Connect with us

Featured

Polisi aliyefyatua bomu lililoua mwandishi akamatwa, kushitakiwa kwa mauaji

POLISI ambaye alifyatua bomu kwa karibu na kusababisha kifo cha Mwandishi wa habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi, anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote, Fikra Pevu limefahamishwa.

Published

on

OLISI ambaye alifyatua bomu kwa karibu na kusababisha kifo cha Mwandishi wa habari wa Channel Ten,  Daudi Mwangosi, anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote, Fikra Pevu imefahamishwa.

Taarifa za kutoka Iringa zimeeleza kwamba kushitakiwa kwa askari huyo, kunafuatia kukamilika kwa uchunguzi wa awali ambao unathibitisha pasi shaka kwamba bomu alilofyatua ndilo lililosababisha kifo cha mwandishi huyo wa habari.

Imethibitishwa kwamba kilichousambaza mwili wa mwandishi huyo ni bomu maalumu linalorushwa kwa kutumia bunduki kwa nia ya kusambaza watu waliokusanyika kwa nia ya kutenda uhalifu na lilirushwa kwa karibu mno kinyume cha masharti na kanuni za matumizi yake.

Bomu hilo hutakiwa kurushwa kutoka umbali wa mita kati ya60 na 80, wakati askari huyo alilirusha kwa karibu mno na akimlenga mwandishi Mwangosi.

Katika tukio hilo, bomu hilo liliusambaratisha mwili wa Mwangosi na kumjeruhi ofisa mmoja wa polisi ambaye anaelezwa kutaka kumsaidia mwandishi huyo ambaye alikua akipigwa na polisi wenzake.

Marehemu Mwangosi aliuawa Jumapili iliyopita katika kijijini cha Nyololo, wilayani Mufindi, mkoani Iringa katika tukio ambalo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walikuwa wakifungua tawi la chama chao, huku Polisi wakitumia nguvu kubwa kuzuia uzinduzi wa tawi hilo.

Continue Reading
28 Comments

28 Comments

 1. juma magombe

  06/09/2012 at 11:22 am

  aliyeuwa aliyetoa oda na walioshiriki wanyongwe eeeeh!

 2. jose

  06/09/2012 at 11:33 am

  Tusubiri tuone kama ni ukweli, ila mpaka sasa ni maendeleo mazuri

 3. MremaHarun

  06/09/2012 at 11:58 am

  Kwa kweli inauma sana mahali tulipofikia na
  Pa hatari sana kwa usalama wa nchi na watanzania .mauaji haya watawala watayalipia siku sio nyingi Mungu hatavumilia haya tena yuko tayari kuijilia nchi hii.

 4. laizo

  06/09/2012 at 12:10 pm

  police wameonyesha uzembe wa hali ya juu kumuuwa mwandishi wa habari, hili linawaumiza vichwa hakukua na ulazima wakumkamata yule mwandishi yy alifika kuchukua matukio. lakini kutikana na police kutumia nguvu kupitakiasi kwa wananchi waliona mwandishi ameisha warekodi hivyo wataonekana wakaamua kumlipua.

 5. saki

  06/09/2012 at 1:13 pm

  Wamekosea kudanganya. mbona shegela wa ccm alisema chadema ndo walimrushia bomb? Inanipa mashaka upeo wa akili ya nchimbi, mwema, tendwa, nape, na hawa mapolisi kwa ujumla.

 6. jerome lemnge

  06/09/2012 at 3:35 pm

  so sad

 7. Daniel Sungi

  06/09/2012 at 4:13 pm

  Ee Mungu, tusaidie Watanzania tusijewaka hasira juu ya Askari hawa wanaoua ndugu zetu kila kukicha na kutualika kuamini kuwa CHADEMA NI WAUAJI!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!. Wakati huo, hawa jamaa wanadunda mitaani kwetu tunawaangalia tu! Pamoja na yote hayo, watanzania watadumu kuwa watazamaji hata lini?

