Connect with us

Featured

Tusipoandika historia yetu, tusije laumu ikipotoshwa!

Published

on

Wengi wangependa kujua/kusoma wasifu rasmi “biography/autobiography” wa wanasiasa kama Benjamin Mkapa, Dkt. Salim A. Salim (moja ya wanadiplomasia nguli ambaye alipata kuiongoza Umoja wa Afrika katika miaka ya 1989 hadi 2001 kama Katibu Mkuu na pia kuwahi kuwa Waziri Mkuu katika serikali ya Mwalimu Nyerere), wafanyabiashara kama Said Salim Bakhressa, Reginald Mengi, wanazuoni kama Profesa Issa Shivji, Haroub Othman. Wanamichezo kama Filbert Bayi, Leodgar Tenga, n.k. ili kufahamu kwa undani wameweza kufika pale walipofika na kuwa na mchango mkubwa mpaka sasa kwa taifa.

==================================================

Uandishi umekuwa ukipungua siku hata siku katika jamii yetu ya Tanzania, lakini haimaanishi hakuna vya kuandikwa, hakuna mafunzo ya kuwekwa katika kumbukumbu kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo! Ni uchaguzi tu ambao wengi wenye taarifa kuamua kutoandika historia ambapo madhara ya uamuzi huu ni makubwa kuliko tabu ya kupitia mchakato wa uandishi.

Ni kweli si kila mmoja ana karama ya uandishi lakini kwa ukuaji wa teknolojia na maendeleo katika tasnia ya uandishi, hata asiye mwandishi anaweza kuandika iwe yeye mwenyewe moja kwa moja au kushiriki katika uandishi pasi kuandika.

Tukiangalia kwa haraka tunaweza kuhoji kwanini hakuna wasifu rasmi “biography/autobiography” za kutosha za watendaji mbalimbali waliopata kushika ofisi za umma hasa ngazi za juu na kutoa mchango mkubwa katika jamii yetu mpaka sasa. Lazima tujiulize, kwani ni kwa kupitia maandiko kama hayo ndipo baadhi ya visa na mikasa ambayo kwao wameipitia inaweza kuwa funzo maridhawa kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Kwani ni thamani kuu kujifunza katika yale wengine walianguka au kuyamudu vyema kuliko kusubiri yatukumbe tena ndipo tupate fundisho!

Ni kwa namna gani, mathalani, majaji waliopata kutumikia mhimili wa mahakama kwa muda mrefu na katika safari ndefu mfano wengine walioanzia toka uhakimu ngazi za wilaya mpaka kufikia ngazi hizo za juu kabisa katika mhimili huo wa sheria safari yao ikawa funzo na yenye kuhamasisha hasa kwa wanaoanza fani hiyo. Kwa ukosefu wa maandiko kama hayo, wengi (hasa kizazi cha sasa) wanaweza hisi wanayoyapitia ni mapya au kuyumbishwa na pia na misukumo mbalimbali. Kuna umuhimu mkubwa wa maandiko haya.

Maandiko haya pia hayapaswi kusubiri hadi muda wa kustaafu au uzeeni. Kuna machache ambayo hata vijana wa sasa wameyapitia katika utendaji wao katika fani mbalimbali ambayo yanaweza kabisa kuwa chachu kwa maendeleo na kupiga hatua katika utendaji endapo yangeliandikwa vyema.

Katika mjadala ambao nilipata kuuibua katika mtandao wa kijamii wa ‘Twitter’, wengi wa wachangiaji walionyesha uhitaji sana wa kuandikwa kwa yale ambayo watu wameyapitia au kukumbana nayo katika utumishi au utendaji kazi wao. Na baadhi walidiriki kuonyesha kiu yao ya kutamani kusoma vitabu vyenye kuelezea misimamo safari walizopitia katika taaluma nk baadhi ya watendaji wa kiserikali, watumishi wa umma, wafanyabiashara, wanasiasa nk. Mifano michache ya kiu ya wachangiaji ilikuwa ni kupata bahati ya kusoma wasifu rasmi “biography/autobiography” wa wanasiasa kama Benjamin Mkapa, (aliyepata kuwa Rais wa Tanzania katika serikali ya awamu ya tatu), Dkt. Salim A. Salim (moja ya wanadiplomasia nguli ambaye alipata kuiongoza Umoja wa Afrika katika miaka ya 1989 hadi 2001 kama Katibu Mkuu na pia kuwahi kuwa Waziri Mkuu katika serikali ya Mwalimu Nyerere), wafanyabiashara kama Said Salim Bakhressa, Reginald Mengi, wanazuoni kama Profesa Issa Shivji, Haroub Othman. Wanamichezo kama Filbert Bayi, Leodgar Tenga, n.k. Haya ni kwa uchache tu, ambayo ni kiu kwa wengi kufahamu kwa undani wameweza kufika pale walipofika na kuwa na mchango mkubwa mpaka sasa kwa taifa. Ni kwa njia zipi, ipi ni misimamo yao katika baadhi ya masuala na nini ndoto zao kwa Taifa letu.

