Connect with us

Siasa

Lowassa aliteka Bunge; kusafisha njia ya Urais 2015?

Published

on

edward lowassaKUCHAGULIWA kwa Edward Lowassa, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond/Dowans, kuwa Mwenyekiti wa Kamati nzito ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, kumethibitisha nguvu kubwa aliyonayo mwanasiasa huyo kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Wachammbuzi mbalimbali katika mtandao maarufu wa JamiiForums na mitandao mingine ya kijamii kama FaceBook na Twitter, wameelezea uamuzi huo wa wabunge wa kumpa madaraka Lowassa na wabunge wengine ambao ni maswahiba zake, ni hatua muhimu kuelekea 2015.

Mmoja wa wachambuzi hao, ‘Fareed’ yeye ameanika wazi kwamba uamuzi huo wa wabunge umetoa nafasi kubwa kwa mafisadi ambao sasa watafanya watakavyo ndani ya Bunge.

Fareed yeye anatoa sababu zifuatazo;

1. Anajitengenezea CV ya kuwa mgombea Urais wa CCM 2015. Moja ya vigezo vikubwa vya CCM ni mgombea wa Urais kuwa na uzoefu wa mambo ya nje. Hapa Lowassa anajipatia CV hiyo kupitia kamati hii ya Bunge.

2. Akiwa mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje, ulinzi na usalama, atakuwa anapata security briefings (taarifa za usalama) na issue zote nyeti, kama Meremeta, rada, Kagoda, usalama wa taifa, Takukuru, polisi, jeshi, nk, vinapitia kwake. Anakuwa na powers ku-summon wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama hapa nchini.

3. Anapata meno ya kumshuhulikia adui wake mkuu kwenye mbio za urais, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, kwani kamati ya mambo ya nje ndiyo inayosimamia wizara ya Membe. Pia Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, naye anakuwa anasimamiwa na kamati hiyo ya Lowassa.

4. Mpambe wa Lowassa, Peter Serukamba, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu ili awashuhulikie kina John Magufuli na Dk. Harisson Mwakyembe wa wizara ya ujenzi.

5. Mpambe mwingine wa Lowassa na Rostam Aziz, January Makamba, amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini ili amfukuze kazi Ngeleja na kumuweka waziri wao mwingine na azime issue za Dowans/Richmond.

6. Zitto Kabwe, ambaye ni mtu wa kina Rostam kabaki kamati ya mashirika ya umma kama kanyaboya. Kamati za PAC na local government wamepewa TLP na UDP ambao ni vibaraka wa CCM kama CUF.

Lowassa, January na Serukamba na wapambe wao wa kamati za upinzani (Zitto, Augustino Mrema, John Cheyo) wanaingia kwenye kamati ya uongozi wa Bunge wakiwa wenyeviti wa kamati za Bunge. Watakuwa na majority vote kwenye kamati ya uongozi wa Bunge. Hii ina maana kuwa watakuwa wana uwezo wa kuamua moja kwa moja shuhuli za Bunge, kanuni, miswada, mwenendo na hoja mbali mbali za Bunge.

Spika Anne Makinda aliyehakikisha kina Lowassa, January, Serukamba na wengine wanapita kuwa kwenye kamati hizi anatajwa kuwa anapokea maelekezo ya Rostam Aziz anayetajwa kuwa ndiye aliyemuweka kuwa Spika. Amewateuwa wajumbe wachovu kwenye kwenye kamati hizi ili watu hawa wakamate uongozi wake.

Mchambuzi mwingine anayejiita ‘Kagemro’ alikua na haya ya kusema:

Kutokana na mambo ambayo leo yametokea mjini Dododma ni dhahiri kuwa kumekuwa na mapinduzi ya wazi ya kuliteka Bunge letu na kuanzia sasa litakuwa halina nguvu tena za kuwawajibisha mafisadi wala hakutakuwa na mtu wa kuzungumza lolote juu ya Mafisadi na ufisadi.

