Connect with us

Featured

Ruvuma: Wanafunzi zaidi ya 500 wanasomea katika vibanda vya nyasi

Mwalimu Onesmo Mbawala alisema idadi kubwa ya wanafunzi wanasomea katika vibanda vya nyasi kutokana na shule yake kuwa na upungufu wa vyumba 12 vya kusomea ambapo vyumba vilivyopo ni vinne tu na kwamba shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1975 ina jumla ya wanafunzi 592.

Published

on

WANAFUNZI wa shule tatu za msingi zaidi ya 500 katika kata ya Rwinga wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wanasomea kwenye madarasa yaliojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi.

Uchunguzi uliofanywa katika shule tatu kati ya saba zilizopo kwenye kata hiyo ambayo ipo mjini Namtumbo umebaini kuwa  katika shule ya msingi Rwinga wanafunzi  296  wanasomea kwenye vibanda vya miti vilivyoezekwa kwa nyasi .

Mwalimu wa taaluma katika shule hiyo Onesmo Mbawala alisema idadi kubwa ya wanafunzi katika shule hiyo wanasomea katika vibanda vya nyasi kutokana na shule hiyo kuwa na upungufu wa vyumba 12 vya kusomea ambapo vyumba vilivyopo ni vinne tu na kwamba shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1975 ina jumla ya wanafunzi 592.

wanafunzi-rwinga-school

Wanafunzi wa darasa la awali wapatao 92 shule ya msingi Rwinga wilayani Namtumbo wakiwa darasani na mwalimu wao

Katika shule ya msingi Selous jumla ya wanafunzi 108 wa madarasa ya tano na sita wanasoma kwenye vibanda vya nyasi hali ambayo walimu wanasema inachangia kushusha taaluma kwa wanafunzi.

wanafunzi-selous-school

Wanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Selous wilayani Namtumbo wakiwa darasani

Mwalimu  wa taaluma katika shule hiyo Sheweji Simba  alisema shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007 ina jumla ya wanafunzi 477 huku ikiwa na vyumba vinne tu vya madarasa kati ya mahitaji ya vyumba nane hali ambayo imesababisha baadhi ya wanafunzi kusomea kwenye vibanda vya nyasi .

Katika shule ya msingi Mkapa ambayo imepewa jina la aliyewahi kuwa kiongozi mkuu wa nchi  Rais mstaafu Benjamin Mkapa pia kuna wanafunzi  wanaosomea kwenye vibanda viwili vya nyasi  kwa kuwa shule hiyo ina vyumba vinne tu kati ya mahitaji ya vyumba nane.

wanafunzi-mkapa-school

Wanafunzi wa shule ya msingi Mkapa wilayani Namtumbo wakiwa darasani na mwalimu wao

Mkuu wa shule hiyo Hans Mwailima alisema shule hiyo yenye wanafunzi 306 madarasa matatu yanasomea katika chumba kimoja  ambapo kuanzia darasa la tatu hadi la sita  wanasomea kwenye vibanda vya nyasi kwa zamu.

“Unajua wanafunzi wana tabia ya kutaniana hivyo endapo darasa moja wakisoma kwenye vibanda vya nyasi kila siku wenzao wanawatania hivyo kukata tamaa na wengine kuwa watoro hivyo tumeamua wote wawe wanasoma kwenye vibanda vya nyasi kwa zamu ili kujenga mvuto wa mazingira ya kusomea’’, alisema.

Mratibu elimu kata ya Rwinga Thomas Komba amekiri shule  tatu kati ya saba katika kata yake ambazo ni Rwinga, Mkapa na Selous wanafunzi kusomea katika vibanda vilivyojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi na kusisitiza kuwa shule za Minazini, Kidagulo, Migelegele na Mandepwende ndizo shule pekee katika kata hiyo ambazo hazina vyumba vya madarasa vilivyoezekwa kwa nyasi.

“Shule zangu  tatu za Rwinga,Mkapa na Selous katika kata yangu zinakabiliwa na upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa hali ni mbaya tunafanya jitihada za kuhamasisha jamii ili waweze kujitolea kufyatua tofali kuzichoma kwa kushirikiana na serikali  ili kupata vyumba zaidi na kumaliza kero hii ya aibu’’, alisisitiza.

Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Kasimu Ntara alidai kuwa kuwa kuwepo kwa madarasa yaliojengwa kwa miti na kuezekwa kwa nyasi katika wilaya hiyo kunatokana na kuanzishwa shule nyingi za msingi.