-wewe-

Makundi haya yanakwenda mbali pia kwa wale ambao bado wapo katika utumishi wao kwa sasa, mathalani wanasiasa vijana kama; Zitto Kabwe, Halima Mdee, John Mnyika, January Makamba ambao kwa hivi karibuni wamekuwa na mvuto na hamasa kwa vijana wengi katika upande huo. Huku kusanifu pia maisha ya wajasiriamali vijana wenye kumiliki makampuni na kuendesha biashara mathalani Mohammed Dewji. Lakini pia wapo wenye kuhamasisha kutokana na mafanikio ambayo wamepiga katika taaluma na kazi zao kama vile Suzan Mashibe kwenye shughuli za anga, Julie Makani katika sekta ya afya. Ni muhimu kuandika historia sahihi ili isije ikaandikwa ndivyo sivyo!

Tumeshuhudia uandishi kama huo ukifanywa kwa wanasiasa machachari wanaochipukia nchi nyingine mfano Afrika Kusini ambako mwandishi Fiona Forde aliandika kitabu juu ya mwanasiasa Julius Malema; “An Inconvenient Youth – Julius Malema and the new ANC”.

Katika kuhakikisha historia haipotei wala kufutika, kuna wengi walishiriki katika ujenzi wa taifa na katika nyanja mbalimbali na kupitia utendaji wao hata kama hawakuwa maarufu sana ila kuna maamuzi waliyopata kuyachukua yatadumu kuwa funzo vizazi kwa vizazi. Bila ya kuwa makini na mafunzo haya tunakuwa jamii inayorudia makosa yale yale kwa nyakati tofauti.

Tuchukulie mfano katika eneo la usafirishaji wa majini ambalo katika miaka ya karibuni tumeshuhudia ajali za kutisha zenye kuangamiza wananchi wengi. Lakini baadhi ya matukio haya yamekuwa yakichangiwa na uzembe. Uzembe ambao miaka kadhaa nyuma ulishakemewa na kwa nyakati zile ambazo tahadhari ilipuuzwa madhara yalijitokeza. Hakuna uandishi wa vitabu wenye kutunza kumbukumbu hizi na uchambuzi wa kina. Nyaraka nyingi za tume ambazo zinaundwa zinaishia kupata vumbi katika makabati na kuliwa na mchwa. Lakini tungalichapa katika mifumo ya vitabu na kufikika kwa wingi na mwananchi yeyote anayetaka kupata maarifa kutokana nayo tungaliweza kupiga hatua.

Katika kuzama kwa meli au vivuko tunaweza pia kukumbuka sakata mathalani la kuzama kwa kivuko cha Kilombero. Kuzama huko kwa kivuko kulitokea kama ajali lakini inaweza kuwa ni moja ya ajali ambazo ni tarajiwa kwani tayari uamuzi wa kununua kivuko hicho ulipingwa vikali na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Miundombinu kwa wakati huo Marehemu Odira Ongara kwa madai kwamba kivuko kile kilikuwa chakavu na kisingeweza kukidhi vigezo vya manunuzi na hata matumizi na kuamua kutokutia sahihi ununuzi wa kivuko hicho. Uamuzi huu ulipuuzwa na kivuko kikanunuliwa kwa uidhinishaji wa viongozi wengine wa juu zaidi, chini ya waziri Mustapha Nyang’anyi na hatimaye maafa ya kuzama na kuua watu ndilo likawa zao. Kuzama huko na maafa hayo vilizua mjadala mkali sana baadaye. Lakini kwa ufinyu wa kuandika na kusoma, haya yamekuwa yakijirudia, makosa yaleyale yamezidi kutusababishia maafa kwa taifa.

