Connect with us

Siasa

Uamuzi wa CHADEMA dhidi ya madiwani: “A Big Mistake!”

Published

on

Kitendo cha Kamati Kuu ya CHADEMA kuwavua uanachama madiwani wake wa Arusha, is “A Big Mistake”!, and there is a price to pay, so Chadema must pay the price which is very high!.

Nimesoma ile taarifa ya maamuzi ya Kamati Kuu ya CHADEMA iliyoletwa humu jukwaani, na thread kadhaa kuhusu uamuzi huo, wengi wa wachangiaji wakiupongeza, hivyo nimeona nitoe maoni yangu, kuwa uamuzi huo is one of the Big Mistakes, CHADEMA had ever made!.

1. Ile sheria ya kulazimisha wawakilishi wa wananchi, lazima wadhaminiwe na vyama, its a bad law, na inakwenda kinyume cha Katiba ya JMT inayotoa uhuru kwa kila raia kushiriki katika uongozi wa serikali tangu ya mitaa hadi serikali kuu, hadi mahakama kuu ilishatoa rulling hicho kipengele kuwa ni ‘unconstitutional’ na kiwe struck out from the books of law!. Naamini CHADEMA hilo wanalifahamu, hivyo kitendo cha kutumia kipengele hicho hicho ambacho ni bad law, to its advantage, is “A Big Mistake!”.

2. Ukishachaguliwa, Diwani au Mbunge, hata kama ulidhaminiwa na chama, wewe, unakuwa umechaguliwa na wananchi, na unakuwa ni mtumishi wa watu na kule kwenye ngazi za maamuzi, Baraza la Madiwani na Bungeni, unawakilisha maslahi ya wananchi waliokutuma, na sio maslahi ya chama kilichokudhamini, japo katika uwakilishi wako, pia maslahi ya chama yatazingatiwa. Kitendo cha chama kuwafukuza wawakilishi halali wa wananchi kwa maslahi ya chama, is “A Big Mistake!”.

3. Sisi ambao hatuna vyama, lakini tuna shauku ya kuona Tanzania inaongozwa na chama mbadala, tumekuwa na imani kubwa sana na CHADEMA kama ndicho chama pekee mbadala ambacho kimethibitisha kikiaminiwa, kinaweza kuleta mabadiliko ya kweli. Hivyo tunategemea CHADEMA kitafanya maamuzi yanayofuata misingi ya haki. Kitendo cha kuwavua uanachama madiwani wake hawa, waliochaguliwa na wananchi, (sio chama) bila kuwasikiliza, ni kuwa “condem Unheard”, which is against principles of Natural Justice, and this is a “A Big Mistake!”.

4. Uzoefu wa siasa za Kanda ya Kaskazini, watu wanachagua watu na sio vyama, ndio maana CCM wanajua wazi kuwa, wao CCM, kuanzia Mwenyekiti wao, sekretariat yake, CC yao na NEC nzima ya CCM, hata wakapige kambi Moshi mjini, wakeshe kwa siku 30 mfululizo usiku na mchana huku wakipiga kampeni ya nguvu kwa kutumia mabilioni yao wanayofisidi, na kuwavisha wanamoshi wote, zile T.Shirt na kofia, pamoja na kulisha pilau la nguvu siku zote 30, Ndesa hawatamng’oa!. Kitendo cha Chadema kuwavua uanachama watu wa watu mjini Arusha, it’s “A Big Mistake!”.

5. Wenzao CCM walipokuja na makelele ya kujivua gamba, nilisema CCM, kuanzia Mwenyekiti wao, na kelele zote za Nape na Chiligati, hawana ubavu wa kuwavua uanachama hao watuhumiwa wa ufisadi kwa kuhofia retaliation ya watu wao, ndio maana mtashuhudia kwenye kampeni za Igunga, CCM lazima impigie magoti RA. Amini nakuambia, hawawezi kuwafanya lolote EL na AC, sana sana watawabembeleza kujiudhuru nyadhifa zao, lakini sio kuwavua uanachama, kwanini Chadema, chama cha matumaini, kifanye makosa ambayo CCM iliyochokwa, haiwezi kuyafanya, ya kuwavua uanachama wachaguliwa wa wananchi?!. That is “A Big Mistake!”.

