Connect with us

Featured

Wasomali wamlipa Lowassa milioni 450, wampa hisa

WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu kwa kutajwa katika kashfa ya mdadi wa umeme uliohusisha kampuni tata ya Richmond Development LLC, Edward Lowassa, amelipwa mamilioni ya fedha na wafanyabiashara wa Kisomali, Fikra Pevu imethibitisha.

Published

on

WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu kwa kutajwa katika kashfa ya mdadi wa umeme uliohusisha kampuni tata ya Richmond Development LLC, Edward Lowassa, amelipwa mamilioni ya fedha na wafanyabiashara wa Kisomali, Fikra Pevu imethibitisha.

Uchunguzi wa muda mrefu wa Fikra Pevu umeonyesha kwamba Wasomali hao kupitia kampuni ya Integrated Properties Investment (T) Limited walimlipa Lowassa Sh milioni 450 kupitia kampuni yake ya Barare Limited. Malipo hayo yalielezwa kuwa ni deni ambalo Lowassa kupitia Barare alikua akiidai kampuni hiyo ya Integrated ambayo kwa Tanzania imekuwa ikijihusisha na uwekezaji katika majengo.

Uchunguzi wa Fikra Pevu umethibitisha kwamba malipo hayo yalifanyika miezi michache kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, na Lowassa na mkewe Regina Mumba Lowassa, walikubali malipo hayo kwa kupewa hisa 7,500 zikiwa na thamani ya Sh 60,000 kwa hisa moja.

Uchunguzi wa muda mrefu wa Fikra Pevu umeonyesha kwamba Wasomali hao kupitia kampuni ya Integrated Properties Investment (T) Limited walimlipa Lowassa Sh milioni 450 kupitia kampuni yake ya Barare Limited. Malipo hayo yalielezwa kuwa ni deni ambalo Lowassa kupitia Barare alikua akiidai kampuni hiyo ya Integrated ambayo kwa Tanzania imekuwa ikijihusisha na uwekezaji katika majengo.

Waraka wa Bodi ya Integrated iliyoidhinisha malipo kwa LowassaWaanzilishi wa Barare Limited

Sehemu ya nyaraka zinazohusiana na Barare Limited

Kampuni ya Barare Limited inamilikiwa na Lowassa na Regina kwa wanaoishi Mtaa wa Mahando namba 407, Masaki, Dar es Salaam, wakati Integrated ikiwa inamilikiwa na kundi la Wasomali, akiwamo Omar Abdi Ali, ambaye ni mfanyabishara na mchumi wa Kimataifa.

Continue Reading
31 Comments

31 Comments

 1. Masele

  16/01/2012 at 6:31 am

  Sioni tatizo la mtu kulipwa haki yake

 2. Juma Kambajeck

  16/01/2012 at 7:49 am

  please notify me any screty/investigative newd

  • ahmed ali

   19/01/2012 at 5:30 pm

   Please notify me if there is any secrety or investigative news.

 3. Fareed

  16/01/2012 at 4:35 pm

  PCCB imchunguze Lowassa kwa tuhuma za ufisadi. Sheria inasema kuwa kiongozi yeyote wa umma akiwa na utajiri wa mashaka (unexplained wealth) anatakiwa kupelekwa mahakamani kujibu mashitaka ya ufisadi. Je, Lowassa amedeclare mali hizi kwa Tume ya Maadili ya Uongozi? Je, Lowassa amepata wapi mali za mabilioni ya shilingi alizojilimbikizia wakati yeye ni kiongozi wa umma na si mfanyabiashara?