Nayasema haya kutokana na mambo yafuatayo;

1.       Uchaguzi wa wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge ni kama ifuatavyo;

(i)      Mwenyekiti wa kamati ya fedha na uchumi ni Abdallah Kigoda

(ii)    Mwenyekiti wa kamati ya katiba ,sheria na utawala ni Pindi Chana

(iii)   Mwenyekiti wa kamati ya mambo ya nje, ulinzi na usalama ni Edward Nyoyai Lowassa

(iv)  Mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ni Magreth Sitta

(v)    Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya jamii ni Jenista Mhagama

(vi)  Mwenyekiti wa kamati ya ardhi, maliasili na mazingira ni ………….

(vii) Mwenyekiti wa kamati ya kilimo,mifugo na maji ni Prof.David Mwakyusa

(viii) Mwenyekiti wa kamati ya Miundombinu ni Peter Serukamba.

(ix)  Mwenyekiti kamati ya hesabu za za serikali za mitaa ni Augustino Mrema.

(x)  Mwenyekiti wa kamati ya hesabu za mashirika ya umma ni Zitto Kabwe

(xi) Mwenyekiti wa kamati ya heswabu za serikali ni John Momose Cheyo.

(xii) Mwenyekiti wa kamati ya viwanda na Biashara ni Mahamoud

(xiii)  Mwenyekiti wa kamati ya nishati na madini ni January Makamba.

Baada ya kuwaangalia wenyeviti hao ni kuwa kamati ya uongozi ya Bunge huwa ina wajumbe ambao ni wenyeviti wote kamati za kudumu pamoja na wafuatao;

(i)   Spika –Anne Makinda

(ii)  Naibu Spika- Job Ndugai

(iii)  Kiongozi waUpinzani- Freeman Mbowe.

(iv)  Mwanasheria Mkuu wa Serikali- Fredrick Werema

(v)  Waziri wa Nchi Bunge na uratibu- Willium Lukuvi.

Hivyo basi utaona kuwa kamati ya uongozi ya Bunge ambayo ina wajumbe 18 .

Kazi za kamati ya uongozi ya Bunge ni;

(i)  Kuendesha bunge siku hadi siku

(ii) Kuamua ni hoja gani zipelekwe Bungeni kujadiliwa

(iii) Kuamua nini kifanywe na Bunge na nini kisifanywe na Spika huwa ni msemaji wake wakishaamua.

Hivyo basi kati ya wajumbe 18 wa kamati ya uongozi ambayo kimsingi ndio Bunge lenyewe utaona kuwa Edward Lowassa amejigeuza na kuwa yeye ndiiye atakuwa anafanya maamuzi yote ndani ya Bunge na kuamua lipi lifanyike na lipi lisifanyike kwani wajumbe 13 wanamuunga mkono yeye ama ni watu wake. hao ni pamoja na ;

(i)      Lowassa

(ii)    Cheyo

(iii)   Serukamba

(iv)  January

(v)    Pindi Chana

(vi)  Jenister

(vii) Mrema

(viii) Zitto

(ix)  Makinda

(x)    Ndugai

(xi)  Lukuvi

(xii) Werema

(xiii)  Mahamoud (mbunge wa Kilwa Kasikazini)

Hivyo utaona jinsi Bunge lilivyotekwa.

Lowassa sasa ataweza kufanya yafuatayo;

(i)      Kumuita Membe na kumpa maelekezo ya kibunge

(ii)    Kumuita Sitta na kumpa maelekezo

(iii)   Kuita upya hoja ya Richmond kupitia January

(iv)  Kumuita Magufuli na Mwakyembe kupitia Serukamba

(v)    Kumuita IGP, DG-TIS kumpa briefing kama mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama.

Hivyo hii inaonyesha kuwa tutakuwa na Bunge la kumi la aina gani.

Yafaa kila mmoja akatafakari na kuchukua hatua nini kifuate baada ya hapo!

Continue Reading
20 Comments

20 Comments

 1. Msanii

  10/02/2011 at 7:45 am

  Sisi wananchi ambao tunapenda kuangalia sinema kama hizi bila kuzingatia madhara yake ndio wa kulaumiwa.
  Hatuwezi kuwa reasonable thinkers endapo Taifa linachezewa na kuvuliwa nguo mbele yetu bila kuchukua hatua.
  Sisi ndio tuliowachagua wabunge, sisi ndio tuliochagua rais na kadhalika. Ni sisi tunaoweza kuwawajibisha endapo vyombo tulivyoviunda kwa mujibu wa katiba vitasita kufanya hivyo.
  Tuendelee kuangalia senema na mwisho wa siku sterling atatoka kwenye screen na kutufanyia actions za kweli tukabaki tunashangaa.

