Connect with us

Featured

Mauaji ya Mwandishi Iringa: Waandishi wataka Waziri, IGP wang’oke

WAKATI Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari (UTPC) ikituma ujumbe mzito mkoani Iringa, Chama cha waandishi wa habari mkoani Mbeya, kimetoa tamko rasmi la kumtaka waziri wa mambo ya ndani, Mkuu wa Jeshi la Polisi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa kujiuzulu mara moja…

Published

on

WAKATI Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari (UTPC) ikituma ujumbe mzito mkoani Iringa, Chama cha waandishi wa habari mkoani Mbeya, kimetoa tamko rasmi la kumtaka waziri wa mambo ya ndani, Mkuu wa Jeshi la Polisi na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa kujiuzulu mara moja kufuatia matukio ya mauaji yanayofanywa na Jeshi la Polsi ikiwemo la Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoani Iringa, Daud Mwangosi.

Tukio la kuuwawa kwa Mwandishi wa Habari, Daudi Mwangosi

Aidha MBPC  imetoa tamko la  kusitisha kuandika habari zozote zinazohusiana na Jeshi la Polisi nchini, kuunda tume  ya uchunguzi wa kifo cha Mwangosi ambaye pia ni mwandishi wa habari wa Channel Ten  itakayowahusisha  wanahabari na wadau wengine na siyo DCI Manumba na maofisa wengine wa jeshi la Polisi na kuvitaka vilabu vyote vya wanahabari nchini kuunga mkono kauli hiyo.

Akitoa tamko hilo lililojadiliwa na wanachama wa Mbeya Press Club,uhindini jijini Mbeya leo,Mwenyekiti wa MBPC,Christopher Nyenyembe amesema wamepokea taarifa ya kifo cha Mwangosi kwa masikitiko makubwa  na wanahabari wameathirika kisaikolojia na kiutendaji.

Nyenyembe ambaye pia ni Mwakilishi wa gazeti la Tanzania Daima mkoani Mbeya   alisema wanahabari mkoani Mbeya wamekubaliana kwa pamoja kutoandika habari za polisi hadi watakapowahakikishia usalama na mazingira mazuri ya kufanya kazi nao kwa kuweka mikataba ya kufanya nao kazi  ikiwemo na vyama vya siasa.

Alisema Viongozi wa juu wenye dhamana ya ulinzi na usalama wamekuwa wakifumbia macho matukio ya Polisi kuuwa raia na kutoa taarifa zisizo sahihi  kutokana na kuwashirikisha polisi hivyo wana kila sababu ya kuwajibika kuhusiana na tukio hilo na mengine yaliyoundiwa tume kwani yanahatarisha uvunjifu wa amani.

“Tunataka waziri wa mambo ya ndani ajiudhuru,IGP Said Mwema,RPC Kamhunda,walioshiriki Nyololo na wale waliohusika kufanya mauaji,lakini pia tunasitisha kuandika habari za Polisi na wanasiasa hadi pande zote  tubaliane kuandikishiana mkataba wa kufanya nao kazi,kwa sababu tunaokufa ni sisi wa chini mbona hata Viongozi wa siasa hawafi,”alisema

Mwenyekiti huyo alisema kuwa Jeshi la Polisi lina maofisa habari wao hivyo waendelee kuwatumia hadi pale watakapotekeleza tamko hilo,na kuhakikisha usalama wa wanahabari katika kazi.

Alisema Mwanahabari huyo amekufa kishujaa akiwa kazini huku akiendelea kutetea haki za mwanahabari mwenzake hadi tone la mwisho la damu  na kwamba ni ushindi mkubwa kwa wanahabari wote na kuendelea kupata ujasiri wa kufanyakazi.

“Tusivunjike moyo ingawa  hali hii inatudhihirisha jinsi tulivyo na mazingira magumu na mwangosi amekufa kutokana na mfumo mbaya wa serikali kutothamini media kama mhimili wa nne wa nchi…sote tumeona alivyouawa kinyama na kikatili haiwezi kuvumilika, tunatoa pole kwa familia, Iringa Press Club na wanahabari wote,”alisema.