  • mapambano yetu

   07/09/2012 at 10:48 pm

   ipo siku polis watajua mbivu na mbichi kwan wataua wengi lakini watakaobaki hawatakubali upumbavu wao uendelee. tunaelekea huko na mazingira wanayatengeneza wenyewe

 8. Bashir omar

  06/09/2012 at 11:01 pm

  Ni jambo la kusikitisha mtu yoyote kupoteza maisha mikononi mwa polisi lakini pia ni kwa bahati mbaya ile tear gas can kumtoka askari, si kusudio lake kumuua yule mwandishi. ukitazama picha yote unagundua katika tukio lile kuna askari watatu wamejeruhiwa na ule mlipuko iweje kuwapiga wao kwa wao. Kibaya ni kitendo kile cha kumburuza marehemu mwangosi kabla ya kuuwawa. Yaliyofuata ilikuwa ni ajali mbaya ya mlipuko wa bomu la machozi inasikitisha sana. nafikiri na yule askari anajuta kwa kitendo kile. mkanganyiko umekuwa ni mkubwa mno hakuna aliyetegemea matokeo hayo mabaya, Si polisi wala cdm.

 9. suluo adam

  07/09/2012 at 11:34 am

  Ni wakati sasa viongozi wakuu wa nchi kulikemea tabia hii mbaya ya polisi kujichukulia sheria mikononi. Kama mwandishi alikuwa na kosa mbona tayari alikuwa mikononi mwao kwanini wasimpeleke mahakamani? Vinginevyo wananchi wana haki ya kuamini kuwa yale ni maagizo toka kwao!

 10. Brayson F.

  07/09/2012 at 4:41 pm

  Sio muda wa kufumbia macho haya matukio mabaya tena (Arusha, Morogoro na Iringa ss) yanayotendwa napolisi. What I know polisi hawawezi kwenda kusambaratisha maandamano yoyote yale bila ruhusa au kibali kutoka kwa wakubwa wao.Hivyo matukio haya yote yanapaswa kuchukuliwa hatua na haki itendeke, we are too tired now kwa stori za hawa viongozi wasioona wakati wanatazama!!!!!

 11. mapambano yetu

  07/09/2012 at 10:43 pm

  tumechoka kudanganywa!!!!! hizo ni propaganda 2. ishu nzima ilisukwa na POLICCM, hakuna kitakacho fanyika zaidi ya kutulaghai. hebu tafakari polisi kutolewa nje ya mkoa tena kwa siri!!!! Huo ulikuwa mpango wa kuinufaisha CCM lkn MUNGU kawaumbua. POLICCM endelea kutimiza wajibu wenu wa kukipendelea chama tawala. ueni, umizeni, teseni, pigeni, wengine pelekeni mistuni mkawang’oe meno kwa praiz lakini mjue yule mtanzania atakaye salia ataendelea kudai haki zake.

  • MSAKA-UHURU

   09/09/2012 at 6:30 pm

   tusipokuwa makini watanzania hakuna hatua yoyote itakayochukuliwa na magamba dhidi ya muuaji….na pengine kama kweli alitumwa kuua basi akifikwa na maji ya shingo huenda akasema ukweli huyo police au wakamuua na yy ili kupoteza ushahidi…. let us be vey keen…!

 12. mood

  09/09/2012 at 11:45 am

  Mungu ailaze roho ya marehemu Daudi mwangosi mahala pema.

 13. ali yusup

  09/09/2012 at 1:07 pm

  sijanywa chai

 14. Adam Nindi

  13/09/2012 at 5:06 pm

  Adam Nindi –Songea

  Hospitali ya Songea ambayo nitegemeo kwa wakaazi wa Mkoa wa Ruvuma ina kabiliwa na Changamoto ya Kukosa ma shine ya Exray kwa kipindi cha mwezi mmoja hivi sasa.