  • PAPAYAI OLE SEKI

   08/02/2012 at 9:43 pm

   MBUNGE WA BABATI-MJINI Bwa.KISYERI CHAMBIRI NI FISADI MKUUKUU
   Jinsi ambavyo Ksyeri Chambiri ameupata Ubunge wa Jimbo la Babati-Mjini ni kwa mtindo ule ule uliowachosha wapiga Kura wa Mkoa wa Mara na wakamkataa na Jimbo likawa limetwaliwa na upinzani. Mbunge huyo alifuja fedha alizolipwa na Serikali kwa ajili ya ukandarasi wa ujenzi wa Barabara ya kuunganisha Makao Makuu ya Mkoa wa Manyara-Babati Mjini na Makao Makuu ya Wilaya za Kiteto na Simanjiro. Fedha hizo alizitumia kununua ukoo wa ki-Iraqw na akapewa jina feki la Orondi na vivyohivyo akaununua ubunge wa Jimbo la Babati-Mjini kupitia wakandarasi wa rushwa akina mzee Sagdai, Mwenyekiti wa CCM -Wilaya ya Babati-Mjini Bwana Mtatuu Ihucha anayejiita ASKOFU pamoja na wasaliti wengineo wa demokrasia.
   Tunapenda kuitahadharisha TAKUKURU kwamba fedha za Halmashauri ya Mji-Babati zitaibwa kupita mizungu ya ndugu huyu. Tangia ameingia Bungeni hajawahi kuzungumza mahitaji ya wana-Babati Mjini kwa ulimi wake na wala hajawahi kuchangia kwa maandishi! Hajawahi kufanya ziara ya kushukuru tangu alipochaguliwa walau katika kata anayoishi kwa hoja kwamba anajua mbinu za kupata KURA za watu wa mjini Babati na sana sana atafanya ziara zake za kuwatembelea wananchi ifikapo nusu ya pili ya mwaka 2014. Kwa maneno yake mwenyewe, wakati huo ataanza kugawa fedha kwa kuwa anajua kiwango cha watu wa Babati kuwa hawataweza kumaliza Milioni 15. Huu ni ukweli kwa kuwa hivi sasa anajizatiti katika kuzikusanya kupitia njia anazozijua kwa kuwa kandarasi zimeota mgawa kwa upande wake kwa kupoteza uaminifu. Wakati akiwa katika shughuli zake nje ya Jimbo lake, vikao vya Halmashauri vinapoitishwa, yeye hupokelewa posho ambazo hakuhudhuria vikaoni kupitia kwa Mpenzi wake-Diwani wa Viti Maalum aitwaye Zainabu Dodo ambaye pia ni Mwenyekiti wa UWT-Wilaya ya Babati Mjini. Huu ni ufisadi mbaya kuwahi kufanywa na kiongozi mwenye wadhifa kama wa Chambiri. Tafadhali Bwana Hosea fuatilia orodha za malipo ya vikao vya Halmashauri ya Mji-Babati na utahakiki wizi huo wa wazi. Fanya utafiti kupitia madiwani wa Halmashuri hiyo ili uzikomboe fedha za Serikali.

 4. Pastor Kessy

  16/01/2012 at 9:10 pm

  Kwani kuna tatizo kaka kama anadai mali yake na si ya uwizi??!!

 5. James

  17/01/2012 at 1:06 am

  Hii ndio Tanzania, viongoz wanajilimbikizia mali huku watoo wanakaa chini shuleni,.Lowasa amekuwa akituhumiwa kuwa na utajiri wa mashaka. mimi nashuri afilisiwe pamoja na viongozi wengine waliopata utajiri kwa njia za kifisadi.

  • Mtanzania Mzalendo

   27/11/2012 at 4:42 pm

   Nakubaliana na wewe lakini kwa serikali ya ccm swala hili la kuwafilisi hailiwezi.
   Watu mbona wanasahau RICHMOND waliyopiga na mkuu wa kaya mpaka wakaanza kuumbuana kwenye vikao halafu wakaizima hoja ghafla.
   Alikuja pia na mvua ya kutengeneza akashtukiwa.
   Vile vile alikuwa akifuja pesa za miradi ya maji.

 6. kukomya

  17/01/2012 at 1:14 am

  Kujihusisha na “Biashara” za namna hii ndiko kunakopelekea viongozi wetu kujiingiza katika ufisadi unaoliangamiza yaifa letu sasa. Kiongozi huyu ni mtuhumiwa wa miduara kadhaa ya rushwa na ufisadi. Ameliingiza taifa katika hasara kubwa na bado anaendelea kwani hakuna wa kum “tame.”

  Ingawa tatizo ni la uroho wa utajiri wa Lowassa, tatizo kubwa zaidi hapa ni kuondolewa kwa Azimio la Arusha na miiko ya uongozi ambapo sasa viongozi wamegeuka wezi na vibakauchumi wa mchana kweupee! Hebu ona sasa, kujiingiza kwake kwenye kampuni ya Vodacom kama shareholder wa moja ya kampuni tanzu zao kunalisababishia taifa hasara kwa wahuni wale kulindwa wasilipe kodi. ]

  Wakati huko Kenya na Uganda Kampuni za Safaricom na MTN zinaongoza kwa kuchangiapato la mataifa hayo hapa kwetu makampuni ya mawasiliano yamegeuka kichomi kwa uchumiwa taifa letu kwa ushirikiano na viongozi wasio na aibu kama hawa tulio nao sasa. Kamwe haiingii akilini kuona kijikampuni kama Group5 Security kuwa juu ya Vodacom, Tigo, Airtel au Zantel kwa kuchangia pato la taifa.

  • savimbiwe

   15/02/2012 at 2:19 pm

   viongozi wanamna hii ndio wanaoendelea kuipeleka nchi shimoni nakuwauwa raia wao, sasa kama sio ukatili uliopita kiasi unaweza kuachia makapuni makubwa kama hayo yafanye biashara bila kulipa kodi wakati unajua kabisa kwamba ndio moja ya vitu vikubwa vinavyochangia kuustawi kwa uchumi then unaacha vifanye kazi bure? badala yake wanakandamiza wananchi kulipa kodi ya ju tofauti na kipato na kusabisha mifumuko ya bei na uchumi kuzid kudidimia kwa tamaa za viongozi mafisadi wasiokuwa wazalendo wala huruma kwa wapiga kura wao, ndo haohao wanaojifanya ni waumini na watoa michango mikubwa ya ujenzi wa makanisa eti kwa kujionyesha kuwa wao ni wasafi na watakatifu wakati wanachi wao wanakufa kwa umasikini kwa kukosa huduma za msingi kama vile hospilali na vifaa vya matibabu,mishahara duni na posho kwa madakitari na waalimu.