Matukio ya kupigwa,kunyang’anywa vifaa vya utendaji wa kazi na kudhalilishwa kwa waandishi wa habari  yametokea mara kwa mara ambapo Mwanahabari wa chombo kimoja cha radio (jina tunalihifadhi) alipigwa bomu la machozi wakati akiripoti laivu katika chombo chake kuhusu tukio la vurugu za wamachinga jijini Mbeya.

Tukio jingine limewahi kutokea maeneo ya Airport  ambapo mwanahabari mmoja amewahi kunyang’anywa kamera  na polisi  akiwa anapiga picha mwili wa marehemu licha ya mwanahabari huyo kuwapa taarifa Polisi katika tukio hilo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti Nyenyembe,alisema taarifa za kuwasiliana na Viongozi wa klabu ya Iringa ambapo taarifa za awali zinasema kuwa mwili wa marehemu Mwangosi unatarajiwa kuzikwa wilayani Rungwe ambako ndiko nyumbani kwa marehemu.

Tayari Umoja wa Vyama vya waandishi wa Habari umemtuma ujumbe mzito mkoani Iringa kufuatilia sakata hilo, kushiriki mazishi na kuangalia hatua zaidi za kuchukua. Marehemu Mwangosi alikua  mjumbe wa Umoja huo.

Imeandikwa na Thompson Mpanji, FikraPevu – Mbeya

Continue Reading
20 Comments

20 Comments

 1. mapambano yetu

  04/09/2012 at 11:54 am

  Hata ninyi wahandishi wengi wenu ni vinyonga.

  Kama kweli hizi habari zimewauma kutoka rohoni basi msiandike habari za CCM na serikali yake. kuhusu vyama vingine andikeni ili ccm na serikali yake waumie.

  Mnajua wazi kuwa ccm wana vyombo vya habari, pia serikali nayo inavyo vyake, so hayo maamuzi ya kusitisha vyama vingine ni sawa na kuendelea kuipigia kampeni serikali ya CCM kwani itatumia mwanya huo kujisafisha kwa kutumia vyombo vyake pamoja na vle vya serikali.

  Tafakari na mchukue hatua, watanzania kwa sasa hutudanganyiki hata mkitumiwa tunajua la kufanya.

 2. mapambano yetu

  04/09/2012 at 12:07 pm

  Sitashangaa mkigeuza ukweli kuwa uongo maana nanyi ni waoga kuliko dr. ulimboka.

  IGP anafanya vikao na viongozi wenu, wakisha Chukua Chao Mapema wanasahau waliyotendewa na mpaka sasa wanausalama wanafanya kila juhudi kuipoza familia ya marehemu na kigogo mmoja wa ccm anatumiwa kwa hili ili kutoa misaada na ahadi tele kwa familia kuipoza na kuwashauri wasiambatane na waandishi habari pamoja na wana CHADEMA. Mda si mrefu hatutasikia chombo chochote kikizungumzia habari hii.

  Tunajua chenu mtachukua lakini jamii isipotoshwe kwa hili.

 3. mwinyimvua

  04/09/2012 at 3:56 pm

  kimsingi masikitiko hayaishi kwa kumpoteza mpiganaji.

  Kwa wanaomfahamu marehemu mwangosi bila shaka hawataacha kubaini umuhimu wake hasa wakati huu atakapokosekana.

  Bila shaka ipo haja sasa waandishi wa habari kuelewa hatari inayotukabili tunapokuwa kazini, hasa na wanasiasa kwani licha ya kuwa katika wajibu wetu wa kitaaluma na kijamii, wenzetu wamekuwa hawana nadhari kwetu na kutufanya kuwa ni wahanga wa matendo yao.

  Kama mwanachama wa Press Club napenda niungane na msimamo wa MBPC kwani ni hatari iliyo ndani yetu na ni vyema nasi tukalielewa hilo badala ya kushabikia mambo kwani wanasiasa wanatutumia na polisi wanatuua na kutunyanyasa badala ya kutulinda.