Mfano wa eneo moja la sekta ya usafirishaji wa maji ni chembe tu katika mengi ambayo yameshajitokeza kwenye sekta nyingine ambapo yamekuwa yakijirudia kila uchao pasi kuwa na funzo kwa kizazi cha sasa wala kile kijacho.

Moja ya hatua muhimu kuelekea maendeleo endelevu na ustawi wa taifa lolote ni pamoja na kuthubutu kuandika na kusoma.

Jukumu hili la kuweka kumbukumbu katika maandishi ni la kila mmoja ambaye amepitia mengi ambayo yanaweza kuwa funzo kwa wengine iwe mazuri au mabaya awe ana uwezo wa kiuandishi au lah, kwani kwa wale ambao hawana uwezo wa kiuandishi au muda wa kuwekeza katika kuandika, wanaweza kabisa kushirikiana na wanahabari ambao kwao uandishi ni sehemu ya kazi yenye kuwapatia kipato. Ndiyo inawezekana kabisa, kwani katika nchi nyingi duniani, waandishi wa habari wamekuwa wakitumia fursa ya kuwa karibu na vyanzo vya taarifa mbalimbali kuandika maandiko kama vitabu aidha kwa niaba ya watu ambao wamepitia visa hivyo, au wametenda masuala yenye kuhitaji kuwekwa katika kumbukumbu au pia kuandika tu masuala nyeti kwa kina kwa ajili ya sasa na vizazi vijavyo.

Tunaweza kujiuliza kwa kina kuna sababu gani kwa waandishi wa habari hususani wa makala ambao kwa muda mrefu wameandika na kuchambua masuala ya rushwa katika sekta ya nishati na madini yaani kusanifu mikataba mibovu ambayo imeingia katika historia ya nchi yetu kama ile ya Richmond au Dowans kutokuwa na vitabu juu ya hayo? Ni kwanini tunaruhusu haya yote ambayo tumeyashuhudia yapotee kwenye vichwa vyetu pasi kuandikwa na kuwa funzo kwa vizazi vya sasa (hususan kwa nchi nyingine) na vizazi vijavyo? Kuna sababu yoyote yenye tija katika hili? Au tutashangazwa pale ambapo wataibuka waandishi toka nchi nyingine na kuandikia juu ya hayo kisha tukahamasika na kukimbilia kuyasoma?

Kuna nyakati zenye mafunzo mengi ya kisiasa ambayo endapo yakiachwa yapite pasi kuandikwa vizuri tunaikatili historia yetu, tukichukua mfano mambo ambayo kundi kama vile G55 ambalo lilikuwapo na kusimamia ajenda nyingi za kisiasa kama vile suala la muungano na nafasi ya Tanganyika. Huko walikuwapo wanasiasa na wabunge kama vile Njelu Kasaka, Jenerali Ulimwengu, hawa wote wapo. Mengi waliyopitia ni tija sana katika hali ya kisiasa sasa na hata baadae. Ni funzo sana kwa wanasiasa wa sasa na hata wa baadae. Tunahitaji sana maandiko yao!

Tunaweza kujiuliza kwa wale ambao walipitia michakato ya kisiasa mathalani kushiriki kwa kina na ukaribu chaguzi kama vile za mwaka 2005 na kushuhudia mikakati ya lile kundi lisemwalo la “wanamtandao” wana sababu gani kutoandika mafunzo yale? Ni woga? Au kwa wale ambao walishiriki kwa kina kampeni na michuano ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na hasa kampeni za upinzani za Dkt. Wilibrod Slaa ambaye alikuwa moja ya mwanasiasa mwenye kugusa mioyo ya wananchi kutoandika tena kwa kiuchambuzi juu ya yaliyojiri kwa kina? Ni woga?

Au tunaweza kujiuliza: Kwanini hakuna uthubutu wa kuandika vitabu juu ya vyama vyetu ambavyo vinaendesha siasa nchini mathalani vyama kama CHADEMA au CUF kwa upande wa upinzani na kile chama tawala cha CCM? Kusanifu ukuaji wake, kuimarika na hata misukosuko ambayo imeshapitia?

