Connect with us

Featured

KABLA YA KIFO, Kanumba alimuita mama yake Dar ili amuage

MAMA Mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mutegoa amezungumza na FikraPevu na kusema alizungumza na mwanae usiku, saa chache kabla ya kifo chake akimuita Dar es Salaam ali waagane. Marehemu Steven Kanumba alifariki Usiku wa kuamkia Jumamosi, Aprili 6, 2012, baada ya kuanguka.

Published

on

MAMA Mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mutegoa amezungumza na FikraPevu na kusema alizungumza na mwanae usiku, saa chache kabla ya kifo chake akimuita Dar es Salaam ali waagane.

Mama huyo, ambaye alikuwa safarini mkoani Kagera, anasema mwanae alimpigia simu akimtaka arudi Dar es salaam waagane kwani alikuwa na safari ya kwenda nchini Marekani.

Akihojiwa na FikraPevu leo mchana katika uwanja wa ndege wa Bukoba akiwa safarini kuelekea  Dar es salaam katika msiba wa mwanae, mzazi huyo alisema usiku wa tukio lililosababisha kifo, Kanumba alimpigia simu na kuongea naye.

Mama huyo mzaliwa wa kijiji cha Itoju kata ya Izigo wilaya ya Muleba Mkoani Kagera na ambaye huishi jijini Dar es salaam, alikuwa mkoani Kagera alikokua amekwenda kumtembelea mama yake ambaye ni bibi yake marehemu Steven Kanumba.

"Mwanangu niliongea naye usiku (Ijumaa Aprili 6, 2012) akiwa mwenye furaha na tulitaniana sana, alisema anatuma nauli nirudi Dar es salaam tuagane kwani alikuwa na safari ya kwenda nchini Marekani,"alisema mama yake Kanumba.

Alisema alipatwa na mshituko alfajiri yake kuambiwa kuwa mtoto wake alikuwa ameaga dunia. Anasema mwanae Kanumba alizaliwa Januari 8, 1984 katika hospitali ya serikali mjini Shinyanga.

Marehemu Steven Kanumba alifariki Usiku wa kuamkia Jumamosi, Aprili 6, 2012, baada ya kuanguka. Sababu za kifo chake hazijaelezwa wazi pamoja na kuwapo taarifa za kuwapo ugomvi kati yake na msichana Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu, ambaye pia ni msanii kijana. Lulu ambaye naye amekutwa na majeraha madogo, anashikiliwa na polisi kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo.

"Sina cha kuongea naomba mniombee katika kipindi hiki kigumu jana nimeongea naye kwenye simu leo naambiwa mwanangu amekufa," aliongeza katika hali ya majonzi

Kwa mujibu wa mzazi huyo Flora Mutegoa marehemu Kanumba ana baba yake mzazi aliyemtaja kwa jina la Charles Kanumba kuwa ni Msukuma mwenyeji wa Mkoa wa Shinyanga.

Alipoulizwa na FikraPevu kama mwanaye aliwahi kumweleza siri na ndoto zake za baadaye alisema alikuwa na matarajio ya kufika mbali zaidi katika sanaa ya uigizaji huku akiomba aachwe apumzike kwani maswali mengine asingeweza kuyajibu.

"Naomba mniombee hali yangu sio nzuri baba yake ni Msukuma mwenyeji wa mkoa wa Shinyanga, maswali mengine niacheni jamani," alisema.

Imeandika na Phinias Bashaya; FikraPevu – Kagera

Continue Reading
36 Comments

36 Comments

 1. Johnson BUTERA

  07/04/2012 at 11:41 pm

  Hata sisi wenyeji wa inchi ya DRC tunasikitishwa sana na kifo ca kijana KANUMBA. Mungu apokee roho yake. Duniani hapa, sisi wote ni wasafiri.
  Binafsi mimi naombeya mama na jamaa lote, kwani ni msiba usiyo easy kuvumilia. Vijana wenzangu hapa kwetu GOMA walizoweya kusema kwamba nilimfanana KANUMBA hata kwetu nyumbani. Kwa mjibu mimi niliwaeleza kwamba sisi wote viumbe vya mwenyezi Mungu. Basi, lakufanya ni kuhimiza Polisi ifanye kazi yake, na aliye chanzo ya kifo hiki aazibiwe kulingana na sheria za serkali ya Tanzania. Huyo dada Lulu, na wangineo nyumbani hapo wahojiwe accordingly kwani kuna sababu iliyo acha wanamwua ndugu yangu huyo.
  MUNGU awe karibu nanyinyi nyote.
  Johnson-BUTERA/GOMA-DRC