 2. Ndonje

  10/02/2011 at 9:05 am

  Ombi langu kwa wabunge waachane na mambo ya kuendeleza kambi zao, huu sio wakati wake,waangalie taifa lilipofikia wajenge upya taifa bila kujali itikadi zao za vyama. Kwa sasa kuna shida nyingi zinazomgusa karibu kila mtanzania wa kawaida. umeme wa mgao, njaa hasa vijijini, nchi kudaiwa mabilioni na wtu binafsi ambao inasemekana ni watanzania wasio na uzalendo nk. hivyo kuondoa haya WABUNGE WASHIKAMANE.

 3. Alfred

  13/02/2011 at 11:03 pm

  Yani kwisha habari.game is over.lowassa is winner.salute rostam.hawa jamaa ni worse

 4. Angelo

  14/02/2011 at 12:39 am

  hii inaonesha wazi kuwa ukombozi wa nchi hii sasa upo mikononi mwa waTanzania wenyewe si katika chama tawala.. naona hawa jamaa wanatuchezea mchezo wa madange.. kwa nini Watanzani atunaendelea kuwa hivi jamani?? hivi inawezekanaje kuwa mtu aliyejiuzulu nafasi ya uwaziri mkuu leo awe kiongozi tena jamani tuwe wawazi:: inawezekanaje hii lakini watanzania kwanini tunawaacha hawa wezi waendelee kutuibia nasi tupo macho… tunataka malaika wa Mungu ndo ashuke ashike hatamu?? no way ni lazima sisi watanzania tafadhali tuamue kama walivyofanya wa Misri kwa kweli lazima kikwete atoke madarakani!!! anajua sisi hatukukmchagua na hivyo yote anayofanya anafanya kwa ajili ya mafisadi wachache!! tumtoe Mshezi huyu jamani kabla nchi yetu haijageuka mahame!! hawezi kuongoza huyu hana sifa hana uwezo mwoga na mjinga hawezi kupambanua mambo hana sauti anaburuzwa tu NI KIBARAKA!!!!!

 5. Mafichoni

  14/02/2011 at 10:18 am

  Yetu macho,tuone basi hiyo 2015,uwepo wa katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi itawezekana?.ladba kwa sabuni ya chuma itawezekana kujisafisha

  • mbunda

   14/09/2011 at 11:40 pm

   TANZANIA KUSHNEI, SERIKALI INAONJESHWA CHATNEY NA KULISHWA PUTNEYH.

   MWAJAMENI TUGAWANE VYAKWETU KILA MTU AFE NA CHAKE..MAANA TUNAVISHWA MIWANI ZA CHUMA SASA.

 6. BARAKA DANIEL

  16/02/2011 at 7:44 pm

  JAMANI WADAU CHA MSINGI NI KUJIEPUSHA NA HII CCM KWANI HAITUFAIDISHI CHOCHOTE ZAIDI YA KUTUNYONYA LASILIMALI ZETU JAMANI HEBU FIKILIENI NI MIAKA MINGAPI CCM IMEONGOZA NCHI HII LAKN CHA AJABU NA CHA KUSHANGAZA CHADEMA IMECHUKUA JIJI LA MWANZA JUZI TU MACHINGA TUMERUHUSIWA KUFANYA BIASHARA BILA YA BUGDHA JE TUKIIPA NCHI NZIMA SI MABOMBA YATATOA MAZIWA JAMANI TUSIFANYE KOSA TENA WAPEDWA……CHECK OUT +255766201280

 7. Felix

  22/02/2011 at 9:45 am

  Fundisho tunalo tumeona yaliyotokea Algeria,Misri ,Libya Gagaffi kajificha hajulikani halipo,Sudan Omari Bashir kaanza kujisalimisha kwa umma.Tumeona sera mbovu za CCM shule za kata zimefelisha kwa 51%,WAMESHNDWA KUTENGENEZA AJIRA KWA WAHITIMU WA VYUO VIKUU NCHINI,Vyombo vya usalama vinafanya siasa badala ya kazi,Mafisadi wanakula bata wakitumia utajiri wetu.Nin kifanyike kuondoa hii kero ya udalali na utapeli kama Dowans,Deep Green Finance,KAGODA na Meremeta moja ni kuishinikiza serikali ijiuzulu nyingine ni kuwafungashia virago kwa kutowapa kura uchaguzi ujao 2015 pamoja na vyama vya upinzani ambao ni vibaraka waoHila za kuwazuia tena wanavyuo kutopiga kura haitowezekana

