Connect with us

Featured

TAFAKARI: Kilichomo kwenye ulimbwende, urembo na uzuri…

Published

on

Urembo siku hizi ni mtaji au daraja la kupata mambo mengi maishani. Ukishabikia sana kujenga tabia njema ukasahau kuboresha urembo basi unaweza kupitwa na fursa mbalimbali ikiwemo uchumba na ndoa. Sijawahi kusikia mwanaume akifanya “waxing ya ndevu” aumie kwa ajili ya kuwa soft ili ndevu zisimkwaruze mwanamke…! Amkeni!

Misemo imesheheni siku hizi utasikia “Mwanamke urembo”!

Hivi uzuri au urembo wa mwanamke wa kiafrika siku hizi ni nini? Wahenga walikuwa na usemi “Uzuri wa mwanamke siyo sura au urembo bali ni tabia njema”. Methali hii sina hakika kama bado inabeba maana yoyote kwa sababu kila mwanamke anahangaikia sana urembo na katika mahangaiko hayo huweza kujikuta akisahau kutunza tabia njema. Kwanini hali imekuwa hivyo, ni swali la kujiuliza.

Urembo siku hizi ni mtaji au daraja la kupata mambo mengi maishani. Ukishabikia sana kujenga tabia njema ukasahau kuboresha urembo basi unaweza kupitwa na fursa mbalimbali ikiwemo uchumba na ndoa. Hata hivyo kwa miaka ya siku hizi watu watakuambia uzuri na urembo siyo lazima uzaliwe navyo bali waweza kununua dukani! Hebu tafakari ndugu msomaji na ujiulize nini kimeleta mabadiliko haya kwa kasi ya ajabu? Inatubidi turudi nyuma kidogo tuangalie urembo wa asili na ule wa dukani ili tuweze kujua hizi mbio za kukimbilia kununua urembo zina maana au ni kupoteza pesa na muda tu?

Hakuna mjadala kwamba, tangu zamani za kale, urembo ulitawala kila kitu cha mwanamke kuanzia nywele, shingo, kifua na matiti, kiuno, nyonga na makalio hadi miguu. Hatuwezi kusahau mikono na kucha zake na hata rangi na wororo wa ngozi. Pia tunaweza kusema kwa uhakika kwamba kila kiungo cha mwanamke kina sifa zake kwa vigezo vya urembo wa kiafrika.

Vigezo vya kiafrika vyakinzana na vya kimamboleo?

Nywele – Kwa asili, waafrika wengi wana nywele kipilipili lakini wako pia wenye nywele za kuteleza, zinazoweza kufananishwa na singa, zisiofungamana kwa mafundo. Nywele husukwa mitindo ya aina mbalimbali, hupakwa mafuta na kuzifanya ziwe laini. Kusuka kuna faida kadhaa kwa nywele za kiafrika. Kwanza ni kurefusha nywele na pili ni kumfanya mwanamke aonekane mrembo na mtanashati na mlimbwende. Makabila mengi yalikuwa na utamaduni wa kurembesha nywele kwa mitindo mbalimbali kama  “mabutu” au “vitunguu”“twende kilioni” au “utii wa Roda”, “jicho la mke-mwenza”, Kilimanjaro” n.k Ukiacha sifa ya urembo, nywele zilikuwa na nafasi ya pekee katika makabila na mila mbalimbali na ziliweza kuashiria mambo mbalimbali. Mathalani, kunyoa nywele kuliweza kuashiria msiba au tukio baya.

Siku hizi, wanawake wa kiafrika hubadilishwa nywele kwa  kusuka nywele za mitindo ya “rasta” “dreadlocks”, “weave-on”n.k. Mitindo hii huchanganya ‘nywele’ za bandia katika nywele za asili na kuzifanya zionekane ndefu na nyororo na huweza kubadilishwa mitindo katika ufungaji. Wanawake huweza kubadilisha kabisa muonekano wa nywele zao za asili kwa kuweka dawa na kuzifanya zilainike na hata kuzibadili rangi. Urembo wa asili polepole unapotea kwa vile kipimo cha uzuri wa nywele kimebadilika na kuakisi umagharibi zaidi. Nywele fupi za kipilipili mara nyingi hazionekani maridadi. Aidha, wanasema kwamba toka waanze kutumia virembesho vya nywele vya namna hii, wanajikuta polepole wakikosa uthubutu wa kukaa na nywele zao  za asili, na pale wanapokuwa na nywele asili, hawajiamini mbele za watu! Wanajiona kama wako tofauti sana na watu wengine.

