufa” nako hakubadilishi hali iliyopo. Kwa ufupi, agizo la serikali kutaka madaktari warudi kazini mara moja linapuuzia kabisa madai yao na linatumia ubabe wa madaraka na bila ya shaka nyuma yake kuna tishio la nguvu za dola kulazimisha madaktari. Kwa vile sababu za msingi zilizosababisha mgomo hazijashughulikiwa – hata zile zinazoweza kushughulikiwa mara moja – basi sababu ya uwepo mgomo haijaondolewa au kupunguzwa.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ambaye ametoa tamko la kuwataka madaktari kurudi kazini

Serikali inaweza kulazimisha madaktari kurudi kazini?
Serikali ina uwezo wa kulazimisha watu warudi kazini lakini haina uwezo wa kulazimisha watu kufanya kazi. Kwa kutumia tishio au hata nguvu serikali inaweza kuvunja mkutano wa madaktari na kuwakamata viongozi wa mgomo huo na yumkini madaktari wanaweza “kurudi kazini”. Hata hivyo madaktari “kurudi kazini” haina maana wanarudi “kufanya kazi”.  Wataweza vipi kufanya kazi yao vizuri kwa uadilifu kama msingi wa malalamiko yao umepuuziwa zaidi ya kuambiwa “madai yenu ni ya msingi na tunayafanyia kazi?”

Kwa vile serikali haiwezi kulazimisha watu kufanya kazi wazo kuwa madaktari wanalazimishwa kurudi mahospitalini katika mazingira yale yale, yakiwa na vikwazo vile vile ni wazo la hatari. Hivi ni kweli tunaamini kuwa madaktari hawa  waliopuuzwa, kudharauliwa na kunyanyaswa wakirudi kuangalia wagonjwa kesho watafanya hivyo vizuri zaidi? Hivi kweli serikali inaamini kuwa maisha ya wagonjwa mikononi mwa madaktari waliopuuzwa yako salama kwa vile madaktari “wamerudi kazini”?

Mgomo wa madaktari husitishwa kwa makubaliano
Mgomo wa madaktari hauwezi kuisha kwa kulazimisha au vitisho kwani kwa kufanya hivyo serikali itajikuta inapanda mbegu za mgomo mwingine labda mkubwa zaidi kuliko wa sasa. Huko India mwishoni mwa mwaka jana (kuanzia Disemba 21) madaktari waligoma jimbo la Jaipur. Mgomo wao ulidumu kwa siku 11 na madaktari zaidi ya 10,000 walishiriki. Mwisho serikali ikawaweka ndani madaktari wapatao 500 lakini mwisho wa siku – na baada ya wagonjwa 60 kudaiwa kufa kwa sababu ya mgomo – serikali ilikubali kuwaachilia madaktari wote toka jela, na kuondoa adhabu ya sheria ya kutokugoma na kukubali kuyafanyia kazi madai ya madaktari. Tarehe 1  Januari madaktari wakarudi kazini baada ya makubaliano ya kusitisha mgomo siku moja kabla yake.

Huko Israeli nako madaktari waligoma  mwaka jana kufuatia suala la maslahi vile vile. Mgomo wao ulidumu kwa siku 158 na mwisho wake mwezi Augusti ulikuwa ni makubaliano ambayo serikali ilikubali kuongeza mishahara ya madaktari na kuboresha mazingira yao ya kazi. Badala ya madaktari kusubiri kufukuzwa madaktari walijiuzulu (mass resignations) katika kuonesha kuwa hawakuwa tayari kuburuzwa na serikali. Waziri wa Fedha wa Israeli akitangaza kuishia kwa mgomo huo alikiri kuwa wamefikia makubaliano na madaktari ambayo yamemaliza “mojawapo ya migomo mikubwa zaidi katika historia ya Israeli”.  Waziri Mkuu Netanyahu alijikuta akikubali kuwa matokeo ya mgomo ule ilikuwa ni kuboresha maslahi ya madaktari lakini vile vile kuleta mabadiliko makubwa katika mfumo wa huduma za afya nchini Israeli.

Huko Kenya vile vile mgomo wa madaktari wa mwishoni mwa mwaja jana uliishia kwa kufikia makubaliano na serikali ambapo serikali ilikubali kuongeza fedha katika kuboresha miundombinu ya afya, kulipa madeni ya nyuma ya madaktari na kutenga fedha zaidi katika mafunzo n.k Mgomo wao uliodumu kwa siku 10 nao ulimalizwa kwa makubaliano.

Kwa ufupi, mgomo huu wa kitaifa wa madaktari haupaswi kumalizwa kwa vitisho, kejeli, kupuuzia au dharau. Mgomo unatakiwa kumalizwa kwa makubaliano. Ndio maana ninaamini bila makubaliano mgomo huu unaweza ukazua mgomo mkubwa zaidi kwani mambo ya msingi hayajakubaliwa. Na kwa kweli haupaswi kuisha bila kuweka makubaliano ya msingi ili kuondoa ulazima wa kugoma tena muda si mrefu ujao.