“Mpango wa uboreshaji wa elimu ya msingi MEM nchini ulisababisha kuanzishwa kwa shule nyingi hivyo  baada ya kuondoka kwa MMEM serikali imeshindwa kumudu ujenzi wa vyumba vya madarasa jitihada zinaendelea kufanyika kukabiliana na upungufu wa vyumba vya madarasa’’, alisisitiza.

Habari hii imeandikwa na Albano Midelo, FikraPevu – Ruvuma

Continue Reading
42 Comments

42 Comments

 1. Geofrey

  11/05/2012 at 9:23 am

  Miaka hamsini ua Uhuru sherehe ilikuwa ya nini sasa. Mijihela yote ile bado…….hali iko hivi. Nchi hii haifai.

  • Moses matinya

   17/05/2012 at 9:39 am

   Hali ya nchi kweli ni mbaya so tuchukue hatua ya kumaliza tabaka tawala kwa kuliweka tabaka lingine na chama mbadala.

 2. Dennis

  11/05/2012 at 11:37 am

  Maskini Tanzania,hivi kweli hata hii buget ya kukimbiza mwenge nchi nzima isingetosha kuwapatia hawa watoto madawati?

  • Mtumishi Wetu

   12/05/2012 at 2:19 pm

   Mkuu wacha hiyo budget ya mwenge je sherehe za muungano budget yake ilikuwa kiasi gani???? Hizo pesa sizingesogeza hata tukapata madara kama 50, kweli Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuwa kupanga ni kuchagua!!!!!

 3. Dennis

  11/05/2012 at 11:39 am

  Ee Mola tupe hekima na huruma,rasilimali zote umetupa tatizo ubinafsi

 4. allen mashauri

  11/05/2012 at 12:31 pm

  Is this a reflection of “MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA?”….the government on power should be accountable

 5. Mahmoud

  11/05/2012 at 12:44 pm

  Umeonaa een.!

  • Solokondo

   12/05/2012 at 1:48 am

   Hahahhhhhhh ccm ccm ccm

 6. Mahmoud

  11/05/2012 at 12:48 pm

  Yaan tukiambiwa cc tuna mabupuru sio marais tunaona watu wanatufanyia masihara…Angalien mambo hayo. Yaani hii nchi yetu hata mtoto mdogo anaweza kuiendesha, au bora yeye anaweza akaiendesha vizuri kuliko huyo tunaemwita ni Rais. Coz hata mtoto mdogo nadhani ungempa mamlaka angeweza kulitatua hili kwanza kabla hata kugarimika na masherehe na maSemina yasio na tija kwa wananchi, isipokua kwa maslahi ya wachache.

 7. HAMISI

  11/05/2012 at 1:30 pm

  Tena kwa ujinga wa viongozi wetu na wasivyokuwa na haya, huchukua picha hizi kwenda kupitishia bakuli. Hii nchi imelaaniwa, au viongozi wamefanya ilaaniwe.

 8. jonathan K

  11/05/2012 at 4:01 pm

  chagua ccm kwa maisha bora
  maisha bora ndio haya kupeana ulaji kuuza rasilimali za nchi,kutenga mafungu makubwa ktk sherehe,matamasha,mavazi nk huku watoto wao wakisoma shule za kimataifa.kuna haja sasa kuamka watanzania kuachana na mfumo nyonyaji.tunalalamika hadi tuchukue hatua sasa

  • Power

   13/05/2012 at 9:01 am

   Mkuu, bahati mbaya hawa watu wa kusini licha ya maisha magumu waliyosababishiwa na ccm, ndiyo kwanza wanaikumbatia kwa juhudi zao zote.

 9. oswald laswai

  11/05/2012 at 10:20 pm

  Inashangaza wanajamii kusikia umasikini jirani na hifadhi ya Selous matatizo yote yanaweza kutatuliwa endapo tutarudi katika maadili Ndugu zangu viongazi wa ngazi za juu hili linawatia aibu msilale lishughulikieni haraka

 10. benard hezron

  12/05/2012 at 1:20 am

  mungu tusaidie watanzania wa tabaka maana tunaliwa sana na tabaka la juu ebu angalia hawa watoto wako kwenye hali mbaya sana.

 11. patrick bida

  12/05/2012 at 2:35 am

  Wala haishangazi!.Hilo ni moja tu kati ya maelfu ya maeneo hapa nchini yenye hali kama hiyo.TEMBEA UONE!! Huko ndipo CCM wanapopatia kura. Maeneo kama haya wasitarajie mapinduzi yoyote ya kielimu kwakuwa ndiyo maeneo yanayotoa na kuandaa zao tawaliwa la milele,zao bubu lisiloweza kuhoji chochote.