Tukija kwenye kifua na matiti, wanawake wa kiafrika kwa asili walichukulia matiti kama chakula cha mtoto na wasichana walipoanza kubalehe na kuota matiti, hayakufichwa kama tunavyoona siku hizi. Katika makabila mengi ya kiafrika matiti ya mwanamke hayakupewa uzito saaana katika urembo kwa vile umuhimu wake ulielekezwa zaidi kwa watoto watakozaliwa. Kitendo cha kunyonyesha ni ushahidi tosha kuwa matiti hayakuwa kitu cha kumfanya mwanamke aonekane “sexy”. Mwanamke aliweza kuvuta ziwa mbele ya mtu yeyote hata baba yake mzazi na kuanza kunyonyesha tena kwa kujiamini sana na kila mtu aliona ni sawa kabisa. Kama matiti yalikuwa na nafasi katika urembo, basi sifa hiyo ilikuwa ya faragha baina ya wapenzi au wana ndoa na haikuzungumziwa waziwazi.  

Siku hizi wanawake wanajikuta wakihangaika sana na matiti yao kwa vile yanahusishwa zaidi na urembo na siyo chakula cha watoto! Wako wanawake wanaokataa kunyonyesha kwa vile ati matiti yao yatachakaa na kuwa kandambili. Uvaaji wa mavazi ya kuacha kifua wazi, na kuvaa sidiria za kunyanyua maziwa kote kunatokana na dhana ya kuhusisha urembo na matiti yaliyosimama na kujaa vizuri. Matiti yaliyolala, kusinyaa au kuanguka hayana nafasi katika mitindo au urembo. Hatuwezi kushangaa pale tunapoona wanawake wakihangaika kutafuta vitu vinavyosadikiwa kurudisha matiti katika hali ile ya “usichana”- matiti yaliyokaa mishale ya saa sita mchana! Kipimo cha uzuri hapa kinawekwa na “wanufaika” ambao siyo watoto wanaohitaji kunyonyeshwa kwa lishe, bali wale wanaofaika kwa kuangalia, kutomasa na hata kunyonya kwa starehe!

Kipindi fulani tulisoma kwenye magazeti na mitandao mbalimbali na hata kuona picha kuhusu mashine ya kichina ya kunyanyua matiti. Mashine hiyo hufanya kazi kwa kutumia umeme na kuvuta kwa vacuum. Zoezi hilo linaloenda kwa gharama ya sh 150,000/= linamtaka mwanamke kuhudhuria huduma hiyo kwa wiki kadhaa ili kupata matokeo yanayotakiwa. Siwezi kujadili zaidi kuhusu chombo hiki ila ninachojua ni kwamba kuvutwa matiti huwa kunauma sana. Sipati picha hawa akina dada wanaohudhuria ‘matibabu’ hayo ya kunyanyua matiti kama wanajali kujua madhara ya kifaa hicho na kama zoezi hilo linafanikiwa kwa kiwango gani ili wapige hesabu kuona kama wanapata faida ya pesa wanayotoa (value for money) maana siku hizi mtu makini hutaka kujua kama kapata thamani ya pesa yake anayotoa.

Kiuno nacho hakina budi kiwe chembamba kilichobeba makalio ya kuweza kumfanya mwanamke akitembea basi ajisikie anaringa kwa kunesanesa. Sina uhakika kama kwa asili makalio makubwa ilikuwa ni ‘ishu’ kwenye urembo kwa maana ya kiafrika, wanawake walijaliwa kuwa na miili iliyojaa hasa kwa mwanamke aliyekwisha kupevuka na hata kuzaa. Mwanamke wa kiafrika “Miss Bantu” kwa sifa ana makalio makubwa na miguu minene kiasi akivaa kitenge au mavazi ya kiafrika basi huweza kuwa na mvuto wa aina yake.