  Hayo yamebainika baada ya watu 17 kupata ajali na kushindwa kupata huduma ya upimaji katika hospitari ya mkoa wa Ruvuma kutokana na mashine ya Exray kuwa mbovu na kusababisha majeruhi kupelekwa hospitali ya Peramiho songea vijijini kilometa 24 kutoka songea mjini ili kwenda kupata huduma Exray

  Kaimu Mganga mfawidhi wa Hospitali ya Songea Mathew Chanangula amesma katika ajali hiyo iliyo tokea katika eneo la Mlima Mkwaya songea vijijini kati ya watu 17 walio pata ajali hiyo mototo mwenye umri wa miaka 2 Daima Rashidi alifariki dunia baada ya kupoteza damu nyingi

  Kaimu Mganga Mfawidhi Mathew Chanangula akieleza wagonjwa walio kimbizwa katika Hospitali ya Peramiho na sabababu zilizo mfanya kuidhinisha kwenda kutibiwa huko amesema ni kutokana wengi kuvunjika mikono miguu na Majeraha makubwa ambayo yalihitaji vipimo vya Exray

  Wagonjwa walio nusurika katika ajali iliyo tokea barabara Mkenda Songea Maeneo ya Mlima Mkwaya wamesema ajali hiyo ilitokana na mwendo wa Kasi na Gari aina ya Center Ilikosa Breki na Dereva baada ya kuona hana Breki alilazimika kuigonga Rand rover iliyo kuwa mbele yake na kuongeza ajali nyingine.

  Wananchi wengi walio ongea na mwandishi huyu wamesema barabara ya Songea Mkenda kuelekea mpakani msumbiji magari mengi yanayo tumika ni Marori. Hata hivyo Roli hizo ni mbovu hakuna gari lenye uhakika linalo elekea mpakani

 15. mwambungu

  13/09/2012 at 6:03 pm

  lakini mwanzoni mwa mkasa huu polisi walisema eti wafuasi wa chadema ndio waliorusha kitu kinachosemekana kuwa bomu baada ya ushahidi wa picha za waandishi wa habari, polisi wameonekana kwamba walikuwa wanaudanganya umma wa watanzania wakiongozwa na RPC wa iringa ashukuriwe mungu kwamba waandishi wa habari JASIRI waliendelea kuchukua matukio ya kinyama waliyofanya hawa askari dhidi ya marehemu DAUD MWANGOSI, wakiongozwa na RPC Kamhanda, inashangaza kuona mpaka sasa huyu RPC hajaachia ngazi sijui nani anamlinda na kwa faida gani, POLISI wanatakiwa watambue kwamba sisi ndfio waajiri wao wakuu wanaishi kwa kutegemea KODI zetu inatia kichefuchefu kuona kwamba Jeshi la polisi linaendeleza tabia CHAFU ya kuua RAIA wasio na hatia je hivi wao wanadhani hoa wanao watumia vibaya watakapo kaa pembeni hali itakuwaje kwa upande wao? HII NI NCHI YETU SOTE WASIJIGEUZE MIUNGU WATU WAKATI KODI ZETU NDIO ZINAENDESHA MAISHA YAO.

 16. Hasani

  15/09/2012 at 3:40 pm

  Mwanadamu amemtawala mwanadamu mwezake kwa Hasara
  Hakuna Serikali itakayofanya vizuri katika dunia yetu

 17. george daudi

  28/09/2012 at 10:45 am

  wanadamu wanafanya kitu kisichowezekana kwenye macho ya mungu,

 18. Emmanuel

  05/10/2012 at 3:08 pm

  Polisi wawe waangalifu kwa raia kwani huyu alikuwa kazini ila kwa dhambi ya kuwanyanyasa raia bila kujua adhabu ya mungu inakuja amejikuta akienda kizimbani peke yake…

  Najiuliza asingekuwa Mwangosi akawa ni raia kama wa Morogoro unadhani angekamatwa na mtu yoyote au kuandikwa na vyombo vya habari mara nyingi hivi?

