Connect with us

Featured

Namtumbo yapiga marufuku vibanda vya nyasi kutumika kuwa darasa

Published

on

HALMASHAURI ya wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma imepiga marufuku shule za msingi zenye upungufu wa vyumba vya madarasa kutumia vibanda vilivyojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi kama vyumba vya madarasa.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Steven Nana katika mahojiano na mwandishi wa makala haya alisema katika mkutano wa Baraza la madiwani uliofanyika mwezi Juni mwaka huu walipendekeza shule zote ambazo zinatumia madarasa ya vibanda vilivyojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi kuvibomoa badala yake kujenga madarasa kwa  kwa kutumia tofali za kuchoma.

"Hadi sasa madiwani katika kata zenye shule ambazo wanafunzi wanasomea vibanda vya nyasi wameitikio wito vibanda vimebomolewa na kujenga vyumba kwa tofali za kuchoma kwa mfano kata za Mgombasi, Luchiri na Msindo,kata ambayo bado hawajatekeleza ni uzembe wa usimamizi wa diwani husika, vibanda vya nyasi sio mazingira rafiki kwa kusomea wakati wa mvua vinavuja na kuathiri taaluma", alisisitiza.

Vibanda vya nyasi bado vinatumika katika shule ya msingi Selous, hapa ni wanafunzi wa darasa la tano wakisoma katika mazingira duni

Hata hivyo alisema wananchi waliamua kujenga vibanda vya nyasi kwa lengo la kukabiliana na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa ambapo alisema serikali ilitoa masharti magumu kwa wananchi kwa kuwataka wajenge vyumba vya madarasa kwa kutumia kokoto kwenye msingi na kujenga kwa theluji badala ya udongo jambo ambalo wananchi walishindwa kumudu gharama za ujenzi.

Kutokana na hali hiyo mwenyekiti huyo anasema walipendekeza wananchi kujenga vyumba vya madarasa kwa udongo na tofali za kuchoma ambapo serikali iliahidi kuchangia vifaa vya kiwandani ambapo hadi sasa tayari wananchi wamefyatua tofali na  fedha zitakapopatikana wanapewa ili kukamilisha ujenzi.

"Halmashauri yangu inakabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha katika mwaka wa fedha wa 2012/2013 ilitengewa shilingi bilioni 16 lakini hadi kufikia mwezi huu Desemba ni asilimia 14 tu ya fedha ndiyo imefika kutoka TAMISEMI, fedha ikipatikana tutazipeleka katika shule kwa ajili ya kukamilisha ujenzi", alisema

Uchunguzi ambao umefanywa katika shule tatu za msingi  kata ya Rwinga wilayani Namtumbo ambazo ni Rwinga, Kidugalo na Mkapa umebaini shule hizo  zimefyatua tofali 80,000 kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa na nyumba za walimu.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mkapa Hans Mwailima akionyesha nyumba ya mwalimu mkuu ambayo inajengwa ,shule hiyo yenye walimu 11 haina nyumba hata moja ya mwalimu

Mwandishi wa makala haya mwezi Mei mwaka huu alifanya uchunguzi katika kata ya Rwinga na kubaini wanafunzi 500 katika shule hizo wanasomea kwenye vibanda vilivyojengwa kwa miti na kuezekwa nyasi na wengine wanasoma madarasa mawili katika chumba kimoja huku wamegeuziana migongo hali ambayo imekuwa inaathiri taaluma katika shule hizo.

Kaimu mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kidugalo yenye wanafunzi 427 Getruda Turuka alisema katika shule hiyo tofali zaidi ya 20,000 zimefyatuliwa na kuchomwa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kukabiliana na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa ambapo shule hiyo ina vyumba vinne kati ya 13 vinavyohitajika.