 7. Mbowe

  17/01/2012 at 11:08 am

  Sioni tatizo mtu kudai haki yake. Kama ni ya wizi basi tusubiri uchunguzi ufanyike then tutajua ukweli wa mambo!! LAKINI SIO BUSARA KUMHUKUMU MTU KWA KUDAI HAKI YAKE!!! Acheni wivu jamani..

  • savimbiwe

   15/02/2012 at 2:31 pm

   Mi ninashangaa sana kwa mtu kama mbowe kusema eti haoni sababu ya mtu kama lowasa kudai haki yake.Haki ipi anayoweza kudai lowasa? uchunguzi fanywe nanani wakati wafanya uchunguzi wenyewe ni mafisadi. huu sio wivu bali ni kutaka kujua uhalali wa kumiliki pesa nyingi kiasi hiki kwa kiongozi, wakati wananchi wanakufa njaa.Watanzania tuamke na tuachane na kukubali majibu mepesi kutoka kwa wanasiasa.

 8. Laizer

  18/01/2012 at 9:53 am

  Siyo suala la wivu au Lowassa kudai haki yake. Hapa suala ni maadili ya uongozi. Maisha yake yote, Lowassa amekuwa ni mtumishi wa umma. Wala hajapata urithi wowote wa utajiri kutoka kwa wazazi wake. Swali la msingi la kujiuliza ni kuwa, kiongozi wa umma kama Lowassa amewezaje kujilimbikizia utajiri mkubwa namna hii? Ni biashara gani anaifanya kwa kutumia ofisi ya umma? Hapa bila shaka Lowassa amejilimbikizia mali nyingi mno kwa njia zinazotia mashaka na kuna uwezekani mkubwa kuwa mali hizi wala hajaziorodhesha kwenye Sekretariat ya Maadili kama ilivyosemwa. Ingekuwa si siasa za kulindana na kuogopana hapa Tanzania, TAKUKURU ingempeleka Lowassa mahakamani kujibu mashitaka ya ufisadi kwa kuwa na utajiri wa mashaka. Kama hizo mali kweli kazipata kwa njia halali, itabidi athibitishe hilo mahakamani. Njia pekee ya kumsafisha Lowassa ni kumpeleka mahakamani, si kwa kutumia makanisa na kununua waandishi wa habari wamwandike vizuri

  • Maliondo

   19/02/2012 at 2:18 pm

   Lowassa ni mtoto wa tarishi enzi za kikoloni na mara baada ya uhuru. wanaomfahamu tangu utoto familia yake walikua watu maskini tu pale Monduli. Kwa historia yake utajiri mkubwa aliyonao ilibidi awe mrithi wa mali nyingi toka kwa wazazi wake. Kwa kuwa maisha yake yote amekua mtumishi utajiri wake mkubwa bila shaka unatokana na rushwa na ukwapuaji mkubwa wa fedha za umma.

 9. john

  18/01/2012 at 11:23 am

  Sasa hapa tatizo ni nini? Kufanya biashara siyo dhambi, wanasiasa wengi wanfanya biashara na tena za kujificha, hii biashara inafanywa kwenye makaratasi yote ya serikali. Nini tatizo? Je hao wanaopelekewa mamilioni ya dola kwenye briefcases majumbani mwao za tenda za barabara na dili chafu za waarabu kama Gaddaffi?

  • LOYAL TZN

   20/01/2012 at 12:28 pm

   kuwe na ukweli ili tusipotoshane jamani kwani maisha magumu halafu uweke uongo watu wanaweza wakatoa maamuzi magumu

 10. Fareed

  19/01/2012 at 3:02 pm

  Kufanya biashara si dhambi, wala kuwa tajiri si kosa. Tunachohoji sisi Watanzania ni kuwa Lowassa amepataje huo utajiri wake wakati hajarithi mali yoyote na maisha yake yote amekuwa ni kiongozi wa umma? Kuna biashara gani kwenye ofisi za umma? Je, amejilimbikiziaje hizo mali zake zote? Swali la msingi zaidi ni kuwa hizi mali zote hizi Lowassa ameziorodhesha serikalini kama inavyotakiwa?

  Mali zake ni pamoja na hekalu la thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1 London, Uingereza, mradi wa kujenga gorofa kwenye kiwanja cha nyumba ya sanaa, Alphatel, Alpha House, Alpha Schools, pamoja na nyumba na viwanja vyake Masaki, Arusha, na nje ya nchi. Kiongozi wa umma anapataje mali zote hizi kwa mshahara wa serikali? PCCB fanyeni kazi yenu!

 11. LOYAL TZN

  20/01/2012 at 11:55 am

  Sitegemei mfanyakazi wa serikali kuwa maskini bali wale wanaotumia madaraka yao vibaya na baadae kusema walikuwa safi huyu ndugu anafanyabiashara za wazi kwani angekuwa mwizi basi isngeliwezekana kujua kuwa ni mmiliki wa kampuni bila kuficha.