  Tabaka kandamizwa lisiloona wala kutambua. Tabaka linaloandaliwa kuviandaa vizazi na vizazi vya tabaka fanana lenye ubongo timamu usofanya kazi yake sawasawa, akili timamu isiyoweza pambanua, macho angavu yasoona, mikono na miguu kamili isoweza kunjuka na kureact. Ni maeneo teseka yenye faida kubwa kwa Utawala.

 12. Mayelle

  12/05/2012 at 5:35 am

  Maisha bora kwa kila Mtanzania, Rais anasafiri safari 400 nje ya nchi kwa muda wa miaka 6, utawala miaka 5, mwaka 1 U Vasco dagama.

 13. agathon

  12/05/2012 at 5:59 am

  Lakini huko ndiko kwa Vita Kawawa halioni hilo?

 14. Verykings

  12/05/2012 at 6:39 am

  Jamani lazima ifike mahali tuseme enough is enough! Watu kodi wnatoa, TRA wanakusanya hadi wanavunja rekodi then provision of social service ndo hivi! We must be wicked!!

  • Ngoma

   12/05/2012 at 9:16 am

   Tatizo posho zinamaliza makusanyo yote!

 15. Kombo

  12/05/2012 at 8:16 am

  Hii nchi inahitaji maombezi. Viongozi wetu hawajitambui, vipaumbele vya Taifa havijulikani na Wananchi hatujui wajibu na uwezo wetu dhidi ya Viongozi wanaotupoteza. Ee Mola itazame Tanzania, Watazame Watanzania….!

 16. Ngoma

  12/05/2012 at 9:15 am

  Inaonyesha mwamko wa elimu nchini, serikali ijitahidi kufikisha uduma hii muhimu kwa wanaoihitaji!.

 17. Prez-Dento

  12/05/2012 at 9:36 am

  Wameikumbatia ccm na ccm inawalisha ujinga mikoa ya kusini inahitaji ukombozi.

 18. Alexander

  12/05/2012 at 9:56 am

  Hayo ndiyo maisha bora kwa kila mtanzania wamejaribu wameweza na wanasonga mbele sasa sijajua kama hawa bado wanasonga nao mbele au wamewaacha nyuma

 19. Paul Kijoka

  12/05/2012 at 11:14 am

  Du! Duniani kuna mambo isee! Hali hii iko Tz nzima na hawa ndo wapiga kura wa CCM

 20. Tume ya katiba

  12/05/2012 at 1:17 pm

  Masikitiko makubwa sana kwa serikali yetu,

  Kwa hakika watoto wana nyuso za furaha lakini kiuhalisia ni huzuni kubwa sana.

  By tume ya katiba

 21. la masia

  12/05/2012 at 1:44 pm

  matatizo ni ye2 cc wnyw wapiga kura,watu hawajapata elimu ya kutosha khs upigaj kura,mambo haya kwa wenzetu kenya hayapo,km una umri wa kupiga kura haujafanya hivyo ni viboko tu maana wanajua ww ndie chanzo cha kutoleta mabadiliko!haya hayawez kwisha kwa upande we2 coz viongozi we2 wanajua hatuwez kuwafanya ki2,uchaguz ukifika wanajua watarudi tu,watanzania tunasikitisha sn.

 22. Mbiti Ya Songo

  12/05/2012 at 1:47 pm

  Kwanza Lawama na ujinga ni za wapiga kura(watanzania) ambao tumeridhia na hali hii ya maisha tuliyo nayo, hivyo na kuiweka serikali madarakani kwa kuipigia kura. Mfano gharama za kuendeshea shughuli za wilaya zote za tanzania zingeweza kujenga shule nk. basi kwa nini serikali isibane matumizi yasiyo ya muhimu na kutafuta mbadala? tanzania ina zaidi ya wilaya 132, kila mkuu wa wilaya anapewa toyota landcruiser, tamani ya gari 1 ni Tsh 80,400,000 zidisha wlaya 132.

  KAZI KWENU WAPIGA KURA

 23. la masia

  12/05/2012 at 1:57 pm

  AIBU!!!

 24. Ndama

  12/05/2012 at 2:57 pm

  “Unajua wanafunzi wakisomea kwenye vibanda vya nyasi hukata tamaa na wengine kuwa watoro’’ kwa mtaji huu wizara bado inatafuta mchawi wa matokeo mabaya???? jamani tuwe wazi hapa ni kwamba mpango wa serikali ni bora elimu kwa kila mtanzania. hata kama utaleta wazungu wafundishe kwa mazingira haya sina hakika kama wanafunzi watafaulu na hii ni kwa s/msingi ukigeuka upande wa pili s/ssecondary ndio balaaaaaaa! Nashauri serikali ibadili policy yake kuhusu elimu badala ya shule nyingi miundo mbinu hafifu + hakuna walimu basi iwe shule chache miundo mbinu mizuri + walimu wa kutosha.