Kanuni za Makubaliano
Sasa, kuna msingi wa kusitisha mgomo ambao unategemea kanuni kadhaa. Naamini, makubaliano ya kusitisha mgomo huu lazima yazingatie lau kanuni zifuatazo.

a.       Wagonjwa wapate nafuu – makubaliano yahakikishe kuwa mwisho wa siku ni wagonjwa wanaopata nafuu katika huduma, matibabu na kupona. Utakuwa ni mgomo mbovu kama baada ya makubaliano maisha ya wagonjwa wetu yanarudi pale pale. Hivyo, mambo yote yatakayokubaliwa lazima yazingatie kuwa Wagonjwa wetu wanapatiwa unafuu wa gharama, huduma, na ubora wa hali ya juu wa huduma hiyo. Nje ya hapo mgomo utakuwa umefeli.

b.      Maslahi ya Madaktari ni lazima yaboreshwe na kuinuliwa. Lengo la (a) haliwezi kufikiwa kama madaktari wataendelea kufanya kazi katika miundo mbinu mibovu na hali mbovu ambazo zinawafanya wasiwe makini au waadilifu. Hata mtu anayejitolea anaweza kujitolea zaidi kama kujitolea kwake kunaonekana na kunawezekana. Hivyo, mishahara na posho za madaktari ziongezwe lau kufikia kiasi wanacholipwa Wabunge. Posho za mazingira magumu, on-call, midnight shifts etc ziongezwe mara moja. Kama tunaweza kumpa mbunge shilingi 200,000 kwa kukaa (azungumze au asizungumze) tunaweza kumlipa daktari kiasi hicho kwa zamu ya usiku au mazingira fulani fulani yatakayokubaliwa. Bila ya shaka maslahi ya wafanyakazi wote wa huduma ya afya ni lazima yaangaliwe kwa upana wake. Hili linaweza kuchukua muda mrefu kidogo kukamilika.

c.       Serikali ni lazima itenge fedha za kutosha kuboresha miundo mbinu ya afya ikiwemo suala la nishati, madawa, na vitendea kazi mbalimbali. Hospitali za serikali ni lazima ziwe na kiwango fulani kisichopungua cha vifaa (minimum standard) ili hospitali ifanye kazi. Serikali ni lazima iwekeze vya kutosha kwenye huduma ya afya ili ndani ya miaka angalau mitatu hii kabla hawajaondolewa madarakani- waoneshe kuwa wamebadilisha sekta hii kwa kiasi kikubwa. Siyo kwa kuongeza “idadi” bali kwa kuongeza “ubora”! Katika kuboresha huduma wa sekta ya afya serikali ni lazima iwawabishe viongozi na watendaji ambao wamechangia kufikisha nchi mahali hapa.

Hivyo, basi kwa kuzingatia kanuni hizo tatu naweza kutoa mapendekezo ya mambo ambayo yanapaswa kukubaliwa na madaktari na serikali ili kusitisha mgomo huu mara moja.

Serikali:
1.       Kufukuzwa mara moja kwa Waziri wa Afya, Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Daktari Mkuu. Hili ni jambo msingi la kwanza kufanywa na serikali kwani hawa watatu walikuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa madaktari hawafikii mahali pa kugoma. Ushahidi wote uliopo wazi hadi hivi sasa umetuonesha kuwa watu hawa watatu wametumia ubabe, dharau na kejeli na kulazimisha mgomo huu. NI LAZIMA WAONDOKE KABLA Mgomo haujasitishwa.

2.       Kutenga fedha za kulipa madeni ya nyuma ya madaktari pamoja na kutenga fedha za kuongeza posho za msingi ambazo zinahusiana na mazingira ya kazi, na usafiri. Kwa vile tayari tunajua serikali inaweza kuongeza posho katikati ya bajeti kwa wabunge tunajua basi inawezekana kufanya hivyo kwa madaktari. Ongezeko la posho hizo liendane na ongezeko la posho walizopewa wabunge. Madaktarii wawe tayari kuahirisha kuongezewa posho hizo endapo posho za wabunge nazo zitafutwa au kupunguzwa.

3.       Serikali itenge fedha sasa hivi kwa ajili ya kufanyia matengenezo vifaa ambavyo havifanyi kazi kwenye mahospitali yetu ikiwemo uagizwaji wa wa vifaa vya kisasa vya kutolea huduma. Kama serikali inaweza kuagiza magari mapya kwa watendaji mbalimbali wa serikali kila mwaka wakati umefika kwa serikali hiyo hiyo kukubali kuagiza vifaa vipya. Kwa kuanzia hospitali zote za mkoa zipatiwe CT Scan kabla ya mwisho wa mwaka huu pamoja na wataalamu wa vifaa hivyo. Hii inazingiatia kanuni ya (a). Vile vile hili linaweza kupatiwa motisha wa kodi (tax incentive). Kama kuna kodi kwenye vifaa vya afya wakati umefika kufuta kodi hizo ili kurahisisha uingizwaje wake nchini.