 8. GERVAS MASHINJI

  26/02/2011 at 12:28 pm

  Akigombea Lowassa urais wajue ccm imekufa kifo cha mende na ci cha membe fisadi aliyejiuzuru kwa ufisadi aje kuongoza nchi? Tanzania kweli imekuwa nchi ya maigizo kwa viongozi wetu 2015 hatutachagua chama bali ni mtu mwenye mapenzi ya kweli kwa nchi yake si CCM wala CHADEMA bali ni yeyote mwenye mapenzi ya kweli kwa watanzania. lakni watanzania ni muda mwafaka kutambua kuwa tulie mchagua awmu zote hizi mbili ndie aliyechafua nchi yetu LOWASSA kaa chini tulikuonaa bado hatujasahau mambo uliyotufanyia watanzania wenzako mwisho (JK NCHI HII SI YA KULITHISHANA MAFISADI KWA MAFISADI,UFISADI WAKO UISHIE AWMU YAKO TUACHE WATANZANIA TUANZE KULIKAVA)

 9. jojo ralph

  20/05/2011 at 12:15 pm

  Watanzania tumekuwa tunafata mkumbo wa kifikara, wengi tumekuwa tukimuhukumu Lowasa bila kujua kuwa nini kafanya, Tumebakia na neno FISADI tu. Lowasa katumiwa na wana mtandao kama mbuzi wa kafara, Hivi hakuna hata jambo moja JEMA ambalo huyu Lowasa kafanya? hebu tuwe waungwana kidogo. Mimi siyo CCM wala sijawahi kuwa, ila sipendi kufata mtazamo kwa mkumbo.

 10. JMSKIPPER

  21/05/2011 at 8:34 pm

  Jojo naungana na wewe kabisa, tumekuwa tukimlaumu Lowasa kwa kiwango kikubwa wakati wahusika wakubwa wameachwa pembeni. Lowasa ameendelea kunyanyaswa, sasa kama hizo tuhuma zipo wabunge si waliongelee bungeni na apelekwe mahakamani kwa nini wanapiga tu kelele kuwa ni fisadi au kisa anaonekana akigombea atawasumbua wapinzani kwenye kinyang’anyiro?

 11. PRINCE

  26/05/2011 at 12:23 pm

  Nashindwa kuelewa kwanini ufisadi wa lowasa umekuwa ni wa vyombo vya habari na hata cku moja sheria haichukui mkondo wake, Au no kusema yeye ni juu ya sheria? Lazima tuliangalie na pia tuwe tunaongea tukiwa na takwim la sivyo tutakuwa tunapotosha jamii. Binafsi namkubali lowasa kama mtendaji na naamini tungekuwa na mawaziri kama yeye tungekuwa mbali.
  NI MTAZAMO TU WANA JAMII

 12. hugo chaves

  26/05/2011 at 5:10 pm

  Tujiulize kwanini mwalim nyerere alimkataa huyu bwana .kushika nyadhifa nzito serikalini .sababu hizo zinatia mashaka miongoni mwa watanzania na zitatumika 2015 kupunguza kura zake pamoja na network nzuri kazi ya ziada inahitjika .Hakuna mtu mwingine ambaye hagharimu chama kumsafisha hadi akubalike? ATAFUTWE mtu hata kama yupo nje ya chama maadam anakubalika na watu wote sawa.apitishwe

  • Mkalachaka

   13/06/2011 at 9:03 am

   Kazi kubwa tunayo kama watanzania, tuamke tufikiri nini la kufanya huko mbele ya safari yaani kabla ya hiyo 2015 vinginevyo tutakuwa hatuna pa kukimbilia!!