6. Chama makini kama CHADEMA, is expected to do the right thing, at the right time. Hatua hii, ya kuwavua uanachama madiwani pendwa Arusha, hata kama it was the right step, imekuja at the wrong time! Wakati wakitafuta justification ya kulitwaa jimbo la Igunga, ndio chama kinaanzisha tifu kanda ya Kaskazini ambako ndiko kwenye mizizi yake, mimi sijui, CHADEMA, imeyafanya hayo kwa kutegemea nini?.

7. Wakati nikiuleta ukosoaji huu, sio vibaya nikiwakumbusha CHADEMA baadhi ya maamuzi yake na matokeo yake. Kumuengua Mwera Tarime, nilisema mapema, kuwa ‘it was a mistake’, matokeo sote tunayajua! Kususia kutangazwa kwa matokeo na kutomtambua rais, nilicoment humu humu, matokeo yake sote tunayajua, na jinsi CHADEMA ilivyonufaika na hatua hizo.

8. Niliwahi kuwapa CHADEMA, ushauri fulani, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA, mlinibeza sana, including viongozi wenu. Mimi nikawasisitizia kuhusu, internal reforms na ‘the winning coalition’ including strategies kuelekea 2015, mpaka leo, bado sijaona, tuendelee kusubiri, ‘the playing ground is not level, and never will it be, hivyo, 2015, tutaingia tena kwenye mechi ile ile, katika mazingira yale yale halafu tutegemee matokeo tofauti?.

9. Angalizo: Naomba kwenye kujadili mada muhimu zinazohusu maslahi ya taifa, nawaombeni sana tujadiliane kwa ustaarabu huku tukipingana kwa hoja na sio kuleta ushabiki wa vyama ama kupinga hoja kwa matusi, kejeli na matukano.

10. Nimetoa angalizo hilo makusudi, kwa vile nafahamu fika, kinachowapata wakosoaji wote wa CHADEMA, lakini kwenye kutoa honest opinion, lazima tuseme ukweli mchungu ambao utawacost CHADEMA dearly!  Afadhali anayekukosoa kwa kukuambia ukweli, kuliko anayekusifia ili hali anaelewa wazi mwishoni utaangamia.

Wasalaam.

Pasco.

Pasco ni political comentator ambaye sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, bali mshabiki wa demokrasia ya kweli ndani ya vyama, na ndani ya bunge. Comments zangu zina ‘neutrality, objectivity, fairness na balance, bila kuendekeza ushabiki wa vyama, bali kutanguliza maslahi ya taifa mbele.

 UPDATE:
Nime happen kukutana na mjumbe mmoja wa CC ya Chadema asubuhi hii, amenifafanulia A-Z ya kilichotokea. Chadema walifanya kila waliloweza ili kuwarudisha kwenye mstari lakini ilishindikana. Hao madiwani walizidi kuitunishia misuli CC ya Chadema, hivyo Chadema kama chama, was left with no option bali kuwatimua.

However, kwa vile Mhe. Lema ni major player on one side, na madiwani on the other, sasa na tusubiri jinsi CC ya Chadema, itakavyomshughulikia, na kwa vile yeye ni mjumbe wa CC hiyo ya Chadema, tutawaomba Chadema, wasilimalize suala lake ndani kwa ndani bila kutoa taarifa kwa umma, ili kupusha dhana ya double standards.

Sasa naanza kuwaelewa Chadema kidogo kidogo.