4.       Serikali ijiwekee viwango (standard) za huduma za afya ambavyo wananchi watarajie kuona kwenye hospitali zao za umma. Hospitali za Umma lazima zionekane zina ubora wa kuweza kushindana na zile za binafsi.

5.       Serikali ifanyie mabadiliko ya sheria inayowapa viongozi haki ya kwenda kutibiwa nje ya nchi kwa gharama za wananchi. Kwa kadiri ya kwamba viongozi wanahaki hiyo hawawezi kuboresha sekta ya afya kwani mahospitali yetu yatakuwa ni mahali pa kupata rufaa tu za kwenda nje. Kiongozi anayetaka kwenda nje ajipeleke kwa fedha zake mwenyewe au jamaa zake au ndugu zake. Kuendelea kuruhusu hilo ni kuendelea kuruhusu kuvuja kwa fedha zetu kwenda nje ya nchi. Endapo viongozi watajua kuwa wao na watoto wao watatabiwa hapa hapa nchini wataona umuhimu na uharaka wa kuboresha hospitali zetu. Kinyume chake wao wanafikiria kuboresha “hospitali zetu” wakati wenyewe wako tayari kwenda kutibiwa kwenye “hospitali za wenzetu”. Kama serikali haitofanya hivi ni matumaini yetu wabunge wa upinzani (ambao nao ni wanufaika wa mfumo huu) wataandaa mswada binafsi wa kuondoa hivi vipengele. Viongozi pekee ambao kwa muda wanaweza kuruhusiwa kuendelea kuangaliwa nje ni wale waliokwisha staafu na wao watapewa nafasi hiyo kwa mwaka mmoja ujao tu baada ya hapo na wao lwao!

6.       Serikali iwe tayari kwa kushirikiana na madaktari kuunda a Special Task Force ambayo itapitia sera na mfumo wetu wa afya na kutoa mapendekezo ndani ya miaka mitatu ya mabadiliko makubwa ya sekta ya afya. STF hiyo iundwe na madaktari na wataalamu wa afya, wa fedha, na wanasheria ili hatimaye ije na mapendekezo ambayo yataanza kuingizwa kwenye bajeti ya mwaka huu ili kufanyia mabadiliko makubwa mfumo wetu wa huduma za afya (major healthcare reform). Waangalie, tatizo liko wapi, fedha zinapotea wapi, nini kibadilishwe na vipi na mwananchi atanufaika vipi katika mabadiliko hayo. Mfumo wa sasa siyo endelevu ni mzigo mkubwa kwa wananchi.

Madaktari
1.       Kama sehemu ya kuonesha wanajali madaktari watangaze kurudi kazini mara baada ya uongozi wa sasa wa Wizara ya Afya kujiuzulu. Mgomo huu kwa kiasi kikubwa umesababishwa na hawa viongozi kwa hiyo kuumaliza ni lazima hawa waguswe. Wafanyakazi wa afya hawawezi kufanya kazi na hawa watu tena – wamepoteza moral legitimacy kuongoza wizara hiyo hasa baada ya kuachilia vifaa vibovu vya kupima HIV kuendelea kutumika nchini na pia kudharau madai ya madaktari hadi mgomo umetokea. Ni lazima waondoke kama sharti la kwanza la madaktari kurudi kazini na kuzuia wauguzi na wataalamu wengine kujiunga kwenye mgomo huu.

2.       Madaktari wawe tayari kupata ongezeko dogo katika  mishahara na mafao mbalimbali wakisubiri STF ije na mapendekezo yake na bajeti mpya. Kiasi gani wakubali inategemea na ofa itakayotolewa na serikali.

3.       Madaktari wawe tayari kurudi kazini mara moja endapo serikali itatenga fedha za dharura kununulia vifaa vya msingi vya huduma ya afya kwa mahospitali yote ya umma. Vitu kama maglovu, sindano, nk ni vitu ambavyo ni lazima viwepo hospitalini. Serikali ikubaliane na madaktari kuwa ndani ya miezi mitatu hospititali zote za umma na za binafsi zitatakiwa kuwa na vifaa vya msingi vya kutolea huduma ya afya. Hii ni pamoja na kutenga fedha za kuhakikisha kuwa hakuna mgonjw anayelala chini kwenye wodi yoyote ile au hospitali yoyote ile. Hii ni mojawapo ya kashfa kubwa za huduma ya afya nchini ni lazima tuondokane nayo.

4.       Madaktari kwa kutumia hiyo STF waandae mapendekezo ya kuboresha elimu na ujuzi wa madaktari ili hatimaye tuweze kupata madaktari wengi zaidi kwa muda mfupi zaidi. Je, nini kinaweza kufanyika kuharakisha mafunzo ya madaktari  yenye ubora wa hali ya juu? Hatuwezi kutumia mfumo wetu wa zamani wa kuandaa madaktari kwani itatuchukua muda mrefu sana kuweza kuziba pengo. Lazima tutumie uwezo wetu kubuni mfumo mzuri wa kufundisha madaktari ili kwa haraka – ikiwezekana ndani ya miaka mitano hivi tuweze kuongeza idadi ya madaktari kwa kiasi kikubwa.

