Connect with us

Education

Waathirika watembea km 87 kufuata ARVs!

Published

on

Takribani wakazi 40 wa kijiji cha Ifinga Kata ya Matumbi Wilaya ya Songea katika Mkoa wa Ruvuma, wanaotumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI, (ARVs) wanalazimika kutembea siku nne kufuata dawa hizo.

Licha ya kutembea umbali huo lakini dawa hizo wanazopatiwa zimebainika kuwa ni bandia, Hospitali ya Peramiho ndio waliokamata madawa hayo bandia ya kupunguza makali ya ugonjwa huo maarufu kama ARVs.

Nilipo ongea naye mmoja wa watumia wa dawa hizo, Partina John alisema kuwa natembea siku nne kwenda  kituo cha afya madaba ambapo ni zaidi ya kilometa 87 kutoka katika kijiji cha Ifinga  hadi katika kituo cha Afya Madaba.

 

mwathirikaPartina anaishi na virusi vya UKIMWI kwa miaka minne ila mumewe Dominic Haule hana maambukizi; ana watoto wawili nao hawana maambukizi na kwa sasa ni mjamzito

“Nikitoka Ifinga saa 12 asubuhi nafika katika kijiji cha Lunyanya naomba hifadhi nalala asubuhi na mapema naanza safari ya kwenda Madaba kituo cha afya  nafika saa 8 mchana, nachukua dawa na kupimwa  na lala kesho yake naanza safari ya kurudi ifinga nikifika lunyanya na lala na asubuhi naanza tena safari hadi ifinga”. Alisema Patrina ambaye anatumia dawa kwa miaka 4 sasa.

Kaimu Mganga mkuu wa Wilaya ya Songea Dokta Daniel Masawe akizungumzia juu ya kuyembea kwa kilometa 87 wa waathirika hao, wanalitambua tatizo hilo na sio kwa kijiji cha Ifinga tu, vijiji vingi vya Songea waathirika wanatembea umbali unaofanana na huo.

Dokta Masawe alisema kuwa, licha ya umbali huo lakini tumekamata madawa mbandia ya kupunguza makali ya ugonjwa huo na kupelekea kupunguza imani kwa waathirika wengi wanaotumia dawa hizo.

“Tumekamata mabox mbalimbali yakiwa yamewekwa madawa bandia ya kupunguza makali ya ugonjwa wa UKIMWI (ARVs) tumeyateketeza kwa kushirikiana na Hospitali ya Peramiho kabla hayaja wafikia watumiaji,” alisema Dokta Masawe.

Wilaya ya Songea ina vituo 12 vya kutoa dawa za kupunguza makali  UKIMWI (ARVs) kati ya hivyo vituo vitatu bado havijasajiliwa. Kitengo cha kupunguza makali ya UKIMWI kwa songea,  kinakabiliwa na changamoto ya kuwa na gali moja, inakuwa vigumu kuviratibu vituo vyote na kupeleka dawa kwa wakati.

Kwa sasa anashindwa kwenda mwenyewe kufuata dawa kwa sababu ni mjamzito na anamtuma mumewe kwenda kuchukua dawa hizo, hiyo inachangia kurudisha nyuma afya yake kutokana na kushindwa kupimwa afya yake na kujua kama dawa zinamsaidia au ana tatizo.

Aliomba serikali kuwasogezea dawa hizo kwa karibu ili kuweza kupunguza kutembea kwa muda mrefu kufuata dawa hizo, wanapita porini kuna wanyama wakali na wanadhoofu afya zao kwa kukosa lishe bora akiwa njiani.

Kwa sasa dawa hizo wanawatuma waume zao kwenda kuchukua katika kituo cha afya cha Madaba, na hutumia kwa  miezi miwili, zinapokwisha wanawatuma tena waume zao kitu ambacho kinasababisha kutokupimwa afya kwa kutokwenda muaathirika mwenyewe.

Kwa sasa kijiji cha Ifinga kina zaidi ya watu 60 kati ya hao 40 wanatumia dawa za kupunguza makali ya UKIMWI na 20 bado hawajaanza kuchukua dawa hizo, kwa mujibu wa sense ya mwaka huu kijiji hicho kina zaidi ya wakazi 3,220.

Diwani wa Kata hiyo Logatus Kianjali alisema kuwa tayali wamepeleka malalamiko hayo katika kitengo cha UKIMWI ili kuweza kuleta dawa hizo katika zahanati ya mission ili kupunguza adha ya kutembea umbali mrefu kwa wagonjwa hao.

Continue Reading
1 Comment

1 Comment

  1. KULWA MAGWA

    06/01/2013 at 9:25 am

    Kimsingi serikali ndiyo yenye jukumu la kuhakikisha kuwa dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi zinapatikana, lakini kinachoonekana ni kuwa haijaweka utaratibu mzuri wa kuzifikisha kila mahali na vijijini ndiko kwenye tatizo kubwa la upatikanaji wa dawa hizo, hapo ndipo uwajibikaji mbaya unapoonekana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Education

Kwanini ni vigumu kuomba msaada?