 19. walwale

  10/10/2012 at 12:14 am

  chochote kinacho zaliwa lazima kife no matter its a human being or political party as long as kimepitia hatua ya kuzaliwa lazima kitakufa je tunakaa upande upi na decisions zetu zipo fair baada ya walio zaliwa tutakapokufa kumaintain au tupo tayati kuwa charged nao its a matte
  r of generations to determine it

 20. Gaston Mbilinyi

  26/12/2012 at 9:45 pm

  Miezi yazidi kukatika tu! Kesi iko wapi? Au upelelezi haujakamika?!? Kweli watz tu maboya! Tunataka afe nani ndo tuchukue hatua? Mitandao Kama hii ndo ilikuwa ndo pakuchangia mawazo juu hatua gani tuwachukulie hawa wajiitao mapolisi pamoja na serikali iliyopo madarakani kwa ujumla wake. Badala yake…..!!!!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Featured

UJASUSI: Jinsi kijana wa kiume kutoka New Zealand alivyojaribu  kumuua Malikia Elizabeth II

Published

on

Shirika la Ujasusi la New Zealand  (SIS) limethibitisha kwa mara ya kwanza kwamba kulikuwa na jaribio la kumuua Malikia Elizabeth II wakati alipotembelea jiji la Kusini la Dunedin mwaka 1981.

Jaribio hilo la kumuua Malikia linalodaiwa kutekelezwa na kijana wa kiume limechochea hamasa ya polisi kutaka kujua ni kwa kiasi gani wanausalama hao walifanikiwa kuzima njama hizo.

Taarifa iliyotolewa na SIS  zinaonesha kuwa kijana huyo, Christopher Lewis (17) alipiga risasi kuelekea kwa Malikia wakati akishuka kwenye gari lake ambapo alikuwa anaenda kushuhudia Maonyesho ya Sayansi yaliyofanyika Oktoba 14, 1981 katika jiji hilo. Tukio hilo lilitokea akiwa katika ziara ya siku 8 kutembelea nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.

“Lewis alidhamiria kumuua Malikia, hata hivyo hakuwa katika nafasi nzuri ya kurusha risasi, hata silaha iliyotumia haikuwa katika umbali wa kuweza kumfikia mhusika,” imesema taarifa iliyotumwa SIS kwa vyombo vya habari.

Lewis ambaye anatajwa kwenye taarifa ya ujasusi kama ‘kijana msumbufu’ hakuhukumiwa kwa jaribio la kutaka kuua au kosa la uhaini. Tukio hilo lilifanywa kuwa siri ili kuzuia sifa mbaya kwa nchi (New Zealand) ambayo ilitembelewa na mgeni wa heshima. Badala yake Lewis alihukumiwa kwa kumiliki silaha kinyume na sheria na kufyatua risasi.

                       Malikia Elizabeth II akiwa ameambatana na walinzi wake alipotembelea New Zealand

Inaelezwa kuwa watu waliohudhuria tukio la kuwasili kwa Malikia walisikia mlio wa risasi lakini Polisi waliokuwa wanasimamia usalama katika eneo hilo la Dunedin waliwaambia kuwa ilikuwa ni sauti ya kuanguka kwa kitu au magari kugongana.

“Uchunguzi wa sasa wa polisi juu milio iliyosikika umefanywa kwa umakini na wawakilishi wa vyombo vya habari wamepata mrejesho kuwa kelele zilisababishwa na baruti”, inaeleza ripoti kutoka SIS iliyotolewa mwaka 1981 baada ya kutokea tukio hilo.

Kulingana taarifa za ujasusi zinaeleza kuwa polisi wamekuwa wakifuatilia nyendo za Lewis tangu 1986 ambapo Malikia alitembelea tena New Zealand wakiogopa kuwa anaweza kutekeleza tena uhalifu huo. Kuwekwa wazi kwa siri hiyo kumewaibua polisi ambao wameanza kuchunguza upya kesi hiyo.

Zaidi ya muongo mmoja uliopita, Lewis alihukumiwa kwa mauaji ya mwanamke mmoja katika mji wa Auckland na kumteka mtoto wa kike ambapo baadaye alimtupa karibu na kanisa.

Kulingana na taarifa mbalimbali za wakati huo zinaeleza kuwa Lewis alijidhuru kwa umeme akiwa gerezani mnamo 1997 akisubiri hukumu ya kuua. Lakini alikana mashtaka ya kuua kwa ujumbe mfupi wa kifo (suicide note).