Umbo lililojaa hasa kuanzia nyonga na kushuka ndicho kilikuwa kipimo cha urembo! Wanawake hawakujali sana kuwa wembamba na wembamba haukuwa kipimo cha uzuri au urembo wa kiafrika. Kwa kipimo cha kisasa, urembo wa mwanamke umekuwa kwenye misukosuko kiasi ambacho imekuwa vigumu kujua urembo hasa ni upi. Wengine watakuambia vigezo vya “Miss Tanzania/Miss World” vyenye kulenga wembamba na urefu ndio kipimo cha kisasa cha mwanamke mrembo. Hapo mdada hutafuta kujikondesha kwa mazoezi, kujinyima chakula  na hata kujitapisha! Wakiwa wajawazito hata chakula hawali kisa wanaogopa watanenepa. Kiafrika ujauzito na uzazi ni kipindi mwanamke alitunzwa kwa milo minono na kunenepeshwa ili akitoka awe amenenepa sana na kuiletea familia hasa mume heshima na sifa! Sasa siku hizi kujikondesha huku sijui kama ni sifa kwa mume au mzazi loh!

Wanawake wako njia panda kwenye vipimo hivi. Wanawake wanatafuta kuwa na makalio makubwa kwa vile wanasikia wanaume wanapenda makalio yaliyojaa, na sina uhakika kama kipimo hiki ni cha kimataifa! Utasikia “Ona kalio la kichina hilo” wakimaanisha mwanamke mwenye makalio makubwa na inasadikiwa wachina wameleta dawa za kuongeza ukubwa wa makalio. Waganga wa jadi nao hawajarudi nyuma katika kujipatia chochote kutokana na huu mkanganyiko wa urembo. Matangazo katika mabango barabarani na magazetini yanawavuta wanawake waende wakapate huduma ya kuongeza makalio na “hips”. Sijui kama uganga huu ulikuwepo toka zamani za kale kusaidia wanawake kwenye urembo ya asili.

Nijuavyo, vipodozi vya asili kama hina, liwa, msandali havikuwa dawa za kienyeji bali vilitokana na mazao na miti iliyoweza kuchumwa na mrembo mwenyewe bila kuhitaji mganga. Kuna wakati suala hili lililetwa hata kwenye vyombo vya juu kama watunga sera na sheria kujaribu kupiga marufuku lakini sijui iliishia wapi. Marufuku hizi zimewahi kuelekezwa kwa vipodozi vya kufanya ngozi iwe nyeupe al-maarufu kama mkorogo. Wataalamu wamejaribu kuiliongelea suala hili kwa kirefu sana na kuonyesha madhara yake. Aidha sheria zimewekwa kupiga marufuku baadhi ya vipodozi na hata kufanya msako madukani na kuwaadhibu wafanya biashara wanaoagiza mali hizo lakini juhudi hizi hazijazaamatunda hata kidogo.

Urembo wako ni kwa faida yako?

Wazungu wana methali isemayo “beauty is in the eyes of the beholder” wakimaanisha uzuri wa mtu uko kwenye macho ya yule anayeuona. Sasa, huu urembo mwenye kuuona ni nani? Je, ni mwenyewe mhusika kwa maana ya “mrembo mwenyewe” au ni wale wanaomuona? Wenye kumuona ni wengi na kila mtu ana haki kuamua kama anachokiona machoni mwake ni  “urembo” au “uzuri” au ni nini. Ninajiuliza, ”Hivi nitajali nini kama wewe unayenitazama utahukumu kuwa mimi siyo mrembo?”. Mpita njia ana haki gani kuniamulia? Wanawake wengi watakuambia, mwanamke unatakiwa uonekane mrembo kwa wenzio na hasa wale wa jinsi tofauti. Hapo kwenye “jinsi” tofauti inabidi tupapigie msatari kwa maana pana kitu kikubwa sana chenye kupelekesha wanawake wahangaike sana kuusaka urembo na uzuri. Katika pita pita yangu nimebahatika kuongea na wanaume kutaka kujua mwanamke mrembo ni yupi na haya yalikuwa ni baadhi ya majibu:

..”Mimi napenda sana mwanamke awe na urembo wa asili – asitumie madawa ya ngozi au nywele”

..”Inategemea… kwangu mimi napenda sana mwanamke mwenye umbo la wastani, asiwe mrefu sana …awe na umbo litakalonifanya nimmudu… (Portable)”

…”sipendi mwanamke mwembamba hata kidogo. Nataka nisikie nyama na siyo mifupa”

“Napenda mwanamke mrefu mwembamba bana…. Huniambii kitu! Minyama uzembe inani put off vibaya sana…”

..”mwanamke mweupe ni ugonjwa wangu”

Hayo ni baadhi ya majibu ya wanaume niliowauliza. Majibu yao yanaashiria mchanganyiko wa tafsiri ya urembo na haya ndio huwachanganya wanawake. Wanawake wako katika mbio za kuwafurahisha wanaume zaidi ya kujifurahisha wao wenyewe. Cha ajabu hapo, hakuna mwanaume aliyezungumzia tabia njema, ikimaanisha tabia njema au mbaya haibadili chochocte kwenye urembo wa mwanamke.