 13. Ntare

  16/06/2011 at 7:48 pm

  Huo ni mtazamo wa mwandishi kuwa Lowassa ameliteka bunge.Lakini ninamtazamo toafauti na siasa za nchi yetu na tukubaliane kuwa Tanzania si kiwanja kizuri cha kuchezea mchezo wa siasa.Leo hii CCM wanataka kutuaminisha kuwa Lowassa amekichafua chama mbele ya wapiga kura na ndio maana wana hasira mpaka kura za mh. JK zilipungua ukilinganisha na mwaka 2005.Nasema hivi si kweli ufisadi wa kimfumo ueitafuna serikali ya CCM hata kabla ya JK kutinga ikulu so tatizo si Lowassa.Na nafikiri huyu jamaa kwa uchapakazi wake anastahili tumpe nchi 2005 tusubiri tuone naamini atavuka vikwazo vyote

 14. Francis Samuel

  24/06/2011 at 12:25 pm

  Hata mimi naona kuwa ana chokitaka huyu jamaa nikutaka kuwania urais 2015 lakini cha kujiuliza ata weza kuushinda uma huu ulio elimika sana

 15. alfred andrew

  23/07/2011 at 9:00 pm

  Ki2 ki1 nafahamu, kwamba; whether they like or not, they have already planted the seed of their own destruction. they made a great mistake to their survival. we, patriots, lets never give up fighting for our future excellency. hey guys, I need every tanzanian to understand this thing, that, changes are not necessary as fast as you may thought. Let us be patient to work on things which the fruit are anticipated with our grandchildren. it is bare truth that hawajui kwamba iko cku nchi hii itakuwa chini ya utawala wa wengine nje ya sisiem. The development of any nation in the world depends upon the exisxtence of creative leaders and uncorruptible one. under the ground of corruption the contry will remain poor. I’ve a single suggestion to Tanzanians that, Let us make trials and errors, I mean let us try to give chance to the oppositional party and I’m sure the devevlopment of our country won’t remin slagish as it is now. I hate the fraud ad corruptible leaders.

 16. Maliwe

  12/08/2011 at 1:49 am

  Salaam wanajamii,
  Yote nilyosoma hapo juu nilichogundua mambo mawili labda watu hawaijui siasa ya nchi yetu au kuna ushabiki wa kimaslahi,kwa kuweka sawa watanzania hatuna uzalendo iwapo uzalenndo utakuwepo hapa kwetu Tanzania kuanzia watu wa chini mpaka wa juu nawaakikishieni nchi hii itakuwa kijani kitupu nikiwa namaana itastawi,maneno haya nitafakari tosha,kwa kumalizia wasiomjua lowasa nawaambieni mtu huyu ni nguzo na akishika nchi hii pale bungeni na mitaani WAPINZANI watakosa la kusema maana kila idara itasafishika.AMINI nichosema

  • julie

   26/08/2011 at 2:19 pm

   well said maliwe!!

   Lowassa ataigeuza hii nchi na kuwa ya kisomi na maendeleo

   mark my words!!

 17. Joshua G

  27/08/2011 at 5:40 pm

  watz sisi wavivu,kutenda na kila kitu,naona sasa hata kufikiri tu wavivu.kila mtu anahaki ya kutoa mawazo na kusikilizwa, ila baadhi ya mawazo ukiyasoma unashangaa.unashindwa kujua kwamba jamaa ni mjinga au mpumbavu,cheo kinakuwa kigumu kumpa labda ukiwaunamsikiliza anawezajua ndicho kitokacho ubongoni au amepindisha tu maneno na yameanzia tu mdomoni ili apate ulaji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Siasa

Sakata la waraka wa Maaskofu KKKT lang’oka na Msajili Mambo ya Ndani

Published

on

Waziri wa Mambo ya Ndani Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii, Merlin Komba ili kupisha uchunguzi wa barua iliyoandikwa ukilitaka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kufuta waraka ilioutoa Machi mwaka huu.

Barua iisambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikiitaka KKKT kuufuta waraka wa Pasaka uliotolewa Machi 24 mwaka huu vinginevyo hatua kali za sheria zitachukuliwa dhidi ya kanisa hilo.

Waraka huo uliopewa jina la ‘Taifa letu amani yetu’ ulisainiwa na maaskofu 27 wa kanisa hilo. Ulijikita kujadili masuala ya jamii, uchumi, siasa, katiba mpya na matukio ambayo yako kinyume na kile lilichokiita tunu na misingi ya Taifa.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Waziri Nchemba amesema Serikali haipingani na dhehebu lolote na pale ambapo kuna uhitaji wa kufanyia kazi jambo kuhusu taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo taratibu huwa zinatumika kuzungumza na sio kama ilivyofanywa taarifa hiyo inayosambaa.