  • Ally Juma

   04/09/2012 at 7:38 pm

   Sikuungi mkono kwa suala moja, vyama vya siasa vinachangia mwananchi kupata haki yake.

   Acha uccm ndg yangu, wanawatumia kwa maslai ya nani? miundombinu mibovu, mishahara haitoshi, katiba mbovu halafu unadai wanatumiwa!!

   Nakushangaa sana kwa sababu kwa haraka unadhani waandishi hawahathiriki na matatizo hayo y kijamii, inamaana unataka wananchi wakiandamana kupinga mfumko wa bei waandishi wawe wapi? walimu wakihitaji maslai bora ili vijana wetu wapate elimu stahili waandishi wawe wapi?

   Madaktari wakidai haki zao ili watoe huduma bora kwa wananchi waandishi wawe wapi? Suala unalolisema linamkono wa serikali kuwapoza kwa maneno mepesi na nyororo bila kuchukua hatua kama ilivyotokea Zanzibar kwenye uchomaji wa makanisa.

   FIKIRI KWA MAKINI NDUGU YANGU USIKUWA MMOJAWAPO UNAYETETEA SUMU huku ukijua watakao angamia na wewe umo.

 4. fatuma ally

  04/09/2012 at 6:33 pm

  ni ujinga kukubali kila amri tena isiyo halali. IGP anaformulate laws zake, anajipa kibali cha kuua, analeta undugu kwenye mambo ya kitaifa. polis wanaua wanaumiza na wengine wanageuzwa vilema yeye anachekelea 2 il-hali aendelee kusifiwa na rais na chama tawala. siwaelewi kabisa hasa ikulu sijui inatoa kauli gani kuhusu hili.

 5. Mwanaid T

  04/09/2012 at 6:39 pm

  waandishi siwaelewi kama kweli mnafikili kwa makini, kaeni na mtafakari hili kwa makini maana tunaona kama mnacheza mchezo wa kuigiza huku maisha ya mwenzenu yamepotea bila hatia.

 6. mwambungu

  04/09/2012 at 7:01 pm

  hivyo ndivyo jeshi la polisi lilivyo jipachika jina baya la uuwaji wa raia badala ya usalama wa raia. lakini je hii yote ni kwa faida ya nani ccm au serikali ya ccm ni mbaya sana vyombo mvya dola kugeuzwa vyuombo vya watu fulani kwa kuwa jeshi la polisi kwa sasa si usalama wa raia inabidi huyu mkuu wa jeshi hili ndg said mwema ajiwajibishe bila kusubiri kuwajibishwa maana kazi imemshinda.

  Na kama hataweza yeye binafsi kujiondoa madarakani inabidi tumpeleke mahakamani mara moja kujibu mashtaka ya mauaji wa raia wasio na hatia. binafsi nimesikitika sana kwa mauaji haya. nimtakie marehemu mwangosi mapumziko mema na wale woote walioo uwawa wakiwa chini ya jeshi la polisi.

  Shime watanzania tupinge kwa nguvu zetu zoote huu uovu unaofanywa na jeshi la polisi kwakutumia kodi zetu nwenyewe kwa kweli huuu ni upuuzi wa kupitiliza.

  • Ally Juma

   04/09/2012 at 7:16 pm

   nakuunga mkono kaka,

 7. Ally Juma

  04/09/2012 at 7:09 pm

  waandishi itisheni maandamano nchi nzima, mnajifanya kuhuzunika na kusikitishwa na jambo hili kumbe hakuna lolote, mnageuza kifo cha mwenzenu kuwa mtaji wenu na kujiingizia kipato mifukoni.

  Kwa sasa mnasubili mpewe chenu ili mtulie na mjadala huu ufungwe. Siwaungi mkono hata kidogo kwa sababu najua mtailaghai jamii, roho za watu ziwe juu juu, huku nyuma mpozwe na kutulia tuli zaidi ya maji ndani ya glass. Mfano halis ni huu: Gazeti la mwanahalis lilifungiwa, mlijifanya kuwa mbogo mkaishia kwenye tamko dhaifu la kutoandika habari za wizara husika.