Wakina dada na wakinamama, kwanini hamfanyi vitu kwa kujifurahisha wenyewe? Wanaume wanaposhinda saloon kunyoa na kufanya scrub hawafanyi kwa ajili yenu bali kwa starehe zao. Mijadala kuhusu wanaume na salon inaonyesha kabisa kuwa wanafanya kujifurahisha na kujipendezesha wao. Sijawahi kusikia mwanaume akifanya “waxing ya ndevu” aumie kwa ajili ya kuwa soft ili ndevu zisimkwaruze mwanamke…! Amkeni!

Mamlaka husika sijui kama mna habari kuhusu hizi teknolojia mpya za kichina… Tungependa kujua kama TFDA, TBS, na nyinginezo mmethibitisha viwango na ubora wa vifaa hivi.

Continue Reading
4 Comments

4 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Featured

UJASUSI: Jinsi kijana wa kiume kutoka New Zealand alivyojaribu  kumuua Malikia Elizabeth II

Published

on

Shirika la Ujasusi la New Zealand  (SIS) limethibitisha kwa mara ya kwanza kwamba kulikuwa na jaribio la kumuua Malikia Elizabeth II wakati alipotembelea jiji la Kusini la Dunedin mwaka 1981.

Jaribio hilo la kumuua Malikia linalodaiwa kutekelezwa na kijana wa kiume limechochea hamasa ya polisi kutaka kujua ni kwa kiasi gani wanausalama hao walifanikiwa kuzima njama hizo.

Taarifa iliyotolewa na SIS  zinaonesha kuwa kijana huyo, Christopher Lewis (17) alipiga risasi kuelekea kwa Malikia wakati akishuka kwenye gari lake ambapo alikuwa anaenda kushuhudia Maonyesho ya Sayansi yaliyofanyika Oktoba 14, 1981 katika jiji hilo. Tukio hilo lilitokea akiwa katika ziara ya siku 8 kutembelea nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.

“Lewis alidhamiria kumuua Malikia, hata hivyo hakuwa katika nafasi nzuri ya kurusha risasi, hata silaha iliyotumia haikuwa katika umbali wa kuweza kumfikia mhusika,” imesema taarifa iliyotumwa SIS kwa vyombo vya habari.

Lewis ambaye anatajwa kwenye taarifa ya ujasusi kama ‘kijana msumbufu’ hakuhukumiwa kwa jaribio la kutaka kuua au kosa la uhaini. Tukio hilo lilifanywa kuwa siri ili kuzuia sifa mbaya kwa nchi (New Zealand) ambayo ilitembelewa na mgeni wa heshima. Badala yake Lewis alihukumiwa kwa kumiliki silaha kinyume na sheria na kufyatua risasi.

                       Malikia Elizabeth II akiwa ameambatana na walinzi wake alipotembelea New Zealand

Inaelezwa kuwa watu waliohudhuria tukio la kuwasili kwa Malikia walisikia mlio wa risasi lakini Polisi waliokuwa wanasimamia usalama katika eneo hilo la Dunedin waliwaambia kuwa ilikuwa ni sauti ya kuanguka kwa kitu au magari kugongana.

“Uchunguzi wa sasa wa polisi juu milio iliyosikika umefanywa kwa umakini na wawakilishi wa vyombo vya habari wamepata mrejesho kuwa kelele zilisababishwa na baruti”, inaeleza ripoti kutoka SIS iliyotolewa mwaka 1981 baada ya kutokea tukio hilo.

Kulingana taarifa za ujasusi zinaeleza kuwa polisi wamekuwa wakifuatilia nyendo za Lewis tangu 1986 ambapo Malikia alitembelea tena New Zealand wakiogopa kuwa anaweza kutekeleza tena uhalifu huo. Kuwekwa wazi kwa siri hiyo kumewaibua polisi ambao wameanza kuchunguza upya kesi hiyo.