 2. MR NICO MUNISHI

  08/04/2012 at 12:44 am

  dah jaman watanzania pengo kubwa sana! hatuna la kufanya bwana! god kachukua kiumbe chake so tuzid kumwombea kijana na si tupo njia moja! wakati wowote kinaweza kuhappen! tusal sana! POLEN SANA WATANZANIA naPOLEN FAMILIA YA MAREHEMU KANUMBA MUNGU AWAPE UVUMILIVU!

 3. elias ndugwa

  08/04/2012 at 12:57 am

  Kila mtu atakufa muda wake ukifika. Kanumba ametangulia na wengine tutafuata. Cha msingi ni kutengeneza njia zetu kwa kutenda mema.

 4. mkereketwa j

  08/04/2012 at 1:17 am

  jaman me camin mtu adondoke tu afe?.lulu ana mambo ya ajabu anatembea na wajomba zake achukuliwe hatua haraka sana.

 5. flora kalinga

  08/04/2012 at 2:39 am

  Nimesikitishwa na kifo hiki cha ghafla kwa kipenzi chetu Kanumba. Poleni sana wanafamilia na wazazi. Hatutakusahau maana umeacha mengi moyoni mwetu. Jamani kifo ni lazima. Umejitayarishaje? na je unaachia jamii yako nini? Utakumbukwa ukiondoka? fanya jambo jema la kuelimisha jamii kwa bidii kama Kanumba na utakumbukwa maana Mungu aweza kukuita saa na wakat wowote tengeneza maisha yako na Mungu wako sasa hasa ninyi vijana ili angalau uweze kufurahia maisha ya milele . Mungu wa Mbinguni aiweke Roho ya mareheu mahali pema peponi. Amina.

 6. mabahasha

  08/04/2012 at 7:01 pm

  ni pigo kwetu sote, pole familia ya kanumba na wasanii wote, wote tumeguswa na msiba huu mkubwa, kifo umekuja mapema mno umemzuia kanumba kufikia dream zake alizokuwa nazo.

  R.I.P BRO, bwana aliyefufuka leo akufufue siku ya mwisho

 7. Lukresia Richald

  09/04/2012 at 9:28 am

  Jamani Watanzania, huu msiba ni mkubwa sana kwetu, kumpoteza KANUMBAn= ni sawa na kuipoteza sanaa hapa Tanzania, ila hatuna jinsi iliyobaki tumuombee Kwa Mungu ili loho yake iwekwe mahali pema peponi. Na huyo LULU Jamani vyombo vya dola vimbane mpaka awatae hao waliomtuma kuifanya kazi hiyo isiyo yake. na shelia ichukuliwe kwa halaka sana.

 8. MORO PRESS CLUB

  09/04/2012 at 10:15 am

  Kifo cha Kanumba kimewagusa wengi watu wa rika na kada mbalimbali kwa sababu amekuwa na mchango mkubwa hapa duniani alitumia muda wake mwingi kuwaburudisha na kuwasilisha ujumbe wa maisha ya wanadamu kwa njia ya sanaa.

  Hakuna Bingwa atakayetembea kifua mbele kwamba yeye amezoea kifo,amezoea kufiwa,kifo hakina mwenyewe,kila ufiwapo unaona kama upo peke yako uliyekumbwa na tatizo hilo,kifo hakizoeleki.

  Mengi yametamkwa mazingira ya kifo cha Ndugu yetu Kanumba,lakini yote kwa yote Mungu amempenda zaidi baada ya kuona kazi aliyomtuma hapa duniani ameifanya kwa ukamilifu,yametimia ameenda kwa mleta na mtoa uzima.

  Mungu Ailaze Roho yake Mahala pema peponi amen.