Licha ya kwamba tofali kwa ajili ya ujenzi zimekamilika, hata hivyo serikali ya kijiji cha Kidugalo ilipanga kuanza ujenzi wa vyumba vya madarasa mapema, lakini uongozi wa Halmashauri uliwazuia kujenga kwa madai kuwa hakuna uwezo wa kuwasaidia vifaa vya viwandani ambavyo ni bati, misumari na saruji.

Walimu katika shule ya msingi Kidugalo wakionyesha tofali ambazo zimeandaliwa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa kwa lengo la kukabiliana na upungufu katika shule hiyo

Said Juma na Tamimu Mwela ni wenyeviti wa vitongoji vya Lilunde na Namwaya wanasema tofali zimekamilika na walitaka kuanza ujenzi wamekwamishwa na Halmashauri kuwazuia kuanza ujenzi katika shule  ya msingi Kidugalo kwa madai kuwa Halmashauri hivi sasa haina fedha.

Katika shule ya msingi Mkapa ambayo haikuwa na nyumba hata moja ya mwalimu, hivi sasa kuna ujenzi wa nyumba ya mwalimu ambayo inaweza kuchukua familia mbili.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Hans Mwailima anasema kamati ya shule kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji umeamua kuanza ujenzi wa nyumba ya mwalimu hali ambayo inaweza kupunguza tatizo la nyumba kwa walimu ambapo hivi sasa walimu wote 10 wanaofundisha katika shule hiyo akiwemo mwalimu mkuu wamepanga.

Hata hivyo amesema shule hiyo yenye wanafunzi 261 ina vyumba vinne tu kati ya mahitaji ya vyumba nane, madawati yaliopo ni 62 kati ya mahitaji ya madawati 106.

Katika shule ya msingi  Rwinga yenye wanafunzi 436, kamati ya shule kwa kushirikiana na serikali ya kijiji wamefyatua tofali zaidi ya 25,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya kusomea ili kuepukana na wanafunzi 187 wa darasa la tatu na awali kusomea kwenye vibanda viwili vya nyasi vilivyojengwa katika shule hiyo.

Hawa ni wanafunzi katika shule ya msingi Kidagulo ambao wanasafiri umbali mrefu kwa lengo la kutafuta maji hali ambayo inaathiri taaluma

Mwalimu mkuu msaidizi katika shule hiyo Hamza Ngonyani amesema kamati ya shule na serikali ya kijiji wamehamasisha michango ambapo kila mzazi alitoa mchango wa shilingi 2000 na kufanikisha kufyatua na kuchoma tofali ambazo zinaweza kujenga vyumba viwili vya madarasa.

Hata hivyo Ngonyani alibainisha kuwa changamoto kubwa iliyopo hivi sasa ni upatikanaji wa vifaa vya kiwandani zikiwemo bati na theluji kutoka Halmashauri ya wilaya ambayo imesema hivi sasa haina pesa za kusaidia kukamilisha ujenzi huo hivyo wameshauriwa kuacha kuanza ujenzi.

Katika shule ya msingi Selous hakuna hatua zozote ambazo zimechukuliwa kwa lengo la kukabiliana na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa ambapo shule hiyo ina wanafunzi zaidi ya 100 wanaosoma katika vibanda vya nyasi.

Baadhi ya walimu wanaofundisha katika shule hiyo ambao hawakutaka kutaja majina yao walidai kuwa baada ya vyombo vya habari kutoa habari kuhusiana na shule hiyo viongozi kutoka Halmashauri walifika,lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika zaidi ya vibanda vilivyopo kuviboresha kwa kuezeka nyasi ili kukabiliana na mvua za masika.

Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo yenye kata 14 ina shule za msingi 107 kati ya hizo shule 105 zinamilikiwa na serikali na shule mbili ni za watu binafsi na mashirika ya dini.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Featured

UJASUSI: Jinsi kijana wa kiume kutoka New Zealand alivyojaribu  kumuua Malikia Elizabeth II

Published

on

Shirika la Ujasusi la New Zealand  (SIS) limethibitisha kwa mara ya kwanza kwamba kulikuwa na jaribio la kumuua Malikia Elizabeth II wakati alipotembelea jiji la Kusini la Dunedin mwaka 1981.