Zaidi ya muongo mmoja uliopita, Lewis alihukumiwa kwa mauaji ya mwanamke mmoja katika mji wa Auckland na kumteka mtoto wa kike ambapo baadaye alimtupa karibu na kanisa.

Kulingana na taarifa mbalimbali za wakati huo zinaeleza kuwa Lewis alijidhuru kwa umeme akiwa gerezani mnamo 1997 akisubiri hukumu ya kuua. Lakini alikana mashtaka ya kuua kwa ujumbe mfupi wa kifo (suicide note).

New Zealand ilipata uhuru mwaka 1947 kutoka kwa Uingereza lakini inamuheshimu Malikia kama kiongozi wa taifa. Ameitembelea nchi hiyo kama Malikia mara 10 na mara ya mwisho ilikuwa 2002.

Continue Reading

Featured

FREEDOM HOUSE: Tanzania ina uhuru kiasi, kufungiwa vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya kisiasa kuididimiza kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa

Published

on

Ripoti mpya iliyotolewa na taasisi huru ya Freedom House imesema misingi ya demokrasia ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kukusanyika imeendelea kudhoofika nchini Tanzania na hali hiyo isiporekebishwa itaingia kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa duniani.

Kulingana na  Freedom House  ambao walichambua data katika nchi 195 za ulimwenguni katika mwaka 2017 wamebaini kuwa nchi 88 zina uhuru,  58 zimejumuishwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku 48 zikiwekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa misingi ya demokrasia ikiwemo uchaguzi usio huru na haki, uhuru wa kujieleza umeendelea kushuka kwa mwaka wa 12 mfufululizo duniani kote. Miongoni mwa matokeo yaliyostaajabisha ni kudhoofika kwa  Marekani ambayo ni mama wa demokrasia kutokana na uchunguzi unaofanywa na Mwendesha Mashtaka Maalumu kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 ambao ulimpa ushindi Rais Donald Trump.

Tanzania imewekwa kwenye nchi 88 ambazo zina uhuru kiasi lakini inatahadharishwa kuwa inaweza kuingia kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa. Tahadhari hiyo inatokana na mwenendo wa viongozi wa serikali kufungia vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kushtakiwa kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa tuhuma za uchochezi na kukamatwa kwa wapinzani wa kisiasa ambao wanakosoa na kutoa mawazo yanayotofautiana na serikali.

Pia utekelezaji wa Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 na Sheria ya Makosa ya Mtandao  ya mwaka 2015 umekuwa ukilalamikiwa na wadau wa maendeleo kuwa ni mkakati wa kudhoofisha uhuru wa kutoa maoni, uwazi na uwajibikaji.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini hivi karibuni kilitoa tamko la tathmini ya uchaguzi mdogo wa marudio wa kuchagua madiwani uliofanyika katika kata 43 kwenye mikoa 19 ya Tanzania  Novemba 24 mwaka jana ambapo kilibaini mambo mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Tathmini hiyo iliibua mambo mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya nguvu ya vyombo vya dola, matukio ya watu kutekwa na watu wasiojulikana, watu kupigwa, kujeruhiwa  kwa lengo la kuharibu na kuvuruga uchaguzi  na vilevile kuwatia hofu wapiga kura.

 

Afrika Mashariki hali bado tete

Tanzania inaungana nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya na Uganda ambazo nazo zimewekwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku za Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini zimejumuishwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa.

Awali Uganda ilikuwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa lakini imepanda hadi kwenye uhuru kiasi kwasababu ya  kuimarika kwa tasnia ya habari na utashi wa wanahabari, blogu na  uhuru wa wananchi kutoa maoni yao licha ya mazingira ya kisiasa kuminywa na utawala wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni.

Rais Museveni mwenye umri wa miaka 73 amekuwepo madarakani  tangu 1986 amefanikiwa kubadilisha sheria  ya ukomo wa umri wa miaka 75 wa kugombea urais ambapo atapata fursa ya kugombea tena mwaka 2021. Chaguzi nchini Uganda zimekuwa zikitawaliwa na vurugu za polisi na wananchi, kuzimwa kwa intaneti na kuwekwa kizuizini kwa viongozi wa upinzani ikiwemo Kizza Besigye wa chama cha Forum for Democratic Change.