Pasco

Kwa discussion (comments) tembelea ~ JamiiForums

Continue Reading
12 Comments

12 Comments

 1. Bakari M Mohamed

  08/08/2011 at 10:35 am

  …Nadhani walichofanya CHADEMA ni utashi wa Katiba ya Chama na utashi wa sheria, kanuni na taratibu za uendeshaji demokrasi kwa mujibu wa utendaji wa pamoja wa chama. Japokuwa inaweza kudhaniwa kwamba CHADEMA kama chama kinaweza kupata gharama kwa kuwafukuza; bado ukweli unabaki palepale kwamba kuwaacha “wahuni” wanaotaka kuendesha chama kama kampuni binafsi wanadhibitiwa. Hivi ndivyo kinavyoweza kufanya chama makini chochote chenye muelekeo wa kujenga wanachama wanaotii Katiba ya Chama kama ilivyokubaliwa na wananchi wenyewe katika kuendesha shughuli za chama.

 2. PETER FREDRICK

  08/08/2011 at 2:08 pm

  CHADEMA wametoa angalizo la makusudi katka uongozi wake na wenyewe waweke maslahi ya TAIFA

 3. liz bayo

  11/08/2011 at 9:52 am

  asante sana bwana pascal kwa kufafanua vizuri maelezo yako na mimi nakuunga mkono sana kwa sababu watu wamekuwa na ushabiki wa chama na hawana uelewa wa jambo linaloendelea, tatizo la udiwani arusha ni kubwa na limeonyesha upendeleo kwa upande mmoja na kwa kuwa madiwani hawa wamewajibishwa kwa kuamua kufanya kazi na meya mbona wabunge wa chadema hawakuwajibishwa kwa kufanya kazi na rais? Hali hiyo inaonyesha kuwa wadogo yani madiwani wamefukuzwa kwasababu waliamua kuungana ili wawaletee maendeleo wananchi wao waliowachagua

  • Peter

   12/08/2011 at 9:19 am

   Unajua kila mtu anaweza kusema chochote kwa vile anavyoelewa lakin ekwli utabaki pale pale kwamba (ktk msafara wa mamba na kenge wamo ivyo madiwani wa chadema ni wasaliti na uongozi auwitaji njaa kama walivvyo fanya madiwani kwa kukubabali kupokea pesa ili wampitishe MAYOR so nawaunga mkono CHADEMA.

 4. daudi

  15/08/2011 at 1:46 am

  nawapongeza sana kwa kuwa munaikumbusha serikari hasa pale inapojisahau. sasa mlete madaftali ya kuwaandikisha wapiga kura wetu mapema.saizi ni kukijenga chama na serikari kwa pamoja. tunaitaji kuwaandikisha wapiga kura wetu mapema na kutambua kila mmoja alipo na namba zake za cm. otherwise simamieni watu walio athirika na maji ya mto tegite wapate haki yao kwani wapiga kura wanataka kujua mmefikia wapi?watawauliza.

 5. Honest

  15/08/2011 at 1:17 pm

  Me nadhani kila uamuzi una risks zake, ila kufanya maamuzi ni bora zaidi ingawa kukaa kimya kama wengine ni maamuzi pia…CDM kama chama c cha kulaumiwa katika wananchi kupoteza wawakilishi ila ni sheria mbouvu na kandamizi za nchi ndio tuzitupie lawama, so wao wamefanya maamuzi kama chama,na naamini itawasaidia kukiendesha chama kwa umakini zaidi…

 6. mazoko

  16/08/2011 at 5:49 pm

  nadhani hapa ndugu yangu umepotea kidogo.Kabla yakujiunga na chama chochote kiwe cha siasa au kijamii nilazima usome masharti ya chama hicho.ukijiunga inamaana umeelewa nakukabiliana na sera zachama hicho.Kwa hawa wa CDM nadhani madiwani wake hawakusoma taratibu za chama na hii ndiyo tatizo kubwa la watu wakati unaingia unachekelea lakini zikifuatwa kanuni na taratibu zikikujeruhi lawama zinaanza sasa kilichofanyika nisawa na itapendeza kama kila chama kitafuata taratibu hizi kuwawajibisha bila woga