Published

on

Ni matarajio au matamanio ya kila mtu kusaidiwa kukamilisha jambo fulani. Iwe kazini au kwenye shughuli yoyote ya kijamii, utahitaji watu wenye ujuzi na maarifa tofauti tofauti kufanikisha malengo yako. Mfano, wachezaji wakiwa uwanjani wanacheza kwa kusaidiana kila mmoja katika nafasi yake ili kuifunga timu pinzani na kuibuka na ushindi.

Hakuna jambo lolote linaloweza kukamilika bila ya kuwa na usaidizi wa namna fulani. Lakini umewahi kujiuliza kwanini ni vigumu kwa watu kuomba msaada?

Jibu linatolewa na Mwanasaikolojia ya Jamii, Heidi Grant anaeleza kuwa, kilichopo nyuma ya kuomba msaada ni hofu ya kukataliwa ambayo imekita mizizi katika saikolojia ya uumbaji wa mwanadamu.

Katika kitabu chake kiitwacho, Reinforcements anaandika kuwa kuomba msaada ni jambo lisilopendeza linalomfanya mtu ajisikie mgonjwa.

Hilo linathibitishwa na Mtaalamu wa Saikolojia mwingine nchini Marekani, Stanley Milgram ambaye alifanya jaribio la utii na mamlaka ambapo aliwaelekeza wanafunzi wake ambao walikuwa wamesimama ndani ya treni kuomba nafasi ya kukaa kwenye viti. Anasema majibu aliyopata ni kwamba wengi wao waliogopa kuomba msaada huo. “Niliogopa ningesingeweza,” alisema mmoja wa wanafunzi.

Lakini  Milgram aliamua  kuomba siti na akakubaliwa , “ Kichwa changu kilizama katikati ya miguu yangu na nilihisi nimepigwa na butwaa,” anaandika. “Sikufanya wajibu wangu. Nilikuwa najisikia kama naenda kupotea.”

Muitiko huo ambao Grant ameuelezea unahusiana na tabia za kijamii ambazo zimeunganishwa kwenye ubongo wa mwanadamu tangu karne nyingi za uumbaji. Kama wanyama wengine, binadamu wameumbwa kupata msaada kutoka kwa familia na jamii zao ili waweze kuishi. Lakini inafika wakati tunaogopa kuomba msaada hata kama tuna shida.

 

Kwanini watu wanaogopa kuomba msaada?

Zipo sababu mbalimbali ambazo zinasababisha watu kuogopa kuomba msaada ni kupoteza  hadhi na heshima katika jamii. Wapo baadhi ya watu wana hadhi fulani ambayo anahisi akiomba msaada kwa watu  atadharaulika. Pia kukataliwa, siyo kila ombi linakubaliwa, mengine yanakatiliwa; hofu hiyo huwazuia watu kuomba msaada. Wakati mwingine ukiomba msaada inakuwa ni njia ya watu kufahamu matatizo yako na kuwaambia wengine; jambo linaloweza kutengeneza huzuni katika maisha.

Grant anaeleza kuwa kuomba msaada kunakuweka wazi zaidi na hatari za kijamii ambazo zinaweza  kudhihirisha unyonge  na kukaribisha maumivu.

Anaeleza zaidi kuwa inatengeneza huzuni, na kukaribisha uwezekano wa kukataliwa. “Hajalishi, ndiyo maana tunaogopa kuomba msaada kama tunavyogoopa maradhi,” ameandika. “Maradhi yanaweza kuwa  na hatari ndogo kwetu ukilinganisha na kuomba msaada.”

Hata hivyo, ni mara chache sana matokeo hasi tuliyoyaona hapo juu kutokea mara tunapoomba msaada. Katika utafiti mwingine, Mwanasaikolojia  Vanessa Bohns alichunguza sampuli ya watu 14,000 ambao walitakiwa kuomba msaada. Na alibaini kuwa idadi kubwa ya walioomba msaada walikuwa na uwezekano mkubwa wa kupata kuliko ambavyo walikuwa wanaamini awali.

Katika semina mbalimbali, Mhamasishaji, Antony Luvanda amekuwa akisisitiza kuwa kuomba msaada siyo ishara ya unyonge bali ni ishara kuwa umeimarika kimaisha.

Kwa maneno mengine, inaweza kuwa rahisi kupata msaada kuliko kuomba.

Continue Reading

Education

Utunzaji nyaraka za serikali katika kijiji cha Magalata

Published

on

NYARAKA mbalimbali za serikali na kumbukumbu za ofisi ya kijiji cha Magalata, kilichoko katika wilaya ya Kishapu, ziko hatarini kuharibika na kulowana na maji iwapo mvua zitanyesha.

(more…)

Continue Reading

Education

Historia ya Shule ya Msingi Nachingwea imebaki katika ‘kava’ la daftari…

Published

on

Historia ya shule ya msingi Kiegei katika kata ya Kiegei wilaya ya Nachingwea mkoa wa Lindi, imebaki katika kava moja tu la daftari, lakini shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa vitabu, vitendea kazi vya kufundishia na walimu.

(more…)

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com