Hayo ni baadhi ya mambo tu yanayoweza kukubaliwa na pande mbili ambayo matokeo yake yatakuwa ni manufaa kwa wananchi. La msingi ni kuwa hatuwezi na hatupaswi kuahirisha huu mgomo kwa vitisho isipokuwa kwa makubaliano. Kuwapa amri madaktari kurudi kazini mara moja ati kwa kufikiria kwamba wasiporudi basi wanafukuzwa kazi na Tanzania italeta madaktari kutoka nje ni kujaribu kukwepa tatizo. Kwanini?

a.       Madaktari wa kigeni hawatakuja kwa kujitolea nao bado watahitaji kulipwa kwani na wenyewe wanatakiwa kuishi maisha ya utu na kufanya kazi mazingira mazuri.

b.      Madaktari mbadala nao wataenda kufanya kazi kwenye mazingira yale yale. Kitakachokuwa kimebadilishwa ni madaktari tu na siyo mazingira ya kazi. Hivyo, wataweza kufanya kazi kwa siku, wiki au mwezi lakini baada ya muda na wao wenyewe watakufanya na yale yale ambayo yametufikisha hapa. Kuleta madaktari wa nje, kutazuia kuvuja kwa damu tu lakini hakutakuwa kumetoa tiba ya kidonda!

c.       Madaktari wetu wenyewe ni madaktari wetu kuwafukuza kazi au kuwaweka nje kwa sababu wamekataa kurudi kazini hakutaondoa ukweli kuwa mfumo wetu wa afya ni mbovu na watu wanakufa pasipo ulazima – bila haja ya mgomo! Madaktari wetu wanagombania kitu kikubwa zaidi hao madaktari mbadala watakuja kutibu tu lakini hawatokuja kupigania kuboresha mfumo wetu wa afya.

d.      Wakileta madaktari wengine halafu wauguzi, madaktari wa meno, madaktari wa dawa ya usingizi nao wakagoma kuunga mkono madaktari wao serikali italeta wauguzi kutoka India, Misri na Israeli? Au mwisho italeta hadi wafagizi kugoka nje?

Kwa ufupi, agizo la Waziri Mkuu kuwa madaktari warudi kazini mara moja bila kufanya nayo makubaliano ni sawasawa na kujaribu kumaliza vita bila kufanya mapatano ya kumaliza mgogoro. Vita havimalizwi kwa truce bali kwa kufanya mapatano ya kumaliza vita (cessation of hostilities). Hili linaweza kufanywa ama kwa kusalimu amri (surrender agreement) ambapo mshindi anatoa terms of surrender (ndivyo inaonekana serikali inafanya) au kwa pande mbili kuona kuwa vita havilipi na hivyo wanaamua kupatana. Ninaamini, serikali inataka kulazimisha surrender bila kupatana. Hii ni hatari kwa huduma ya afya. Ni makubaliano tu yatamaliza mgogoro, makubaliano ambayo yatazingatia madai ya madaktari, yatakubali na kuanza kutekeleza sehemu ya madai hayo kama hatua za kujenga imani na vile vile kuweka utaratibu wa kuona mambo mengine yaliyokubaliwa yanatimizwa bila kuchelewa na katika muda muafaka.

Nje ya hapo, mgomo huu utaduma na hautakoma kwa haraka au kwa vitisho kwani hata madaktari wakikubali kurudi kazini, hakuna mtu anayeweza kuwalazimisha kufanya kazi, na hata wakilazimika kufanya kazi watakuwa wamepewa sababu nyingine ya kufanya mgomo mwingine huko mbeleni. Ndugu zangu, ni bora ujue madaktari wamegoma na wamegoma kuliko kutokujua kuwa daktari anayekuhudumia amegoma moyoni.

Lakini hakuna kibaya zaidi kama kumshambulia mtu badala ya hoja. Katika vitu vya kushangaza sana Waziri Mkuu ameamua kufanya mashambulizi ya mtu – ad hominem – kwa Dr. Ulimboka katika kuonesha kuwa hoja za madaktari hazina msingi. Hivi, ni kweli kuwa Dr. Ulimboka akiacha kushiriki kwenye mgomo huu manake ni kuwa madai ya madaktari yanafutika? Serikali inaweza kabisa kushambulia watu au mtu yeyote katika kujaribu kuonesha kuwa inawajua watu hao na inaweza kuwasema vibaya vyovyote vile lakini ukweli wa hoja zao utasimama ulivyo.

Ukiona watu wanamshambulia mtu badala ya hoja zake, manake ni kuwa tayari wameshindwa hoja sasa wanataka kutumia nguvu! Kama watu wengine wanavyouliza mbona hatujaambiwa mambo ya wabunge ambao wamesimama kutetea posho? Au na yeye watu waanze kuulizia kwanini anatetea wafanyabiashara wakubwa kuchukua maeneo makubwa ya ardhi nchini? Hoja zijibiwa kwe hoja siyo viroja!