  Huu ni udhaifu mkubwa ningekuwa mimi ningeshauri habari zote nzuri za serikali ya CCM na za Chama tawala zisitolewe kabisa. pili mabaya yote yanayofanywa na serikali na chama chake yapewe kipaumbele. Sasa ninyi mnataka chenu ili msusie habari zote za vyama vya siasa ili ccm na serikali wanufaike kwa sababu wanavyombo vyao. Acheni woga itisheni maandamano nchi nzima ili wananchi tuwaunge mkono kuishinikiza serikali kutenda haki mahali husika. videos zipo tume ya nini kufanya uchunguzi kama sio kwamba mnataka kupeana ulaji?

  Serikal inasema vikao havikuwa halali kwa sababu ya sensa, lakini mbona dr. bilal aliendelea mkutano wa hadhara kuitangaza ccm? msitufanye wajinga, waandishi wengi ni mamluki wa ccm ndiyo maana hamwezi kutoa maamzi stahiki. nawashauri kama hamtaweza kuchukua hatua stahili basi kuweni kimya kuliko kutulaghai sisi huku mkiwa na chenu mifukoni. Kumbukeni leo ni yule, kesho waweza kuwa wewe au mwanao, mzazi wako, rafiki au jirani.

  UNGANISHENI JAMII NA WATANZANIA WOTE TUANDAMANE KUPINGA UBABAISHAJI HUU

 8. lavavan

  05/09/2012 at 10:37 am

  hivi ni kwann siku zote lawama zote ziende upande mmoja tu,watanzania tuangalie kwa makini mambo haya tujiulize nini chanzo ndipo tuanze kulaumu

  • Ally Juma

   05/09/2012 at 4:35 pm

   we maoni yako ni yapi kuhusu hili?

 9. Ahadi Malamso

  05/09/2012 at 12:57 pm

  Waziri wa mambo ya ndani ameunda tume, itafute majibu ya maswali, ambayo hata mtoto mdogo anayajua majibu hayo. Tume inatakiwa kumtaja aliye amuru polisi wakawapige raia wasio na hatia hata kusababisha vifo. Na hatimaye wote wafikishwe mahakamani.

  • Ally Juma

   05/09/2012 at 4:38 pm

   itamaliza leo hiyo tume? mauaji ya arusha tume ilisemaje?, ya dr. ulimboka? mauaji ya songea? morogoro? tupo!

 10. GODBLESS NKYA

  05/09/2012 at 1:58 pm

  WAZIRI, IGP WAONDOKE, RPC

  • Ally Juma

   05/09/2012 at 4:38 pm

   waondoke tu

 11. Ally waitara

  05/09/2012 at 5:19 pm

  mh! huu mziki mnene

 12. juma magombe

  06/09/2012 at 11:18 am

  inauma sana kuona serikali yetu imetugeuka!
  Dah, nakumbuka usemi usemao…mafahali wawili wagombanapo nyasi hupata shida! Jamani tanzania ya leo si ile tena ya kisiwa cha amani, bali ni kisiwa cha mauwaji, uporaji wa mali za wanyonge, yaani ni nchi iliyo jaa uchafu wa kila aina wa manyanyaso
  Kiukweli katika tanzania ya leo maskini kama mimi hatuna haki kabisa, leo hii kauwawa mwandishi imesikika lakini ningeuwawa miye au maskini mwenzangu hata jirani yangu hasingejua..
  Inauma sana, serikali yetu kutugeuka, jesi la polisi halitufai kabisa lipo kwa ajili ya maslai binafsi na si kwaajili ya kutulinda watanzania!

  Jamani watanzania, narudia tena jeshi la polisi halitufai………….!

 13. mohamed malibiche

  06/09/2012 at 9:53 pm

  imefika wakati serikali igeuke nyuma na kuangalia wapi tulikuwa, mshikamano tulionao, na hali halisi ya sasa kwa kweli hali iliyopo hivi sasa ni mbaya na kinyume na maadili ya mtanzania kwa kweli tumefika katika red point.

 14. Meshack K.

  07/09/2012 at 6:54 am

  Tuacheni ujinga! Vunja ukimya…!