  Heri ya huyu, wanzake wengi wantumia watu na wao kujificha pale wanapostaafu ndio wanajionyesha kaka edo weka mambo wazi kwani wenzio wanajificha ile tender zote wajitumie wao kupitia vivuli vyao na pia ukiwa nazo basi hautatuibia au hautakopa kwamba ukishinda uzirudishe kaza buti tusonge mbele tunahitaji watu kama wewe tajiri na mchapakazi bila kuangalia alichonacho si kukaa tu kwenye kiti cha kuzunguka na kutembelea shangingi lenye thamani ya madawati ya shule za sekondari 4 kaka unatakiwa kumalizia ile ndoto yako ya ujenzi wa mashule kupitia nguvu za umma.

  Sasa ni kuzalisha walimu na kununua vitendea kazi,maabara ,umeme wa jua ,umeme wa kinjesi cha wanyama, nk tanakuombea ili litimie kwani TANZANIA BILA WAJINGA INAWEZEKANA AU TAZANIA NA WASOMI INAWEZEKANA TENA KWA GHARAMA NDOGO -TUKISHIRIKISHWA TATATENDA HONGERA KAKA HONGERENI WATANZANIA WOTE!!!!!!!!!!

 12. LOYAL TZN

  20/01/2012 at 12:00 pm

  TANZANIA BILA WAJINGA INAWEZEKANA AU TANZANIA NA WASOMI INAWEZEKANA TENA KWA GHARAMA NDOGO – TUKISHIRIKISHWA TUTATENDA HONGERA KAKA HONGERENI WATANZANIA WOTE!!!!!!!!!!!!!!!!!!

 13. Jeremia Issa

  20/01/2012 at 12:25 pm

  tanzania tunaelekea wapi, sisi vijana na watoto wetu tutapata nini kilicho baki miaka 20 ijayo?????
  Haya mambo yana tia hasira sana……..

 14. JOHN MTANGOO

  24/01/2012 at 10:51 am

  jamani siku hizi mtu akifanikiwa lazima ataitwa FREEMASON au FISADI. Mimi nasema tutofautishe wivu wa kutojituma na ufisadi. tutofautishe uvivu wa kufikiri na ufisadi. tutofautisha mawazo finyu ya kijamaa ya kupewa kila kitu na serikali na mawazo chanya ya kibepari ya RIZIKI YA MBWA IKO MIGUUNI MWAKE! watanzania hatujitumi na ni wavivu sana! hatutaki kazi ila tunataka maneno. Ukishapata kidogo unajisahau unaanza umalaya na kamari! Bosi akiondoka kazini hakuna moyo wa kujituma mpaka ufuatiliwe. Ni mara ngapi wachezaji wa YANGA na SIMBA wanafukuza kocha eti kwa sababu ya mazoezi magumu! TUSIPOKUWA MAKINI WATANZANIA WOTE TUTAKUWA KAMA HARUNA MOSHI BOBAN ASIYEONA NAFASI NA KUITUMIA KWA KULEWA MASIFA NA BAADAE TUTABAKI KULAUMU WALIOFANIKIWA! HEBU KILA MTU AONDOA WAZO LA UFISADI WA LOWASA NA AWEKE KWENYE JUHUDI ZA KUFANIKIWA BINAFSI!!

  • HAN=MDU

   29/01/2012 at 9:07 pm

   KWELI ND YANGU WIVU WIVU TU UNATUSUMBUA WABONGOI

 15. KANYASU

  26/01/2012 at 10:57 am

  HAPA SIONI TATIZO,KAMA LOWASA AMEFANYA BIASHARA HALALI WIVU WA NINI? au kumbe ukiwa kiongozi unatakiwa ufe masikini?

 16. bintimbwana

  26/01/2012 at 1:38 pm

  Tunakwenda pabaya. Tunatafutana na kuchokoana. Vijana kweli tutafika. Basi na turudishe nchi yetu kwenye Ujamaa ili tuanze foleni za sukari, chumvi, petrol na hata maji ya kunywa. Jamani wakataa pema pabaya pawaita.

  • zahir mlawa

   08/03/2012 at 2:40 pm

   mwenye ushahidi anaweza kwenda mahakamani kumshtaki huyo mtu kwa kupata hela kwa njia ya rushwa

 17. lugeye

  03/02/2012 at 12:29 am

  hiyo ni haki yake na it seems mh lowasa si fisadi kamawanavyodai bali ni mjasiliamali,kumbe ana biashara zake nzuri tu

 18. savimbiwe

  15/02/2012 at 2:41 pm

  watanzania mnaonaje mchawi tukamkabidhi mtoto amlee(LOWASA tumpe uraisi wa nchi 2015) manake imesha kuwa kero sasa kila kukicha unasikia habari za lowasa na zote ni za kifisadi na za kujilimbikizia sii pesa tu bali mamilioni ya pesa pamoja na kushika viwanja vikubwa sehemu za mijini.Labda siku moja itatokea miujiza na tutaweza kujua hawa viongozi wetu wanatupeleka wapi watanzania.

 19. Mt

  19/02/2012 at 10:51 am

  Nipe namba ya Rowasa niongee naye ili anipe uwazi kwani sina uhakika kama kweli yanayoandikwa hapa anayasoma au la!