 7. Mugerezi

  16/08/2011 at 6:35 pm

  Walichofanya CHADEMA siyo KOSA kama ulivyojaza maelezo kibao bali wao wamefanya kilichotakiwa kufanyika. Ni kweli kisheria mtu binafsi anaweza kugombea akachaguliwa hivyo anakuwa na maamuzi kama yeye. Sasa hawa watu wa CHADEMA kabla ya kucahguliwa na wanachi walijichagua? Au walipitishwa na vikao halali vya chama? Na je CHADEMA wamekataa mwafaka? Au njia iliyotumika ndiyo hawaihafiki? Lazima tukune bongo zetu kuelewa kinacheendelea. Katika kumbukumbu zangu CHADEMA hawahawa wanaosemwa kuwa wamekosea waliwai kushirikiana na CCM KIGOMA na wakaongoza kwa zamu ile halmashauri. Hivyo wanaweza bali hawa WAHUNI waliamua wao kama wao ilitakiwa wafuate taratibu ikiwa ni pamoja na kwenda kwenye vikao halali. Kama unaona vikao hivyo havikutendei haki unastep down simple. Hakuna kubembelezwa. The decision was right, they must be responsible for their actions.

 8. Ernest Felix Chacha

  21/08/2011 at 6:52 pm

  Kwa namna moja au nyingine kilichofanywa na CDM arusha ni sahihi

 9. Joseph Migunda

  26/08/2011 at 11:40 am

  Jamani, CDM ndicho chama kinachotambuliwa na tume ya uchaguzi. Hao madiwani ambao tunasema sasa kwamba kuwa wanawawakilisha wananchi walipata hiyo ridhaa awali kwa kuwa wanachama wa CDM. Heshima ya chama ipo hapo na lazima itambuliwe kwanza. Ni CDM ndicho kiliona kwa busara zake kuwa hao waliokuwa madiwani sasa walifaa kugombea nafasi hizo na wakawapitisha na kushinda, hilo ni jambo lingine ambalo busara za CDM lazima zitambuliwe. Kimsingi chama hakikutoa mamlaka wala waraka wa kuwapa nguvu wachaguliwa hawa wa udiwani kwamba watakapo pata udiwani basi wanauwezo wa kupanga maamuzi yao wenyewe hata kama hayaendani na ilani ya chama chao. Tunatambua kuwa wao wana nguvu kwa sasa kwa vile chama kimewapa hiyo nguvu ila kutumia nguvu hizo dhidi ya chama kilekile ni uhaini ambao hautakiwi kuvumilika. Kimsingi unapoongelea suala la natural justice, lazima lipitwe na athari za uwiano huo wa kimaamuzi kwa waliowengi na sio vinginevyo. Kama watu watano wanahatari ya kuhatarisha mustakabali wa watu million tano basi hapa ni lazima kuokoa waliowengi ambao ni salama “serve the survivors”. Kwa hakika mustakabali wa chama ni muhimu zaidi kuliko wa mtu mmoja mmoja. Ni kweli kwamba maamuzi haya yanaweza kuigharimu CDM ila gharama yake isingeweza kuizidi ile ya kutochukua uamuzi kama huo, sababu ni hizi;
  1. waliotimuliwa wangeachwa basi wangekuwa wanajigamba kuwa kwa nafasi zao kama wawakilishi wanaweza wakaingiza mada na maamuzi yao kwenye chama n yakikataliwa basi wanauwezo wa kuyasimamia hata kama hayazingatii maslahi ya chama.
  2. walio nje ya Arusha wangeanza kutumia loophole hiyo kuanzisha mambo ambayo yangekisumbua chama na hivyo chama kuwa na muda mwingi wa kushughulikia watu wachache badala ya kuwahangaikia waTZ.
  3. CDM kama chama kingeushangaza umma kwa kutofanya maamuzi kama ambavyo tumezoea kuona huko CCM na kwingineko. Kimsingi sio rahisi maamuzi ya aina yoyote yangetolewa kutoka bila kuwa na mianya ya watu kuhoji, lakini hiyo ndiyo siasa yenyewe. Lazima tukubali kubeba RISKS kama kweli tunataka kufanya kazi katikati ya jamii iliyoathiriwa na rushwa na kukata tamaa.