 15. Meshack K.

  07/09/2012 at 7:05 am

  Kuhusu kukamatwa askari aliyeuwa sio dawa, mbona waliobaki ni vibaraka na wamefundishwa kufanya alichofanya huyo mmoja. kazi bado, tena naona kama anaonewa tu maana kama kweli alisomea anatambua kabisa alichofanya kuwa ni kutii amri, atafutwe aliyemtuma na mwingine na yeye awe wa mwisho kuhukumiwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Featured

UJASUSI: Jinsi kijana wa kiume kutoka New Zealand alivyojaribu  kumuua Malikia Elizabeth II

Published

on

Shirika la Ujasusi la New Zealand  (SIS) limethibitisha kwa mara ya kwanza kwamba kulikuwa na jaribio la kumuua Malikia Elizabeth II wakati alipotembelea jiji la Kusini la Dunedin mwaka 1981.

Jaribio hilo la kumuua Malikia linalodaiwa kutekelezwa na kijana wa kiume limechochea hamasa ya polisi kutaka kujua ni kwa kiasi gani wanausalama hao walifanikiwa kuzima njama hizo.

Taarifa iliyotolewa na SIS  zinaonesha kuwa kijana huyo, Christopher Lewis (17) alipiga risasi kuelekea kwa Malikia wakati akishuka kwenye gari lake ambapo alikuwa anaenda kushuhudia Maonyesho ya Sayansi yaliyofanyika Oktoba 14, 1981 katika jiji hilo. Tukio hilo lilitokea akiwa katika ziara ya siku 8 kutembelea nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.

“Lewis alidhamiria kumuua Malikia, hata hivyo hakuwa katika nafasi nzuri ya kurusha risasi, hata silaha iliyotumia haikuwa katika umbali wa kuweza kumfikia mhusika,” imesema taarifa iliyotumwa SIS kwa vyombo vya habari.

Lewis ambaye anatajwa kwenye taarifa ya ujasusi kama ‘kijana msumbufu’ hakuhukumiwa kwa jaribio la kutaka kuua au kosa la uhaini. Tukio hilo lilifanywa kuwa siri ili kuzuia sifa mbaya kwa nchi (New Zealand) ambayo ilitembelewa na mgeni wa heshima. Badala yake Lewis alihukumiwa kwa kumiliki silaha kinyume na sheria na kufyatua risasi.

                       Malikia Elizabeth II akiwa ameambatana na walinzi wake alipotembelea New Zealand

Inaelezwa kuwa watu waliohudhuria tukio la kuwasili kwa Malikia walisikia mlio wa risasi lakini Polisi waliokuwa wanasimamia usalama katika eneo hilo la Dunedin waliwaambia kuwa ilikuwa ni sauti ya kuanguka kwa kitu au magari kugongana.

“Uchunguzi wa sasa wa polisi juu milio iliyosikika umefanywa kwa umakini na wawakilishi wa vyombo vya habari wamepata mrejesho kuwa kelele zilisababishwa na baruti”, inaeleza ripoti kutoka SIS iliyotolewa mwaka 1981 baada ya kutokea tukio hilo.

Kulingana taarifa za ujasusi zinaeleza kuwa polisi wamekuwa wakifuatilia nyendo za Lewis tangu 1986 ambapo Malikia alitembelea tena New Zealand wakiogopa kuwa anaweza kutekeleza tena uhalifu huo. Kuwekwa wazi kwa siri hiyo kumewaibua polisi ambao wameanza kuchunguza upya kesi hiyo.

Zaidi ya muongo mmoja uliopita, Lewis alihukumiwa kwa mauaji ya mwanamke mmoja katika mji wa Auckland na kumteka mtoto wa kike ambapo baadaye alimtupa karibu na kanisa.

Kulingana na taarifa mbalimbali za wakati huo zinaeleza kuwa Lewis alijidhuru kwa umeme akiwa gerezani mnamo 1997 akisubiri hukumu ya kuua. Lakini alikana mashtaka ya kuua kwa ujumbe mfupi wa kifo (suicide note).