 20. Asungwile

  19/02/2012 at 11:00 am

  Mheshimiwa Luluhasa alikwishafahamika tangu mbio za kumtafuta mgombea Uraisi kwa tiketi ya CCM(1995) kuwa ana utajiri usioelezeka chanzo chake. Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alimkataa.Sisi leo tunamfagilia.
  Ilisadikika kuwa yawezekana ukwasi aliokuwa nao ulitokana na nafasi zake za uongozi alizoshika katika utumishi wa umma.
  Tangu hapo hajaacha kutafuta nafasi za uongozi kwa kuwa ndiyo kiini cha ukwasi wake pia kizingti chake kiliishatoweka na hakuna mtu mwingine anyeweza kumwambia kwa ujasiri kuwa” Eee bwana tupishe kwakuwa ukipewa nafasi utaitumia kwa manufaa yako binafsi kutumia rasimali unazopaswa kuzitumia kwa wote”. Akiacha uongozi hawezi tena kupata fedha au hata kuendesha biashara zake. Angalikuwa ni mjasiriamali kweli angalijivua gamba kama Rice Tamu.
  Kuwa mjasiriamali si kosa na mjasiriamali mara zote huangalia fursa ( opportunity to exploit) na kuitumia mara moja. Luluhasa amekuwa akiona fursa na kuutumia kwa faida yake na Taifa kidogo.
  Watu wa aina hii wapo katika kila taaluma mfano wanasiasa, madaktri, waalimu, waandishi wa habari usalama wa Taifa orodha ni ndefu. Wakati mwingine watumishi wenye jukumu la kuzuia wamekuwa wakitoa ushirikiano mzuri kufanikisha nia mbaya. Ukimwangalia Luluhasa ni mjasiriamali hatari sana, ikiwa aliweza kuona fursa wakati wa uongozi wa awamu ya kwanza, wakati wa Azimio la Arusha itakuwaje leo wakati wa uongozi holela. Hoja hapa ni kuzidiana tu, lakini kama kutumia fursa kwa manufaa binafsi asiye na kosa na awe wa kwanza kutosa jiwe. Mwalimu alitosa jiwe kwa Luluhasa kwa kuwa alikuwa huru. Hakuwa na mzigo. Viongozi wa sasa wanamizigo wanaogopa kubebeshwa mara wakimgusa Luluhasa.
  Lakini, kwa upande wa pili kazi ya serikali, yenye vyombo vya usalama na ulinzi wanakuwa wapi mpaka mtumishi wa umma anapata mwanya wa kutumia nafasi yake vibaya katika utumishi wa umma? Jukumu kubwa la serikali yoyote duniani ni kusimamia watumishi wake vizuri na kuona hawakiuki sheria na maadili ya kazi zao. Kushituka baada ya mtumishi kuwa tayari amejilimbikizia mali ni sawa na mlinzi wa benki kuacha benki yake wazi ili mwizi aibe na baada ya kuanza kuzitumia pesa halafu mlinzi ananza kumtilia shaka kuwa huenda aliiba katika benki ninayoilinda. Jambo hili halitakuwa na maana sana.
  Tatizo hili ni kubwa mpaka hapo tutakapotenganisha biashara na utumishi wa umma na kuwasimamia vizuri watumishi.Tukisema wasipewe uongozi kwa sababu wana mali, hili pia litakuwa Taifa la wabaguzi kwa misingi ya mali na katiba yetu inakataza kubagua watu wake kwa misingi ya aina yoyote ile. Hoja watu wapewe uongozi lakini waangaliwe na kusimamiwa ili wasitumie vibaya madaraka yao. Wakigundulika wachukuliwe hatua kali

 21. bujhuj

  16/11/2012 at 2:27 pm

  Mbombo jilipo, LOWASSA UNANUKA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Featured

UJASUSI: Jinsi kijana wa kiume kutoka New Zealand alivyojaribu  kumuua Malikia Elizabeth II

Published

on

Shirika la Ujasusi la New Zealand  (SIS) limethibitisha kwa mara ya kwanza kwamba kulikuwa na jaribio la kumuua Malikia Elizabeth II wakati alipotembelea jiji la Kusini la Dunedin mwaka 1981.

Jaribio hilo la kumuua Malikia linalodaiwa kutekelezwa na kijana wa kiume limechochea hamasa ya polisi kutaka kujua ni kwa kiasi gani wanausalama hao walifanikiwa kuzima njama hizo.

Taarifa iliyotolewa na SIS  zinaonesha kuwa kijana huyo, Christopher Lewis (17) alipiga risasi kuelekea kwa Malikia wakati akishuka kwenye gari lake ambapo alikuwa anaenda kushuhudia Maonyesho ya Sayansi yaliyofanyika Oktoba 14, 1981 katika jiji hilo. Tukio hilo lilitokea akiwa katika ziara ya siku 8 kutembelea nchi wanachama wa Jumuiya ya Madola.