  Mi nadhani uwakilishi wa watu wa Arusha bado upo, madiwani wao watawakilisha matatizo yao mbele ya watawala na watasiadiwa tu ikibidi. Ila sio hekima kukumbuka kuwa hata kama sasa madiwani hawa ni wawakilishi wasio na chama bado ni muhimu kuacknowledge kuwa ni CDM nyuma yao iliyowafanya wawe hivyo.

  MI NADHANI MAAMUZI HAYA NA YA AINA HII NI MUHIMU NA LAZIMA KUPIGA MOYO KONDE ILI MAMBO YAENDE KWA MSTARI ULIONYOOKA.

 10. mimi

  04/09/2011 at 12:07 pm

  Mawazoyako siyo

 11. Tumbo

  29/09/2011 at 11:09 am

  CDM kuwafukuza madiwani wake si vibaya kwa sbb hawakutii katiba ya chama na kanuni,miongozo mbalimbali inayofanya cdm kuwa chama pinzani makini zaidi ukilinganisha na presure group zinginezo!
  Uzalendo umepotea! kizazi hiki kimelelewa ndani ya tamaa,ubinafsi na ufisadi uliokithiri kila mtu anataka kujilimbikizia mali. Lazima wawepo watanzania watakaoongoza kurudisha uzalendo na kuleta viongozi wenye kujali utznia

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Siasa

Sakata la waraka wa Maaskofu KKKT lang’oka na Msajili Mambo ya Ndani

Published

on

Waziri wa Mambo ya Ndani Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii, Merlin Komba ili kupisha uchunguzi wa barua iliyoandikwa ukilitaka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kufuta waraka ilioutoa Machi mwaka huu.

Barua iisambazwa kwenye mitandao ya kijamii ikiitaka KKKT kuufuta waraka wa Pasaka uliotolewa Machi 24 mwaka huu vinginevyo hatua kali za sheria zitachukuliwa dhidi ya kanisa hilo.

Waraka huo uliopewa jina la ‘Taifa letu amani yetu’ ulisainiwa na maaskofu 27 wa kanisa hilo. Ulijikita kujadili masuala ya jamii, uchumi, siasa, katiba mpya na matukio ambayo yako kinyume na kile lilichokiita tunu na misingi ya Taifa.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Waziri Nchemba amesema Serikali haipingani na dhehebu lolote na pale ambapo kuna uhitaji wa kufanyia kazi jambo kuhusu taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo taratibu huwa zinatumika kuzungumza na sio kama ilivyofanywa taarifa hiyo inayosambaa.

“Serikali inalinda uhuru wa kuabudu na waumini hivyo huo waraka una maudhui kama matatu, ni barua batili na tunaendelea kuchunguza kama imetengenezwa basi imetengenezwaje, kwani haujapita kwetu.” amesema Waziri Mwigulu.

Kutokana na msimamo huo wa serikali, Waziri Nchemba, amemsimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Sheria na Usajili wa Jumuiya za Kidini na Vyama vya Kijamii, Merlin Komba, kupisha uchunguzi wa barua iliyoandikwa kwa maaskofu wa KKKT.

“Hivyo basi, namsimamisha Msajili wa hizo taasisi kupisha uchunguzi na ikithibitika ni za Wizara tuweze kujua maana jambo hilo halijapita kwa Waziri, Katibu Mkuu na wala si maelekezo ya serikali,” amesema.

Hata hivyo, amewatoa hofu viongozi wa dini kutokana na sakata hilo na kuwataka waendelee na majukumu yao huku ikitahadharisha jamii kuwa makini na taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

“Tunawaomba viongozi wa dini waendelee na kazi zao, nasema jamii iwe macho na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya jamii na wasifanyie kazi taarifa hizo. Viongozi wa dini wasiwe na taharuki na taarifa hizo, hazina baraka za Serikali na wasisite kuwasiliana na Serikali kujua uhalali wake,” amesema.