Kwa upande wa Kenya ambayo imekuwa ikisifika kwa kuimarisha misingi ya demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo kwa mara ya kwanza mahakama ilifanikiwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Urais yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta uliofanyika Agosti 2018. Uchaguzi ulirudiwa na Rais Kenyatta alichaguliwa tena.

Marudio ya uchaguzi yalilamikiwa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa hayakuzingatia haki za binadamu ambapo watu ambao walipinga uchaguzi huo walikumbana na mkono wa dola. Matendo hayo ndiyo yaliiweka Kenya kwenye kundi la nchi zilizo na uhuru kiasi.

Burundi na Sudan Kusini zimewekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa kutokana na mapigano ya kikabila ambayo yamedhoofisha mfumo wa kisiasa wa kuongoza nchi. Vyombo vya habari na wananchi wanaotoa maoni tofauti na serikali wamekuwa wakiteswa, kufungwa na kuuwawa.

Chanzo: Freedom House           – Nchi zisizo na  uhuru  – Nchi zenye uhuru     – nchi zenye uhuru kiasi   

 

Hali ilivyo Afrika

Afrika kama zilivyo nchi za Afrika Mashariki hali ya demokrasia siyo ya kuridhisha ikizingatiwa kuwa asilimia 11 ya wakazi wapatao bilioni 1.02 wa bara hilo ndio wana uhuru wa kweli, huku 52% wana uhuru kiasi na 37% hawa uhuru kabisa.

Ripoti ya Freedom House inaeleza kuwa waliangazia nchi 49 za Afrika na kugundua kuwa nchi 8 (18%) ndio zina uhuru wa kweli, nchi 22 (43%) zina uhuru kiasi na 19 (39%) hazina uhuru kabisa. Nchi zinazotajwa kuwa na uhuru ni Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Ghana, Togo, Senegal na Kisiwa cha Sao Tome.

 Sababu ya nchi nyingi za Afrika kuwepo kwenye kundi la zisizo na uhuru ni matokeo ya viongozi kukaa madarakani muda mrefu, vurugu za kisiasa na kikabila ambazo zimekuwa zikihatarisha haki za binadamu.

 

Demokrasia ya Dunia

Demokrasia ya dunia inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kisiasa kuliko wakati mwingine ambapo mwaka 2017 ulishuhudia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo kuminywa kwa  uchaguzi huru na kweli, haki za watu wachache, uhuru wa kujieleza, utawala wa sheria.

Nchi 71 kati ya 195 zimeshuhudiwa zikiteteleka katika kulinda haki za kisiasa na jamii ambapo ni nchi 35 tu ndizo zimeweza kulinda haki hizo. Kudhoofika kwa demokrasia kunaendelea kushuka kwa miaka 12 mfululizo na hatua muhimu zisipochukuliwa amani ya dunia itawekwa rehani.

Marekani ambayo ni bingwa wa demokrasia duniani nayo imeripotiwa na taasisi ya Freedom House kudhoofika katika kulinda haki za kisiasa na kijamii na kuzua mgongano wa mawazo miongoni mwa nchi zinazoibukia katika kujenga demokrasia ya dunia.

Tangu kuisha kwa vita baridi, nchi nyingi ziliachana na utawala wa kiimla na kugeukia demokrasia ya vyama vingi lakini hali hiyo imeanza kujitokeza tena ambapo idadi ya viongozi wanaoongoza kwa udikteta inaongezeka.

 

Uhuru wa nchi moja unategemea uhuru wa nchi zote

Demokrasia itabaki kuwa tunu muhimu kwa jamii zilizostaarabika, ikifungua milango ya uwazi, mawazo na fursa mpya na zaidi ya yote kulinda uhuru wa mtu mmoja mmoja. Ikiwa watu duniani kote wanadai mazingira mazuri ya kisiasa ni dhahiri wanakumbatia misingi ya demokrasia: uchaguzi huru, uhuru wa kujieleza, uwazi na uwajibikaji wa serikali, utawala wa sheria ambao hauingiliwi na polisi, jeshi au taasisi nyingine za nchi.