 9. diablo gatto

  10/04/2012 at 11:16 am

  inah lilah waina ilaih rajighuniii waislamu twasema hivo rip kanumba

  • kagana

   12/05/2012 at 6:21 pm

   Nami nakuunga mkono na “Allah” amlaze panapostahili marehem KANUMBA.

 10. sipavange

  10/04/2012 at 6:01 pm

  Hata mimi pia ni mmoja kati ya watu walioguswa sana na kifo cha kanumba.Yote tumuachie mungu kwani yeye ni mweza wa kila alitakalo kulifanya.R.I.P STEVE

 11. elibarick makala

  10/04/2012 at 6:39 pm

  tangulia rafiki hatuna neno zuri zaidi ya kua tulikupenda sana mpendwa wetu steve.

 12. MGISA

  11/04/2012 at 11:31 am

  kula nafs dhaikatu lmaut( Kila nafsi itaonja mauti)

 13. boston wakwetu

  11/04/2012 at 2:52 pm

  Nimeguswa sana nikikumbuka flamu yake ya kimazingara waliipatia sana na mungu amuweke pema peponi, kutangulia ndio kugumu kila mtu atapita hapo

 14. Rjy

  11/04/2012 at 3:29 pm

  Lulu wewe ni shetani mwenye umbo la binaadamu!! umekuja kugharikisha dunia? wewe ni ibilisi usiye na haya. haya sasa umeshamtoa roho Kanumba furahi sasa. Unajidai utakunywa sumu kunywa ufutike ulimwenguni tumechona navituko vyako!!!

  • filbonde

   15/04/2012 at 7:32 pm

   wacha kumuhukumu lulu, hakuna aliethibitisha kuwa kanumba kauawa na lulu au kasukumwa,mbona humlaumu kanumba kutembea na vitoto chini ya miaka 18??

   Hujui km ana kosa la kubaka?? walikuwa chumbani wanafanya umalaya wao, hivyo wote walikuwa ni malaya na kanumba kafa kwenye umalaya, Lulu ana makosa yake nae ya kufanya mapenzi akiwa chini ya miaka 18 na kukubali kufanywa na watu wakubwa kiumri kwake, lkn wote ni MALAYA TU.

 15. Rjy

  11/04/2012 at 3:35 pm

  Namuhurumia sana mama yako nadhani amejuta kukuzaa…. U- star siyo vituko mdogo wangu, ukiwa star mwenye heshima wengi watakuheshimu. Waswahili husema ngoma ikivuma sana haikawii kupasuka sasa hayo yamekufika. Hebu kunywa sumu uone utamu wa kutokwa na roho!!

 16. Raky

  11/04/2012 at 3:35 pm

  Namuhurumia sana mama yako nadhani amejuta kukuzaa…. U- star siyo vituko mdogo wangu, ukiwa star mwenye heshima wengi watakuheshimu. Waswahili husema ngoma ikivuma sana haikawii kupasuka sasa hayo yamekufika. Hebu kunywa sumu uone utamu wa kutokwa na roho!!

 17. hz

  11/04/2012 at 3:39 pm

  Lulu ukinywa sumu tutasema “Yule Malaya kapumzika”

 18. Bora

  11/04/2012 at 3:40 pm

  Jamani jamani poleni sana nduguzangu wa tanzania kwamsiba huo,
  kwakweli kila nafsi itaonja umauti,
  kifo ca kanumba kinaskitisha mno kwasababu nica ghafla na watu kamahao huwa hawadumu, na huyo lulu asiseme uongo huwa alitumwa asemevizuri naye akamatiwe atuwa kwaharaka baada yakufanya tokeo ilo kwanini akimbie!!! alikifanya kwamakuskudi,ata samson aliwuwawaga na mkewe kwasababu ya pesa nahuyo utakuta alikubaliwa pesa. Namchukia sana lulu

 19. Nicholaus Kisusi

  11/04/2012 at 4:36 pm

  Mungu amulaze mahali pema peponi AMINA

 20. Geofrey Rutta

  12/04/2012 at 12:36 am

  Kazi ya Mungu haina makosa R.I.P the great SK!