Waziri Nchemba amesema waraka wa viongozi wa dini uliotolewa miezi iliyopita ni jambo lililopita na hakukuwa na haja ya kuendeleza malumbano yasiyo na tija kwenye jamii.

Katika waraka wa ujumbe wa pasaka uliosomwa katika makanisa ya Kilutheri kote nchini Tanzania na kusambaa katika mitandao ya kijamii, baraza hilo limeorodhesha mambo kadhaa ambayo wameyataja kuwa ndio tishio la umoja na amani ya nchi hiyo.

Utekwaji wa watu wa hivi karibuni, utesaji, kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa, muaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi ni baadhi tu ya mambo yaliyotajwa katika waraka huo.

Lakini pia Watanzania wamekuwa na hisia tofauti kuhusu viongozi wa dini kuzungumzia hali ya kisiasa nchini. Waraka wa KKKT ulikuja mwezi mmoja baada ya ule wa maaskofu wa kanisa katoliki ambao nao ulionya juu ya kuminywa kwa haki ya kufanya shughuli za kisiasa kama mikutano ya hadhara na maandamano.

Baada ya nyaraka hizo mbili kutolewa na Maaskofu, baadhi ya mambo yaliyokuwa yakilalamikiwa yalipata ufumbuzi ikiwemo kupungua kwa mauaji na uteswaji wa raia kulikuwa kunafanywa na watu wasiojulikana.

Continue Reading

Jamii

Waziri Mkuu Majaliwa: Hatutangazi nyongeza ya mshahara hadharani kuepusha athari kwa jamii

Published

on

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameweka wazi kuwa serikali haitatangaza nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma hadharani ili kuepusha athari kwa jamii ikiwemo kupanda kwa bei ya bidhaa.

Akizungumza leo Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu (CHADEMA), Susan Lymo ambaye alitaka kufahamu kwanini Serikali imewanyima au imeshindwa kuwalipa watumishi wa umma nyongeza ya mishahara ambayo ni haki yao ya msingi kulingana na miaka waliyokaa kazini.

Akijibu swali la Mbunge huyo, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali ina utaratibu wa kutoa nyongeza ya mishahara kwa watumishi wake lakini haitangazi kwa wananchi wote kama ambavyo imekuwa ikifanyika kwenye sherehe za wafanyakazi za Mei Mosi kila mwaka.

Amesema Serikali ikitangaza mishahara hadharani inaweza kusababisha usumbufu kwa watu wasio watumishi wa umma na inaweza kupandisha bei ya bidhaa na kuathiri mwenendo wa mahitaji ya wananchi sokoni.

Nyongeza za mishahara ambazo zinatangazwa hadharani, mara nyingi zina athari yake sio kwamba Serikali haikusudii kutoa nyongeza ya mshahara kwa mwaka, lakini unapotumia Mei Mosi kutangaza nyongeza ya mshahara unaleta athari kwenye jamii kwasababu vitu vinaweza vikapanda bei, vikawasumbua hata na wananchi ambao hawalipwi mshahara,” amesema Waziri Mkuu.

Amebainisha kuwa siyo lazima Serikali itangaze hadharani kila inapoongeza mishahara kwa watumishi wa umma lakini ifahamike kuwa Serikali ina utaratibu wake mzuri wa kuboresha stahiki za wafanyakazi wake kila mwaka.

Suala la nyongeza ya mishahara liko Serikalini na Mhe Rais ameishawahakikishia wafanyakazi atawaongeza mishahara na sio lazima litangazwe hadharani. Mshahara ni suala la mtu binafsi hata ukiongezwa leo kuwa tumeitangaza leo tumeongeza mshahara kwa kiwango hiki. Ukifanya hivi tayari umeleta kupanda kwa gharama’” amebainisha Waziri Mkuu.