“Lewis alidhamiria kumuua Malikia, hata hivyo hakuwa katika nafasi nzuri ya kurusha risasi, hata silaha iliyotumia haikuwa katika umbali wa kuweza kumfikia mhusika,” imesema taarifa iliyotumwa SIS kwa vyombo vya habari.

Lewis ambaye anatajwa kwenye taarifa ya ujasusi kama ‘kijana msumbufu’ hakuhukumiwa kwa jaribio la kutaka kuua au kosa la uhaini. Tukio hilo lilifanywa kuwa siri ili kuzuia sifa mbaya kwa nchi (New Zealand) ambayo ilitembelewa na mgeni wa heshima. Badala yake Lewis alihukumiwa kwa kumiliki silaha kinyume na sheria na kufyatua risasi.

                       Malikia Elizabeth II akiwa ameambatana na walinzi wake alipotembelea New Zealand

Inaelezwa kuwa watu waliohudhuria tukio la kuwasili kwa Malikia walisikia mlio wa risasi lakini Polisi waliokuwa wanasimamia usalama katika eneo hilo la Dunedin waliwaambia kuwa ilikuwa ni sauti ya kuanguka kwa kitu au magari kugongana.

“Uchunguzi wa sasa wa polisi juu milio iliyosikika umefanywa kwa umakini na wawakilishi wa vyombo vya habari wamepata mrejesho kuwa kelele zilisababishwa na baruti”, inaeleza ripoti kutoka SIS iliyotolewa mwaka 1981 baada ya kutokea tukio hilo.

Kulingana taarifa za ujasusi zinaeleza kuwa polisi wamekuwa wakifuatilia nyendo za Lewis tangu 1986 ambapo Malikia alitembelea tena New Zealand wakiogopa kuwa anaweza kutekeleza tena uhalifu huo. Kuwekwa wazi kwa siri hiyo kumewaibua polisi ambao wameanza kuchunguza upya kesi hiyo.

Zaidi ya muongo mmoja uliopita, Lewis alihukumiwa kwa mauaji ya mwanamke mmoja katika mji wa Auckland na kumteka mtoto wa kike ambapo baadaye alimtupa karibu na kanisa.

Kulingana na taarifa mbalimbali za wakati huo zinaeleza kuwa Lewis alijidhuru kwa umeme akiwa gerezani mnamo 1997 akisubiri hukumu ya kuua. Lakini alikana mashtaka ya kuua kwa ujumbe mfupi wa kifo (suicide note).

New Zealand ilipata uhuru mwaka 1947 kutoka kwa Uingereza lakini inamuheshimu Malikia kama kiongozi wa taifa. Ameitembelea nchi hiyo kama Malikia mara 10 na mara ya mwisho ilikuwa 2002.

Continue Reading

Featured

FREEDOM HOUSE: Tanzania ina uhuru kiasi, kufungiwa vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya kisiasa kuididimiza kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa

Published

on

Ripoti mpya iliyotolewa na taasisi huru ya Freedom House imesema misingi ya demokrasia ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kukusanyika imeendelea kudhoofika nchini Tanzania na hali hiyo isiporekebishwa itaingia kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa duniani.

Kulingana na  Freedom House  ambao walichambua data katika nchi 195 za ulimwenguni katika mwaka 2017 wamebaini kuwa nchi 88 zina uhuru,  58 zimejumuishwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku 48 zikiwekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa.

Ripoti hiyo imebainisha kuwa misingi ya demokrasia ikiwemo uchaguzi usio huru na haki, uhuru wa kujieleza umeendelea kushuka kwa mwaka wa 12 mfufululizo duniani kote. Miongoni mwa matokeo yaliyostaajabisha ni kudhoofika kwa  Marekani ambayo ni mama wa demokrasia kutokana na uchunguzi unaofanywa na Mwendesha Mashtaka Maalumu kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka 2016 ambao ulimpa ushindi Rais Donald Trump.

Tanzania imewekwa kwenye nchi 88 ambazo zina uhuru kiasi lakini inatahadharishwa kuwa inaweza kuingia kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa. Tahadhari hiyo inatokana na mwenendo wa viongozi wa serikali kufungia vyombo vya habari, kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kushtakiwa kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa tuhuma za uchochezi na kukamatwa kwa wapinzani wa kisiasa ambao wanakosoa na kutoa mawazo yanayotofautiana na serikali.

Pia utekelezaji wa Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 na Sheria ya Makosa ya Mtandao  ya mwaka 2015 umekuwa ukilalamikiwa na wadau wa maendeleo kuwa ni mkakati wa kudhoofisha uhuru wa kutoa maoni, uwazi na uwajibikaji.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini hivi karibuni kilitoa tamko la tathmini ya uchaguzi mdogo wa marudio wa kuchagua madiwani uliofanyika katika kata 43 kwenye mikoa 19 ya Tanzania  Novemba 24 mwaka jana ambapo kilibaini mambo mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu.

Tathmini hiyo iliibua mambo mbalimbali ikiwemo matumizi mabaya ya nguvu ya vyombo vya dola, matukio ya watu kutekwa na watu wasiojulikana, watu kupigwa, kujeruhiwa  kwa lengo la kuharibu na kuvuruga uchaguzi  na vilevile kuwatia hofu wapiga kura.