 25. badili tabia

  12/05/2012 at 6:51 pm

  kidumu chama cha mapinduzi

 26. Mussa

  13/05/2012 at 5:53 am

  Kwa kweli hali ni mbaya, tangu waanze kula, ni matrilioni mangapi? Hakuna anayefilisiwa tangu kesi zianze! Sioni nuru katika miaka mitatu ijayo kwa Chama Tawala

 27. praygod

  13/05/2012 at 2:44 pm

  hali inatisha kwel kwan ha2jengi bal 2nabomoa

  • Lembris L Mollel

   16/05/2012 at 12:03 am

   Tusipokomaa Kijana nakwambia tutauzwa! Hakuna ubomozi hapa.

 28. praygod

  13/05/2012 at 2:53 pm

  hali inatisha tz

 29. MIZAMBWA

  14/05/2012 at 5:03 pm

  Lakini hawa watu wa Songea si ndio wale wale Capt. John Komba akiwaimbia ” WATANZANIA WOTE, WATANZANIA WAPUMBAZWA, WATANZANIA WOTE … WATANZANIA WATANZANIA WAPUMBAZWA. NAMBARI WANI.. NAMBARI WANI EEE, NAMBARI WANI NI CCM. WANGONI WOTE TIENI, TIENI, WOTE TIENI TIENI TIENI KWA MOYO MMOJAAAA NAMBARI WANI EEE.. NAMBARI WANI NI CCM..

  kisha wanamshangilia mgoni mwenzao; sasa leo wanalalamika nini ikiwa wanapenda uzalendo kwa kumfuhisha John Komba.

  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!

 30. MIZAMBWA

  15/05/2012 at 2:43 pm

  SErikali itumie Change ya RADA kuelekeza katika elimu kwa shule za vijijini ili vijana wetu wapate elimu bora kwa kuwawekea mazingira mazuri ya kusoma.

  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!

 31. kabuzi

  15/05/2012 at 3:47 pm

  “Lakini hawa watu wa Songea si ndio wale wale Capt. John Komba akiwaimbia ” WATANZANIA WOTE, WATANZANIA WAPUMBAZWA, WATANZANIA WOTE … WATANZANIA WATANZANIA WAPUMBAZWA. NAMBARI WANI.. NAMBARI WANI EEE, NAMBARI WANI NI CCM. WANGONI WOTE TIENI, TIENI, WOTE TIENI TIENI TIENI KWA MOYO MMOJAAAA NAMBARI WANI EEE.. NAMBARI WANI NI CCM..”
  Nimeipenda hii yako MIZAMBWA; naikubali sana. Huko ndiko wanasema ccm ni baba ccm ni mama. Poleni sana.

 32. Lembris L Mollel

  15/05/2012 at 11:59 pm

  Hiyo ndiyo:

  Ari Mpya

  Kazi Mpya

  Nguvu Mpya.

  Tusipokomaa na hawa mafisadi watatuuza mchana kweupeeeeeeeeeeee!!!!

 33. Mbatizaji

  16/05/2012 at 8:57 am

  Hamna wizi wala nini. Ni wivu wenu tu. Acheni wivu wa kike. Mwenye wivu ajinyonge. Maisha bora bado yaja.

 34. Moses matinya

  17/05/2012 at 9:34 am

  Kazi ipo wajomba,kwa kila jambo huanza na antagonist clas so huu ndio muda wetu vijana kuleta changes ili ccm ife kifo cha natural death kwa maslahi ya taifa.

 35. lcs

  03/06/2012 at 2:07 am

  Marehemu Julius Kambarage Nyerere alipochukuwa nchi hii kwa wakoloni kama angekuwa mbinafsi kweli hatungekuwa pale aliptuacha na kuondoka mwaka 1999

  Nasema hivyo kwa sababu kama tukianza na elimu alijitahidi kujenga shule nyingi sana za msingi, sekondari , vyuo vya elimu, vyuo vya ufundi vyuo vikuu /Chuo kikuu Dar es salaam/chuo cha Ardhi, vyou vya elimu ya juu kama mzumbe, vyegezi nk

  Kwei nasema kwa uchungu akajitahidi kuwepo na Azimio la Arusha mwaka 1967 ili tuu kuhakukisha hakuna ufisadi katika utawala wake.

  Katika secta ya maji baada ya kurithi bwawa la nyumba ya Mungu aalijitahidi kujenga Mtera, Kdatu kuweka Umeme wa Gridi

  Katika secta ya madini alikataa kuchimba madini yaliendelea kuchimbwa ya mwadui mkataba uliokuwepo kabla ya uhuru.