Ni hatari kwa wagonjwa.

 

Makala hii imeandaliwa na M. M. Mwanakijiji  

http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/217636-mgomo-wa-madaktari-hautaisha-kwa-vitisho-na-dola%3B-ni-kwa-makubaliano-tu.html
Continue Reading
5 Comments

5 Comments

 1. ANIE

  30/01/2012 at 11:51 am

  ulichokisema juu kinatosha kabisa mheshmiwa pinda aache ku2mia jaziba kuwakandamiza madaktar watu wanaosinzia bungen anaona wanastahil nyongeza hawa wanaokesha na wagonjwa wanaonekana hawastahili Serikali ijue kabisa isipoweka usawa katika secta nyeti inatuangamiza na kujiangamiza yenyewe kwan badala ya kusonga mbele muda mwingi itatumia kutatua migomo, we pinda ingekuwa wewe ni Dkt unashurutishwa kurudi kazin bila kujua nn hatma yako ungekubali,?Tusitumie nafas tulizonazo kuwabana wengine kwan mungu hapend

 2. MAWAZO

  30/01/2012 at 9:57 pm

  Nilimsikiliza Mh. Waziri Mkuu alivyokuwa anajibu madai ya madaktari na alijitahidi kushawishi umma kuwa madai yao mengi yalikuwa ya ubinafsi. Sina shida na hili kama kweli aliyokuwa anatuambuia katika runinga ndiyo wanayodai, hususani HUO MSHAHARA NA MAPOSHO wanayodai! Ambacho sikikupenda katika hoja zake ni pale mwishoni alipoleta ulghai wa hoja (fallacies). Alijikita kutuonesha namana Dr. Ulimboka alivyombaya na hafai ktk jamii na hususani katika fani ya utabibu; kwa kweli hii ni “ad hominem” angejikita zaidi kwenye hoja kuliko kutuonesha kuwa kuyo kiongozi alivyo. Kama ni Kweli wangemdeal kimya kimya.

 3. MAWAZO

  30/01/2012 at 10:25 pm

  MWANAKIJIJI NIMEZIKUBALI HOJA ZAKO. NI VEMA SERIKALI NA MADAKTARI WAKAZIZINGATIA NA KUCHUKUA HATUA ILI KUTUOKOA WANYONGE KWANI KATK VITA HIVI TUTAKAOATHIRIKA NI SISI TUSIOKUWA NA UWEZO WAKWENDA KWENYE HOSPITALI BINAFSI AU KUTIBIWA INDIA. CHONDE CHONDE WAZIRI MKUU NA MADAKITARI.

 4. ELIZABETH

  31/01/2012 at 3:15 pm

  Nakupongeza mwanakijiji kwa jinsi ulivyochambua mada.Nashukuru kwa jinsi ulivyoweka bayana uroho wa viongozi wetu.

  Wao pekee ndio wana haki ya kila kitu mwingine ukidai tu haki yako unasakiziwa dola na vitisho vya kutimuliwa kazi.Na ktk hoja za madaktari kuna kipengele cha huduma mbovu na uwajibikaji mbovu wa viongozi na serikali ktkl huduma za afya kwa wananchi wake hilo hawajalijibia hata kidogo.Wanang’ang’ania tu posho na mishahara tuliyopendekeza kulikoni! Mazingira ya kazi kwa madaktari ni mabovu.

  Mahospitali yamebaki majengo,na watumishi madawa na vifaa tiba hakuna.Hii inapelekea hata watanzania tunaowahudumia wanapata huduma duni hili mheshimiwa mbonna halizungumzii?Na haya tunayodai tupate asilimia kubwa yapo ktk standing order ya serikali wengine serikalini wanapata kwa nini madaktari tu ndio wanyimwe na wakiuliza wanatishiwa je hii ni HAKI kweli??? Mishahara wanaweza waka negotiate lakini haki nyingine wapate madaktari.

 5. moremoney

  31/01/2012 at 7:34 pm

  why the hell should the government care for us, if PINDA fells ill he is immediately taken to india for medication..ironically on tax payers money( our money..) WATANZANIA TUMEZIDI UPOLE ITS TIME TUAMKE AND FIGHT FOR OUT RIGHTS, EVEN IF WE HAVE TO SHED OUR OWN BLOOD

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Featured

UJASUSI: Jinsi kijana wa kiume kutoka New Zealand alivyojaribu  kumuua Malikia Elizabeth II

Published

on

Shirika la Ujasusi la New Zealand  (SIS) limethibitisha kwa mara ya kwanza kwamba kulikuwa na jaribio la kumuua Malikia Elizabeth II wakati alipotembelea jiji la Kusini la Dunedin mwaka 1981.

Jaribio hilo la kumuua Malikia linalodaiwa kutekelezwa na kijana wa kiume limechochea hamasa ya polisi kutaka kujua ni kwa kiasi gani wanausalama hao walifanikiwa kuzima njama hizo.