New Zealand ilipata uhuru mwaka 1947 kutoka kwa Uingereza lakini inamuheshimu Malikia kama kiongozi wa taifa. Ameitembelea nchi hiyo kama Malikia mara 10 na mara ya mwisho ilikuwa 2002.

Continue Reading

Featured

FREEDOM HOUSE: Tanzania ina uhuru kiasi, kufungiwa vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya kisiasa kuididimiza kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa

Published

on

Ripoti mpya iliyotolewa na taasisi huru ya Freedom House imesema misingi ya demokrasia ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kukusanyika imeendelea kudhoofika nchini Tanzania na hali hiyo isiporekebishwa itaingia kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa duniani.

Kulingana na  Freedom House  ambao walichambua data katika nchi 195 za ulimwenguni katika mwaka 2017 wamebaini kuwa nchi 88 zina uhuru,  58 zimejumuishwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku 48 zikiwekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa misingi ya demokrasia ikiwemo uchaguzi usio huru na haki, uhuru wa kujieleza umeendelea kushuka kwa mwaka wa 12 mfufululizo duniani kote. Miongoni mwa matokeo yaliyostaajabisha ni kudhoofika kwa  Marekani ambayo ni mama wa demokrasia kutokana na uchunguzi unaofanywa na Mwendesha Mashtaka Maalumu kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 ambao ulimpa ushindi Rais Donald Trump.

Tanzania imewekwa kwenye nchi 88 ambazo zina uhuru kiasi lakini inatahadharishwa kuwa inaweza kuingia kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa. Tahadhari hiyo inatokana na mwenendo wa viongozi wa serikali kufungia vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kushtakiwa kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa tuhuma za uchochezi na kukamatwa kwa wapinzani wa kisiasa ambao wanakosoa na kutoa mawazo yanayotofautiana na serikali.

Pia utekelezaji wa Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 na Sheria ya Makosa ya Mtandao  ya mwaka 2015 umekuwa ukilalamikiwa na wadau wa maendeleo kuwa ni mkakati wa kudhoofisha uhuru wa kutoa maoni, uwazi na uwajibikaji.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini hivi karibuni kilitoa tamko la tathmini ya uchaguzi mdogo wa marudio wa kuchagua madiwani uliofanyika katika kata 43 kwenye mikoa 19 ya Tanzania  Novemba 24 mwaka jana ambapo kilibaini mambo mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Tathmini hiyo iliibua mambo mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya nguvu ya vyombo vya dola, matukio ya watu kutekwa na watu wasiojulikana, watu kupigwa, kujeruhiwa  kwa lengo la kuharibu na kuvuruga uchaguzi  na vilevile kuwatia hofu wapiga kura.

 

Afrika Mashariki hali bado tete

Tanzania inaungana nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya na Uganda ambazo nazo zimewekwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku za Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini zimejumuishwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa.

Awali Uganda ilikuwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa lakini imepanda hadi kwenye uhuru kiasi kwasababu ya  kuimarika kwa tasnia ya habari na utashi wa wanahabari, blogu na  uhuru wa wananchi kutoa maoni yao licha ya mazingira ya kisiasa kuminywa na utawala wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni.

Rais Museveni mwenye umri wa miaka 73 amekuwepo madarakani  tangu 1986 amefanikiwa kubadilisha sheria  ya ukomo wa umri wa miaka 75 wa kugombea urais ambapo atapata fursa ya kugombea tena mwaka 2021. Chaguzi nchini Uganda zimekuwa zikitawaliwa na vurugu za polisi na wananchi, kuzimwa kwa intaneti na kuwekwa kizuizini kwa viongozi wa upinzani ikiwemo Kizza Besigye wa chama cha Forum for Democratic Change.

Kwa upande wa Kenya ambayo imekuwa ikisifika kwa kuimarisha misingi ya demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo kwa mara ya kwanza mahakama ilifanikiwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Urais yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta uliofanyika Agosti 2018. Uchaguzi ulirudiwa na Rais Kenyatta alichaguliwa tena.