“Serikali inalinda uhuru wa kuabudu na waumini hivyo huo waraka una maudhui kama matatu, ni barua batili na tunaendelea kuchunguza kama imetengenezwa basi imetengenezwaje, kwani haujapita kwetu.” amesema Waziri Mwigulu.

Kutokana na msimamo huo wa serikali, Waziri Nchemba, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii, Merlin Komba, kupisha uchunguzi wa barua iliyoandikwa kwa maaskofu wa KKKT.

“Hivyo basi, namsimamisha Msajili wa hizo taasisi kupisha uchunguzi na ikithibitika ni za Wizara tuweze kujua maana jambo hilo halijapita kwa Waziri, Katibu Mkuu na wala si maelekezo ya serikali,” amesema.

Hata hivyo, amewatoa hofu viongozi wa dini kutokana na sakata hilo na kuwataka waendelee na majukumu yao huku ikitahadharisha jamii kuwa makini na taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Tunawaomba viongozi wa dini waendelee na kazi zao, nasema jamii iwe macho na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya jamii na wasifanyie kazi taarifa hizo. Viongozi wa dini wasiwe na taharuki na taarifa hizo, hazina baraka za Serikali na wasisite kuwasiliana na Serikali kujua uhalali wake,” amesema.

Waziri Nchemba amesema waraka wa viongozi wa dini uliotolewa miezi iliyopita ni jambo lililopita na hakukuwa na haja ya kuendeleza malumbano yasiyo na tija kwenye jamii.

Katika waraka wa ujumbe wa pasaka uliosomwa katika makanisa ya Kilutheri kote nchini Tanzania na kusambaa katika mitandao ya kijamii, baraza hilo limeorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi hiyo.

Utekwaji wa watu wa hivi karibuni, utesaji, kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa, muaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi ni baadhi tu ya mambo yaliyotajwa katika waraka huo.

Lakini pia Watanzania wamekuwa na hisia tofauti kuhusu viongozi wa dini kuzungumzia hali ya kisiasa nchini. Waraka wa KKKT ulikuja mwezi mmoja baada ya ule wa maaskofu wa kanisa katoliki ambao nao ulionya juu ya kuminywa kwa haki ya kufanya shughuli za kisiasa kama mikutano ya hadhara na maandamano.

Baada ya nyaraka hizo mbili kutolewa na Maaskofu, baadhi ya mambo yaliyokuwa yakilalamikiwa yalipata ufumbuzi ikiwemo kupungua kwa mauaji na uteswaji wa raia kulikuwa kunafanywa na watu wasiojulikana.

Continue Reading

Jamii

Waziri Mkuu Majaliwa: Hatutangazi nyongeza ya mshahara hadharani kuepusha athari kwa jamii

Published

on

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameweka wazi kuwa serikali haitatangaza nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma hadharani ili kuepusha athari kwa jamii ikiwemo kupanda kwa bei ya bidhaa.

Akizungumza leo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu (CHADEMA), Susan Lymo ambaye alitaka kufahamu kwanini Serikali imewanyima au imeshindwa kuwalipa watumishi wa umma nyongeza ya mishahara ambayo ni haki yao ya msingi kulingana na miaka waliyokaa kazini.

Akijibu swali la Mbunge huyo, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali ina utaratibu wa kutoa nyongeza ya mishahara kwa watumishi wake lakini haitangazi kwa wananchi wote kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwenye sherehe za wafanyakazi za Mei Mosi kila mwaka.

Amesema Serikali ikitangaza mishahara hadharani inaweza kusababisha usumbufu kwa watu wasio watumishi wa umma na inaweza kupandisha bei ya bidhaa na kuathiri mwenendo wa mahitaji ya wananchi sokoni.

Nyongeza za mishahara ambazo zinatangazwa hadharani, mara nyingi zina athari yake sio kwamba Serikali haikusudii kutoa nyongeza ya mshahara kwa mwaka, lakini unapotumia Mei Mosi kutangaza nyongeza ya mshahara unaleta athari kwenye jamii kwasababu vitu vinaweza vikapanda bei, vikawasumbua hata na wananchi ambao hawalipwi mshahara,” amesema Waziri Mkuu.