New Zealand ilipata uhuru mwaka 1947 kutoka kwa Uingereza lakini inamuheshimu Malikia kama kiongozi wa taifa. Ameitembelea nchi hiyo kama Malikia mara 10 na mara ya mwisho ilikuwa 2002.

Continue Reading

Featured

FREEDOM HOUSE: Tanzania ina uhuru kiasi, kufungiwa vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya kisiasa kuididimiza kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa

Published

on

Ripoti mpya iliyotolewa na taasisi huru ya Freedom House imesema misingi ya demokrasia ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kukusanyika imeendelea kudhoofika nchini Tanzania na hali hiyo isiporekebishwa itaingia kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa duniani.

Kulingana na  Freedom House  ambao walichambua data katika nchi 195 za ulimwenguni katika mwaka 2017 wamebaini kuwa nchi 88 zina uhuru,  58 zimejumuishwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku 48 zikiwekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa misingi ya demokrasia ikiwemo uchaguzi usio huru na haki, uhuru wa kujieleza umeendelea kushuka kwa mwaka wa 12 mfufululizo duniani kote. Miongoni mwa matokeo yaliyostaajabisha ni kudhoofika kwa  Marekani ambayo ni mama wa demokrasia kutokana na uchunguzi unaofanywa na Mwendesha Mashtaka Maalumu kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 ambao ulimpa ushindi Rais Donald Trump.

Tanzania imewekwa kwenye nchi 88 ambazo zina uhuru kiasi lakini inatahadharishwa kuwa inaweza kuingia kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa. Tahadhari hiyo inatokana na mwenendo wa viongozi wa serikali kufungia vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kushtakiwa kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa tuhuma za uchochezi na kukamatwa kwa wapinzani wa kisiasa ambao wanakosoa na kutoa mawazo yanayotofautiana na serikali.

Pia utekelezaji wa Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 na Sheria ya Makosa ya Mtandao  ya mwaka 2015 umekuwa ukilalamikiwa na wadau wa maendeleo kuwa ni mkakati wa kudhoofisha uhuru wa kutoa maoni, uwazi na uwajibikaji.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini hivi karibuni kilitoa tamko la tathmini ya uchaguzi mdogo wa marudio wa kuchagua madiwani uliofanyika katika kata 43 kwenye mikoa 19 ya Tanzania  Novemba 24 mwaka jana ambapo kilibaini mambo mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Tathmini hiyo iliibua mambo mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya nguvu ya vyombo vya dola, matukio ya watu kutekwa na watu wasiojulikana, watu kupigwa, kujeruhiwa  kwa lengo la kuharibu na kuvuruga uchaguzi  na vilevile kuwatia hofu wapiga kura.

 

Afrika Mashariki hali bado tete

Tanzania inaungana nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya na Uganda ambazo nazo zimewekwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku za Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini zimejumuishwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa.

Awali Uganda ilikuwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa lakini imepanda hadi kwenye uhuru kiasi kwasababu ya  kuimarika kwa tasnia ya habari na utashi wa wanahabari, blogu na  uhuru wa wananchi kutoa maoni yao licha ya mazingira ya kisiasa kuminywa na utawala wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni.

Rais Museveni mwenye umri wa miaka 73 amekuwepo madarakani  tangu 1986 amefanikiwa kubadilisha sheria  ya ukomo wa umri wa miaka 75 wa kugombea urais ambapo atapata fursa ya kugombea tena mwaka 2021. Chaguzi nchini Uganda zimekuwa zikitawaliwa na vurugu za polisi na wananchi, kuzimwa kwa intaneti na kuwekwa kizuizini kwa viongozi wa upinzani ikiwemo Kizza Besigye wa chama cha Forum for Democratic Change.

Kwa upande wa Kenya ambayo imekuwa ikisifika kwa kuimarisha misingi ya demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo kwa mara ya kwanza mahakama ilifanikiwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Urais yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta uliofanyika Agosti 2018. Uchaguzi ulirudiwa na Rais Kenyatta alichaguliwa tena.