  Alikataa kwasababu alijua sera za magharibi sers za trace passing sera za kuhamisha mali kwani hatuna vitendea kazi

  Lakini hebu baada ya kuondoka ni jambo gani jipya lililofanyika watanzania wenzangu dola ya marekani imeshuka tangu pale alipokufa kutoka mamia kwenda maelfu maana yake ni nini hakuna tena mazao hakuna tena pamba ya kupeleka nyingi , nchi inaagiza vitu vingi kuliko mauzo nje

  Mali asili zikaanza kuhamishwa, bustani ya bunge, wanyawa tausi, mikataba ya uvunaji wanyama Loliondo ,nk machimbo ya Gesi ambayo tulitarajia yangeinua uchumi kwa kuwasha umeme nchi nzima imekuwa ndoto

  Elimu ndiyo hii inaendelea kushuka madasara sasa yanaendelea kuwa ya nyasi baada ya miaka 50 ya Uhuru

  Hebu kila mtanzania ajiulize je hii ni vema inapendeza kuona matabaka baada ya kuvunjwa azimio la Arusha na kuanzisha Azimio la Zanzibar

  Hebu tufahamu muda wetu wa kuishi hapa duniani ni miaka 70 hebu tupendani tuache kulimbikiza mali ambazo hatuna kazi nazo tuache uchoyo .

  Kweli nasema kama Mwalimu Nyerere angekuwa mchoyo familia yake ingekuwa milionea ona baadhi ya watoto wake wamo upinzani haipendezi

  Hebu tubadilike kwani wakati mwalimu anaanzisha vyama vingi alisema kiongozi mzuri atatoka CCM sasa kwanini atoke CCM aende upinzani

  Kwanini viongozi tuliopewa dhamana ya kuongoza Taifa hili tusiwe kama Mwalimu Nyerere tubadilike ili tuwaamini viongozi waliopewa jukumu hilo

  Je kweli inaendelea kupendeza kuona baada ya nusu karne watoto wetu bado wanasomea kwenye nyumba za nyasi makuti na wachache wako kwenye shule za kulipia

  Naomba tuangalie hapa Songea kama mfano

 36. Mpenda Wakoloni

  20/07/2012 at 11:28 pm

  ndugu yangu hii ni afadhali isiwepo hapo. Inatia uchungu sana kuiskia mdomo wa binadamu unaahidi maisha bora halafu watoto hawa wanasoma kwenye vibanda vya nyasi.
  Halafu mdomo huo huo unajisifu kuwa umeleta maendeleo. HAYA YA KUSOMEA KWENYE VIBANDA VYA NYASI? Yeyote anayesifia mtawala lazima naye anafaidika na kutawala kwao. Damn country.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Featured

UJASUSI: Jinsi kijana wa kiume kutoka New Zealand alivyojaribu  kumuua Malikia Elizabeth II

Published

on

Shirika la Ujasusi la New Zealand  (SIS) limethibitisha kwa mara ya kwanza kwamba kulikuwa na jaribio la kumuua Malikia Elizabeth II wakati alipotembelea jiji la Kusini la Dunedin mwaka 1981.

Jaribio hilo la kumuua Malikia linalodaiwa kutekelezwa na kijana wa kiume limechochea hamasa ya polisi kutaka kujua ni kwa kiasi gani wanausalama hao walifanikiwa kuzima njama hizo.

Taarifa iliyotolewa na SIS  zinaonesha kuwa kijana huyo, Christopher Lewis (17) alipiga risasi kuelekea kwa Malikia wakati akishuka kwenye gari lake ambapo alikuwa anaenda kushuhudia Maonyesho ya Sayansi yaliyofanyika Oktoba 14, 1981 katika jiji hilo. Tukio hilo lilitokea akiwa katika ziara ya siku 8 kutembelea nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.

“Lewis alidhamiria kumuua Malikia, hata hivyo hakuwa katika nafasi nzuri ya kurusha risasi, hata silaha iliyotumia haikuwa katika umbali wa kuweza kumfikia mhusika,” imesema taarifa iliyotumwa SIS kwa vyombo vya habari.

Lewis ambaye anatajwa kwenye taarifa ya ujasusi kama ‘kijana msumbufu’ hakuhukumiwa kwa jaribio la kutaka kuua au kosa la uhaini. Tukio hilo lilifanywa kuwa siri ili kuzuia sifa mbaya kwa nchi (New Zealand) ambayo ilitembelewa na mgeni wa heshima. Badala yake Lewis alihukumiwa kwa kumiliki silaha kinyume na sheria na kufyatua risasi.