Maana jamii yetu inapenda kusoma hayo, na ndiyo maana tunaona baadhi ya wananchi wamekuwa wakinunua vitabu juu ya namna ambavyo siasa za Kenya zimekuwa zikiendeshwa mathalani vitabu kama “Politics of Betrayal” (Siasa ya Usaliti) cha Joe Khamis au kile cha “Peeling back the Mask” cha Miguna Miguna. Hivyo ni miongoni mwa vitabu vya jirani wenzetu ambao wamekuwa wakiandika yale ambayo wanapitia na kuwa funzo kwa sasa na baadae. Achilia mbali nchi zilizoendelea kama vile Marekani ambako baadhi wamekuwa wakisoma vitabu vingi juu ya namna siasa zimeendeshwa mathalani namna Rais wa sasa, Barrack Obama amekuwa akiendesha kampeni zake na hatimaye ushindi katika vitabu maarufu kama kile cha “Audacity to win” cha aliyekuwa meneja wa kampeni za rais huyo Barrack Obama kwa mwaka 2008 bwana David Plouffe.

Hatuwezi kupiga hatua kimaendeleo endapo hata masuala ambayo yapo katika uwezo wetu hatuyatekelezi na kuyapa kipaumbele! Tunasaliti kuandika historia yetu wenyewe hivyo ni fursa baadaye kwa kila yeyote yule anayeweza kunena juu ya hilo kuja na kile anachopenda kisikike. Ukweli hasa wa mambo unapotea na kuachwa upotoshaji uote mizizi!

Continue Reading
5 Comments

5 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Featured

UJASUSI: Jinsi kijana wa kiume kutoka New Zealand alivyojaribu  kumuua Malikia Elizabeth II

Published

on

Shirika la Ujasusi la New Zealand  (SIS) limethibitisha kwa mara ya kwanza kwamba kulikuwa na jaribio la kumuua Malikia Elizabeth II wakati alipotembelea jiji la Kusini la Dunedin mwaka 1981.

Jaribio hilo la kumuua Malikia linalodaiwa kutekelezwa na kijana wa kiume limechochea hamasa ya polisi kutaka kujua ni kwa kiasi gani wanausalama hao walifanikiwa kuzima njama hizo.

Taarifa iliyotolewa na SIS  zinaonesha kuwa kijana huyo, Christopher Lewis (17) alipiga risasi kuelekea kwa Malikia wakati akishuka kwenye gari lake ambapo alikuwa anaenda kushuhudia Maonyesho ya Sayansi yaliyofanyika Oktoba 14, 1981 katika jiji hilo. Tukio hilo lilitokea akiwa katika ziara ya siku 8 kutembelea nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.

“Lewis alidhamiria kumuua Malikia, hata hivyo hakuwa katika nafasi nzuri ya kurusha risasi, hata silaha iliyotumia haikuwa katika umbali wa kuweza kumfikia mhusika,” imesema taarifa iliyotumwa SIS kwa vyombo vya habari.

Lewis ambaye anatajwa kwenye taarifa ya ujasusi kama ‘kijana msumbufu’ hakuhukumiwa kwa jaribio la kutaka kuua au kosa la uhaini. Tukio hilo lilifanywa kuwa siri ili kuzuia sifa mbaya kwa nchi (New Zealand) ambayo ilitembelewa na mgeni wa heshima. Badala yake Lewis alihukumiwa kwa kumiliki silaha kinyume na sheria na kufyatua risasi.

                       Malikia Elizabeth II akiwa ameambatana na walinzi wake alipotembelea New Zealand

Inaelezwa kuwa watu waliohudhuria tukio la kuwasili kwa Malikia walisikia mlio wa risasi lakini Polisi waliokuwa wanasimamia usalama katika eneo hilo la Dunedin waliwaambia kuwa ilikuwa ni sauti ya kuanguka kwa kitu au magari kugongana.

“Uchunguzi wa sasa wa polisi juu milio iliyosikika umefanywa kwa umakini na wawakilishi wa vyombo vya habari wamepata mrejesho kuwa kelele zilisababishwa na baruti”, inaeleza ripoti kutoka SIS iliyotolewa mwaka 1981 baada ya kutokea tukio hilo.

Kulingana taarifa za ujasusi zinaeleza kuwa polisi wamekuwa wakifuatilia nyendo za Lewis tangu 1986 ambapo Malikia alitembelea tena New Zealand wakiogopa kuwa anaweza kutekeleza tena uhalifu huo. Kuwekwa wazi kwa siri hiyo kumewaibua polisi ambao wameanza kuchunguza upya kesi hiyo.

