Connect with us

Investigative

Majivu yatumika kupanga uzazi na utoaji mimba Mbeya

Published

on

LICHA ya Serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kutoa elimu ya kutumia njia za kisasa za uzazi wa mpango kote nchini, baadhi ya wanawake katika wilaya ya Mbeya Vijijini na Jiji la Mbeya wamekuwa wakitumia majivu kama njia ya kupanga uzazi na kutoa mimba zisizotarajiwa.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa makala hii katika mji wa Mbalizi Mbeya Vijijini na kata ya Manga na Foresti Jijini Mbeya umebaini kuwa wanaoongoza kwa kutumia njia hiyo ni pamoja na wake za watu na wahudumu wa Bar.

Wanawake waliohojiwa wakiwemo wawili kati yao ambao wakawa na mahusiano na mwandishi wa makala haya ili kukamilisha uchunguzi, walisema kuwa majivu hayo wanakunywa kikombe kimoja kila baada ya kumaliza kufanya tendo la ndoa na wanaume ambao wana mahusiano nao ya kimapenzi na wengine waume zao.

‘’Majivu unatakiwa unywe ndani ya masaa 12 baada ya kutoka kufanya tendo la ndoa ili mimba isitunge’’ anasema Mama Angel mkazi wa eneo la Mama John ambaye ni mke wa mtu.

Mama Angel anakiri kuwa amewahi kutoa mimba kwa njia za kisasa ambayo haikuwa mimba ya mumewe na alipoambiwa kuwa kuna njia zingine za kujikinga ikiwemo kunywa majivu baada ya tendo la ndoa ameendelea kutumia njia hiyo kwa miaka mitatu sasa.

‘’Kule hospitali nilitundikiwa maji ya uchungu ambayo yanaongeza njia na ndani ya masaa matatu mimba ikatoka’’ anasema Mama Angel bila kutaja hospitali aliyotolea mimba.

Uchunguzi huo uliofanywa mwezi Octoba na Novemba 2012, umebaini kuwa kwa sasa wanawake wengi hawapendi kutumia njia za uzazi wa mpango wa kisasa mfano Sindano, vipandikizi na vidonge kwa madai kuwa huduma hizo zina madhara.

Wanawake 43 waliohojiwa wakiwemo wake za watu 13 walisema kuwa madhara waliyoyapata baada ya kutumia njia za uzazi wa mpango wa kisasa ni pamoja na kupoteza hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Baadhi walisema kuwa wanaogopa kufanyiwa upasuaji (kusafishwa) kunakotokana na uvimbe unaosadikika kutokea baada ya kutumia kwa muda mrefu huduma hizo za kisasa hasa vidonge maarufu kama majira.

‘’Tarehe za Hedhi hubadilika na kutoeleweka baada ya kutumia dawa hizo za uzazi wa mpango wa kisasa zikiwemo sindano na vidonge’’ anasema Naomi Haule ambaye ni mhudumu wa Bar.

Wengine ambao waliomba hifadhi ya majina yao, wanasema mbali na kutumia majivu kama njia ya uzazi wa mpango kuzuia mimba na utoaji mimba, baadhi yao wanatumia kisamvu, Vidonge vya uzazi wa mpango maarufu kama (Majira) na majani ya mti unaojulikana kwa jina la Songwa kutoa mimba zisizotarajiwa.

‘’Wake za watu wanaopata mimba ambazo si za waume wao, wafanyabiashara na wahudumu wa Bar siyo siri tunaongoza katika kutumia njia hizi na utoaji mimba kwa njia za kienyeji’’ anasema Rehema Mwakitalu akiwa na wenzake eneo la Mwanjelwa ambaye pia ni muhudumu wa Bar.

Walipoulizwa kuwa kwanini wasitumie njia za kisasa katika utoaji mimba walisema kuwa kikwazo ni gharama za utoaji mimba kwa njia za kisasa ambapo mwanamke mwenye mimba ya mwezi mmoja hutozwa Shilingi 40,000 ili asaidiwe kutoa mimba hiyo.

Walizitaja hospitali ambazo zinahusika kutoa mimba hizo kwa siri kuwa ni pamoja na hospitali ya wazazi Meta na zahanati zingine za madaktari binafsi zilizopo eneo la Nzovwe, Mama John na Uyole.

Aidha mbali na hospitali hizo, wanawake hao walisema kuwa pia kuna waganga na wakunga wa jadi wanaowasaidia kutoa mimba hizo ambazo wanadai kuwa hazikutarajiwa na kwamba wakunga hao wapo eneo la Mapelele wilaya ya Mbeya na Iwambi Jijini Mbeya.

Kuhusu maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi wanasema; ‘’ Ni bora kupata ukimwi kuliko mimba kwasababu ukipata ukimwi unajulikana baada ya mud asana na unapata dawa za kurefusha maisha lakini mimba ukipata huwezi kuendelea na starehe na ukijifungua unalazimika kulea mtoto kwa muda mrefu huku na wanaume wengi hawaeleweki kwenye matunzo’’ wanasema wanawake hao.

Wanawake wahudumu wa Bar walipoulizwa kuwa kwanini wanatumia zaidi majivu kama njia ya uzazi wa Mpango na utoaji Mimba walisema kuwa baadhi ya wanaume huwa hawapendi kutumia mipira (Condom) wakati wa kujamiiana hivyo baada ya tendo la ndoa wanalazimika kutumia njia hiyo kama moja ya njia rahisi ya kuzuia mimba kutotunga.