 21. cheby

  12/04/2012 at 12:47 pm

  we lulu kila mwaka una miaka 17 we miaka yako haisogei mwenzetu? nina mianka kama miwili nasikia unamiaka kumi na saba huna jipya.mala ya mwisho niliona umeandikwa kwenye gazeti kama una miaka 17 kwa nini unaenda club na kwa nini unaendesha gari na kwanini unafanya mambo ya ajabu yanayo kuzidi umri.ulijibu mwenyewe hiyo skendo kua umekua uachwe usifatiliwe maana umesha fikisha miaka ya kufanya hayo yote sasa yamekufika ya mauaji unarudisha miaka nyuma.mi naamini lulu anamiaka zaidi ya kumi na nane hayo mengine ni kujitetea wesema ukweli kama hujahusika na kifo chake ueleweke.umebakwa chumbani kwake ulikua unafata nini?na kwa nini hukukaa sebleni?huna utoto wewe mambo yako yalizidi hata uliyo yafanya.sema uongo kwa mwanadamu lkn Mungu anajua miaka yako na ulichomfanyia kanumba.

 22. filbonde

  15/04/2012 at 7:18 pm

  jamani msimlaumu lulu kwa kifo cha kanumba,hakuna anaeweza kuthibitisha kuwa marehemu alisukumwa na kanumba wakiwa chumbani,ila zaidi anaejuwa ni lulu pekee,kwa hiyo tusiwe kimbelembele kujifanya eti tuna uchungu mkubwa sana na marehemu na kutaka kumuhukumu lulu,chumbani walikuwa wawili tu na inajulikana km wale walikuwa wapenzi,km kulaumu pia mlaumuni na marehemu kufanya mapenzi na mtoto mdogo km yule ambae kisheria marehemu alikuwa anabaka,kwani hakufika miaka 18,kwa hiyo tusiwe tunajifanya eti tuna uchungu sana na kanumba kwa kuwa amefariki,tujaribu sana kuwa wawazi na tusiwe wanafik.

 23. MESHACK FRANK

  16/04/2012 at 12:27 pm

  ishini kama mtaishi milele na ishini kama kufa kesho R.I.P the great

 24. ntulugu

  17/04/2012 at 10:27 am

  jamani kama tunaamin kuwa MWENYEZI MUNGU YUPO ninaiman ndo ataeamua kuhusu lulu na Bro kanumba, rest in peace bro, namhala

 25. catty manota

  17/04/2012 at 2:29 pm

  RIP Kanumba,msimhukumu lulu mapenzi hayaangalii umri wenyewe waliridhiana,tuwe wawazi tusiangalie upande mmoja.vp kama lulu angekufa mikononi mwa kanumba?

 26. teo nico

  19/04/2012 at 2:12 pm

  msihukumu msije nanyi mkahukumiwa

 27. moses masyenene

  10/05/2012 at 7:46 am

  siku zako za kuishi zikifika kikomo utakufa tu.Kumbuka kila .afsi itaonja mauti,inapasa ujililie wewe na nafsi yako.

 28. kagana

  12/05/2012 at 6:24 pm

  “Allah” Amlaze marehm Kanumba panapostahili aaamiiin.

 29. kihimbo

  16/07/2012 at 4:21 pm

  Du,kwa hali ya vurugu,utekaji nyara na mamboo mengine yanayoendelea Tanzania,haki ya nani akifufuka archtecture wa nchi hii,machozi lazima alie,ataanguka harafu atakufa mara ya pili,are we tired with peace in Tanzania?Sisi wengine bado tunaipenda nchi yetu na tunataka tuishi kwa amani na upendo,waliochoka na amani wahamie Syria kuna viwanja vya bure huko wanagawa,msituharibie nchi bwana.

 30. BRAVOLTAJ

  20/10/2012 at 4:00 pm

  Pole sana kwa mauti .

 31. muuti

  23/10/2012 at 3:53 pm

  jamani maswala mazito kuhusu kanumba tuache korti iamuru

 32. irene

  25/10/2012 at 12:19 pm

  RIP kanumba hata cc ni wapita njia tu

 33. Kibwana

  09/11/2012 at 5:04 pm

  RIP kanumba! tutakukumbuka sana!!!