Zaidi ya muongo mmoja uliopita, Lewis alihukumiwa kwa mauaji ya mwanamke mmoja katika mji wa Auckland na kumteka mtoto wa kike ambapo baadaye alimtupa karibu na kanisa.

Kulingana na taarifa mbalimbali za wakati huo zinaeleza kuwa Lewis alijidhuru kwa umeme akiwa gerezani mnamo 1997 akisubiri hukumu ya kuua. Lakini alikana mashtaka ya kuua kwa ujumbe mfupi wa kifo (suicide note).

New Zealand ilipata uhuru mwaka 1947 kutoka kwa Uingereza lakini inamuheshimu Malikia kama kiongozi wa taifa. Ameitembelea nchi hiyo kama Malikia mara 10 na mara ya mwisho ilikuwa 2002.

Continue Reading

Featured

FREEDOM HOUSE: Tanzania ina uhuru kiasi, kufungiwa vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya kisiasa kuididimiza kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa

Published

on

Ripoti mpya iliyotolewa na taasisi huru ya Freedom House imesema misingi ya demokrasia ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kukusanyika imeendelea kudhoofika nchini Tanzania na hali hiyo isiporekebishwa itaingia kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa duniani.

Kulingana na  Freedom House  ambao walichambua data katika nchi 195 za ulimwenguni katika mwaka 2017 wamebaini kuwa nchi 88 zina uhuru,  58 zimejumuishwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku 48 zikiwekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa misingi ya demokrasia ikiwemo uchaguzi usio huru na haki, uhuru wa kujieleza umeendelea kushuka kwa mwaka wa 12 mfufululizo duniani kote. Miongoni mwa matokeo yaliyostaajabisha ni kudhoofika kwa  Marekani ambayo ni mama wa demokrasia kutokana na uchunguzi unaofanywa na Mwendesha Mashtaka Maalumu kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 ambao ulimpa ushindi Rais Donald Trump.

Tanzania imewekwa kwenye nchi 88 ambazo zina uhuru kiasi lakini inatahadharishwa kuwa inaweza kuingia kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa. Tahadhari hiyo inatokana na mwenendo wa viongozi wa serikali kufungia vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kushtakiwa kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa tuhuma za uchochezi na kukamatwa kwa wapinzani wa kisiasa ambao wanakosoa na kutoa mawazo yanayotofautiana na serikali.

Pia utekelezaji wa Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 na Sheria ya Makosa ya Mtandao  ya mwaka 2015 umekuwa ukilalamikiwa na wadau wa maendeleo kuwa ni mkakati wa kudhoofisha uhuru wa kutoa maoni, uwazi na uwajibikaji.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini hivi karibuni kilitoa tamko la tathmini ya uchaguzi mdogo wa marudio wa kuchagua madiwani uliofanyika katika kata 43 kwenye mikoa 19 ya Tanzania  Novemba 24 mwaka jana ambapo kilibaini mambo mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Tathmini hiyo iliibua mambo mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya nguvu ya vyombo vya dola, matukio ya watu kutekwa na watu wasiojulikana, watu kupigwa, kujeruhiwa  kwa lengo la kuharibu na kuvuruga uchaguzi  na vilevile kuwatia hofu wapiga kura.

 

Afrika Mashariki hali bado tete

Tanzania inaungana nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya na Uganda ambazo nazo zimewekwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku za Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini zimejumuishwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa.

Awali Uganda ilikuwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa lakini imepanda hadi kwenye uhuru kiasi kwasababu ya  kuimarika kwa tasnia ya habari na utashi wa wanahabari, blogu na  uhuru wa wananchi kutoa maoni yao licha ya mazingira ya kisiasa kuminywa na utawala wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni.

Rais Museveni mwenye umri wa miaka 73 amekuwepo madarakani  tangu 1986 amefanikiwa kubadilisha sheria  ya ukomo wa umri wa miaka 75 wa kugombea urais ambapo atapata fursa ya kugombea tena mwaka 2021. Chaguzi nchini Uganda zimekuwa zikitawaliwa na vurugu za polisi na wananchi, kuzimwa kwa intaneti na kuwekwa kizuizini kwa viongozi wa upinzani ikiwemo Kizza Besigye wa chama cha Forum for Democratic Change.