Walipoulizwa kama wanajua madhara ya kutumia huduma ya majivu na kisamvu kwa muda mrefu kama huduma ya uzazi wa mpango na utoaji mimba walisema kuwa hofu yao ni kwamba wanaweza kupata kansa au kutozaa tena.

‘’Ili kuepukana na kupata madhara ya kansa yanayoweza kutokana na majivu, huwa mtu akinywa basi siku hiyo anatakiwa kunywa maji kwa wingi ili kupunguza kemikali zitokanazo na majivu’’ anasema Asha Juma.

Anasema yeye ni Mama wa watoto watatu na tangu amepata mtoto wake wa kwanza mwaka 1998 amekuwa akitumia majivu kila baada ya tendo la ndoa.

Na kwamba alipojaribisha kutumia vidonge alisumbuliwa na nyonga na kukosa hamu ya tendo la ndoa hatimaye akaenda kusafishwa na alipojaribisha sindano pia alipata madhara ya kukosa hamu ya tendo la ndoa ambapo mpaka sasa anatumia Majivu kama njia salama kwake ya uzazi wa mpango

Baadhi ya madaktari waliohojiwa kwa sharti la kutoandika majina yao gazetini wamekiri kuhusika na biashara ya utoaji mimba kwa njia za kisasa na kuzitaja njia wanazotumia.

‘’Wenzetu kuna sheria za utotaji mimba lakini ajabu hapa Tanzania tunakataza wakati watu wengi wanatoa mimba tena hasa wake za watu na njia ambazo wengi tunazitumia kwa usalama zaidi ni kuwatundikia Drip za maji ya uchungu na vidonge vya uchungu vinavyoongeza njia kwa mwanamke’’wanasema madaktari hao kwa nyakati tofauti.

Siku wanazotumia zaidi ni siku za Jumapili ambapo wanasema kuwa baada ya kumaliza utoaji huo wa mimba wanawake hao wanatoka wakiwa salama na kuwapatia dawa za kutuliza maumivu na kuwashawishi kula vyakula na vinywaji vya kuongeza damu.

Uchunguzi zaidi umebaini kuwa, katika sayansi ya akili watu wanaojamiiana huwa wanatumia kinga mara ya kwanza na ya pili baada ya kuanza mahusiano na huwa hawatumii tena kinga baada ya kukutana mara ya tatu na nne na kuendelea.

Sanjari na hayo imebainika kuwa wauguzi wengi huwa hawatumii njia za kisasa za uzazi wa mpango licha ya kuendelea kuwashawishi wananchi wengine kutumia njia hizo kwa madai kuwa vidonge hivyo huwa wakimeza haviyeyuki.

‘’Sisi wengi hatutumii kwasababu kuna madhara makubwa ukitumia kwa muda mrefu ambapo ukitaka kuzaa unalazimika kwenda kusafishwa kizazi na vidonge hivyo haviyeyuki na inatia hofu kuwa ukikwanguliwa unaweza usizae tena’’ walisema baadhi ya wauguzi wa hospitali za Ifisi Mbalizi na hospitali ya wazazi Meta kwa sharti la kutotaja majina yao.

Mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto mkoa wa Mbeya Prisca Butuyuyu, anasema kuwa mila na desturi ni tatizo katika utumiaji sahihi wa uzazi wa mpango na kwamba katika wilaya ya Mbeya Vijijini mwaka 2011 vilitokea vizazi hai 38 kati ya 100,000 na vifo 113.

Kwa upande wa Jiji la Mbeya mwaka 2011 anasema vizazi vilikuwa 109 kati ya 100,000 na vifo vilikuwa 363 ambapo katika uzazi huo hospitali ya wazazi meta ndiyo inahusika zaidi na inahudumia wanawake pia wanaotoka nje ya Jiji la Mbeya.

Continue Reading
7 Comments

7 Comments

 1. majaliwa john

  21/01/2013 at 2:48 pm

  kwel dunian kuna mambo

 2. MWILE

  16/10/2013 at 9:33 pm

  siamini kama majivu ni kinga

 3. yohana simon

  05/03/2017 at 1:47 pm

  je kama mimba ya mwezi mmoja majivu yaweza kutumika?

 4. yohana simon

  05/03/2017 at 1:48 pm

  nipo Mwapoi_ maswa

 5. LUKCY

  15/01/2018 at 5:08 pm

  majivu yanaweza kutoa mimba ya mwezi mmoja na inakuwaje jinsi ya kunywa?

 6. LUKCY

  15/01/2018 at 5:15 pm

  nomba msaada wenu tafadhari

 7. Donatien

  30/01/2018 at 6:57 pm

  Je,mimba Ya Mwezi Umoja,inaweza Toka Kwa Majivu? Na Wanaikunywa Je?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Investigative

‘UBESHI’: Safari ya Vijana Kuifikia Almasi Mwadui-Shinyanga

Published

on

MAJUZI nilikuwa katika utafiti wa namna gani Madini ya Almas yanayopatikana katika Mji Mdogo wa Maganzo Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga umewanufaisha wananchi wanaozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui.

(more…)

Continue Reading

Investigative

Hofu ya Usalama kwa wafanyakazi GGM Yatanda

Published

on

SIKU chache baada ya moto kuzuka ndani ya mgodi wa Geita (GGM) na kuteketeza mali zenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 25,hofu kubwa ya kupoteza maisha imeibuka kwa uongozi na wafanyakazi wa mgodi huo.

(more…)

Continue Reading

Investigative

If we can’t give people’s priorities the attention they deserve, why ask them to prioritize?

Published

on

In a move intended to empower the citizens and give them mandate to decide on their own development priorities, the government adopted the decentralization policy.

(more…)

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com