Jaribio hilo la kumuua Malikia linalodaiwa kutekelezwa na kijana wa kiume limechochea hamasa ya polisi kutaka kujua ni kwa kiasi gani wanausalama hao walifanikiwa kuzima njama hizo.

Taarifa iliyotolewa na SIS  zinaonesha kuwa kijana huyo, Christopher Lewis (17) alipiga risasi kuelekea kwa Malikia wakati akishuka kwenye gari lake ambapo alikuwa anaenda kushuhudia Maonyesho ya Sayansi yaliyofanyika Oktoba 14, 1981 katika jiji hilo. Tukio hilo lilitokea akiwa katika ziara ya siku 8 kutembelea nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.

“Lewis alidhamiria kumuua Malikia, hata hivyo hakuwa katika nafasi nzuri ya kurusha risasi, hata silaha iliyotumia haikuwa katika umbali wa kuweza kumfikia mhusika,” imesema taarifa iliyotumwa SIS kwa vyombo vya habari.

Lewis ambaye anatajwa kwenye taarifa ya ujasusi kama ‘kijana msumbufu’ hakuhukumiwa kwa jaribio la kutaka kuua au kosa la uhaini. Tukio hilo lilifanywa kuwa siri ili kuzuia sifa mbaya kwa nchi (New Zealand) ambayo ilitembelewa na mgeni wa heshima. Badala yake Lewis alihukumiwa kwa kumiliki silaha kinyume na sheria na kufyatua risasi.

                       Malikia Elizabeth II akiwa ameambatana na walinzi wake alipotembelea New Zealand

Inaelezwa kuwa watu waliohudhuria tukio la kuwasili kwa Malikia walisikia mlio wa risasi lakini Polisi waliokuwa wanasimamia usalama katika eneo hilo la Dunedin waliwaambia kuwa ilikuwa ni sauti ya kuanguka kwa kitu au magari kugongana.

“Uchunguzi wa sasa wa polisi juu milio iliyosikika umefanywa kwa umakini na wawakilishi wa vyombo vya habari wamepata mrejesho kuwa kelele zilisababishwa na baruti”, inaeleza ripoti kutoka SIS iliyotolewa mwaka 1981 baada ya kutokea tukio hilo.

Kulingana taarifa za ujasusi zinaeleza kuwa polisi wamekuwa wakifuatilia nyendo za Lewis tangu 1986 ambapo Malikia alitembelea tena New Zealand wakiogopa kuwa anaweza kutekeleza tena uhalifu huo. Kuwekwa wazi kwa siri hiyo kumewaibua polisi ambao wameanza kuchunguza upya kesi hiyo.

Zaidi ya muongo mmoja uliopita, Lewis alihukumiwa kwa mauaji ya mwanamke mmoja katika mji wa Auckland na kumteka mtoto wa kike ambapo baadaye alimtupa karibu na kanisa.

Kulingana na taarifa mbalimbali za wakati huo zinaeleza kuwa Lewis alijidhuru kwa umeme akiwa gerezani mnamo 1997 akisubiri hukumu ya kuua. Lakini alikana mashtaka ya kuua kwa ujumbe mfupi wa kifo (suicide note).

New Zealand ilipata uhuru mwaka 1947 kutoka kwa Uingereza lakini inamuheshimu Malikia kama kiongozi wa taifa. Ameitembelea nchi hiyo kama Malikia mara 10 na mara ya mwisho ilikuwa 2002.

Continue Reading

Featured

FREEDOM HOUSE: Tanzania ina uhuru kiasi, kufungiwa vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya kisiasa kuididimiza kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa

Published

on

Ripoti mpya iliyotolewa na taasisi huru ya Freedom House imesema misingi ya demokrasia ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kukusanyika imeendelea kudhoofika nchini Tanzania na hali hiyo isiporekebishwa itaingia kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa duniani.