Kwa upande wa Kenya ambayo imekuwa ikisifika kwa kuimarisha misingi ya demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo kwa mara ya kwanza mahakama ilifanikiwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Urais yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta uliofanyika Agosti 2018. Uchaguzi ulirudiwa na Rais Kenyatta alichaguliwa tena.

Marudio ya uchaguzi yalilamikiwa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa hayakuzingatia haki za binadamu ambapo watu ambao walipinga uchaguzi huo walikumbana na mkono wa dola. Matendo hayo ndiyo yaliiweka Kenya kwenye kundi la nchi zilizo na uhuru kiasi.

Burundi na Sudan Kusini zimewekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa kutokana na mapigano ya kikabila ambayo yamedhoofisha mfumo wa kisiasa wa kuongoza nchi. Vyombo vya habari na wananchi wanaotoa maoni tofauti na serikali wamekuwa wakiteswa, kufungwa na kuuwawa.

Chanzo: Freedom House           – Nchi zisizo na  uhuru  – Nchi zenye uhuru     – nchi zenye uhuru kiasi   

 

Hali ilivyo Afrika

Afrika kama zilivyo nchi za Afrika Mashariki hali ya demokrasia siyo ya kuridhisha ikizingatiwa kuwa asilimia 11 ya wakazi wapatao bilioni 1.02 wa bara hilo ndio wana uhuru wa kweli, huku 52% wana uhuru kiasi na 37% hawa uhuru kabisa.

Ripoti ya Freedom House inaeleza kuwa waliangazia nchi 49 za Afrika na kugundua kuwa nchi 8 (18%) ndio zina uhuru wa kweli, nchi 22 (43%) zina uhuru kiasi na 19 (39%) hazina uhuru kabisa. Nchi zinazotajwa kuwa na uhuru ni Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Ghana, Togo, Senegal na Kisiwa cha Sao Tome.

 Sababu ya nchi nyingi za Afrika kuwepo kwenye kundi la zisizo na uhuru ni matokeo ya viongozi kukaa madarakani muda mrefu, vurugu za kisiasa na kikabila ambazo zimekuwa zikihatarisha haki za binadamu.

 

Demokrasia ya Dunia

Demokrasia ya dunia inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kisiasa kuliko wakati mwingine ambapo mwaka 2017 ulishuhudia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo kuminywa kwa  uchaguzi huru na kweli, haki za watu wachache, uhuru wa kujieleza, utawala wa sheria.

Nchi 71 kati ya 195 zimeshuhudiwa zikiteteleka katika kulinda haki za kisiasa na jamii ambapo ni nchi 35 tu ndizo zimeweza kulinda haki hizo. Kudhoofika kwa demokrasia kunaendelea kushuka kwa miaka 12 mfululizo na hatua muhimu zisipochukuliwa amani ya dunia itawekwa rehani.

Marekani ambayo ni bingwa wa demokrasia duniani nayo imeripotiwa na taasisi ya Freedom House kudhoofika katika kulinda haki za kisiasa na kijamii na kuzua mgongano wa mawazo miongoni mwa nchi zinazoibukia katika kujenga demokrasia ya dunia.

Tangu kuisha kwa vita baridi, nchi nyingi ziliachana na utawala wa kiimla na kugeukia demokrasia ya vyama vingi lakini hali hiyo imeanza kujitokeza tena ambapo idadi ya viongozi wanaoongoza kwa udikteta inaongezeka.

 

Uhuru wa nchi moja unategemea uhuru wa nchi zote

Demokrasia itabaki kuwa tunu muhimu kwa jamii zilizostaarabika, ikifungua milango ya uwazi, mawazo na fursa mpya na zaidi ya yote kulinda uhuru wa mtu mmoja mmoja. Ikiwa watu duniani kote wanadai mazingira mazuri ya kisiasa ni dhahiri wanakumbatia misingi ya demokrasia: uchaguzi huru, uhuru wa kujieleza, uwazi na uwajibikaji wa serikali, utawala wa sheria ambao hauingiliwi na polisi, jeshi au taasisi nyingine za nchi.