Marudio ya uchaguzi yalilamikiwa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa hayakuzingatia haki za binadamu ambapo watu ambao walipinga uchaguzi huo walikumbana na mkono wa dola. Matendo hayo ndiyo yaliiweka Kenya kwenye kundi la nchi zilizo na uhuru kiasi.

Burundi na Sudan Kusini zimewekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa kutokana na mapigano ya kikabila ambayo yamedhoofisha mfumo wa kisiasa wa kuongoza nchi. Vyombo vya habari na wananchi wanaotoa maoni tofauti na serikali wamekuwa wakiteswa, kufungwa na kuuwawa.

Chanzo: Freedom House           – Nchi zisizo na  uhuru  – Nchi zenye uhuru     – nchi zenye uhuru kiasi   

 

Hali ilivyo Afrika

Afrika kama zilivyo nchi za Afrika Mashariki hali ya demokrasia siyo ya kuridhisha ikizingatiwa kuwa asilimia 11 ya wakazi wapatao bilioni 1.02 wa bara hilo ndio wana uhuru wa kweli, huku 52% wana uhuru kiasi na 37% hawa uhuru kabisa.

Ripoti ya Freedom House inaeleza kuwa waliangazia nchi 49 za Afrika na kugundua kuwa nchi 8 (18%) ndio zina uhuru wa kweli, nchi 22 (43%) zina uhuru kiasi na 19 (39%) hazina uhuru kabisa. Nchi zinazotajwa kuwa na uhuru ni Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Ghana, Togo, Senegal na Kisiwa cha Sao Tome.

 Sababu ya nchi nyingi za Afrika kuwepo kwenye kundi la zisizo na uhuru ni matokeo ya viongozi kukaa madarakani muda mrefu, vurugu za kisiasa na kikabila ambazo zimekuwa zikihatarisha haki za binadamu.

 

Demokrasia ya Dunia

Demokrasia ya dunia inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kisiasa kuliko wakati mwingine ambapo mwaka 2017 ulishuhudia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo kuminywa kwa  uchaguzi huru na kweli, haki za watu wachache, uhuru wa kujieleza, utawala wa sheria.

Nchi 71 kati ya 195 zimeshuhudiwa zikiteteleka katika kulinda haki za kisiasa na jamii ambapo ni nchi 35 tu ndizo zimeweza kulinda haki hizo. Kudhoofika kwa demokrasia kunaendelea kushuka kwa miaka 12 mfululizo na hatua muhimu zisipochukuliwa amani ya dunia itawekwa rehani.

Marekani ambayo ni bingwa wa demokrasia duniani nayo imeripotiwa na taasisi ya Freedom House kudhoofika katika kulinda haki za kisiasa na kijamii na kuzua mgongano wa mawazo miongoni mwa nchi zinazoibukia katika kujenga demokrasia ya dunia.

Tangu kuisha kwa vita baridi, nchi nyingi ziliachana na utawala wa kiimla na kugeukia demokrasia ya vyama vingi lakini hali hiyo imeanza kujitokeza tena ambapo idadi ya viongozi wanaoongoza kwa udikteta inaongezeka.

 

Uhuru wa nchi moja unategemea uhuru wa nchi zote

Demokrasia itabaki kuwa tunu muhimu kwa jamii zilizostaarabika, ikifungua milango ya uwazi, mawazo na fursa mpya na zaidi ya yote kulinda uhuru wa mtu mmoja mmoja. Ikiwa watu duniani kote wanadai mazingira mazuri ya kisiasa ni dhahiri wanakumbatia misingi ya demokrasia: uchaguzi huru, uhuru wa kujieleza, uwazi na uwajibikaji wa serikali, utawala wa sheria ambao hauingiliwi na polisi, jeshi au taasisi nyingine za nchi.

Hata hivyo, Karne ya 21 imeshuhudia ugumu wa kuifanya demokrasia kuwa endelevu ambapo baadhi ya nchi zinatekeleza lakini zingine zinapuuza. Utawala wa kidekteta wa Urusi na China unatambua wazi ili uendelee kuwepo unahitaji kuimarisha demokrasia katika nchi nyingine ili ziendelee kufaidika na mahusiano ya kidiplomasia. Ukuaji wa  demokrasia ni kulinda haki za watu wote duniani kupitia utandawazi   

Continue Reading

Afya

Is Tanzania’s Adolescent Fertility Rate Three Times Higher Than Global Counterparts?