                       Malikia Elizabeth II akiwa ameambatana na walinzi wake alipotembelea New Zealand

Inaelezwa kuwa watu waliohudhuria tukio la kuwasili kwa Malikia walisikia mlio wa risasi lakini Polisi waliokuwa wanasimamia usalama katika eneo hilo la Dunedin waliwaambia kuwa ilikuwa ni sauti ya kuanguka kwa kitu au magari kugongana.

“Uchunguzi wa sasa wa polisi juu milio iliyosikika umefanywa kwa umakini na wawakilishi wa vyombo vya habari wamepata mrejesho kuwa kelele zilisababishwa na baruti”, inaeleza ripoti kutoka SIS iliyotolewa mwaka 1981 baada ya kutokea tukio hilo.

Kulingana taarifa za ujasusi zinaeleza kuwa polisi wamekuwa wakifuatilia nyendo za Lewis tangu 1986 ambapo Malikia alitembelea tena New Zealand wakiogopa kuwa anaweza kutekeleza tena uhalifu huo. Kuwekwa wazi kwa siri hiyo kumewaibua polisi ambao wameanza kuchunguza upya kesi hiyo.

Zaidi ya muongo mmoja uliopita, Lewis alihukumiwa kwa mauaji ya mwanamke mmoja katika mji wa Auckland na kumteka mtoto wa kike ambapo baadaye alimtupa karibu na kanisa.

Kulingana na taarifa mbalimbali za wakati huo zinaeleza kuwa Lewis alijidhuru kwa umeme akiwa gerezani mnamo 1997 akisubiri hukumu ya kuua. Lakini alikana mashtaka ya kuua kwa ujumbe mfupi wa kifo (suicide note).

New Zealand ilipata uhuru mwaka 1947 kutoka kwa Uingereza lakini inamuheshimu Malikia kama kiongozi wa taifa. Ameitembelea nchi hiyo kama Malikia mara 10 na mara ya mwisho ilikuwa 2002.

Continue Reading

Featured

FREEDOM HOUSE: Tanzania ina uhuru kiasi, kufungiwa vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya kisiasa kuididimiza kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa

Published

on

Ripoti mpya iliyotolewa na taasisi huru ya Freedom House imesema misingi ya demokrasia ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kukusanyika imeendelea kudhoofika nchini Tanzania na hali hiyo isiporekebishwa itaingia kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa duniani.

Kulingana na  Freedom House  ambao walichambua data katika nchi 195 za ulimwenguni katika mwaka 2017 wamebaini kuwa nchi 88 zina uhuru,  58 zimejumuishwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku 48 zikiwekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa misingi ya demokrasia ikiwemo uchaguzi usio huru na haki, uhuru wa kujieleza umeendelea kushuka kwa mwaka wa 12 mfufululizo duniani kote. Miongoni mwa matokeo yaliyostaajabisha ni kudhoofika kwa  Marekani ambayo ni mama wa demokrasia kutokana na uchunguzi unaofanywa na Mwendesha Mashtaka Maalumu kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 ambao ulimpa ushindi Rais Donald Trump.

Tanzania imewekwa kwenye nchi 88 ambazo zina uhuru kiasi lakini inatahadharishwa kuwa inaweza kuingia kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa. Tahadhari hiyo inatokana na mwenendo wa viongozi wa serikali kufungia vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kushtakiwa kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa tuhuma za uchochezi na kukamatwa kwa wapinzani wa kisiasa ambao wanakosoa na kutoa mawazo yanayotofautiana na serikali.

Pia utekelezaji wa Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 na Sheria ya Makosa ya Mtandao  ya mwaka 2015 umekuwa ukilalamikiwa na wadau wa maendeleo kuwa ni mkakati wa kudhoofisha uhuru wa kutoa maoni, uwazi na uwajibikaji.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini hivi karibuni kilitoa tamko la tathmini ya uchaguzi mdogo wa marudio wa kuchagua madiwani uliofanyika katika kata 43 kwenye mikoa 19 ya Tanzania  Novemba 24 mwaka jana ambapo kilibaini mambo mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Tathmini hiyo iliibua mambo mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya nguvu ya vyombo vya dola, matukio ya watu kutekwa na watu wasiojulikana, watu kupigwa, kujeruhiwa  kwa lengo la kuharibu na kuvuruga uchaguzi  na vilevile kuwatia hofu wapiga kura.

 

Afrika Mashariki hali bado tete

Tanzania inaungana nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya na Uganda ambazo nazo zimewekwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku za Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini zimejumuishwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa.