Marudio ya uchaguzi yalilamikiwa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa hayakuzingatia haki za binadamu ambapo watu ambao walipinga uchaguzi huo walikumbana na mkono wa dola. Matendo hayo ndiyo yaliiweka Kenya kwenye kundi la nchi zilizo na uhuru kiasi.

Burundi na Sudan Kusini zimewekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa kutokana na mapigano ya kikabila ambayo yamedhoofisha mfumo wa kisiasa wa kuongoza nchi. Vyombo vya habari na wananchi wanaotoa maoni tofauti na serikali wamekuwa wakiteswa, kufungwa na kuuwawa.

Chanzo: Freedom House           – Nchi zisizo na  uhuru  – Nchi zenye uhuru     – nchi zenye uhuru kiasi   

 

Hali ilivyo Afrika

Afrika kama zilivyo nchi za Afrika Mashariki hali ya demokrasia siyo ya kuridhisha ikizingatiwa kuwa asilimia 11 ya wakazi wapatao bilioni 1.02 wa bara hilo ndio wana uhuru wa kweli, huku 52% wana uhuru kiasi na 37% hawa uhuru kabisa.

Ripoti ya Freedom House inaeleza kuwa waliangazia nchi 49 za Afrika na kugundua kuwa nchi 8 (18%) ndio zina uhuru wa kweli, nchi 22 (43%) zina uhuru kiasi na 19 (39%) hazina uhuru kabisa. Nchi zinazotajwa kuwa na uhuru ni Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Ghana, Togo, Senegal na Kisiwa cha Sao Tome.

 Sababu ya nchi nyingi za Afrika kuwepo kwenye kundi la zisizo na uhuru ni matokeo ya viongozi kukaa madarakani muda mrefu, vurugu za kisiasa na kikabila ambazo zimekuwa zikihatarisha haki za binadamu.

 

Demokrasia ya Dunia

Demokrasia ya dunia inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kisiasa kuliko wakati mwingine ambapo mwaka 2017 ulishuhudia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo kuminywa kwa  uchaguzi huru na kweli, haki za watu wachache, uhuru wa kujieleza, utawala wa sheria.

Nchi 71 kati ya 195 zimeshuhudiwa zikiteteleka katika kulinda haki za kisiasa na jamii ambapo ni nchi 35 tu ndizo zimeweza kulinda haki hizo. Kudhoofika kwa demokrasia kunaendelea kushuka kwa miaka 12 mfululizo na hatua muhimu zisipochukuliwa amani ya dunia itawekwa rehani.

Marekani ambayo ni bingwa wa demokrasia duniani nayo imeripotiwa na taasisi ya Freedom House kudhoofika katika kulinda haki za kisiasa na kijamii na kuzua mgongano wa mawazo miongoni mwa nchi zinazoibukia katika kujenga demokrasia ya dunia.

Tangu kuisha kwa vita baridi, nchi nyingi ziliachana na utawala wa kiimla na kugeukia demokrasia ya vyama vingi lakini hali hiyo imeanza kujitokeza tena ambapo idadi ya viongozi wanaoongoza kwa udikteta inaongezeka.

 

Uhuru wa nchi moja unategemea uhuru wa nchi zote

Demokrasia itabaki kuwa tunu muhimu kwa jamii zilizostaarabika, ikifungua milango ya uwazi, mawazo na fursa mpya na zaidi ya yote kulinda uhuru wa mtu mmoja mmoja. Ikiwa watu duniani kote wanadai mazingira mazuri ya kisiasa ni dhahiri wanakumbatia misingi ya demokrasia: uchaguzi huru, uhuru wa kujieleza, uwazi na uwajibikaji wa serikali, utawala wa sheria ambao hauingiliwi na polisi, jeshi au taasisi nyingine za nchi.

Hata hivyo, Karne ya 21 imeshuhudia ugumu wa kuifanya demokrasia kuwa endelevu ambapo baadhi ya nchi zinatekeleza lakini zingine zinapuuza. Utawala wa kidekteta wa Urusi na China unatambua wazi ili uendelee kuwepo unahitaji kuimarisha demokrasia katika nchi nyingine ili ziendelee kufaidika na mahusiano ya kidiplomasia. Ukuaji wa  demokrasia ni kulinda haki za watu wote duniani kupitia utandawazi   

Continue Reading

Afya

Is Tanzania’s Adolescent Fertility Rate Three Times Higher Than Global Counterparts?