Kulingana na  Freedom House  ambao walichambua data katika nchi 195 za ulimwenguni katika mwaka 2017 wamebaini kuwa nchi 88 zina uhuru,  58 zimejumuishwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku 48 zikiwekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa misingi ya demokrasia ikiwemo uchaguzi usio huru na haki, uhuru wa kujieleza umeendelea kushuka kwa mwaka wa 12 mfufululizo duniani kote. Miongoni mwa matokeo yaliyostaajabisha ni kudhoofika kwa  Marekani ambayo ni mama wa demokrasia kutokana na uchunguzi unaofanywa na Mwendesha Mashtaka Maalumu kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 ambao ulimpa ushindi Rais Donald Trump.

Tanzania imewekwa kwenye nchi 88 ambazo zina uhuru kiasi lakini inatahadharishwa kuwa inaweza kuingia kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa. Tahadhari hiyo inatokana na mwenendo wa viongozi wa serikali kufungia vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kushtakiwa kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa tuhuma za uchochezi na kukamatwa kwa wapinzani wa kisiasa ambao wanakosoa na kutoa mawazo yanayotofautiana na serikali.

Pia utekelezaji wa Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 na Sheria ya Makosa ya Mtandao  ya mwaka 2015 umekuwa ukilalamikiwa na wadau wa maendeleo kuwa ni mkakati wa kudhoofisha uhuru wa kutoa maoni, uwazi na uwajibikaji.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini hivi karibuni kilitoa tamko la tathmini ya uchaguzi mdogo wa marudio wa kuchagua madiwani uliofanyika katika kata 43 kwenye mikoa 19 ya Tanzania  Novemba 24 mwaka jana ambapo kilibaini mambo mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Tathmini hiyo iliibua mambo mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya nguvu ya vyombo vya dola, matukio ya watu kutekwa na watu wasiojulikana, watu kupigwa, kujeruhiwa  kwa lengo la kuharibu na kuvuruga uchaguzi  na vilevile kuwatia hofu wapiga kura.

 

Afrika Mashariki hali bado tete

Tanzania inaungana nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya na Uganda ambazo nazo zimewekwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku za Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini zimejumuishwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa.

Awali Uganda ilikuwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa lakini imepanda hadi kwenye uhuru kiasi kwasababu ya  kuimarika kwa tasnia ya habari na utashi wa wanahabari, blogu na  uhuru wa wananchi kutoa maoni yao licha ya mazingira ya kisiasa kuminywa na utawala wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni.

Rais Museveni mwenye umri wa miaka 73 amekuwepo madarakani  tangu 1986 amefanikiwa kubadilisha sheria  ya ukomo wa umri wa miaka 75 wa kugombea urais ambapo atapata fursa ya kugombea tena mwaka 2021. Chaguzi nchini Uganda zimekuwa zikitawaliwa na vurugu za polisi na wananchi, kuzimwa kwa intaneti na kuwekwa kizuizini kwa viongozi wa upinzani ikiwemo Kizza Besigye wa chama cha Forum for Democratic Change.

Kwa upande wa Kenya ambayo imekuwa ikisifika kwa kuimarisha misingi ya demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo kwa mara ya kwanza mahakama ilifanikiwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Urais yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta uliofanyika Agosti 2018. Uchaguzi ulirudiwa na Rais Kenyatta alichaguliwa tena.

Marudio ya uchaguzi yalilamikiwa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa hayakuzingatia haki za binadamu ambapo watu ambao walipinga uchaguzi huo walikumbana na mkono wa dola. Matendo hayo ndiyo yaliiweka Kenya kwenye kundi la nchi zilizo na uhuru kiasi.