 34. hard

  21/12/2012 at 12:44 pm

  watu wanomwona lulu muuaji, wajiulize je kama lulu ndio angekutwa amekufa, na ukichukulia ni mwanamke mwenye mwili mdohga je kanumba angetazamwaje na jamii. mi nadhani tuache kulaumu sidhani lulu ni muuaji, nadhani ni bahati mbaya tu inaweza kumtokea mtu yoyote. naskitika kusema kuwa mara nyingi wanawake wanaonekana ni malaya wahuni kuliko wanaume wanaofanya hivyo.watu waache kuchanganya maisha ya mtu na kifo na waache kuwatazama wanawake kama watu waovu kuliko wanaume. kiufupi wanawake wanafanya yote kwaajili ya wanaume hata kuweka makalio makubwa kuvaa nusu uchi, kukuza makalio, kujichubua wanafanya haya kwasababu ya wanaume,lulu anamatatizo yake kama binadamu lakini haipelekei yeye kuonekana kama mtu mbaya kihivyo.tuache ushabiki

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Featured

UJASUSI: Jinsi kijana wa kiume kutoka New Zealand alivyojaribu  kumuua Malikia Elizabeth II

Published

on

Shirika la Ujasusi la New Zealand  (SIS) limethibitisha kwa mara ya kwanza kwamba kulikuwa na jaribio la kumuua Malikia Elizabeth II wakati alipotembelea jiji la Kusini la Dunedin mwaka 1981.

Jaribio hilo la kumuua Malikia linalodaiwa kutekelezwa na kijana wa kiume limechochea hamasa ya polisi kutaka kujua ni kwa kiasi gani wanausalama hao walifanikiwa kuzima njama hizo.

Taarifa iliyotolewa na SIS  zinaonesha kuwa kijana huyo, Christopher Lewis (17) alipiga risasi kuelekea kwa Malikia wakati akishuka kwenye gari lake ambapo alikuwa anaenda kushuhudia Maonyesho ya Sayansi yaliyofanyika Oktoba 14, 1981 katika jiji hilo. Tukio hilo lilitokea akiwa katika ziara ya siku 8 kutembelea nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.

“Lewis alidhamiria kumuua Malikia, hata hivyo hakuwa katika nafasi nzuri ya kurusha risasi, hata silaha iliyotumia haikuwa katika umbali wa kuweza kumfikia mhusika,” imesema taarifa iliyotumwa SIS kwa vyombo vya habari.

Lewis ambaye anatajwa kwenye taarifa ya ujasusi kama ‘kijana msumbufu’ hakuhukumiwa kwa jaribio la kutaka kuua au kosa la uhaini. Tukio hilo lilifanywa kuwa siri ili kuzuia sifa mbaya kwa nchi (New Zealand) ambayo ilitembelewa na mgeni wa heshima. Badala yake Lewis alihukumiwa kwa kumiliki silaha kinyume na sheria na kufyatua risasi.

                       Malikia Elizabeth II akiwa ameambatana na walinzi wake alipotembelea New Zealand

Inaelezwa kuwa watu waliohudhuria tukio la kuwasili kwa Malikia walisikia mlio wa risasi lakini Polisi waliokuwa wanasimamia usalama katika eneo hilo la Dunedin waliwaambia kuwa ilikuwa ni sauti ya kuanguka kwa kitu au magari kugongana.

“Uchunguzi wa sasa wa polisi juu milio iliyosikika umefanywa kwa umakini na wawakilishi wa vyombo vya habari wamepata mrejesho kuwa kelele zilisababishwa na baruti”, inaeleza ripoti kutoka SIS iliyotolewa mwaka 1981 baada ya kutokea tukio hilo.

Kulingana taarifa za ujasusi zinaeleza kuwa polisi wamekuwa wakifuatilia nyendo za Lewis tangu 1986 ambapo Malikia alitembelea tena New Zealand wakiogopa kuwa anaweza kutekeleza tena uhalifu huo. Kuwekwa wazi kwa siri hiyo kumewaibua polisi ambao wameanza kuchunguza upya kesi hiyo.

Zaidi ya muongo mmoja uliopita, Lewis alihukumiwa kwa mauaji ya mwanamke mmoja katika mji wa Auckland na kumteka mtoto wa kike ambapo baadaye alimtupa karibu na kanisa.