Amebainisha kuwa siyo lazima Serikali itangaze hadharani kila inapoongeza mishahara kwa watumishi wa umma lakini ifahamike kuwa Serikali ina utaratibu wake mzuri wa kuboresha stahiki za wafanyakazi wake kila mwaka.

Suala la nyongeza ya mishahara liko Serikalini na Mhe Rais ameishawahakikishia wafanyakazi atawaongeza mishahara na sio lazima litangazwe hadharani. Mshahara ni suala la mtu binafsi hata ukiongezwa leo kuwa tumeitangaza leo tumeongeza mshahara kwa kiwango hiki. Ukifanya hivi tayari umeleta kupanda kwa gharama’” amebainisha Waziri Mkuu.

Ameongeza kuwa mkakati wa Serikali ni kupunguza gharama za mahitaji kwenye masoko ili kuzuia mfuko wa bei za bidhaa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu Mjaliwa amesema Serikali inaendelea kufanya sensa ya watumishi wote nchi nzima na zoezi hilo likikamilika itaboresha nyongeza ya mwaka, nyongeza ya mishahara na upandishaji wa madaraja.

Awali katika swali lake, Mbunge Lyima amesema Serikali inakiuka Sheria ya Utumishi wa Umma ya kuwapatia watumishi stahiki zao na kuwapunguzia motisha ya kufanya kazi kwa ufanisi katika maeneo yao ya kazi na kuathiri mafao baada ya kustaafu.

Hoja ya Mbunge huyo ni muendelezo wa malalamiko ya watumishi dhidi ya Serikali kwamba hawajapata stahiki zao tangu ilipoanza zoezi la ukakiki wa watumishi wa umma mwaka 2015. Katika zoezi hilo watumishi zaidi ya 9,000 walibainika kutokukidhi vigezo vya utumishi na hivyo kuondolewa kazini.

Huenda kauli aliyoitoa Waziri Mkuu leo Bungeni inaweza ikatofautiana na ile ya Rais John Magufuli aliyoitoa wakati wa sherehe za Mei Mosi, 2018 mijini Iringa ambapo alinukuliwa akisema hawezi kutoa nyongeza ya mishahara akidai Serikali haina fedha.

Kwangu mimi ninafikiria hizi pesa tunazotoa kwa ajili ya elimu bure ni nzuri kuliko fedha hizo kuzipeleka kuongezea mishahara, naona bora kuwapa mikopo wanafunzi wa vyuo vikuu kuliko kuongezea wafanyakazi mishahara,

Nikisema nitaongeza hizo pesa mimi nitazitoa wapi? naogopa kusema uongo. Hata mimi napenda kupandishiwa mshahara lakini kwa hali halisi ya sasa hivi lazima niwaeleze ukweli,” alinukuliwa Rais Magufuli.

Hata hivyo alibainisha kuwa kabla ya kuondoka madarakani ataboresha maslahi ya wafanyakazi wa umma, “Nawaahidi, kipindi changu cha urais hakitaisha kabla sijapandisha mishahara kwa wafanyakazi, kupandisha kwangu haitakuwa kwa shilingi elfu kumi, itakuwa ni kupandisha kwelikwel.”

Continue Reading

Jamii

Maaskofu KKKT wapewa siku 10 kufuta waraka

Published

on

Serikali imetoa siku 10 kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), kuufuta kwa maandishi waraka wao waliotuoa Machi 24 mwaka huu na kisha kuujulisha Umma kwa njia mbalimbali walizotumia kuusambaza.

Kanisa la KKKT kupitia Baraza lake la Maaskofu lilitoa waraka uliopewa jina la ‘Taifa Letu Amani Yetu’ wakati wa Pasaka ambao mbali na masuala ya kiroho, ulibainisha mambo kadhaa yanayogusa mstakabali wa taifa.

Katika mitandao ya kijamii leo imesambazwa barua yenye kumbukumbu no. SO.748/25 inayoonyesha imeandikwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Wizara ya Mambo ya Ndani kwenda kwa Mwenyekiti /askofu Mkuu wa KKKT iliyoandikwa Mei 30, 2018 ikitoa maelekezo ya kufutwa waraka huo ndani ya siku 10 tangu ilipoandikwa barua hiyo.