Burundi na Sudan Kusini zimewekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa kutokana na mapigano ya kikabila ambayo yamedhoofisha mfumo wa kisiasa wa kuongoza nchi. Vyombo vya habari na wananchi wanaotoa maoni tofauti na serikali wamekuwa wakiteswa, kufungwa na kuuwawa.

Chanzo: Freedom House           – Nchi zisizo na  uhuru  – Nchi zenye uhuru     – nchi zenye uhuru kiasi   

 

Hali ilivyo Afrika

Afrika kama zilivyo nchi za Afrika Mashariki hali ya demokrasia siyo ya kuridhisha ikizingatiwa kuwa asilimia 11 ya wakazi wapatao bilioni 1.02 wa bara hilo ndio wana uhuru wa kweli, huku 52% wana uhuru kiasi na 37% hawa uhuru kabisa.

Ripoti ya Freedom House inaeleza kuwa waliangazia nchi 49 za Afrika na kugundua kuwa nchi 8 (18%) ndio zina uhuru wa kweli, nchi 22 (43%) zina uhuru kiasi na 19 (39%) hazina uhuru kabisa. Nchi zinazotajwa kuwa na uhuru ni Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Ghana, Togo, Senegal na Kisiwa cha Sao Tome.

 Sababu ya nchi nyingi za Afrika kuwepo kwenye kundi la zisizo na uhuru ni matokeo ya viongozi kukaa madarakani muda mrefu, vurugu za kisiasa na kikabila ambazo zimekuwa zikihatarisha haki za binadamu.

 

Demokrasia ya Dunia

Demokrasia ya dunia inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kisiasa kuliko wakati mwingine ambapo mwaka 2017 ulishuhudia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo kuminywa kwa  uchaguzi huru na kweli, haki za watu wachache, uhuru wa kujieleza, utawala wa sheria.

Nchi 71 kati ya 195 zimeshuhudiwa zikiteteleka katika kulinda haki za kisiasa na jamii ambapo ni nchi 35 tu ndizo zimeweza kulinda haki hizo. Kudhoofika kwa demokrasia kunaendelea kushuka kwa miaka 12 mfululizo na hatua muhimu zisipochukuliwa amani ya dunia itawekwa rehani.

Marekani ambayo ni bingwa wa demokrasia duniani nayo imeripotiwa na taasisi ya Freedom House kudhoofika katika kulinda haki za kisiasa na kijamii na kuzua mgongano wa mawazo miongoni mwa nchi zinazoibukia katika kujenga demokrasia ya dunia.

Tangu kuisha kwa vita baridi, nchi nyingi ziliachana na utawala wa kiimla na kugeukia demokrasia ya vyama vingi lakini hali hiyo imeanza kujitokeza tena ambapo idadi ya viongozi wanaoongoza kwa udikteta inaongezeka.

 

Uhuru wa nchi moja unategemea uhuru wa nchi zote

Demokrasia itabaki kuwa tunu muhimu kwa jamii zilizostaarabika, ikifungua milango ya uwazi, mawazo na fursa mpya na zaidi ya yote kulinda uhuru wa mtu mmoja mmoja. Ikiwa watu duniani kote wanadai mazingira mazuri ya kisiasa ni dhahiri wanakumbatia misingi ya demokrasia: uchaguzi huru, uhuru wa kujieleza, uwazi na uwajibikaji wa serikali, utawala wa sheria ambao hauingiliwi na polisi, jeshi au taasisi nyingine za nchi.

Hata hivyo, Karne ya 21 imeshuhudia ugumu wa kuifanya demokrasia kuwa endelevu ambapo baadhi ya nchi zinatekeleza lakini zingine zinapuuza. Utawala wa kidekteta wa Urusi na China unatambua wazi ili uendelee kuwepo unahitaji kuimarisha demokrasia katika nchi nyingine ili ziendelee kufaidika na mahusiano ya kidiplomasia. Ukuaji wa  demokrasia ni kulinda haki za watu wote duniani kupitia utandawazi   

Continue Reading

Afya

Is Tanzania’s Adolescent Fertility Rate Three Times Higher Than Global Counterparts?