Kulingana na taarifa mbalimbali za wakati huo zinaeleza kuwa Lewis alijidhuru kwa umeme akiwa gerezani mnamo 1997 akisubiri hukumu ya kuua. Lakini alikana mashtaka ya kuua kwa ujumbe mfupi wa kifo (suicide note).

New Zealand ilipata uhuru mwaka 1947 kutoka kwa Uingereza lakini inamuheshimu Malikia kama kiongozi wa taifa. Ameitembelea nchi hiyo kama Malikia mara 10 na mara ya mwisho ilikuwa 2002.

Continue Reading

Featured

FREEDOM HOUSE: Tanzania ina uhuru kiasi, kufungiwa vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya kisiasa kuididimiza kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa

Published

on

Ripoti mpya iliyotolewa na taasisi huru ya Freedom House imesema misingi ya demokrasia ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kukusanyika imeendelea kudhoofika nchini Tanzania na hali hiyo isiporekebishwa itaingia kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa duniani.

Kulingana na  Freedom House  ambao walichambua data katika nchi 195 za ulimwenguni katika mwaka 2017 wamebaini kuwa nchi 88 zina uhuru,  58 zimejumuishwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku 48 zikiwekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa misingi ya demokrasia ikiwemo uchaguzi usio huru na haki, uhuru wa kujieleza umeendelea kushuka kwa mwaka wa 12 mfufululizo duniani kote. Miongoni mwa matokeo yaliyostaajabisha ni kudhoofika kwa  Marekani ambayo ni mama wa demokrasia kutokana na uchunguzi unaofanywa na Mwendesha Mashtaka Maalumu kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 ambao ulimpa ushindi Rais Donald Trump.

Tanzania imewekwa kwenye nchi 88 ambazo zina uhuru kiasi lakini inatahadharishwa kuwa inaweza kuingia kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa. Tahadhari hiyo inatokana na mwenendo wa viongozi wa serikali kufungia vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kushtakiwa kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa tuhuma za uchochezi na kukamatwa kwa wapinzani wa kisiasa ambao wanakosoa na kutoa mawazo yanayotofautiana na serikali.

Pia utekelezaji wa Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 na Sheria ya Makosa ya Mtandao  ya mwaka 2015 umekuwa ukilalamikiwa na wadau wa maendeleo kuwa ni mkakati wa kudhoofisha uhuru wa kutoa maoni, uwazi na uwajibikaji.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini hivi karibuni kilitoa tamko la tathmini ya uchaguzi mdogo wa marudio wa kuchagua madiwani uliofanyika katika kata 43 kwenye mikoa 19 ya Tanzania  Novemba 24 mwaka jana ambapo kilibaini mambo mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Tathmini hiyo iliibua mambo mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya nguvu ya vyombo vya dola, matukio ya watu kutekwa na watu wasiojulikana, watu kupigwa, kujeruhiwa  kwa lengo la kuharibu na kuvuruga uchaguzi  na vilevile kuwatia hofu wapiga kura.

 

Afrika Mashariki hali bado tete

Tanzania inaungana nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya na Uganda ambazo nazo zimewekwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku za Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini zimejumuishwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa.

Awali Uganda ilikuwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa lakini imepanda hadi kwenye uhuru kiasi kwasababu ya  kuimarika kwa tasnia ya habari na utashi wa wanahabari, blogu na  uhuru wa wananchi kutoa maoni yao licha ya mazingira ya kisiasa kuminywa na utawala wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni.

Rais Museveni mwenye umri wa miaka 73 amekuwepo madarakani  tangu 1986 amefanikiwa kubadilisha sheria  ya ukomo wa umri wa miaka 75 wa kugombea urais ambapo atapata fursa ya kugombea tena mwaka 2021. Chaguzi nchini Uganda zimekuwa zikitawaliwa na vurugu za polisi na wananchi, kuzimwa kwa intaneti na kuwekwa kizuizini kwa viongozi wa upinzani ikiwemo Kizza Besigye wa chama cha Forum for Democratic Change.

Kwa upande wa Kenya ambayo imekuwa ikisifika kwa kuimarisha misingi ya demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo kwa mara ya kwanza mahakama ilifanikiwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Urais yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta uliofanyika Agosti 2018. Uchaguzi ulirudiwa na Rais Kenyatta alichaguliwa tena.