 

Afrika Mashariki hali bado tete

Tanzania inaungana nchi nyingine za Afrika Mashariki ikiwemo Kenya na Uganda ambazo nazo zimewekwa kwenye kundi la nchi zenye uhuru kiasi huku za Rwanda, Burundi na Sudan ya Kusini zimejumuishwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa.

Awali Uganda ilikuwa kwenye nchi zisizo na uhuru kabisa lakini imepanda hadi kwenye uhuru kiasi kwasababu ya  kuimarika kwa tasnia ya habari na utashi wa wanahabari, blogu na  uhuru wa wananchi kutoa maoni yao licha ya mazingira ya kisiasa kuminywa na utawala wa muda mrefu wa Rais Yoweri Museveni.

Rais Museveni mwenye umri wa miaka 73 amekuwepo madarakani  tangu 1986 amefanikiwa kubadilisha sheria  ya ukomo wa umri wa miaka 75 wa kugombea urais ambapo atapata fursa ya kugombea tena mwaka 2021. Chaguzi nchini Uganda zimekuwa zikitawaliwa na vurugu za polisi na wananchi, kuzimwa kwa intaneti na kuwekwa kizuizini kwa viongozi wa upinzani ikiwemo Kizza Besigye wa chama cha Forum for Democratic Change.

Kwa upande wa Kenya ambayo imekuwa ikisifika kwa kuimarisha misingi ya demokrasia katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo kwa mara ya kwanza mahakama ilifanikiwa kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa Urais yaliyompa ushindi Rais Uhuru Kenyatta uliofanyika Agosti 2018. Uchaguzi ulirudiwa na Rais Kenyatta alichaguliwa tena.

Marudio ya uchaguzi yalilamikiwa na baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuwa hayakuzingatia haki za binadamu ambapo watu ambao walipinga uchaguzi huo walikumbana na mkono wa dola. Matendo hayo ndiyo yaliiweka Kenya kwenye kundi la nchi zilizo na uhuru kiasi.

Burundi na Sudan Kusini zimewekwa kwenye kundi la nchi zisizo na uhuru kabisa kutokana na mapigano ya kikabila ambayo yamedhoofisha mfumo wa kisiasa wa kuongoza nchi. Vyombo vya habari na wananchi wanaotoa maoni tofauti na serikali wamekuwa wakiteswa, kufungwa na kuuwawa.

Chanzo: Freedom House           – Nchi zisizo na  uhuru  – Nchi zenye uhuru     – nchi zenye uhuru kiasi   

 

Hali ilivyo Afrika

Afrika kama zilivyo nchi za Afrika Mashariki hali ya demokrasia siyo ya kuridhisha ikizingatiwa kuwa asilimia 11 ya wakazi wapatao bilioni 1.02 wa bara hilo ndio wana uhuru wa kweli, huku 52% wana uhuru kiasi na 37% hawa uhuru kabisa.

Ripoti ya Freedom House inaeleza kuwa waliangazia nchi 49 za Afrika na kugundua kuwa nchi 8 (18%) ndio zina uhuru wa kweli, nchi 22 (43%) zina uhuru kiasi na 19 (39%) hazina uhuru kabisa. Nchi zinazotajwa kuwa na uhuru ni Afrika Kusini, Namibia, Botswana, Ghana, Togo, Senegal na Kisiwa cha Sao Tome.

 Sababu ya nchi nyingi za Afrika kuwepo kwenye kundi la zisizo na uhuru ni matokeo ya viongozi kukaa madarakani muda mrefu, vurugu za kisiasa na kikabila ambazo zimekuwa zikihatarisha haki za binadamu.

 

Demokrasia ya Dunia

Demokrasia ya dunia inakabiliwa na mzozo mkubwa wa kisiasa kuliko wakati mwingine ambapo mwaka 2017 ulishuhudia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwemo kuminywa kwa  uchaguzi huru na kweli, haki za watu wachache, uhuru wa kujieleza, utawala wa sheria.

Nchi 71 kati ya 195 zimeshuhudiwa zikiteteleka katika kulinda haki za kisiasa na jamii ambapo ni nchi 35 tu ndizo zimeweza kulinda haki hizo. Kudhoofika kwa demokrasia kunaendelea kushuka kwa miaka 12 mfululizo na hatua muhimu zisipochukuliwa amani ya dunia itawekwa rehani.

Marekani ambayo ni bingwa wa demokrasia duniani nayo imeripotiwa na taasisi ya Freedom House kudhoofika katika kulinda haki za kisiasa na kijamii na kuzua mgongano wa mawazo miongoni mwa nchi zinazoibukia katika kujenga demokrasia ya dunia.

Tangu kuisha kwa vita baridi, nchi nyingi ziliachana na utawala wa kiimla na kugeukia demokrasia ya vyama vingi lakini hali hiyo imeanza kujitokeza tena ambapo idadi ya viongozi wanaoongoza kwa udikteta inaongezeka.