Published

on

The Comprehensive Community-Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT), an organization ​which works to provide affordable medical and rehabilitative services for mothers and newborns throughout Dar-es-Salaam, marked World Contraception Day on September 26 with a call for more efforts to meet the reproductive health needs of teens between 15 and 19 years old.

The report highlights a worrying statistic — Tanzania’s adolescents are having almost three times as many children on average as their global counterparts, with 135 births per 1000 girls reported in the country, compared to an average of 44 per 1000 girls aged 15–19 worldwide in 2015.

CCRBT attributes the high adolescent fertility rate to a lack of access to contraceptive services, with Technical Advisor for Nursing Bola Abbas saying, that only about 8 per cent of current family planning clients are between the ages of 15 to 19.

On a national scale, Abbas explains, demand for family planning among adolescent girls is still very low, with only one out of every three of those who are sexually active within the 15 to 19 age group using modern contraceptive methods.

So the question is, how does Tanzania’s adolescent fertility rate compare to that of the rest of the world?

Pesacheck investigated the claim that Tanzanian adolescents are having three times as many children as their peers in the rest of the world and found that the statement is TRUE for the following reasons:

Tanzania’s adolescent fertility numbers are rather high, with 4.4% of girls aged 15 having given birth according to the country’s Demographic and Health Survey.

The Sustainable Development Goals call for countries to ensure universal access to sexual and reproductive healthcare services, including family planning, information and education, and the integration of reproductive health into national strategies and programmes by 2030.

The indicators for this goal are the proportion of women of reproductive age (15–49 years) who have their need for family planning satisfied with modern methods, and the adolescent birth rate (10–14 years and 15–19 years) per 1,000 women in that age group.

For several sub-Saharan countries, Tanzania included, access to modern family planning methods is low for this particular age group, and as a result, the regional average is 105 births per 1,000, which is more than double the global average.

Tanzania’s National Bureau of Statistics produced a national fertility and nuptiality report based on data from the 2012 national census, which shows that Adolescent Fertility Rate (AFR) was 81 births per 1,000 women aged 15–19.

The report further shows that in 2012, 23.3% of adolescent girls in the country had given birth to at least one child. Additionally, 42.2% of girls who had never attended school had given birth, compared to just 9% of those who had reached university.

This shows that there is a need for contraceptive access for teenage girls in Tanzania, especially for girls in rural areas and those with limited access to education.

The Tanzania Demographic and Health Survey 2015–16 indicates that 27% of girls aged 15–19 have given birth. Crude birth rates for girls aged 15–19 show that there 135 births per 1,000 girls in Mainland Tanzania and 132 per 1,000 girls in Zanzibar, way above the global average of 44. The data also shows that contraceptive access for this age group is also quite low, with 10.4% of girls aged 15–49 using any form of contraception.

It would therefore appear that the lack of access to contraceptives is contributing to the increased likelihood of adolescent girls getting pregnant.

So the claim by CCBRT that Tanzania’s adolescent fertility rate is almost three times the global average is TRUE. This is driven largely by a lack of access to contraceptives for young people in the 15–19 age group, and the relatively high levels of poverty that have driven many out of school and into early marriage.

As a result, the country is unlikely to meet the Sustainable Development Goal of overall good health and wellbeing of mothers unless it puts measures in place to ensure universal access to sexual and reproductive health-care services for girls and women of all ages.

Do you want us to fact-check something a politician or other public figure has said about public finances? Complete this form, or reach out to us on any of the contacts below, and we’ll help ensure you’re not getting bamboozled.

This report was written by PesaCheck Fellow Belinda Japhet, a Communications Consultant, Online Editor based in Tanzania. The infographics are by PesaCheck Fellow Brian Wachanga, who is a Kenyan civic technologist interested in data visualisation. This report was edited by PesaCheck Managing Editor Eric Mugendi.

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com