Marudio ya uchaguzi yalilamikiwa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa hayakuzingatia haki za binadamu ambapo watu ambao walipinga uchaguzi huo walikumbana na mkono wa dola. Matendo hayo ndiyo yaliiweka Kenya kwenye kundi la nchi zilizo na uhuru kiasi.

Burundi na Sudan Kusini zimewekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa kutokana na mapigano ya kikabila ambayo yamedhoofisha mfumo wa kisiasa wa kuongoza nchi. Vyombo vya habari na wananchi wanaotoa maoni tofauti na serikali wamekuwa wakiteswa, kufungwa na kuuwawa.

Chanzo: Freedom House           – Nchi zisizo na  uhuru  – Nchi zenye uhuru     – nchi zenye uhuru kiasi   

 

Hali ilivyo Afrika

Afrika kama zilivyo nchi za Afrika Mashariki hali ya demokrasia siyo ya kuridhisha ikizingatiwa kuwa asilimia 11 ya wakazi wapatao bilioni 1.02 wa bara hilo ndio wana uhuru wa kweli, huku 52% wana uhuru kiasi na 37% hawa uhuru kabisa.

Ripoti ya Freedom House inaeleza kuwa waliangazia nchi 49 za Afrika na kugundua kuwa nchi 8 (18%) ndio zina uhuru wa kweli, nchi 22 (43%) zina uhuru kiasi na 19 (39%) hazina uhuru kabisa. Nchi zinazotajwa kuwa na uhuru ni Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Ghana, Togo, Senegal na Kisiwa cha Sao Tome.

 Sababu ya nchi nyingi za Afrika kuwepo kwenye kundi la zisizo na uhuru ni matokeo ya viongozi kukaa madarakani muda mrefu, vurugu za kisiasa na kikabila ambazo zimekuwa zikihatarisha haki za binadamu.

 

Demokrasia ya Dunia

Demokrasia ya dunia inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kisiasa kuliko wakati mwingine ambapo mwaka 2017 ulishuhudia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo kuminywa kwa  uchaguzi huru na kweli, haki za watu wachache, uhuru wa kujieleza, utawala wa sheria.

Nchi 71 kati ya 195 zimeshuhudiwa zikiteteleka katika kulinda haki za kisiasa na jamii ambapo ni nchi 35 tu ndizo zimeweza kulinda haki hizo. Kudhoofika kwa demokrasia kunaendelea kushuka kwa miaka 12 mfululizo na hatua muhimu zisipochukuliwa amani ya dunia itawekwa rehani.

Marekani ambayo ni bingwa wa demokrasia duniani nayo imeripotiwa na taasisi ya Freedom House kudhoofika katika kulinda haki za kisiasa na kijamii na kuzua mgongano wa mawazo miongoni mwa nchi zinazoibukia katika kujenga demokrasia ya dunia.

Tangu kuisha kwa vita baridi, nchi nyingi ziliachana na utawala wa kiimla na kugeukia demokrasia ya vyama vingi lakini hali hiyo imeanza kujitokeza tena ambapo idadi ya viongozi wanaoongoza kwa udikteta inaongezeka.

 

Uhuru wa nchi moja unategemea uhuru wa nchi zote

Demokrasia itabaki kuwa tunu muhimu kwa jamii zilizostaarabika, ikifungua milango ya uwazi, mawazo na fursa mpya na zaidi ya yote kulinda uhuru wa mtu mmoja mmoja. Ikiwa watu duniani kote wanadai mazingira mazuri ya kisiasa ni dhahiri wanakumbatia misingi ya demokrasia: uchaguzi huru, uhuru wa kujieleza, uwazi na uwajibikaji wa serikali, utawala wa sheria ambao hauingiliwi na polisi, jeshi au taasisi nyingine za nchi.