Published

on

The Comprehensive Community-Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT), an organization ​which works to provide affordable medical and rehabilitative services for mothers and newborns throughout Dar-es-Salaam, marked World Contraception Day on September 26 with a call for more efforts to meet the reproductive health needs of teens between 15 and 19 years old.

The report highlights a worrying statistic — Tanzania’s adolescents are having almost three times as many children on average as their global counterparts, with 135 births per 1000 girls reported in the country, compared to an average of 44 per 1000 girls aged 15–19 worldwide in 2015.

CCRBT attributes the high adolescent fertility rate to a lack of access to contraceptive services, with Technical Advisor for Nursing Bola Abbas saying, that only about 8 per cent of current family planning clients are between the ages of 15 to 19.

On a national scale, Abbas explains, demand for family planning among adolescent girls is still very low, with only one out of every three of those who are sexually active within the 15 to 19 age group using modern contraceptive methods.

So the question is, how does Tanzania’s adolescent fertility rate compare to that of the rest of the world?

Pesacheck investigated the claim that Tanzanian adolescents are having three times as many children as their peers in the rest of the world and found that the statement is TRUE for the following reasons:

Tanzania’s adolescent fertility numbers are rather high, with 4.4% of girls aged 15 having given birth according to the country’s Demographic and Health Survey.

The Sustainable Development Goals call for countries to ensure universal access to sexual and reproductive healthcare services, including family planning, information and education, and the integration of reproductive health into national strategies and programmes by 2030.

The indicators for this goal are the proportion of women of reproductive age (15–49 years) who have their need for family planning satisfied with modern methods, and the adolescent birth rate (10–14 years and 15–19 years) per 1,000 women in that age group.

For several sub-Saharan countries, Tanzania included, access to modern family planning methods is low for this particular age group, and as a result, the regional average is 105 births per 1,000, which is more than double the global average.

Tanzania’s National Bureau of Statistics produced a national fertility and nuptiality report based on data from the 2012 national census, which shows that Adolescent Fertility Rate (AFR) was 81 births per 1,000 women aged 15–19.

The report further shows that in 2012, 23.3% of adolescent girls in the country had given birth to at least one child. Additionally, 42.2% of girls who had never attended school had given birth, compared to just 9% of those who had reached university.

This shows that there is a need for contraceptive access for teenage girls in Tanzania, especially for girls in rural areas and those with limited access to education.

The Tanzania Demographic and Health Survey 2015–16 indicates that 27% of girls aged 15–19 have given birth. Crude birth rates for girls aged 15–19 show that there 135 births per 1,000 girls in Mainland Tanzania and 132 per 1,000 girls in Zanzibar, way above the global average of 44. The data also shows that contraceptive access for this age group is also quite low, with 10.4% of girls aged 15–49 using any form of contraception.

It would therefore appear that the lack of access to contraceptives is contributing to the increased likelihood of adolescent girls getting pregnant.

So the claim by CCBRT that Tanzania’s adolescent fertility rate is almost three times the global average is TRUE. This is driven largely by a lack of access to contraceptives for young people in the 15–19 age group, and the relatively high levels of poverty that have driven many out of school and into early marriage.

As a result, the country is unlikely to meet the Sustainable Development Goal of overall good health and wellbeing of mothers unless it puts measures in place to ensure universal access to sexual and reproductive health-care services for girls and women of all ages.

Do you want us to fact-check something a politician or other public figure has said about public finances? Complete this form, or reach out to us on any of the contacts below, and we’ll help ensure you’re not getting bamboozled.

This report was written by PesaCheck Fellow Belinda Japhet, a Communications Consultant, Online Editor based in Tanzania. The infographics are by PesaCheck Fellow Brian Wachanga, who is a Kenyan civic technologist interested in data visualisation. This report was edited by PesaCheck Managing Editor Eric Mugendi.

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com