 

Uhuru wa nchi moja unategemea uhuru wa nchi zote

Demokrasia itabaki kuwa tunu muhimu kwa jamii zilizostaarabika, ikifungua milango ya uwazi, mawazo na fursa mpya na zaidi ya yote kulinda uhuru wa mtu mmoja mmoja. Ikiwa watu duniani kote wanadai mazingira mazuri ya kisiasa ni dhahiri wanakumbatia misingi ya demokrasia: uchaguzi huru, uhuru wa kujieleza, uwazi na uwajibikaji wa serikali, utawala wa sheria ambao hauingiliwi na polisi, jeshi au taasisi nyingine za nchi.

Hata hivyo, Karne ya 21 imeshuhudia ugumu wa kuifanya demokrasia kuwa endelevu ambapo baadhi ya nchi zinatekeleza lakini zingine zinapuuza. Utawala wa kidekteta wa Urusi na China unatambua wazi ili uendelee kuwepo unahitaji kuimarisha demokrasia katika nchi nyingine ili ziendelee kufaidika na mahusiano ya kidiplomasia. Ukuaji wa  demokrasia ni kulinda haki za watu wote duniani kupitia utandawazi   

Continue Reading

Afya

Is Tanzania’s Adolescent Fertility Rate Three Times Higher Than Global Counterparts?

Published

on

The Comprehensive Community-Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT), an organization ​which works to provide affordable medical and rehabilitative services for mothers and newborns throughout Dar-es-Salaam, marked World Contraception Day on September 26 with a call for more efforts to meet the reproductive health needs of teens between 15 and 19 years old.

The report highlights a worrying statistic — Tanzania’s adolescents are having almost three times as many children on average as their global counterparts, with 135 births per 1000 girls reported in the country, compared to an average of 44 per 1000 girls aged 15–19 worldwide in 2015.

CCRBT attributes the high adolescent fertility rate to a lack of access to contraceptive services, with Technical Advisor for Nursing Bola Abbas saying, that only about 8 per cent of current family planning clients are between the ages of 15 to 19.

On a national scale, Abbas explains, demand for family planning among adolescent girls is still very low, with only one out of every three of those who are sexually active within the 15 to 19 age group using modern contraceptive methods.

So the question is, how does Tanzania’s adolescent fertility rate compare to that of the rest of the world?

Pesacheck investigated the claim that Tanzanian adolescents are having three times as many children as their peers in the rest of the world and found that the statement is TRUE for the following reasons:

Tanzania’s adolescent fertility numbers are rather high, with 4.4% of girls aged 15 having given birth according to the country’s Demographic and Health Survey.

The Sustainable Development Goals call for countries to ensure universal access to sexual and reproductive healthcare services, including family planning, information and education, and the integration of reproductive health into national strategies and programmes by 2030.

The indicators for this goal are the proportion of women of reproductive age (15–49 years) who have their need for family planning satisfied with modern methods, and the adolescent birth rate (10–14 years and 15–19 years) per 1,000 women in that age group.

For several sub-Saharan countries, Tanzania included, access to modern family planning methods is low for this particular age group, and as a result, the regional average is 105 births per 1,000, which is more than double the global average.

Tanzania’s National Bureau of Statistics produced a national fertility and nuptiality report based on data from the 2012 national census, which shows that Adolescent Fertility Rate (AFR) was 81 births per 1,000 women aged 15–19.

The report further shows that in 2012, 23.3% of adolescent girls in the country had given birth to at least one child. Additionally, 42.2% of girls who had never attended school had given birth, compared to just 9% of those who had reached university.

This shows that there is a need for contraceptive access for teenage girls in Tanzania, especially for girls in rural areas and those with limited access to education.

The Tanzania Demographic and Health Survey 2015–16 indicates that 27% of girls aged 15–19 have given birth. Crude birth rates for girls aged 15–19 show that there 135 births per 1,000 girls in Mainland Tanzania and 132 per 1,000 girls in Zanzibar, way above the global average of 44. The data also shows that contraceptive access for this age group is also quite low, with 10.4% of girls aged 15–49 using any form of contraception.

It would therefore appear that the lack of access to contraceptives is contributing to the increased likelihood of adolescent girls getting pregnant.

So the claim by CCBRT that Tanzania’s adolescent fertility rate is almost three times the global average is TRUE. This is driven largely by a lack of access to contraceptives for young people in the 15–19 age group, and the relatively high levels of poverty that have driven many out of school and into early marriage.

As a result, the country is unlikely to meet the Sustainable Development Goal of overall good health and wellbeing of mothers unless it puts measures in place to ensure universal access to sexual and reproductive health-care services for girls and women of all ages.

Do you want us to fact-check something a politician or other public figure has said about public finances? Complete this form, or reach out to us on any of the contacts below, and we’ll help ensure you’re not getting bamboozled.

This report was written by PesaCheck Fellow Belinda Japhet, a Communications Consultant, Online Editor based in Tanzania. The infographics are by PesaCheck Fellow Brian Wachanga, who is a Kenyan civic technologist interested in data visualisation. This report was edited by PesaCheck Managing Editor Eric Mugendi.

Continue Reading

Muhimu Kusoma

Copyright © 2020 FikraPevu.com