Ameongeza kuwa mkakati wa Serikali ni kupunguza gharama za mahitaji kwenye masoko ili kuzuia mfuko wa bei za bidhaa.

Hata hivyo, Waziri Mkuu Mjaliwa amesema Serikali inaendelea kufanya sensa ya watumishi wote nchi nzima na zoezi hilo likikamilika itaboresha nyongeza ya mwaka, nyongeza ya mishahara na upandishaji wa madaraja.

Awali katika swali lake, Mbunge Lyima amesema Serikali inakiuka Sheria ya Utumishi wa Umma ya kuwapatia watumishi stahiki zao na kuwapunguzia motisha ya kufanya kazi kwa ufanisi katika maeneo yao ya kazi na kuathiri mafao baada ya kustaafu.

Hoja ya Mbunge huyo ni muendelezo wa malalamiko ya watumishi dhidi ya Serikali kwamba hawajapata stahiki zao tangu ilipoanza zoezi la ukakiki wa watumishi wa umma mwaka 2015. Katika zoezi hilo watumishi zaidi ya 9,000 walibainika kutokukidhi vigezo vya utumishi na hivyo kuondolewa kazini.

Huenda kauli aliyoitoa Waziri Mkuu leo Bungeni inaweza ikatofautiana na ile ya Rais John Magufuli aliyoitoa wakati wa sherehe za Mei Mosi, 2018 mijini Iringa ambapo alinukuliwa akisema hawezi kutoa nyongeza ya mishahara akidai Serikali haina fedha.

Kwangu mimi ninafikiria hizi pesa tunazotoa kwa ajili ya elimu bure ni nzuri kuliko fedha hizo kuzipeleka kuongezea mishahara, naona bora kuwapa mikopo wanafunzi wa vyuo vikuu kuliko kuongezea wafanyakazi mishahara,

Nikisema nitaongeza hizo pesa mimi nitazitoa wapi? naogopa kusema uongo. Hata mimi napenda kupandishiwa mshahara lakini kwa hali halisi ya sasa hivi lazima niwaeleze ukweli,” alinukuliwa Rais Magufuli.

Hata hivyo alibainisha kuwa kabla ya kuondoka madarakani ataboresha maslahi ya wafanyakazi wa umma, “Nawaahidi, kipindi changu cha urais hakitaisha kabla sijapandisha mishahara kwa wafanyakazi, kupandisha kwangu haitakuwa kwa shilingi elfu kumi, itakuwa ni kupandisha kwelikwel.”

Continue Reading

Jamii

Maaskofu KKKT wapewa siku 10 kufuta waraka

Published

on

Serikali imetoa siku 10 kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), kuufuta kwa maandishi waraka wao waliotuoa Machi 24 mwaka huu na kisha kuujulisha Umma kwa njia mbalimbali walizotumia kuusambaza.

Kanisa la KKKT kupitia Baraza lake la Maaskofu lilitoa waraka uliopewa jina la ‘Taifa Letu Amani Yetu’ wakati wa Pasaka ambao mbali na masuala ya kiroho, ulibainisha mambo kadhaa yanayogusa mstakabali wa taifa.

Katika mitandao ya kijamii leo imesambazwa barua yenye kumbukumbu no. SO.748/25 inayoonyesha imeandikwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Wizara ya Mambo ya Ndani kwenda kwa Mwenyekiti /askofu Mkuu wa KKKT iliyoandikwa Mei 30, 2018 ikitoa maelekezo ya kufutwa waraka huo ndani ya siku 10 tangu ilipoandikwa barua hiyo.

Ikiwa na kichwa cha habari ‘Ujumbe wa Baraza la Maaskofu wa KKKT’ barua hiyo inaeleza baraza hilo halitambuliki kisheria katika ofisi ya msajili.

