Connect with us

Investigative

Samaki wanatoweka ziwa Rukwa

Published

on

“SAMAKI wengi wametoweka akiwemo  aina ya kachinga ambaye ni maarufu katika ziwa Rukwa kutokana na ladha yake  hivi sasa hatumuoni tena’’,anasema  mvuvi Stanley Rwamba(65) wa kijiji cha Totowe Bonde la Songwe Chunya mkoani Mbeya.

Rwamba anabainisha kuwa jamii ya Samaki ambao wapo katika hatari ya kutoweka katika ziwa Rukwa  ni ngogo,shibe na kachinga ambao walikuwa wanapatikana kwa wingi wakati wa mvua miaka kumi iliyopita.

Sensa ya samaki ambayo ilifanywa mwaka 1999 katika ziwa Rukwa ilibaini kuwa   ziwa hilo linazalisha samaki tani 7000 kwa mwaka wakiwemo aina tatu za kambale ambazo ni kibonde,singa na poroko, magege, dagaa, kapimoja na kachinga.

Uvuvi  wa kutumia  kokoro unaofanyika katika fukwe za ziwa Rukwa katika kata za Totowe, Ivuna na Kamsamba mkoani Mbeya  umechangia kusababisha samaki katika ziwa hilo kupungua kwa kasi.   

Wavuvi kwenye fukwe hizo wamebainika kutumia nyavu za kokoro kuvulia samaki licha ya kwamba nyavu hizo haziruhusiwi kisheria kwa kuwa zinaharibu  mazalia ya samaki pamoja na kuvua samaki wadogo.

 

Samaki wanaotoweka ziwa Rukwa kutokana na matumizi ya kokoro

Fukwe ambazo uvuvi wa kutumia kokoro umekithiri katika kata ya Totowe  ni  Handeni, Ihovyo, Mtanda, Kambipotea, Kwaboko, Mchangani na Kisiwani.Wavuvi wamekuwa wanavua bila kuwa na hofu ya kukamatwa na maofisa uvuvi ambao wanadaiwa kuchangia hali hiyo kuendelea kwa kuwa hawaonekani katika sehemu zao za kazi.

Staniley Rwamba mvuvi mkongwe katika ziwa Rukwa anasema wavuvi wameamua kutumia kokoro ambazo haziruhusiwi kisheria   kutokana na samaki wanaoruhisiwa kuvuliwa kisheria katika ziwa hilo kuanza kutoweka.

Hata hivyo wavuvi ambao walikuwa wanavua  katika ziwa hilo kila mahali walionekana kukosa samaki ,ambapo wavuvi wanadai hali hiyo inachangiwa na idadi kubwa ya ng’ombe ambao wametia kambi kwenye fukwe za ziwa Rukwa ambapo hula malisho ambayo ni mazalia ya samaki ndani ya ziwa hilo.

Bonifasi Yamlinga ni mvuvi katika fukwe ya Mchangani anasema maelfu ya ng’ombe kila siku wanaingizwa hadi mita 300 ndani ya ziwa Rukwa kula nyasi ambazo ni mazalia ya samaki .

Yamlinga anabainisha kuwa licha ya samaki wengi wanaovuliwa ziwa Rukwa upande wa Chunya kuwa ni wale ambao hawaruhusiwi kuvuliwa kisheria, amedai hakuna afisa samaki wa kata anayehoji uhalali wa kuvua samaki hao hali ambayo inasababisha wavuvi kuwa huru na kuendelea kufanya uvuvi haramu katika ziwa Rukwa.

Hata hivyo afisa uvuvi na maliasili wa Halmashauri ya wilaya Mbozi Agrey Ngalunga baada ya kuona samaki wengi wachanga wanaovuliwa ziwa Rukwa katika kata za Ivuna na Kamsamba   serikali ilitoa ombi kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ili wafunge shughuli za uvuvi kwa miezi minne kuanzia Januari hadi Aprili kila mwaka  ili samaki waweze kuzaliana.

Hata hivyo Ngalunga anabainisha kuwa ombi hilo ambalo walituma barua mwaka jana bado halijakubaliwa na wizara husika.Ameongeza kuwa Halmashauri imetengeneza boti ya kufanyia doria ziwani yenye thamani shilingi milioni 4.8

Anabainisha zaidi kuwa  kwa kutumia boti hilo  mwaka  2010 wameweza kukamata kokoro 133 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 79.5  na nyavu ndogo chini ya nchi tatu 56 zenye thamani ya shilingi 168,000 ambazo hazikubaliki kisheria.