Published

on

The Comprehensive Community-Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT), an organization ​which works to provide affordable medical and rehabilitative services for mothers and newborns throughout Dar-es-Salaam, marked World Contraception Day on September 26 with a call for more efforts to meet the reproductive health needs of teens between 15 and 19 years old.

The report highlights a worrying statistic — Tanzania’s adolescents are having almost three times as many children on average as their global counterparts, with 135 births per 1000 girls reported in the country, compared to an average of 44 per 1000 girls aged 15–19 worldwide in 2015.

CCRBT attributes the high adolescent fertility rate to a lack of access to contraceptive services, with Technical Advisor for Nursing Bola Abbas saying, that only about 8 per cent of current family planning clients are between the ages of 15 to 19.

On a national scale, Abbas explains, demand for family planning among adolescent girls is still very low, with only one out of every three of those who are sexually active within the 15 to 19 age group using modern contraceptive methods.

So the question is, how does Tanzania’s adolescent fertility rate compare to that of the rest of the world?

Pesacheck investigated the claim that Tanzanian adolescents are having three times as many children as their peers in the rest of the world and found that the statement is TRUE for the following reasons:

Tanzania’s adolescent fertility numbers are rather high, with 4.4% of girls aged 15 having given birth according to the country’s Demographic and Health Survey.

The Sustainable Development Goals call for countries to ensure universal access to sexual and reproductive healthcare services, including family planning, information and education, and the integration of reproductive health into national strategies and programmes by 2030.

The indicators for this goal are the proportion of women of reproductive age (15–49 years) who have their need for family planning satisfied with modern methods, and the adolescent birth rate (10–14 years and 15–19 years) per 1,000 women in that age group.

For several sub-Saharan countries, Tanzania included, access to modern family planning methods is low for this particular age group, and as a result, the regional average is 105 births per 1,000, which is more than double the global average.

Tanzania’s National Bureau of Statistics produced a national fertility and nuptiality report based on data from the 2012 national census, which shows that Adolescent Fertility Rate (AFR) was 81 births per 1,000 women aged 15–19.

The report further shows that in 2012, 23.3% of adolescent girls in the country had given birth to at least one child. Additionally, 42.2% of girls who had never attended school had given birth, compared to just 9% of those who had reached university.

This shows that there is a need for contraceptive access for teenage girls in Tanzania, especially for girls in rural areas and those with limited access to education.

The Tanzania Demographic and Health Survey 2015–16 indicates that 27% of girls aged 15–19 have given birth. Crude birth rates for girls aged 15–19 show that there 135 births per 1,000 girls in Mainland Tanzania and 132 per 1,000 girls in Zanzibar, way above the global average of 44. The data also shows that contraceptive access for this age group is also quite low, with 10.4% of girls aged 15–49 using any form of contraception.

It would therefore appear that the lack of access to contraceptives is contributing to the increased likelihood of adolescent girls getting pregnant.

So the claim by CCBRT that Tanzania’s adolescent fertility rate is almost three times the global average is TRUE. This is driven largely by a lack of access to contraceptives for young people in the 15–19 age group, and the relatively high levels of poverty that have driven many out of school and into early marriage.

As a result, the country is unlikely to meet the Sustainable Development Goal of overall good health and wellbeing of mothers unless it puts measures in place to ensure universal access to sexual and reproductive health-care services for girls and women of all ages.

Do you want us to fact-check something a politician or other public figure has said about public finances? Complete this form, or reach out to us on any of the contacts below, and we’ll help ensure you’re not getting bamboozled.

This report was written by PesaCheck Fellow Belinda Japhet, a Communications Consultant, Online Editor based in Tanzania. The infographics are by PesaCheck Fellow Brian Wachanga, who is a Kenyan civic technologist interested in data visualisation. This report was edited by PesaCheck Managing Editor Eric Mugendi.

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com