Connect with us

Investigative

Wanawake 906 wapoteza maisha kwa sababu za uzazi

Published

on

LICHA ya Serikali kutambua na kusema kuwa Lengo la Milenia ni kufikia vifo 54 kwa kila vizazi hai 1,000 ifikapo mwaka 2015, wanawake 906 wamefariki dunia kwa matatizo ya uzazi mkoani Mbeya.

Akizungumza katika mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi ofisni kwake mwishoni mwa mwaka 2012, Mratibu wa huduma za Afya na mtoto katika Hospitali ya mkoa wa Mbeya Prisca Butuyuyu alisema kuwa kati ya vifo hivyo wilaya ya Mbeya Jiji ndiyo inayoongoza kwa vifo vilivyotokana na uzazi na kufuatiwa na wilaya ya Mbarali.

‘’Wilaya ya Mbeya City inaongoza kuwa na vifo vingi ambapo kwa kipindi cha mwaka 2011 vifo vimetokea 363 sawa na asilimia109, Mbarali vifo 172 sawa na asilimia 58, Chunya 150 sawa na asilimia 63, wilaya ya Ileje vifo 145 sawa na asilimia 33 na wilaya ya Rungwe vifo 133 sawa na asilimia 55’’

‘’Wilaya zingine ni wilaya ya Mbeya Vijijini vifo 113 sawa na asilimia 38, Wilaya ya Mbozi vifo 105 sawa na asilimia 45 a wilaya ya Kyela vifo 88 sawa na asilimia 67 na katika takwimu hizi wilaya ya Kyela kuna uhalisia tofauti na wilaya zingine’’ alisema Butuyuyu.

Anazitaja baadhi ya sababu ambazo zinasababisha vifo vitokanavyo na uzazi kuwa ni pamoja na ugonjwa wa Maralia, damu kupungua kwa mama mjamzito, kutokwa kwa damu nyingi wakati wa kujifungua, uambukizi wa homa kali, huduma hafifu, VVU na kifafa cha Mimba.

Anakiri kuwa vifo hivyo na takwimu walizonazo kama Hospitali ya mkoa inadhihilisha kuwa hawajafikia kiwango cha kuridhisha cha jamii kupata uelewa madhubuti wa kujifungulia katika vituo vya Afya na Hospitali kwani asilimia 40 wanajifungulia nje ya vituo vya huduma ikiwemo nyumbani ama kwa Wakunga wa jadi na ndiyo maana jedwali (Grafu) la vifo linapanda na kushuka.

Alitoa wito kwa viongozi wa kata na vijiji kusaidiana na Wizara ya afya na ustawi wa jamii kwa kutoa elimu kupitia mikutano ya adhara kwa jamii hususan wakinamama wajawazito kuondokana na dhana ya kujifungulia majumbani au kwa wakunga wa jadi ili kuondokana na changamoto hiyo inayochangiwa na uelewa mdogo wa kushiriki katika vituo vya afya na zahanati hususan vijijini.

Alisema katika kukabiliana na hilo wizara ya afya inamikakati kabambe ya kuhakikisha kuwa elimu hiyo inatolewa vijijini ambapo ndio kuna changamoto kubwa ya mwamko duni ya wakinamama wajawazito kujifungulia katika vituo vya afya na zahanati.

Alisema kuwa utafiti uliofanywa umegundua changamoto hiyo inachangiwa na kuwepo kwa uhaba wa vyombo vya usafiri ubovu wa miundombinu na umbali wa vituo vya afya na kwamba serikali kupitia wizara ya afya inatakiwa kufanya jitihada za haraka kusogeza huduma za afya vijijini ili kunusuru vifo vya wakinamama wajawazito wakati wa kujifungua na watoto.

":Hii ni changamoto kubwa kwa serikali na kwamba mikakati inatakiwa kuwepo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kutosha kwa jamii kutambua umuhimu wa kujifungulia katika vituo vya afya na zahanati ili kuondokana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza wakati wa kujifungua ikiwa ni pamoja na kupatiwa kinga za kuzuia maradhi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto"Alisema Butuyuyu.

Aidha alisema takwimu za mkoa wa Mbeya katika kipindi cha mwaka 2011 kwa wilaya ya Ileje ndio inayoongoza kwa tatizo hilo kutokana na kuwa na idadi ndogo ya akina mama wanaojifungulia kwenye vituo vya afya.

Alisema katika wilaya ya Ileje ni asilimia 33 tu ya akina mama wajawazito walijifungulia kwenye vituo ambapo asilimia 57 walijifungulia majumbani huku wilaya ya mbeya mjini ndio ambayo ina idadi kubwa ya akina mama wanaojifungulia kwenye vituo ambapo asilimia 109 ya akina mama wajawazito walijifungua kwenye vituo vya afya .

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Investigative

‘UBESHI’: Safari ya Vijana Kuifikia Almasi Mwadui-Shinyanga

Published

on

MAJUZI nilikuwa katika utafiti wa namna gani Madini ya Almas yanayopatikana katika Mji Mdogo wa Maganzo Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga umewanufaisha wananchi wanaozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui.

(more…)

Continue Reading

Investigative

Hofu ya Usalama kwa wafanyakazi GGM Yatanda

Published

on

SIKU chache baada ya moto kuzuka ndani ya mgodi wa Geita (GGM) na kuteketeza mali zenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 25,hofu kubwa ya kupoteza maisha imeibuka kwa uongozi na wafanyakazi wa mgodi huo.

(more…)

Continue Reading

Investigative

If we can’t give people’s priorities the attention they deserve, why ask them to prioritize?

Published

on

In a move intended to empower the citizens and give them mandate to decide on their own development priorities, the government adopted the decentralization policy.

(more…)

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com