“Unaelekezwa kuufuta waraka husika kwa maandishi na kuujulisha umma kuwa taasisi yako haikuwa na haina uwezo kisheria kufanya kile mlichokifanya. Maandishi hayo yaufikie umma wa Watanzania kwa kupitia vyombo vya habari na njia zingine zilezile zilizotumika kuufikisha waraka ule mliouita ‘Ujumbe wa Baraza la Maaskofu KKKT’.

Hata hivyo, barua hiyo imetoa onyo kali kwa taasisi hiyo dini nchi kutekeleza agizo mara moja la sivyo itachukuliwa hatua za kisheria.

“Maelekezo haya yatekelezwe ndani ya siku kumi tangu kupokea kwa barua hii vinginevyo hatua kali zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi ya taasisi hii,” inasema barua hiyo.

Ikumbukwe kuwa  waraka huo ulisainiwa na maaskofu 27 wa kanisa hilo nchini na kutaja baadhi ya mambo hayo kuwa ni pamoja na utekaji, utesaji, kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, vitisho, ubambikiziaji wa kesi, na matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi.ni hali ya kijamii na kiuchumi, maisha ya siasa, na masuala mtambuka likiwamo suala la Katiba Mpya.

Waraka uliongeza pia kwamba uhuru wa kujieleza, kutoa na kupokea habari umeendelea kutoweka nchini huku ukionya kubanwa na hatimaye kuelekea kupungua kwa uhuru wa Bunge, Mahakama, na Tume ya Uchaguzi, ukisema hatua hii ni pamoja na kudhoofishwa kwa serikali za Mitaa.

Lakini kabla ya KKKT kutoa waraka wao, Kanisa Katoliki nalo lilitoa waraka kama huo likionya baadhi ya mambo ikiwemo uminywaji wa misingi ya demokrasia ya vyama vingi na uhuru wa kujieleza.

Baada ya kusambaa kwa waraka huo, yalijitokeza mambo mengi ikiwemo kutofautiana na kwa mawazo ya wananchi kuhusu wajibu wa viongozi wa dini katika kutoa ushauri, kuonya au kukemea pale mambo yanapoenda mrama.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Maaskofu wa KKKT

Hata hivyo, barua hiyo imepokelewa kwa hisia tofauti na watumiaji wa mitandao ya kijamii ikizingatiwa kuwa suala hilo lilijadiliwa na kupita, iweje linaibuka tena wakati huu ambapo kuna utulivu na yale mambo waliyoyapigia kelele na maaskofu  yamepungua ikiwemo kuteswa, kupotea kwa watu na vitisho dhidi ya viongozi wa kisiasa.

 

Wananchi bado wanawaamini viongozi wa dini

Wadau mbalimbali wa masuala ya kijamii wamesema kama kweli barua hiyo imetolewa na serikali, inaweza kuchochea taharuki zaidi kwa waumini wa kanisa hilo na wananchi kwasababu linagusa moja kwa moja imani zao.

Amebainisha kuwa bado waumini wengi wana imani na viongozi wao dini na kwamba yale wanayotamka yanakuwa na nia njema kwa jamii yao. Na katika muktadha huo serikali inapaswa kuwa makini ili kuepusha matatizo zaidi yanayoweza kutokea.

Akizungumza na FikraPevu, Katibu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena amesema kama serikali ilibaini kuna tatizo kwenye usajili wa Baraza la Maaskofu la KKKT ingekaa na wahusika na kulimaliza kuliko kujitokeza hadharani na kuendeleza jambo ambalo limepita.

“Mimi namwamini Mungu kuliko serikali na viongozi wangu wa dini hasa Maaskofu. Hivyo serikali inapaswa kuwa makini na mambo yanayogusa imani za watu. Katika hili walipaswa kutafakari sana jinsi ya kushughulika nalo. Vinginevyo halina afya kwa ustawi wa taifa letu,” amesema Meena.

Amesema Maaskofu walitimiza wajibu wao wa kuonya kabla mambo hayajaharibika na serikali inapaswa kuyafanyika kazi yale yalyotajwa kwenye waraka au kukaa kimya ili kuepusha migongano isiyo na faida kwa taifa.

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com