Hata hivyo, Karne ya 21 imeshuhudia ugumu wa kuifanya demokrasia kuwa endelevu ambapo baadhi ya nchi zinatekeleza lakini zingine zinapuuza. Utawala wa kidekteta wa Urusi na China unatambua wazi ili uendelee kuwepo unahitaji kuimarisha demokrasia katika nchi nyingine ili ziendelee kufaidika na mahusiano ya kidiplomasia. Ukuaji wa  demokrasia ni kulinda haki za watu wote duniani kupitia utandawazi   

Continue Reading

Afya

Is Tanzania’s Adolescent Fertility Rate Three Times Higher Than Global Counterparts?

Published

on

The Comprehensive Community-Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT), an organization ​which works to provide affordable medical and rehabilitative services for mothers and newborns throughout Dar-es-Salaam, marked World Contraception Day on September 26 with a call for more efforts to meet the reproductive health needs of teens between 15 and 19 years old.

The report highlights a worrying statistic — Tanzania’s adolescents are having almost three times as many children on average as their global counterparts, with 135 births per 1000 girls reported in the country, compared to an average of 44 per 1000 girls aged 15–19 worldwide in 2015.

CCRBT attributes the high adolescent fertility rate to a lack of access to contraceptive services, with Technical Advisor for Nursing Bola Abbas saying, that only about 8 per cent of current family planning clients are between the ages of 15 to 19.

On a national scale, Abbas explains, demand for family planning among adolescent girls is still very low, with only one out of every three of those who are sexually active within the 15 to 19 age group using modern contraceptive methods.

So the question is, how does Tanzania’s adolescent fertility rate compare to that of the rest of the world?

Pesacheck investigated the claim that Tanzanian adolescents are having three times as many children as their peers in the rest of the world and found that the statement is TRUE for the following reasons:

Tanzania’s adolescent fertility numbers are rather high, with 4.4% of girls aged 15 having given birth according to the country’s Demographic and Health Survey.

The Sustainable Development Goals call for countries to ensure universal access to sexual and reproductive healthcare services, including family planning, information and education, and the integration of reproductive health into national strategies and programmes by 2030.

The indicators for this goal are the proportion of women of reproductive age (15–49 years) who have their need for family planning satisfied with modern methods, and the adolescent birth rate (10–14 years and 15–19 years) per 1,000 women in that age group.

For several sub-Saharan countries, Tanzania included, access to modern family planning methods is low for this particular age group, and as a result, the regional average is 105 births per 1,000, which is more than double the global average.

Tanzania’s National Bureau of Statistics produced a national fertility and nuptiality report based on data from the 2012 national census, which shows that Adolescent Fertility Rate (AFR) was 81 births per 1,000 women aged 15–19.

The report further shows that in 2012, 23.3% of adolescent girls in the country had given birth to at least one child. Additionally, 42.2% of girls who had never attended school had given birth, compared to just 9% of those who had reached university.

This shows that there is a need for contraceptive access for teenage girls in Tanzania, especially for girls in rural areas and those with limited access to education.

The Tanzania Demographic and Health Survey 2015–16 indicates that 27% of girls aged 15–19 have given birth. Crude birth rates for girls aged 15–19 show that there 135 births per 1,000 girls in Mainland Tanzania and 132 per 1,000 girls in Zanzibar, way above the global average of 44. The data also shows that contraceptive access for this age group is also quite low, with 10.4% of girls aged 15–49 using any form of contraception.

It would therefore appear that the lack of access to contraceptives is contributing to the increased likelihood of adolescent girls getting pregnant.

So the claim by CCBRT that Tanzania’s adolescent fertility rate is almost three times the global average is TRUE. This is driven largely by a lack of access to contraceptives for young people in the 15–19 age group, and the relatively high levels of poverty that have driven many out of school and into early marriage.

As a result, the country is unlikely to meet the Sustainable Development Goal of overall good health and wellbeing of mothers unless it puts measures in place to ensure universal access to sexual and reproductive health-care services for girls and women of all ages.

Do you want us to fact-check something a politician or other public figure has said about public finances? Complete this form, or reach out to us on any of the contacts below, and we’ll help ensure you’re not getting bamboozled.

This report was written by PesaCheck Fellow Belinda Japhet, a Communications Consultant, Online Editor based in Tanzania. The infographics are by PesaCheck Fellow Brian Wachanga, who is a Kenyan civic technologist interested in data visualisation. This report was edited by PesaCheck Managing Editor Eric Mugendi.

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com