Taarifa iliyotolewa na SIS  zinaonesha kuwa kijana huyo, Christopher Lewis (17) alipiga risasi kuelekea kwa Malikia wakati akishuka kwenye gari lake ambapo alikuwa anaenda kushuhudia Maonyesho ya Sayansi yaliyofanyika Oktoba 14, 1981 katika jiji hilo. Tukio hilo lilitokea akiwa katika ziara ya siku 8 kutembelea nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.

“Lewis alidhamiria kumuua Malikia, hata hivyo hakuwa katika nafasi nzuri ya kurusha risasi, hata silaha iliyotumia haikuwa katika umbali wa kuweza kumfikia mhusika,” imesema taarifa iliyotumwa SIS kwa vyombo vya habari.

Lewis ambaye anatajwa kwenye taarifa ya ujasusi kama ‘kijana msumbufu’ hakuhukumiwa kwa jaribio la kutaka kuua au kosa la uhaini. Tukio hilo lilifanywa kuwa siri ili kuzuia sifa mbaya kwa nchi (New Zealand) ambayo ilitembelewa na mgeni wa heshima. Badala yake Lewis alihukumiwa kwa kumiliki silaha kinyume na sheria na kufyatua risasi.

                       Malikia Elizabeth II akiwa ameambatana na walinzi wake alipotembelea New Zealand

Inaelezwa kuwa watu waliohudhuria tukio la kuwasili kwa Malikia walisikia mlio wa risasi lakini Polisi waliokuwa wanasimamia usalama katika eneo hilo la Dunedin waliwaambia kuwa ilikuwa ni sauti ya kuanguka kwa kitu au magari kugongana.

“Uchunguzi wa sasa wa polisi juu milio iliyosikika umefanywa kwa umakini na wawakilishi wa vyombo vya habari wamepata mrejesho kuwa kelele zilisababishwa na baruti”, inaeleza ripoti kutoka SIS iliyotolewa mwaka 1981 baada ya kutokea tukio hilo.

Kulingana taarifa za ujasusi zinaeleza kuwa polisi wamekuwa wakifuatilia nyendo za Lewis tangu 1986 ambapo Malikia alitembelea tena New Zealand wakiogopa kuwa anaweza kutekeleza tena uhalifu huo. Kuwekwa wazi kwa siri hiyo kumewaibua polisi ambao wameanza kuchunguza upya kesi hiyo.

Zaidi ya muongo mmoja uliopita, Lewis alihukumiwa kwa mauaji ya mwanamke mmoja katika mji wa Auckland na kumteka mtoto wa kike ambapo baadaye alimtupa karibu na kanisa.

Kulingana na taarifa mbalimbali za wakati huo zinaeleza kuwa Lewis alijidhuru kwa umeme akiwa gerezani mnamo 1997 akisubiri hukumu ya kuua. Lakini alikana mashtaka ya kuua kwa ujumbe mfupi wa kifo (suicide note).

New Zealand ilipata uhuru mwaka 1947 kutoka kwa Uingereza lakini inamuheshimu Malikia kama kiongozi wa taifa. Ameitembelea nchi hiyo kama Malikia mara 10 na mara ya mwisho ilikuwa 2002.

Continue Reading

Featured

FREEDOM HOUSE: Tanzania ina uhuru kiasi, kufungiwa vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya kisiasa kuididimiza kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa

Published

on

Ripoti mpya iliyotolewa na taasisi huru ya Freedom House imesema misingi ya demokrasia ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kukusanyika imeendelea kudhoofika nchini Tanzania na hali hiyo isiporekebishwa itaingia kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa duniani.

Kulingana na  Freedom House  ambao walichambua data katika nchi 195 za ulimwenguni katika mwaka 2017 wamebaini kuwa nchi 88 zina uhuru,  58 zimejumuishwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku 48 zikiwekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa misingi ya demokrasia ikiwemo uchaguzi usio huru na haki, uhuru wa kujieleza umeendelea kushuka kwa mwaka wa 12 mfufululizo duniani kote. Miongoni mwa matokeo yaliyostaajabisha ni kudhoofika kwa  Marekani ambayo ni mama wa demokrasia kutokana na uchunguzi unaofanywa na Mwendesha Mashtaka Maalumu kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 ambao ulimpa ushindi Rais Donald Trump.

Tanzania imewekwa kwenye nchi 88 ambazo zina uhuru kiasi lakini inatahadharishwa kuwa inaweza kuingia kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa. Tahadhari hiyo inatokana na mwenendo wa viongozi wa serikali kufungia vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kushtakiwa kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa tuhuma za uchochezi na kukamatwa kwa wapinzani wa kisiasa ambao wanakosoa na kutoa mawazo yanayotofautiana na serikali.