Ikiwa na kichwa cha habari ‘Ujumbe wa Baraza la Maaskofu wa KKKT’ barua hiyo inaeleza baraza hilo halitambuliki kisheria katika ofisi ya msajili.

“Unaelekezwa kuufuta waraka husika kwa maandishi na kuujulisha umma kuwa taasisi yako haikuwa na haina uwezo kisheria kufanya kile mlichokifanya. Maandishi hayo yaufikie umma wa Watanzania kwa kupitia vyombo vya habari na njia zingine zilezile zilizotumika kuufikisha waraka ule mliouita ‘Ujumbe wa Baraza la Maaskofu KKKT’.

Hata hivyo, barua hiyo imetoa onyo kali kwa taasisi hiyo dini nchi kutekeleza agizo mara moja la sivyo itachukuliwa hatua za kisheria.

“Maelekezo haya yatekelezwe ndani ya siku kumi tangu kupokea kwa barua hii vinginevyo hatua kali zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi ya taasisi hii,” inasema barua hiyo.

Ikumbukwe kuwa  waraka huo ulisainiwa na maaskofu 27 wa kanisa hilo nchini na kutaja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na utekaji, utesaji, kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi.ni hali ya kijamii na kiuchumi, maisha ya siasa, na masuala mtambuka likiwamo suala la Katiba Mpya.

Waraka uliongeza pia kwamba uhuru wa kujieleza, kutoa na kupokea habari umeendelea kutoweka nchini huku ukionya kubanwa na hatimaye kuelekea kupungua kwa uhuru wa Bunge, Mahakama, na Tume ya Uchaguzi, ukisema hatua hii ni pamoja na kudhoofishwa kwa serikali za Mitaa.

Lakini kabla ya KKKT kutoa waraka wao, Kanisa Katoliki nalo lilitoa waraka kama huo likionya baadhi ya mambo ikiwemo uminywaji wa misingi ya demokrasia ya vyama vingi na uhuru wa kujieleza.

Baada ya kusambaa kwa waraka huo, yalijitokeza mambo mengi ikiwemo kutofautiana na kwa mawazo ya wananchi kuhusu wajibu wa viongozi wa dini katika kutoa ushauri, kuonya au kukemea pale mambo yanapoenda mrama.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Maaskofu wa KKKT

Hata hivyo, barua hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti na watumiaji wa mitandao ya kijamii ikizingatiwa kuwa suala hilo lilijadiliwa na kupita, iweje linaibuka tena wakati huu ambapo kuna utulivu na yale mambo waliyoyapigia kelele na maaskofu  yamepungua ikiwemo kuteswa, kupotea kwa watu na vitisho dhidi ya viongozi wa kisiasa.

 

Wananchi bado wanawaamini viongozi wa dini

Wadau mbalimbali wa masuala ya kijamii wamesema kama kweli barua hiyo imetolewa na serikali, inaweza kuchochea taharuki zaidi kwa waumini wa kanisa hilo na wananchi kwasababu linagusa moja kwa moja imani zao.

Amebainisha kuwa bado waumini wengi wana imani na viongozi wao dini na kwamba yale wanayotamka yanakuwa na nia njema kwa jamii yao. Na katika muktadha huo serikali inapaswa kuwa makini ili kuepusha matatizo zaidi yanayoweza kutokea.

Akizungumza na FikraPevu, Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena amesema kama serikali ilibaini kuna tatizo kwenye usajili wa Baraza la Maaskofu la KKKT ingekaa na wahusika na kulimaliza kuliko kujitokeza hadharani na kuendeleza jambo ambalo limepita.

“Mimi namwamini Mungu kuliko serikali na viongozi wangu wa dini hasa Maaskofu. Hivyo serikali inapaswa kuwa makini na mambo yanayogusa imani za watu. Katika hili walipaswa kutafakari sana jinsi ya kushughulika nalo. Vinginevyo halina afya kwa ustawi wa taifa letu,” amesema Meena.

Amesema Maaskofu walitimiza wajibu wao wa kuonya kabla mambo hayajaharibika na serikali inapaswa kuyafanyika kazi yale yalyotajwa kwenye waraka au kukaa kimya ili kuepusha migongano isiyo na faida kwa taifa.

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com