Hata hivyo, Karne ya 21 imeshuhudia ugumu wa kuifanya demokrasia kuwa endelevu ambapo baadhi ya nchi zinatekeleza lakini zingine zinapuuza. Utawala wa kidekteta wa Urusi na China unatambua wazi ili uendelee kuwepo unahitaji kuimarisha demokrasia katika nchi nyingine ili ziendelee kufaidika na mahusiano ya kidiplomasia. Ukuaji wa  demokrasia ni kulinda haki za watu wote duniani kupitia utandawazi   

Continue Reading

Afya

Is Tanzania’s Adolescent Fertility Rate Three Times Higher Than Global Counterparts?

Published

on

The Comprehensive Community-Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT), an organization ​which works to provide affordable medical and rehabilitative services for mothers and newborns throughout Dar-es-Salaam, marked World Contraception Day on September 26 with a call for more efforts to meet the reproductive health needs of teens between 15 and 19 years old.

The report highlights a worrying statistic — Tanzania’s adolescents are having almost three times as many children on average as their global counterparts, with 135 births per 1000 girls reported in the country, compared to an average of 44 per 1000 girls aged 15–19 worldwide in 2015.

CCRBT attributes the high adolescent fertility rate to a lack of access to contraceptive services, with Technical Advisor for Nursing Bola Abbas saying, that only about 8 per cent of current family planning clients are between the ages of 15 to 19.

On a national scale, Abbas explains, demand for family planning among adolescent girls is still very low, with only one out of every three of those who are sexually active within the 15 to 19 age group using modern contraceptive methods.

So the question is, how does Tanzania’s adolescent fertility rate compare to that of the rest of the world?

Pesacheck investigated the claim that Tanzanian adolescents are having three times as many children as their peers in the rest of the world and found that the statement is TRUE for the following reasons:

Tanzania’s adolescent fertility numbers are rather high, with 4.4% of girls aged 15 having given birth according to the country’s Demographic and Health Survey.

The Sustainable Development Goals call for countries to ensure universal access to sexual and reproductive healthcare services, including family planning, information and education, and the integration of reproductive health into national strategies and programmes by 2030.

The indicators for this goal are the proportion of women of reproductive age (15–49 years) who have their need for family planning satisfied with modern methods, and the adolescent birth rate (10–14 years and 15–19 years) per 1,000 women in that age group.

For several sub-Saharan countries, Tanzania included, access to modern family planning methods is low for this particular age group, and as a result, the regional average is 105 births per 1,000, which is more than double the global average.

Tanzania’s National Bureau of Statistics produced a national fertility and nuptiality report based on data from the 2012 national census, which shows that Adolescent Fertility Rate (AFR) was 81 births per 1,000 women aged 15–19.

The report further shows that in 2012, 23.3% of adolescent girls in the country had given birth to at least one child. Additionally, 42.2% of girls who had never attended school had given birth, compared to just 9% of those who had reached university.

This shows that there is a need for contraceptive access for teenage girls in Tanzania, especially for girls in rural areas and those with limited access to education.

The Tanzania Demographic and Health Survey 2015–16 indicates that 27% of girls aged 15–19 have given birth. Crude birth rates for girls aged 15–19 show that there 135 births per 1,000 girls in Mainland Tanzania and 132 per 1,000 girls in Zanzibar, way above the global average of 44. The data also shows that contraceptive access for this age group is also quite low, with 10.4% of girls aged 15–49 using any form of contraception.

It would therefore appear that the lack of access to contraceptives is contributing to the increased likelihood of adolescent girls getting pregnant.

So the claim by CCBRT that Tanzania’s adolescent fertility rate is almost three times the global average is TRUE. This is driven largely by a lack of access to contraceptives for young people in the 15–19 age group, and the relatively high levels of poverty that have driven many out of school and into early marriage.

As a result, the country is unlikely to meet the Sustainable Development Goal of overall good health and wellbeing of mothers unless it puts measures in place to ensure universal access to sexual and reproductive health-care services for girls and women of all ages.

Do you want us to fact-check something a politician or other public figure has said about public finances? Complete this form, or reach out to us on any of the contacts below, and we’ll help ensure you’re not getting bamboozled.

This report was written by PesaCheck Fellow Belinda Japhet, a Communications Consultant, Online Editor based in Tanzania. The infographics are by PesaCheck Fellow Brian Wachanga, who is a Kenyan civic technologist interested in data visualisation. This report was edited by PesaCheck Managing Editor Eric Mugendi.

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com