Hata hivyo, Karne ya 21 imeshuhudia ugumu wa kuifanya demokrasia kuwa endelevu ambapo baadhi ya nchi zinatekeleza lakini zingine zinapuuza. Utawala wa kidekteta wa Urusi na China unatambua wazi ili uendelee kuwepo unahitaji kuimarisha demokrasia katika nchi nyingine ili ziendelee kufaidika na mahusiano ya kidiplomasia. Ukuaji wa  demokrasia ni kulinda haki za watu wote duniani kupitia utandawazi   

Continue Reading

Afya

Is Tanzania’s Adolescent Fertility Rate Three Times Higher Than Global Counterparts?

Published

on

The Comprehensive Community-Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT), an organization ​which works to provide affordable medical and rehabilitative services for mothers and newborns throughout Dar-es-Salaam, marked World Contraception Day on September 26 with a call for more efforts to meet the reproductive health needs of teens between 15 and 19 years old.

The report highlights a worrying statistic — Tanzania’s adolescents are having almost three times as many children on average as their global counterparts, with 135 births per 1000 girls reported in the country, compared to an average of 44 per 1000 girls aged 15–19 worldwide in 2015.

CCRBT attributes the high adolescent fertility rate to a lack of access to contraceptive services, with Technical Advisor for Nursing Bola Abbas saying, that only about 8 per cent of current family planning clients are between the ages of 15 to 19.

On a national scale, Abbas explains, demand for family planning among adolescent girls is still very low, with only one out of every three of those who are sexually active within the 15 to 19 age group using modern contraceptive methods.

So the question is, how does Tanzania’s adolescent fertility rate compare to that of the rest of the world?

Pesacheck investigated the claim that Tanzanian adolescents are having three times as many children as their peers in the rest of the world and found that the statement is TRUE for the following reasons:

Tanzania’s adolescent fertility numbers are rather high, with 4.4% of girls aged 15 having given birth according to the country’s Demographic and Health Survey.

The Sustainable Development Goals call for countries to ensure universal access to sexual and reproductive healthcare services, including family planning, information and education, and the integration of reproductive health into national strategies and programmes by 2030.

The indicators for this goal are the proportion of women of reproductive age (15–49 years) who have their need for family planning satisfied with modern methods, and the adolescent birth rate (10–14 years and 15–19 years) per 1,000 women in that age group.

For several sub-Saharan countries, Tanzania included, access to modern family planning methods is low for this particular age group, and as a result, the regional average is 105 births per 1,000, which is more than double the global average.

Tanzania’s National Bureau of Statistics produced a national fertility and nuptiality report based on data from the 2012 national census, which shows that Adolescent Fertility Rate (AFR) was 81 births per 1,000 women aged 15–19.

The report further shows that in 2012, 23.3% of adolescent girls in the country had given birth to at least one child. Additionally, 42.2% of girls who had never attended school had given birth, compared to just 9% of those who had reached university.

This shows that there is a need for contraceptive access for teenage girls in Tanzania, especially for girls in rural areas and those with limited access to education.

The Tanzania Demographic and Health Survey 2015–16 indicates that 27% of girls aged 15–19 have given birth. Crude birth rates for girls aged 15–19 show that there 135 births per 1,000 girls in Mainland Tanzania and 132 per 1,000 girls in Zanzibar, way above the global average of 44. The data also shows that contraceptive access for this age group is also quite low, with 10.4% of girls aged 15–49 using any form of contraception.

It would therefore appear that the lack of access to contraceptives is contributing to the increased likelihood of adolescent girls getting pregnant.

So the claim by CCBRT that Tanzania’s adolescent fertility rate is almost three times the global average is TRUE. This is driven largely by a lack of access to contraceptives for young people in the 15–19 age group, and the relatively high levels of poverty that have driven many out of school and into early marriage.

As a result, the country is unlikely to meet the Sustainable Development Goal of overall good health and wellbeing of mothers unless it puts measures in place to ensure universal access to sexual and reproductive health-care services for girls and women of all ages.

Do you want us to fact-check something a politician or other public figure has said about public finances? Complete this form, or reach out to us on any of the contacts below, and we’ll help ensure you’re not getting bamboozled.

This report was written by PesaCheck Fellow Belinda Japhet, a Communications Consultant, Online Editor based in Tanzania. The infographics are by PesaCheck Fellow Brian Wachanga, who is a Kenyan civic technologist interested in data visualisation. This report was edited by PesaCheck Managing Editor Eric Mugendi.

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com