Pia utekelezaji wa Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 na Sheria ya Makosa ya Mtandao  ya mwaka 2015 umekuwa ukilalamikiwa na wadau wa maendeleo kuwa ni mkakati wa kudhoofisha uhuru wa kutoa maoni, uwazi na uwajibikaji.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini hivi karibuni kilitoa tamko la tathmini ya uchaguzi mdogo wa marudio wa kuchagua madiwani uliofanyika katika kata 43 kwenye mikoa 19 ya Tanzania  Novemba 24 mwaka jana ambapo kilibaini mambo mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Tathmini hiyo iliibua mambo mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya nguvu ya vyombo vya dola, matukio ya watu kutekwa na watu wasiojulikana, watu kupigwa, kujeruhiwa  kwa lengo la kuharibu na kuvuruga uchaguzi  na vilevile kuwatia hofu wapiga kura.

 

Afrika Mashariki hali bado tete

Tanzania inaungana nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya na Uganda ambazo nazo zimewekwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku za Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini zimejumuishwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa.

Awali Uganda ilikuwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa lakini imepanda hadi kwenye uhuru kiasi kwasababu ya  kuimarika kwa tasnia ya habari na utashi wa wanahabari, blogu na  uhuru wa wananchi kutoa maoni yao licha ya mazingira ya kisiasa kuminywa na utawala wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni.

Rais Museveni mwenye umri wa miaka 73 amekuwepo madarakani  tangu 1986 amefanikiwa kubadilisha sheria  ya ukomo wa umri wa miaka 75 wa kugombea urais ambapo atapata fursa ya kugombea tena mwaka 2021. Chaguzi nchini Uganda zimekuwa zikitawaliwa na vurugu za polisi na wananchi, kuzimwa kwa intaneti na kuwekwa kizuizini kwa viongozi wa upinzani ikiwemo Kizza Besigye wa chama cha Forum for Democratic Change.

Kwa upande wa Kenya ambayo imekuwa ikisifika kwa kuimarisha misingi ya demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo kwa mara ya kwanza mahakama ilifanikiwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Urais yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta uliofanyika Agosti 2018. Uchaguzi ulirudiwa na Rais Kenyatta alichaguliwa tena.

Marudio ya uchaguzi yalilamikiwa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa hayakuzingatia haki za binadamu ambapo watu ambao walipinga uchaguzi huo walikumbana na mkono wa dola. Matendo hayo ndiyo yaliiweka Kenya kwenye kundi la nchi zilizo na uhuru kiasi.

Burundi na Sudan Kusini zimewekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa kutokana na mapigano ya kikabila ambayo yamedhoofisha mfumo wa kisiasa wa kuongoza nchi. Vyombo vya habari na wananchi wanaotoa maoni tofauti na serikali wamekuwa wakiteswa, kufungwa na kuuwawa.

Chanzo: Freedom House           – Nchi zisizo na  uhuru  – Nchi zenye uhuru     – nchi zenye uhuru kiasi   

 

Hali ilivyo Afrika

Afrika kama zilivyo nchi za Afrika Mashariki hali ya demokrasia siyo ya kuridhisha ikizingatiwa kuwa asilimia 11 ya wakazi wapatao bilioni 1.02 wa bara hilo ndio wana uhuru wa kweli, huku 52% wana uhuru kiasi na 37% hawa uhuru kabisa.

Ripoti ya Freedom House inaeleza kuwa waliangazia nchi 49 za Afrika na kugundua kuwa nchi 8 (18%) ndio zina uhuru wa kweli, nchi 22 (43%) zina uhuru kiasi na 19 (39%) hazina uhuru kabisa. Nchi zinazotajwa kuwa na uhuru ni Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Ghana, Togo, Senegal na Kisiwa cha Sao Tome.

 Sababu ya nchi nyingi za Afrika kuwepo kwenye kundi la zisizo na uhuru ni matokeo ya viongozi kukaa madarakani muda mrefu, vurugu za kisiasa na kikabila ambazo zimekuwa zikihatarisha haki za binadamu.

 

Demokrasia ya Dunia

Demokrasia ya dunia inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kisiasa kuliko wakati mwingine ambapo mwaka 2017 ulishuhudia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo kuminywa kwa  uchaguzi huru na kweli, haki za watu wachache, uhuru wa kujieleza, utawala wa sheria.

Nchi 71 kati ya 195 zimeshuhudiwa zikiteteleka katika kulinda haki za kisiasa na jamii ambapo ni nchi 35 tu ndizo zimeweza kulinda haki hizo. Kudhoofika kwa demokrasia kunaendelea kushuka kwa miaka 12 mfululizo na hatua muhimu zisipochukuliwa amani ya dunia itawekwa rehani.

Marekani ambayo ni bingwa wa demokrasia duniani nayo imeripotiwa na taasisi ya Freedom House kudhoofika katika kulinda haki za kisiasa na kijamii na kuzua mgongano wa mawazo miongoni mwa nchi zinazoibukia katika kujenga demokrasia ya dunia.

Tangu kuisha kwa vita baridi, nchi nyingi ziliachana na utawala wa kiimla na kugeukia demokrasia ya vyama vingi lakini hali hiyo imeanza kujitokeza tena ambapo idadi ya viongozi wanaoongoza kwa udikteta inaongezeka.