Kulingana na Ngalunga  mwaka 2010 kamati ya ulinzi na usalama  wilaya ya Mbozi kwa kushirikiana na kikosi cha usimamizi wa raslimali uvuvi cha Tunduma wameweza kukamata  nyavu haramu kwenye maduka mjini Tunduma zipatazo 2236  zenye thamani zaidi ya shilingi milioni 137 ambazo ziliteketezwa hadharani kwa moto.

Utafiti umebaini kuwa samaki aina ya kachinga wanaovuliwa katika ziwa Rukwa  kwenye fukwe za kata ya Totowe wilayani Chunya na kata za Kamsamba na Ivuna wilayani Mbozi wameanza kutoweka katika  ziwa hilo na pale wanapopatikana wanauzwa kwa bei ya juu.
Wavuvi kutoka fukwe za Kwaboko, Mtanda, Handeni na kisiwani ambao ni Peter Sasawata,Staniley Rwamba na John Sichalwe  wanadai kuwa kutoweka kwa aina hiyo ya samaki  kunatokana na kina cha maji kupungua,uvuvi wa kutumia kokoro unaofanywa na baadhi ya wavuvi  katika ziwa hilo pamoja na mifugo mingi inayokula nyasi ambazo ni mazalia ya samaki.

Peter Sasawata mvuvi katika ziwa Rukwa anasema  kuwa kwa  wiki moja hadi mbili wavuvi wamekuwa wakivua si zaidi ya samaki watano   aina  ya kachinga ambapo miaka michache nyuma samaki hao walikuwa wanapatikana kwa wingi,ameshauri  juhudi za watalaamu  na serikali zinahitajika ili  kukabiliana na uharibifu wa mazalia ya samaki ili kuzinusuru aina mbalimbali za samaki.

John Sichalwe amewataja samaki wengine ambao hivi sasa wameanza kutoweka kuwa ni magege na kapimoja na kwamba samaki aina ya  kambare bado wanapatikana kwa wingi kwa kuwa samaki hao wanapenda kuishi katika matope ambayo yapo mengi ndani ya ziwa Rukwa ambalo kina chake kimejaa tope na mchanga.

Hata hivyo Sera ya Taifa ya mazingira ya mwaka 1997 kuhusu sekta ya uvuvi kifungu cha 60 inaelekeza wazi kuwa uvuvi utaendelezwa  vema kwa kutumia vifaa vya uvuvi vinavyofaa na njia bora za kuendeleza bidhaa zinazotokana na uvuvi ambapo  njia zinazoharibu mazingira katika uvuvi zitadhibitiwa kwa sheria na kuhakikisha  unafuu wa upatikanaji wa vifaa bora vya uvuvi .

hotuba ya kambi ya upinzani wizara ya uvuvi na mifugo katika Bunge la bajeti la mwaka 2011 iliyotolewa na Silvester Kasulumbayi ilisema lipo tatizo kubwa la serikali kushindwa kusimamia sekta  ya uvuvi na kusababisha kuendelea kuvuliwa kwa samaki wachanga wanaotokana na tatizo la uvuvi haramu.

“ Kupambana na uvuvi haramu huku nyavu ndogo na vifaa vingine vikiendelea kuingia nchini kunakwamisha jitihada zote…. swali la kujiuliza….. kwa nini upande wa nchi jirani za Kenya na Uganda hawana tatizo la nyavu ndogo? Huu ni mradi haramu wa maafisa uvuvi wa Tanzania dhidi ya wavuvi wetu’’,anadai msemaji mkuu wa kambi ya upinzani.

Continue Reading
Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Investigative

‘UBESHI’: Safari ya Vijana Kuifikia Almasi Mwadui-Shinyanga

Published

on

MAJUZI nilikuwa katika utafiti wa namna gani Madini ya Almas yanayopatikana katika Mji Mdogo wa Maganzo Wilayani Kishapu mkoani Shinyanga umewanufaisha wananchi wanaozunguka Mgodi wa Almasi wa Mwadui.

(more…)

Continue Reading

Investigative

Hofu ya Usalama kwa wafanyakazi GGM Yatanda

Published

on

SIKU chache baada ya moto kuzuka ndani ya mgodi wa Geita (GGM) na kuteketeza mali zenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 25,hofu kubwa ya kupoteza maisha imeibuka kwa uongozi na wafanyakazi wa mgodi huo.

(more…)

Continue Reading

Investigative

If we can’t give people’s priorities the attention they deserve, why ask them to prioritize?

Published

on

In a move intended to empower the citizens and give them mandate to decide on their own development priorities, the government adopted the decentralization policy.

(more…)

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com