Awali Uganda ilikuwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa lakini imepanda hadi kwenye uhuru kiasi kwasababu ya  kuimarika kwa tasnia ya habari na utashi wa wanahabari, blogu na  uhuru wa wananchi kutoa maoni yao licha ya mazingira ya kisiasa kuminywa na utawala wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni.

Rais Museveni mwenye umri wa miaka 73 amekuwepo madarakani  tangu 1986 amefanikiwa kubadilisha sheria  ya ukomo wa umri wa miaka 75 wa kugombea urais ambapo atapata fursa ya kugombea tena mwaka 2021. Chaguzi nchini Uganda zimekuwa zikitawaliwa na vurugu za polisi na wananchi, kuzimwa kwa intaneti na kuwekwa kizuizini kwa viongozi wa upinzani ikiwemo Kizza Besigye wa chama cha Forum for Democratic Change.

Kwa upande wa Kenya ambayo imekuwa ikisifika kwa kuimarisha misingi ya demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo kwa mara ya kwanza mahakama ilifanikiwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Urais yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta uliofanyika Agosti 2018. Uchaguzi ulirudiwa na Rais Kenyatta alichaguliwa tena.

Marudio ya uchaguzi yalilamikiwa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa hayakuzingatia haki za binadamu ambapo watu ambao walipinga uchaguzi huo walikumbana na mkono wa dola. Matendo hayo ndiyo yaliiweka Kenya kwenye kundi la nchi zilizo na uhuru kiasi.

Burundi na Sudan Kusini zimewekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa kutokana na mapigano ya kikabila ambayo yamedhoofisha mfumo wa kisiasa wa kuongoza nchi. Vyombo vya habari na wananchi wanaotoa maoni tofauti na serikali wamekuwa wakiteswa, kufungwa na kuuwawa.

Chanzo: Freedom House           – Nchi zisizo na  uhuru  – Nchi zenye uhuru     – nchi zenye uhuru kiasi   

 

Hali ilivyo Afrika

Afrika kama zilivyo nchi za Afrika Mashariki hali ya demokrasia siyo ya kuridhisha ikizingatiwa kuwa asilimia 11 ya wakazi wapatao bilioni 1.02 wa bara hilo ndio wana uhuru wa kweli, huku 52% wana uhuru kiasi na 37% hawa uhuru kabisa.

Ripoti ya Freedom House inaeleza kuwa waliangazia nchi 49 za Afrika na kugundua kuwa nchi 8 (18%) ndio zina uhuru wa kweli, nchi 22 (43%) zina uhuru kiasi na 19 (39%) hazina uhuru kabisa. Nchi zinazotajwa kuwa na uhuru ni Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Ghana, Togo, Senegal na Kisiwa cha Sao Tome.

 Sababu ya nchi nyingi za Afrika kuwepo kwenye kundi la zisizo na uhuru ni matokeo ya viongozi kukaa madarakani muda mrefu, vurugu za kisiasa na kikabila ambazo zimekuwa zikihatarisha haki za binadamu.

 

Demokrasia ya Dunia

Demokrasia ya dunia inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kisiasa kuliko wakati mwingine ambapo mwaka 2017 ulishuhudia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo kuminywa kwa  uchaguzi huru na kweli, haki za watu wachache, uhuru wa kujieleza, utawala wa sheria.

Nchi 71 kati ya 195 zimeshuhudiwa zikiteteleka katika kulinda haki za kisiasa na jamii ambapo ni nchi 35 tu ndizo zimeweza kulinda haki hizo. Kudhoofika kwa demokrasia kunaendelea kushuka kwa miaka 12 mfululizo na hatua muhimu zisipochukuliwa amani ya dunia itawekwa rehani.

Marekani ambayo ni bingwa wa demokrasia duniani nayo imeripotiwa na taasisi ya Freedom House kudhoofika katika kulinda haki za kisiasa na kijamii na kuzua mgongano wa mawazo miongoni mwa nchi zinazoibukia katika kujenga demokrasia ya dunia.

Tangu kuisha kwa vita baridi, nchi nyingi ziliachana na utawala wa kiimla na kugeukia demokrasia ya vyama vingi lakini hali hiyo imeanza kujitokeza tena ambapo idadi ya viongozi wanaoongoza kwa udikteta inaongezeka.

 

Uhuru wa nchi moja unategemea uhuru wa nchi zote

Demokrasia itabaki kuwa tunu muhimu kwa jamii zilizostaarabika, ikifungua milango ya uwazi, mawazo na fursa mpya na zaidi ya yote kulinda uhuru wa mtu mmoja mmoja. Ikiwa watu duniani kote wanadai mazingira mazuri ya kisiasa ni dhahiri wanakumbatia misingi ya demokrasia: uchaguzi huru, uhuru wa kujieleza, uwazi na uwajibikaji wa serikali, utawala wa sheria ambao hauingiliwi na polisi, jeshi au taasisi nyingine za nchi.