 

Uhuru wa nchi moja unategemea uhuru wa nchi zote

Demokrasia itabaki kuwa tunu muhimu kwa jamii zilizostaarabika, ikifungua milango ya uwazi, mawazo na fursa mpya na zaidi ya yote kulinda uhuru wa mtu mmoja mmoja. Ikiwa watu duniani kote wanadai mazingira mazuri ya kisiasa ni dhahiri wanakumbatia misingi ya demokrasia: uchaguzi huru, uhuru wa kujieleza, uwazi na uwajibikaji wa serikali, utawala wa sheria ambao hauingiliwi na polisi, jeshi au taasisi nyingine za nchi.

Hata hivyo, Karne ya 21 imeshuhudia ugumu wa kuifanya demokrasia kuwa endelevu ambapo baadhi ya nchi zinatekeleza lakini zingine zinapuuza. Utawala wa kidekteta wa Urusi na China unatambua wazi ili uendelee kuwepo unahitaji kuimarisha demokrasia katika nchi nyingine ili ziendelee kufaidika na mahusiano ya kidiplomasia. Ukuaji wa  demokrasia ni kulinda haki za watu wote duniani kupitia utandawazi   

Continue Reading

Afya

Is Tanzania’s Adolescent Fertility Rate Three Times Higher Than Global Counterparts?

Published

on

The Comprehensive Community-Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT), an organization ​which works to provide affordable medical and rehabilitative services for mothers and newborns throughout Dar-es-Salaam, marked World Contraception Day on September 26 with a call for more efforts to meet the reproductive health needs of teens between 15 and 19 years old.

The report highlights a worrying statistic — Tanzania’s adolescents are having almost three times as many children on average as their global counterparts, with 135 births per 1000 girls reported in the country, compared to an average of 44 per 1000 girls aged 15–19 worldwide in 2015.

CCRBT attributes the high adolescent fertility rate to a lack of access to contraceptive services, with Technical Advisor for Nursing Bola Abbas saying, that only about 8 per cent of current family planning clients are between the ages of 15 to 19.

On a national scale, Abbas explains, demand for family planning among adolescent girls is still very low, with only one out of every three of those who are sexually active within the 15 to 19 age group using modern contraceptive methods.

So the question is, how does Tanzania’s adolescent fertility rate compare to that of the rest of the world?

Pesacheck investigated the claim that Tanzanian adolescents are having three times as many children as their peers in the rest of the world and found that the statement is TRUE for the following reasons:

Tanzania’s adolescent fertility numbers are rather high, with 4.4% of girls aged 15 having given birth according to the country’s Demographic and Health Survey.

The Sustainable Development Goals call for countries to ensure universal access to sexual and reproductive healthcare services, including family planning, information and education, and the integration of reproductive health into national strategies and programmes by 2030.

The indicators for this goal are the proportion of women of reproductive age (15–49 years) who have their need for family planning satisfied with modern methods, and the adolescent birth rate (10–14 years and 15–19 years) per 1,000 women in that age group.

For several sub-Saharan countries, Tanzania included, access to modern family planning methods is low for this particular age group, and as a result, the regional average is 105 births per 1,000, which is more than double the global average.

Tanzania’s National Bureau of Statistics produced a national fertility and nuptiality report based on data from the 2012 national census, which shows that Adolescent Fertility Rate (AFR) was 81 births per 1,000 women aged 15–19.

The report further shows that in 2012, 23.3% of adolescent girls in the country had given birth to at least one child. Additionally, 42.2% of girls who had never attended school had given birth, compared to just 9% of those who had reached university.

This shows that there is a need for contraceptive access for teenage girls in Tanzania, especially for girls in rural areas and those with limited access to education.

The Tanzania Demographic and Health Survey 2015–16 indicates that 27% of girls aged 15–19 have given birth. Crude birth rates for girls aged 15–19 show that there 135 births per 1,000 girls in Mainland Tanzania and 132 per 1,000 girls in Zanzibar, way above the global average of 44. The data also shows that contraceptive access for this age group is also quite low, with 10.4% of girls aged 15–49 using any form of contraception.

It would therefore appear that the lack of access to contraceptives is contributing to the increased likelihood of adolescent girls getting pregnant.

So the claim by CCBRT that Tanzania’s adolescent fertility rate is almost three times the global average is TRUE. This is driven largely by a lack of access to contraceptives for young people in the 15–19 age group, and the relatively high levels of poverty that have driven many out of school and into early marriage.

As a result, the country is unlikely to meet the Sustainable Development Goal of overall good health and wellbeing of mothers unless it puts measures in place to ensure universal access to sexual and reproductive health-care services for girls and women of all ages.

Do you want us to fact-check something a politician or other public figure has said about public finances? Complete this form, or reach out to us on any of the contacts below, and we’ll help ensure you’re not getting bamboozled.

This report was written by PesaCheck Fellow Belinda Japhet, a Communications Consultant, Online Editor based in Tanzania. The infographics are by PesaCheck Fellow Brian Wachanga, who is a Kenyan civic technologist interested in data visualisation. This report was edited by PesaCheck Managing Editor Eric Mugendi.

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com