Hata hivyo, Karne ya 21 imeshuhudia ugumu wa kuifanya demokrasia kuwa endelevu ambapo baadhi ya nchi zinatekeleza lakini zingine zinapuuza. Utawala wa kidekteta wa Urusi na China unatambua wazi ili uendelee kuwepo unahitaji kuimarisha demokrasia katika nchi nyingine ili ziendelee kufaidika na mahusiano ya kidiplomasia. Ukuaji wa  demokrasia ni kulinda haki za watu wote duniani kupitia utandawazi   

Continue Reading

Afya

Is Tanzania’s Adolescent Fertility Rate Three Times Higher Than Global Counterparts?

Published

on

The Comprehensive Community-Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT), an organization ​which works to provide affordable medical and rehabilitative services for mothers and newborns throughout Dar-es-Salaam, marked World Contraception Day on September 26 with a call for more efforts to meet the reproductive health needs of teens between 15 and 19 years old.

The report highlights a worrying statistic — Tanzania’s adolescents are having almost three times as many children on average as their global counterparts, with 135 births per 1000 girls reported in the country, compared to an average of 44 per 1000 girls aged 15–19 worldwide in 2015.

CCRBT attributes the high adolescent fertility rate to a lack of access to contraceptive services, with Technical Advisor for Nursing Bola Abbas saying, that only about 8 per cent of current family planning clients are between the ages of 15 to 19.

On a national scale, Abbas explains, demand for family planning among adolescent girls is still very low, with only one out of every three of those who are sexually active within the 15 to 19 age group using modern contraceptive methods.

So the question is, how does Tanzania’s adolescent fertility rate compare to that of the rest of the world?

Pesacheck investigated the claim that Tanzanian adolescents are having three times as many children as their peers in the rest of the world and found that the statement is TRUE for the following reasons:

Tanzania’s adolescent fertility numbers are rather high, with 4.4% of girls aged 15 having given birth according to the country’s Demographic and Health Survey.

The Sustainable Development Goals call for countries to ensure universal access to sexual and reproductive healthcare services, including family planning, information and education, and the integration of reproductive health into national strategies and programmes by 2030.

The indicators for this goal are the proportion of women of reproductive age (15–49 years) who have their need for family planning satisfied with modern methods, and the adolescent birth rate (10–14 years and 15–19 years) per 1,000 women in that age group.

For several sub-Saharan countries, Tanzania included, access to modern family planning methods is low for this particular age group, and as a result, the regional average is 105 births per 1,000, which is more than double the global average.

Tanzania’s National Bureau of Statistics produced a national fertility and nuptiality report based on data from the 2012 national census, which shows that Adolescent Fertility Rate (AFR) was 81 births per 1,000 women aged 15–19.

The report further shows that in 2012, 23.3% of adolescent girls in the country had given birth to at least one child. Additionally, 42.2% of girls who had never attended school had given birth, compared to just 9% of those who had reached university.

This shows that there is a need for contraceptive access for teenage girls in Tanzania, especially for girls in rural areas and those with limited access to education.

The Tanzania Demographic and Health Survey 2015–16 indicates that 27% of girls aged 15–19 have given birth. Crude birth rates for girls aged 15–19 show that there 135 births per 1,000 girls in Mainland Tanzania and 132 per 1,000 girls in Zanzibar, way above the global average of 44. The data also shows that contraceptive access for this age group is also quite low, with 10.4% of girls aged 15–49 using any form of contraception.

It would therefore appear that the lack of access to contraceptives is contributing to the increased likelihood of adolescent girls getting pregnant.

So the claim by CCBRT that Tanzania’s adolescent fertility rate is almost three times the global average is TRUE. This is driven largely by a lack of access to contraceptives for young people in the 15–19 age group, and the relatively high levels of poverty that have driven many out of school and into early marriage.

As a result, the country is unlikely to meet the Sustainable Development Goal of overall good health and wellbeing of mothers unless it puts measures in place to ensure universal access to sexual and reproductive health-care services for girls and women of all ages.

Do you want us to fact-check something a politician or other public figure has said about public finances? Complete this form, or reach out to us on any of the contacts below, and we’ll help ensure you’re not getting bamboozled.

This report was written by PesaCheck Fellow Belinda Japhet, a Communications Consultant, Online Editor based in Tanzania. The infographics are by PesaCheck Fellow Brian Wachanga, who is a Kenyan civic technologist interested in data visualisation. This report was edited by PesaCheck Managing Editor Eric Mugendi.

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com